Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima: Tamko La Nane

Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na wakati hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambapo watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo Zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu dunia katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza nafsi Yangu na wanafaa kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu. Kama sehemu kubwa ya maneno Yangu haingeelekezwa kwa udhaifu wa mwanadamu, angejigamba na kutia mambo chumvi, na angehubiri na kubuni nadharia zenye kuvutia, ni kama aliye na maarifa yote na anayejua yote kuhusu masuala duniani. Nani bado huthubutu kujigamba kati ya wale waliokuwa waaminifu Kwangu hapo awali, na ambao leo hii wanasimama imara mbele Yangu? Ni nani asiyefurahia matarajio yake mwenyewe kisiri? Wakati Sikufichua waziwazi, mwanadamu hakuwa na mahali pa kujificha na aliteswa na aibu. Ingekuwa mbaya zaidi kiasi gani Mimi Ninapozungumza kupitia njia nyingine? Wanadamu wangekuwa na hisia kubwa zaidi za kuwa wadeni, wangeamini kwamba hakuna kitu kingeweza kuwatibu, na wote wangefungwa vizuri na kutokuwa na hisia kwao. Mwanadamu anapopoteza matumaini, saluti ya ufalme husikika kwa urasmi, ambayo ni “wakati ambapo Roho aliyeongezwa nguvu mara saba Huanza kufanya kazi,” kama lilivyoongelewa na mwanadamu, kwa maneno mengine, wakati maisha ya ufalme huanza kwa urasmi duniani, yaani, wakati uungu Wangu huja kufanya kazi moja kwa moja (bila kufikiriwa na ubongo). Watu wote wanakuwa na shughuli nyingi kama nyuki; inaonekana ni kama wamefufuliwa, ni kama wameamshwa kutoka katika ndoto, na punde wanapoamka, wanapigwa na butwaa kwa kujikuta katika hali kama hiyo. Katika siku za awali, Nilisema mengi kuhusu ujenzi wa kanisa, Nilifichua siri nyingi, na wakati ujenzi wa kanisa ulifikia kilele chake, ulifikia kikomo cha ghafla. Hata hivyo, ujenzi wa ufalme ni tofauti. Wakati vita katika ulimwengu wa kiroho vinapofika hatua yake ya mwisho tu ndipo Nianzapo upya duniani. Hiyo ni kusema, ni wakati tu mwanadamu anapotaka kurudi nyuma ndipo Ninaanza kwa urasmi na kuinua kazi Yangu mpya. Tofauti kati ya ujenzi wa ufalme na ujenzi wa kanisa ni kwamba, katika ujenzi wa kanisa, Nilifanya kazi katika ubinadamu ulioongozwa na uungu. Nilishughulika moja kwa moja na asili ya zamani ya mwanadamu, moja kwa moja Nilifichua nafsi mbaya ya mwanadamu, na kuweka wazi kiini cha mwanadamu. Kwa sababu hii mwanadamu alikuja kujijua mwenyewe kwa msingi huu, na hivyo aliridhishwa katika moyo na kwa neno. Katika ujenzi wa ufalme Ninatenda moja kwa moja katika hali ya uungu Wangu, na kuruhusu watu wote kujua kile Nilicho nacho na nilicho kwa msingi wa maarifa ya maneno Yangu, hatimaye kuwaruhusu kupata ufahamu Wangu Mimi Niliye katika mwili. Hivyo hukomesha harakati zote za wanadamu kutafuta Mungu asiye dhahiri, na hukomesha nafasi ya Mungu mbinguni katika moyo wa mwanadamu, ambayo ni kusema, linaruhusu mwanadamu kujua matendo Yangu katika mwili Wangu, na hivyo linahitimisha wakati Wangu duniani.

Ujenzi wa ufalme unalenga ulimwengu wa kiroho moja kwa moja. Kwa maneno mengine, vita vya ulimwengu wa kiroho vimewekwa wazi miongoni mwa watu Wangu wote, na kutoka kwa hii inaweza kuonekana kwamba watu wote daima wamo vitani, sio tu katika kanisa, lakini hata zaidi katika wakati wa ufalme, na kwamba hata ingawa mwanadamu yuko katika mwili, ulimwengu wa kiroho unafichuliwa moja kwa moja, na mwanadamu anajihusisha na maisha ya ulimwengu wa kiroho. Hivyo, mnapoanza kuwa waaminifu, lazima mjiandae vizuri kwa ajili ya hatua ya kazi Yangu inayofuata. Mnapaswa kutoa moyo wenu wote, na ni kwa kufanya hivi tu ndio mnaweza kukidhi Moyo Wangu. Sijali kuhusu chochote ambacho mwanadamu alifanya hapo awali katika kanisa; leo, Najali kuhusu yanayotendeka katika ufalme. Katika mpango Wangu, Shetani amewahi kushindana na kila hatua, na, kama foili[a] ya hekima Yangu amejaribu siku zote kutafuta njia na namna ya kuvuruga mpango Wangu wa awali. Lakini Ningeweza kukabiliwa na miradi yake ya udanganyifu? Vyote mbinguni na duniani vinanitumikia—njama za udanganyifu za shetani zingeweza kuwa tofauti? Huku ndiko hasa kukutana kwa hekima Yangu, ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu matendo Yangu, na ni kanuni ambayo mpango Wangu wa usimamizi mzima unafanywa kupitia. Wakati wa ujenzi wa ufalme, bado Mimi Siepuki njama za udanganyifu za Shetani, ila Naendelea kufanya kazi ambayo lazima Nifanye. Kati ya vitu vyote katika ulimwengu, Nimechagua matendo ya Shetani kama foili Yangu. Je, hii si hekima Yangu? Je, si haya ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu kazi yangu? Katika tukio la kuingia katika wakati wa ufalme, mabadiliko makubwa hutokea katika mambo yote mbinguni na duniani, na wao husherehekea na kufurahi. Je, nyinyi mna tofauti yoyote? Ni nani asiyejisikia mtamu kama asali katika moyo wake? Ni nani asiyebubujikwa na furaha katika moyo wake? Ni nani asiyecheza kwa furaha? Ni nani asiyesema maneno ya sifa?

Katika yote Niliyonena na kusema kuhusu hapo juu, je, mnapata kufahamu malengo na asili ya matamko Yangu, au la? Kama Singeuliza swali hili, watu wengi wangeamini kuwa Ninabubujikwa na maneno tu, na hawangeweza kutambua chanzo cha maneno Yangu. Mkiyatafakari kwa makini, mtajua umuhimu wa maneno Yangu. Ungefanya vyema kwa kuyasoma kwa karibu: Ni yapi kati ya maneno hayo yasiyo ya faida kwako? Ni yapi yasiyo kwa ajili ya ukuaji wa maisha yako? Ni yapi yasiyozungumzia hali halisi ya ulimwengu wa kiroho? Watu wengi sana wanaamini hakuna maana katika maneno Yangu, ya kuwa hayana maelezo yoyote na tafsiri. Je, maneno Yangu kweli ni dhahania sana na yasiyoeleweka? Je, mnatii kwa kweli maneno Yangu? Je, mnayakubali maneno Yangu kwa kweli? Je, hamyachukulii kama kidude cha watoto kuchezea? Je, huyatumii kama mavazi ya kuficha uchi wa sura yako mbaya? Katika dunia hii kubwa, ni nani amechunguzwa na Mimi binafsi? Ni nani ameyasikia mwenyewe maneno ya Roho Wangu? Watu wengi sana hututusa tu gizani, wengi sana huomba wakiwa na shida, wengi sana hutazama kwa matumaini wakiwa na njaa na baridi, wengi sana wamefungwa na Shetani, ilhali wengi sana bado hawajui wanakofaa kugeukia, wengi sana hunisaliti wakiwa katika furaha, wengi sana hawana shukrani, na wengi sana ni waaminifu kwa njama za udanganyifu za shetani. Nani kati yenu ni Ayubu? Petro ni nani? Kwa nini Nimetaja mara kwa mara jina la Ayubu? Na mbona Nimemtaja Petro mara nyingi? Je, mmewahi kufahamu matumaini Yangu kwenu? Mnapaswa kuchukua muda zaidi kuwaza mambo ya aina hii.

Petro alikuwa mwaminifu Kwangu kwa miaka mingi, ilhali hakunung’unika kamwe wala kuwa na moyo wa kulalamika, na hata Ayubu hakuwa wa kulinganishwa naye. Kwa miaka na dahari watakatifu, pia, wamekuwa wenye upungufu kuliko yeye. Yeye hakufuatilia kunijua Mimi tu lakini pia alinijua wakati ambapo Shetani alikuwa anaendeleza njama zake za udanganyifu. Hii ilisababisha miaka mingi ya huduma iliyoupendeza nafsi Yangu, na kwa sababu hii Shetani hakuweza kumnyonya. Petro alitumia imani ya Ayubu, bado pia alifahamu wazi upungufu wake. Ingawa Ayubu alikuwa na imani kubwa, alikosa ujuzi wa masuala katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo alisema maneno mengi ambayo hayakulingana na hali halisi; hii inaonyesha kwamba maarifa yake bado hayakuwa ya kina, na hayakuwa na uwezo wa kufanywa kuwa kamilifu. Na hivyo, Petro siku zote alitazamia kupata hisia ya roho, na daima alilenga kuchunguza mienendo ya ulimwengu wa kiroho. Kwa sababu hii, hakuwa tu na uwezo wa kutambua kitu cha matakwa Yangu, lakini pia alielewa kidogo juu ya njama za udanganyifu za Shetani, na hivyo elimu yake ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyingine yoyote katika enzi.

Kutokana na matukio ya Petro si vigumu kuona kwamba mtu akitaka kunijua, lazima awe makini kwa kuzingatia kwa uangalifu katika roho. Sikuulizi kwamba “utoe” kiasi kikubwa Kwangu kwa nje; hili ni la umuhimu wa ziada. Iwapo hunijui, basi imani yote, upendo na uaminifu unaozungumzia ni ndoto tu, ni povu, na wewe hakika utakuwa mtu ambaye ana majivuno makubwa mbele Zangu lakini hajijui mwenyewe, ndipo wewe utanaswa tena na Shetani na hutaweza kujitoa; utakuwa mwana wa kuteseka milele, na utakuwa chombo cha uharibifu. Lakini kama wewe huna hisia na hujali kuhusu maneno Yangu, basi bila shaka unanipinga Mimi. Hii ni kweli, na ingekuwa vyema utazame kupitia lango la ulimwengu wa kiroho uone roho nyingi na tofauti tofauti zilizoadibiwa na Mimi. Ni wapi kati yao hawakukaa tu na hawakujali, na hawakuyakubali maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuwa na shaka kwa maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakujaribu kuyashika maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakutumia maneno Yangu kama silaha ya kujikinga itakayotumiwa kujilinda? Wao hawakutafuta maarifa Yangu kwa njia ya maneno Yangu, lakini waliyatumia kama vitu vya kuchezea. Katika hili, je, wao si walinipinga moja kwa moja? Maneno Yangu ni nani? Ni nani Roho Yangu? Mara nyingi Mimi Nimeyanena maneno haya kwenu, lakini maono yenu yamewahi kuwa ya kiwango cha juu na yenye uwazi? Matukio yenu yamewahi kuwa ya kweli? Ninawakumbusha mara nyingine: Iwapo hamyajui maneno Yangu, hamyakubali, na wala hamyaweki katika matendo, basi bila shaka mtakuwa chombo cha kuadibu Kwangu! Nyinyi kwa hakika mtakuwa waathirika wa Shetani!

Februari 29, 1992

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp