Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza)

Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, “Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika. Iwapo hukumu Yako itaonyesha tabia Yako, na kuruhusu tabia Yako ya haki kuonekana na viumbe wote, na iwapo inaweza kufanya upendo wangu Kwako uwe safi zaidi, ili niweze kufikia mfano wa mwenye haki, basi hukumu Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo. Najua kwamba bado kuna mengi ndani yangu yaliyo ya uasi, na kwamba mimi bado sifai kuja mbele Yako. Ningependa unihukumu hata zaidi, iwe ni kupitia mazingira ya uhasama au mateso makubwa; haijalishi jinsi Utakavyonihukumu, kwangu itakuwa ya thamani. Upendo Wako ni mkuu, na mimi niko tayari kujiweka katika huruma Yako bila malalamiko hata kidogo.” Huu ni ufahamu wa Petro baada ya yeye kuiona kazi ya Mungu, na pia ni ushahidi wa upendo wake kwa Mungu. Leo hii, nyinyi tayari mmeshashindwa—lakini ni jinsi gani ushindi huu unaonekana ndani yenu? Baadhi ya watu wanasema, “Ushindi Wangu ni neema kuu na kuinuliwa kwa Mungu. Ni sasa tu ndipo ninapotambua kwamba maisha ya mwanadamu ni bure na yasiyo na maana. Kuishi hakuna maana, afadhali nife. Ingawa mtu anatumia maisha yake kukimbia huku na kule, kuzalisha na kuongeza kizazi baada ya kizazi cha watoto, mtu hatimaye huwachwa bila chochote. Leo, baada tu ya kushindwa na Mungu ndio nimeona kwamba hakuna thamani ya kuishi kwa njia hii; kwa kweli ni maisha yasiyo na maana. Afadhali nife na kuyasahau haya!” Je, watu kama hao ambao wameshindwa wanaweza kukombolewa na Mungu? Je, wanaweza kuwa vielelezo na mifano? Watu kama hao ni somo katika kutoshughulika, hawana matarajio, na wala kujitahidi kujiboresha wenyewe! Ingawa wao huhesabiwa kama walioshindwa na Mungu, watu kama hao wasioshughulika hawawezi kufanywa wakamilifu. Karibu mwishoni mwa maisha yake, baada ya yeye kufanywa kuwa mkamilifu, Petro akasema, “Ee Mungu! Kama ningeweza kuishi miaka michache zaidi ya hapa, ningependa kufikia usafi zaidi na upendo wa ndani Kwako.” Alipokuwa karibu kusulubiwa, katika moyo wake akaomba, “Ee Mungu! Wakati Wako umewadia, wakati ulionitayarishia umefika. Mimi lazima nisulubiwe kwa ajili Yako, lazima niwe na ushuhuda huu Kwako, na ninatumai kwamba upendo wangu utaweza kukidhi mahitaji Yako, na kwamba unaweza kuwa safi zaidi. Leo, kuwa na uwezo wa kufa kwa ajili Yako, na kusulubiwa kwa ajili Yako, ni faraja na ya kutia moyo kwangu, kwa maana hakuna kinachonifurahisha kuliko kuweza kusulubiwa kwa ajili Yako na kukidhi matakwa Yako, na kuweza kujitoa Kwako, kutoa maisha yangu Kwako. Ee Mungu! Wewe ni wa kupendeza kweli! Kama Ungeniruhusu niishi, ningenuia kukupenda zaidi. Mradi tu ninaishi, mimi nitakupenda. Natamani kukupenda kwa undani zaidi. Unanihukumu, Unaniadibu, na kunijaribu kwa sababu mimi si mwenye haki, kwa sababu nimetenda dhambi. Na tabia Yako ya haki inakuwa dhahiri zaidi kwangu. Hii ni baraka kwangu, kwa maana ninapata uwezo wa kukupenda kwa undani zaidi, na mimi niko tayari kukupenda kwa njia hii hata kama Hunipendi. Mimi niko tayari kutazama tabia Yako ya haki, kwa maana inafanya niweze kuishi maisha ya maana zaidi. Mimi ninahisi kwamba maisha yangu sasa ni ya maana zaidi, kwa maana nimesulubiwa kwa ajili Yako, na ni jambo la maana kufa kwa ajili Yako. Hata hivyo bado mimi sijaridhika, kwa maana najua kidogo sana kukuhusu, najua kwamba siwezi kutimiza matakwa Yako kikamilifu, na kuwa nimekulipa kidogo mno. Katika maisha yangu, sijaweza kurudisha nafsi yangu Kwako kikamilifu; Niko mbali sana na hili. Nikitazama nyuma kwa wakati huu, mimi huhisi kuwa nina mzigo mkubwa wa madeni kwako, na sina muda mwingine ila huu kwa ajili ya kurekebisha makosa yangu na upendo wote ambao sijakulipa Wewe.”

Mwanadamu lazima azingatie kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na hapaswi kuridhika na hali yake ya sasa. Kuishi kama mfano wa Petro, lazima awe na maarifa na uzoefu wa Petro. Mtu lazima ashikilie mambo ambayo ni ya juu na zaidi ya yaliyo makuu. Ni lazima yeye afuatilie kwa ndani zaidi, usafi zaidi wa upendo wa Mungu, na maisha ambayo yana thamani na umuhimu. Haya tu ndiyo maisha; hivi tu ndivyo mwanadamu atakuwa sawa na Petro. Lazima kuzingatia kuwa makini kwa kuingia kwako kwa upande mwema, na lazima uhakikishe kwamba haurudi nyuma kwa ajili ya urahisi wa kitambo na kupuuza mambo mengine makubwa, zaidi maalum, na zaidi kwa ukweli wa vitendo. Upendo wako lazima uwe wa vitendo, na lazima utafute njia ya kujitoa katika upotovu huu, maisha yasiyo na kujali ambayo hayana tofauti na ya mnyama. Lazima uishi maisha ya maana, maisha ya thamani, na usijipumbaze, au kufanya maisha yako kama kitu cha kuchezea. Kwa kila mtu ambaye anatumai kumpenda Mungu, hakuna ukweli usioweza kupatikana, na hakuna haki wasioweza kusimama imara nayo. Unafaa kuishije maisha Yako? Unapaswa kumpenda Mungu vipi na kutumia upendo huu ili kukidhi hamu Yake? Hakuna kubwa zaidi katika maisha Yako. Zaidi ya yote, lazima uwe na matarajio hayo na uvumilivu, na hupaswi kuwa kama wanyonge wasio na nia. Lazima ujifunze jinsi ya kupitia maisha ya maana, na kuuona ukweli wa maana, na hupaswi kujichukua kipurukushani katika njia hiyo. Bila wewe kujua, maisha Yako yatakupita tu; na baada ya hapo, je utakuwa una fursa nyingine ya kumpenda Mungu? Je, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu baada ya kufa? Lazima uwe na matarajio na dhamiri sawa na ya Petro; maisha Yako ni lazima yawe na maana, na usifanye mchezo na nafsi yako! Kama mwanadamu, na kama mtu ambaye anamfuata Mungu, ni lazima uweze kufikiria kwa makini jinsi unavyoendesha maisha yako, jinsi unapaswa kujitoa mwenyewe kwa Mungu, jinsi unapaswa kuwa na imani yenye maana zaidi katika Mungu, na jinsi, kwa kuwa wewe unampenda Mungu, unapaswa kumpenda Yeye kwa njia ambayo ni safi zaidi, nzuri zaidi, na bora zaidi. Leo hii, huwezi tu kuridhika na jinsi wewe umeshindwa, lakini lazima pia uzingatie njia ambayo utatembelea siku zijazo. Lazima uwe na matarajio na ujasiri wa kufanywa mkamilifu, na hupaswi daima kufikiria kwamba huwezi. Je, ukweli una maonevu? Je, ukweli huwapinga watu kwa makusudi? Kama wewe utaufuata ukweli, je unaweza kukushinda? Kama wewe utasimama imara kwa ajili ya haki, je utakuangusha chini? Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli haukutambui, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha; Iwapo unaishi katika mwanga, na hujaweza kuupata mwanga, sio kwa sababu ni vigumu kwa mwanga kukuangazia, lakini kwa sababu wewe hujaweka makini kwa kuwepo kwa mwanga, na hivyo mwanga umeondoka kwa kimya. Kama huwezi kufuata, basi inaweza kusemwa kwamba wewe ni taka usiye na maana, na huna ujasiri katika maisha Yako, na huna roho ya kupinga nguvu za giza. Wewe ni mdhaifu mno! Huwezi kutoroka nguvu za Shetani ambazo zimekuzingira, na kuwa uko tayari tu kuishi haya maisha ya usalama na kufa katika ujinga. Kile unachopaswa kufanya ni kutekeleza azma Yako ya kuwa mshinde; huu ni wajibu wako uliokushikilia. Kama wewe umeridhika na kushindwa, basi unafukuza kuwepo kwa mwanga. Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli, lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli, lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli, na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi. Hili ndilo unalopaswa kufanya. Msitupilie mbali ukweli kwa ajili ya maisha ya amani ya familia, na lazima msiipoteze heshima na uadilifu wa maisha kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Unapaswa kufuata yote ambayo ni ya kupendeza na mema, na unapaswa kufuata njia katika maisha ambayo ni ya maana zaidi. Kama wewe unaishi maisha ya kishenzi, na wala hufuati malengo yoyote, je, si huko ni kupoteza maisha Yako? Ni nini unachoweza kupata kutoka kwa maisha ya aina hii? Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja, na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima; hakuna maana ya kuwepo kwao!

Mungu humuadibu na kumhukumu mwanadamu kwa sababu inatakiwa vile na kazi Yake, na zaidi ya hayo, kwa sababu yanahitajika na mwanadamu. Mwanadamu anahitaji kuadibiwa na kuhukumiwa, na ni vile tu ndivyo anaweza kufikia upendo wa Mungu. Leo, mmeshawishiwa kikamilifu, lakini wakati mnapokutana na kizingiti kidogo mtakuwa mashakani; kimo chenu bado ni kidogo mno, na nyinyi bado mnahitaji kupata adabu na hukumu hiyo zaidi ili mfikie ufahamu zaidi. Leo, mna heshima kidogo kwa Mungu, na mnamcha Mungu, na mnajua Yeye ni Mungu wa kweli, lakini hamna upendo mkubwa wa Kwake, na bado hamjafikia upendo safi; maarifa yenu ni ya juujuu, na kimo chenu bado hakitoshi. Wakati nyinyi mnapatana na mazingira, bado hamjashuhudia, sehemu ndogo ya kuingia kwenu ndiyo makini, na nyinyi hamjui jinsi ya kufanya mazoezi. Watu wengi ni watazamaji tu na si watendaji; wao humpenda Mungu tu kwa siri katika nyoyo zao, lakini hawana njia ya mazoezi, wala hawafahamu vizuri malengo yao ni nini. Wale ambao wamefanywa wakamilifu hawana tu ubinadamu wa kawaida, lakini wanao ukweli unaozidi vipimo vya dhamiri, na kwamba ni kuu zaidi kuliko viwango ya dhamiri; wao hawatumii tu dhamiri yao kulipia upendo wa Mungu, lakini, zaidi ya hayo, wanajua Mungu, na wameona kwamba Mungu ni mzuri, na Anastahili upendo wa mtu, na kwamba kuna mambo mengi ya upendo katika Mungu ambayo mtu hana budi ila kumpenda Mungu. Upendo wa Mungu wa wale ambao wamekuwa wakamilifu ni kwa ajili ya kutimiza matarajio yao binafsi. Upendo wao ni wa papo hapo, upendo usiouliza chochote, na usio wa kubadilisha na kitu. Wanampenda Mungu kwa sababu ya ufahamu wao Kwake, na sio kwa sababu nyingine. Watu kama hawa hawajali kama Mungu anawapa neema au la, wanaridhishwa na kumridhisha Mungu. Hawabishani na Mungu wapate kitu kwa badala yake, wala kupima upendo wao kwa Mungu na dhamiri: Umenipa, kwa hivyo nitakupenda kwa badala yake; kama Wewe Hunipi, basi sina chochote cha kukupa kwa badala yake. Wale ambao wamekuwa wakamilifu daima huamini kwamba Mungu ni Muumba, kwamba Yeye hufanya kazi Yake juu yao, na kwamba, kwa vile wao wako na fursa hii, na hali, na kufuzu kuwa na uwezo wa kufanywa wakamilifu, azma yao ni kuishi kwa kudhihirisha maisha yaliyo na maana, na wanapaswa kumridhisha Mungu. Ni kama yale aliyopitia Petro: Alipokuwa katika hatua ya udhaifu, alisali kwa Mungu na kusema, “Ee Mungu! Bila kujali wakati au mahali, Unajua kuwa mimi daima hukukumbuka. Haijalishi wakati au mahali, Unajua kuwa mimi nataka kukupenda, lakini kimo changu ni kidogo mno, mimi ni mdhaifu mno na sina nguvu, upendo wangu ni mdogo sana, na uaminifu wangu kwako pia mdogo. Ikilinganishwa na upendo Wako, mimi sifai kuishi. Natamani tu kwamba maisha yangu yasiwe bure, na kwamba nisiweze tu kulipa upendo wako, lakini, kwamba niweze kukukabidhi vyote nilivyo navyo. Kama naweza kukuridhisha, basi kama kiumbe, mimi nitakuwa na amani moyoni, na sitauliza chochote zaidi. Ingawa mimi ni mdhaifu na asiye na nguvu sasa, siwezi kusahau ushauri Wako, na siwezi kusahau upendo Wako. Sasa sifanyi kitu chochote zaidi ya kulipa upendo wako. Ee Mungu, ninahisi kuwa mbaya! Ninawezaje kukupa upendo ulio moyoni mwangu, nitafanyaje yote ninayoweza, na niwe na uwezo wa kutimiza matakwa Yako, na kuwa na uwezo wa kukupa kila nilicho nacho? Unajua udhaifu wa mwanadamu; ninawezaje kuustahili upendo wako? Ee Mungu! Unajua mimi ni wa kimo kidogo, kwamba upendo wangu pia ni mdogo. Jinsi gani niweze kufanya jinsi niwezavyo katika aina hii ya mazingira? Ninajua napaswa kuulipa upendo Wako, najua kwamba napaswa kutoa yote niliyo nayo Kwako, lakini leo kimo changu ni kidogo mno. Naomba kwamba Wewe Unipe nguvu, na kunipa ujasiri, ili niweze kuwa na upendo safi zaidi na kujitoa kwa ajili Yako, na niweze kutoa yote niliyo nayo Kwako; sitaweza kuulipa upendo Wako tu, lakini zaidi nitaweza kupitia adabu Yako, hukumu na majaribu, na hata laana kali zaidi. Umeniruhusu kutazama upendo wako, na sina uwezo wa kutokukupenda Wewe, na ingawa mimi ni mdhaifu na asiye na nguvu leo, inawezekanaje nikusahau Wewe? Upendo wako, adabu na hukumu imenisababisha mimi kujua Wewe, lakini nahisi sina uwezo wa kutimiza upendo Wako kwa hakika, kwa maana Wewe ni Mkuu zaidi. Nitawezaje kutoa yote niliyo nayo kwa Muumba?” Hilo ndilo lilikuwa ombi la Petro, ilhali kimo chake kilikuwa duni. Wakati huu, alijisikia kama kisu kilikuwa kinasukumwa katika moyo wake na alikuwa katika maumivu makali; hakujua cha kufanya katika hali hiyo. Hata hivyo bado aliendelea kuomba: “Ee Mungu! Mwanadamu ni wa kimo cha kitoto, dhamiri yake ni dhaifu, na kitu tu naweza kufikia ni kurejesha upendo Wako. Leo, mimi sijui jinsi ya kukidhi tamaa Yako, au kufanya yote ninayoweza, au kutoa yote niliyonayo, au jinsi ya kukukabidhi yote niliyonayo Kwako. Licha ya Hukumu Yako, licha ya adabu Yako, licha ya yote uliyonipa, licha ya yale Unachukua kutoka kwangu, Niokoe kutokana na aina yoyote ya lalamiko Kwako kutoka kwangu. Mara nyingi, wakati uliniadibu na kunihukumu, nilijinung’unikia, na sikuwa na uwezo wa kufikia usafi, au wa kutimiza matakwa Yako. Ulipaji wangu wa upendo Wako ulizaliwa kutokana na lazima, na katika wakati huu najichukia hata zaidi.” Ilikuwa ni kwa sababu yeye alitaka upendo safi zaidi wa Mungu kwamba Petro aliomba kwa njia hii. Alikuwa akitafuta, na kumwomba, na, zaidi ya hayo, alikuwa akiishtaki nafsi yake, na kukiri dhambi zake kwa Mungu. Alijisikia mdeni kwa Mungu, na aliichukia nafsi yake, ilhali alikuwa pia kwa kiasi fulani mwenye huzuni na asiyeshughulika. Yeye daima aliona hivyo, kama kwamba hakuwa mzuri wa kutosha kwa ajili ya matakwa ya Mungu, na kuwa hakuweza kufanya bora zaidi. Katika hali kama hiyo, Petro bado alifuata imani ya Ayubu. Aliona jinsi imani ya Ayubu ilivyokuwa kubwa, kwa maana Ayubu aliona kwamba yote yalifanywa na Mungu, na ilikuwa ni ya asili ya Mungu kuchukua kila kitu kutoka kwake, na kwamba Mungu angempa yeyote ambaye Angependa kumpa—hivyo ndivyo ilivyokuwa tabia ya haki ya Mungu. Ayubu hakuwa na malalamiko, na bado aliweza kumtukuza Mungu. Petro pia alijua mwenyewe, na katika moyo wake akaomba, “Leo mimi siwezi kuridhika na kulipa upendo Wako kwa kutumia dhamiri yangu na kwa upendo wowote ninaokupa, kwa sababu mawazo yangu yamepotoshwa sana, na kwa sababu mimi sina uwezo wa kukuona Wewe kama Muumba. Kwa sababu mimi bado sifai kukupenda, lazima kukamilisha uwezo wa kutoa yote niliyonayo Kwako, na hivyo nitafanya kwa hiari. Ni lazima nijue yote Uliyofanya, na sina budi, na mimi lazima nitazame upendo Wako, na kuwa na uwezo wa kusema sifa Zako, na kutaja jina lako takatifu, ili Uweze kupata utukufu mwingi kupitia kwangu. Mimi niko tayari kusimama imara katika ushuhuda huu Kwako. Ee Mungu! Upendo wako ni wenye thamani na wa kupendeza; jinsi gani mimi ningetaka kuishi katika mikono ya yule mwovu? Je, mimi sikuumbwa na Wewe? Ningewezaje kuishi chini ya miliki ya Shetani? Ningependa nafsi yangu nzima iishi chini ya adabu Yako. Sitaki kuishi chini ya miliki ya yule mwovu. Kama mimi ninaweza kutakaswa, na ninaweza kutoa yote niliyonayo Kwako, mimi niko tayari kutoa mwili wangu na akili kwa hukumu na adabu Yako, kwa maana mimi nachukizwa na Shetani, na sina nia ya kuishi chini ya uwanja wake. Kupitia hukumu Yako kwangu, umenionyesha tabia Yako ya haki; Nina furaha, na sina malalamiko hata kidogo. Kama mimi nina uwezo wa kutekeleza jukumu la kiumbe, mimi niko tayari kuwa maisha yangu yote yaambatane na hukumu Yako, kwa njia ambayo mimi nitapata kujua tabia Yako ya haki, na kujiondolea ushawishi wa yule mwovu.” Petro aliomba hivyo kila mara, na daima alitaka hivyo, na aliufikia ulimwengu wa juu. Hakuweza tu kuulipa upendo wa Mungu, lakini, la muhimu zaidi, yeye alitimiza wajibu wake kama kiumbe. Hakutuhumiwa tu na dhamiri yake, lakini alikuwa pia na uwezo wa kuvuka viwango vya dhamiri. Maombi yake yaliendelea kwenda mbele za Mungu, hivyo kwamba matarajio yake yalikuwa milele juu, na upendo wake kwa Mungu ulikuwa milele mkuu. Ingawa yeye alipitia maumivu makali, bado hakusahau kumpenda Mungu, na bado alitaka kufikia uwezo wa kuelewa mapenzi ya Mungu. Kwa maombi yake yalitamkwa maneno yafuatayo: Sijatimiza chochote zaidi ya ulipaji wa upendo wako. Sijatoa ushuhuda Kwako mbele ya Shetani, sijajiweka huru mwenyewe kutokana na ushawishi wa Shetani, na bado naishi miongoni mwa umbo la mwili. Ningependa kutumia upendo wangu kumshinda shetani, na kumwaibisha, na hivyo kuridhisha hamu Yako. Ningependa kujitoa mzima kwako, nisijitoe hata kidogo kwa Shetani, kwani Shetani ni adui Wako. Zaidi ya alivyoendelea kwa njia hii, ndivyo alivyozidi kusongeshwa, na ndivyo ujuzi wake wa mambo haya ulivyozidi kukua. Bila kujua, alitambua kwamba anapaswa kujikwamua kutokana na ushawishi wa Shetani, na kujirudisha mwenyewe kabisa kwa Mungu. Huo ndio ulimwengu alioufikia. Alikuwa anauzidi kwa mbali ushawishi wa Shetani, na kujitoa mwenyewe kwenye raha na starehe za mwili, na alikuwa tayari kupitia kwa kina zaidi adabu zote na hukumu ya Mungu. Alisema, “Hata ingawa ninaishi katika adabu Yako, na huku kukiwa na hukumu Yako, bila kujali ugumu unaohusiana na maisha, bado mimi sina nia ya kuishi chini ya miliki ya Shetani, sina nia ya kuteseka na hila za Shetani. Mimi nina furaha kuishi kwenye laana Yako, na ninapata uchungu kwa kuishi katika baraka za shetani. Nakupenda kwa kuishi katika hukumu Yako, na hii huniletea furaha kuu. Adabu Yako na hukumu ni yenye uadilifu na takatifu; ni vyema ukinitakasa, na hata zaidi kuniokoa. Ninapenda niishi maisha yangu yote katika hukumu Yako na kuwa chini ya uchungaji Wako. Sina nia ya kuishi chini ya mamlaka ya Shetani hata kwa dakika moja; Napenda kutakaswa na Wewe, kuteseka kwa ugumu wa maisha, na sina nia ya kutumiwa na kuhadaiwa na shetani. Mimi, kiumbe hiki, nafaa nitumike na Wewe, nijazwe na Wewe, nihukumiwe na Wewe, na kuadibiwa na Wewe. Nafaa hata nipokee laana kutoka Kwako. Moyo wangu hufurahi wakati Uko tayari kunibariki, kwa maana nimeona upendo Wako. Wewe ni Muumba, na mimi ni kiumbe: Sifai kukusaliti Wewe na kuishi chini ya himaya ya Shetani, wala sifai kutumiwa na Shetani. Mimi nafaa kuwa farasi wako, au ng'ombe, badala ya kuishi kwa ajili ya Shetani. Afadhali niishi katika adabu Yako, bila neema ya kimwili, na hii itanipa raha na starehe hata kama ningepoteza neema Yako. Ingawa neema Yako haiko nami, mimi nafurahia kuadibiwa na kuhukumiwa na Wewe; Hii ndiyo baraka Yako nzuri zaidi, neema Yako kuu. Ingawa Wewe daima ni Mkuu na mwenye ghadhabu kwangu, bado mimi siwezi kukuacha, bado sina uwezo wa kukupenda vya kutosha. Ningependelea kuishi katika nyumba Yako, Ningependa kulaaniwa, kuadibiwa, na kuchapwa na Wewe, na sina nia ya kuishi chini ya himaya ya Shetani, wala mimi sina nia ya kukimbilia na kushughulika kwa ajili ya mwili tu, zaidi ya hayo siko tayari kuishi kwa ajili ya mwili.” Upendo wa Petro ulikuwa upendo safi. Huu ni ujuzi wa kufanywa mkamilifu, na ni ulimwengu wa juu wa kufanywa mkamilifu, na hakuna maisha yaliyo na maana zaidi ya haya. Alikubali adabu ya Mungu na hukumu, aliipenda tabia ya Mungu ya haki, na hakuna jambo kuhusu Petro lililokuwa la thamani zaidi ya hili. Alisema, “Shetani ananipa starehe za mwili, lakini mimi sithamini hayo. Adabu ya Mungu na hukumu inakuja juu yangu—na katika hili mimi nimeneemeka, katika hili mimi ninapata starehe, na katika hili mimi nimebarikiwa. Kama si kwa hukumu Yake, mimi singeweza kumpenda Mungu, bado ningeishi chini ya himaya ya Shetani, bado ningedhibitiwa nayo, na ningekuwa naamuriwa nayo. Kama ingekuwa vile, singewahi kuwa binadamu wa kweli, kwa maana singeweza kumtosheleza Mungu, na singejitoa kikamilifu kwa Mungu. Japokuwa Mungu Hanibariki, na kuniacha bila faraja ndani yangu, kana kwamba moto mkuu unachoma ndani yangu, na hakuna amani au furaha, na hata ingawa adabu na nidhamu ya Mungu kamwe iko na mimi, katika adabu ya Mungu na hukumu ninao uwezo wa kuona tabia Yake ya haki. Mimi hupata furaha katika hili; hakuna kitu cha thamani zaidi au cha maana zaidi ya hili katika maisha. Ingawa ulinzi Wake na huduma vimekuwa adabu kali, hukumu, laana na mipigo, bado mimi hupata starehe katika mambo haya, kwani yanaweza kunitakasa bora zaidi, yanaweza kunibadilisha, yanaweza kunileta karibu na Mungu zaidi, yanaweza kufanya niweze kumpenda Mungu zaidi, na yanaweza kufanya upendo wangu kwa Mungu uwe safi zaidi. Hii inanifanya niwe na uwezo wa kutimiza wajibu wangu kama kiumbe, na inanichukua mbele za Mungu na kuniweka mbali na ushawishi wa Shetani, ili nisije tena nikamtumikia Shetani. Wakati siishi chini ya himaya ya Shetani, na ninaweza kutoa kila kitu nilicho nacho na kile ninachoweza kwa ajili ya Mungu, bila kubakisha chochote—hapo ndipo nitakuwa nimeridhika kikamilifu. Ni adabu ya Mungu na hukumu Yake ndiyo iliyoniokoa, na maisha yangu hayawezi kutengwa kutoka kwenye adabu na hukumu ya Mungu. Maisha yangu hapa duniani yamo chini ya himaya ya Shetani, na isingekuwa huduma na ulinzi na adabu ya Mungu na hukumu Yake, ningeliishi daima chini ya himaya ya Shetani, na, zaidi ya hayo, singekuwa na nafasi au njia ya kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Ni wakati tu ambapo adabu ya Mungu na hukumu kamwe hainiachi, ndio nitakapokuwa na uwezo wa kutakaswa na Mungu. Ni kwa maneno makali na tabia ya haki ya Mungu, na hukumu kuu ya Mungu, ndipo nimepata ulinzi mkuu, na kuishi katika mwanga, na kupokea baraka za Mungu. Kuwa na uwezo wa kutakaswa, na kujiweka huru kutokana na Shetani, na kuishi chini ya utawala wa Mungu—hii ndiyo baraka kubwa zaidi katika maisha yangu leo.” Huu ndio ulimwengu wa juu zaidi aliopitia Petro.

Hizi ndizo hali ambazo mwanadamu lazima afikie baada ya kufanywa mkamilifu. Kama huwezi kufikia kiasi hiki, basi huwezi kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Mwanadamu anaishi katika mwili, ambayo ina maana anaishi katika kuzimu ya binadamu, na bila hukumu na adabu ya Mungu, mwanadamu ni mchafu kama Shetani. Mwanadamu atawezaje kuwa mtakatifu? Petro aliamini kwamba adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu! Petro aliomba, “Ee Mungu! Mradi tu Wewe unaniadibu na kunihukumu, nitajua kwamba Wewe hujaniacha. Hata kama Huwezi kunipa furaha au amani, na kufanya niishi katika mateso, na kunirudi mara nyingi, bora tu Hutaniacha moyo wangu utakuwa na amani. Leo hii, adabu Yako na hukumu umekuwa ulinzi wangu bora na baraka yangu kubwa. Neema unayonipa inanilinda. Neema unayoweka juu yangu leo ni kielelezo cha tabia Yako ya haki, na ni adabu na hukumu; zaidi ya hayo, ni majaribu, na, zaidi ya hapo, ni maisha ya mateso.” Petro alikuwa na uwezo wa kuweka kando raha ya mwili na kutafuta mapenzi zaidi na ulinzi zaidi, kwa sababu alikuwa amepata neema nyingi kutoka kwa adabu na hukumu ya Mungu. Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na yupo katika mwili; kama yeye hatatakaswa na kupokea ulinzi wa Mungu, basi mwanadamu atakuwa milele mpotovu zaidi. Kama yeye anataka kumpenda Mungu, basi lazima atakaswe na kuokolewa. Petro aliomba, “Mungu, wakati Unanitendea wema ninapata furaha, na kuhisi faraja; wakati unaniadibu, najisikia faraja kubwa zaidi na furaha. Ingawa mimi ni mdhaifu, na kuvumilia mateso yasiyotajika, ingawa kuna machozi na huzuni, Unajua kwamba huzuni huu ni kwa sababu ya kutotii kwangu, na kwa sababu ya udhaifu wangu. Mimi ninalia kwa sababu siwezi kukidhi hamu Yako, nahisi huzuni na majuto kwa sababu mimi sitoshi kwa mahitaji Yako, lakini niko tayari kufikia ulimwengu huu, niko tayari kufanya yote niwezayo ili nikuridhishe. Adabu Yako imeniletea ulinzi, na kunipa wokovu bora; hukumu Yako inazidi ustahimili Wako na uvumilivu Wako. Bila adabu Yako na hukumu, singefurahia huruma Yako na rehema. Leo, naona zaidi kwamba upendo wako umepita mipaka ya mbinguni na kumahiri wote. Upendo wako sio tu huruma na fadhili; hata zaidi ya hayo, ni adabu na hukumu. Adabu Yako na hukumu imenipa mengi. Bila adabu Yako na hukumu, hakuna hata mmoja angetakaswa, na hakuna hata mmoja angeweza kupata upendo wa Muumba. Ingawa nimevumilia mamia ya majaribio na mateso, na hata nimekuwa karibu na kifo, mateso hayo[a] yameniruhusu kukujua Wewe kwa kweli na kupata wokovu mkuu. Kama adabu Yako, hukumu na nidhamu vingeondoka kutoka kwangu, basi ningeishi gizani, chini ya himaya ya Shetani. Mwili wa binadamu una faida gani? Kama adabu Yako na hukumu ingeniwacha, ingekuwa kana kwamba Roho Wako alikuwa ameniacha, ni kama Wewe Haukuwa tena pamoja nami. Kama ingekuwa vile, ni jinsi gani ningeendelea kuishi? Kama Wewe utanipa ugonjwa, na kuchukua uhuru wangu, naweza kuendelea kuishi, lakini adabu Yako na hukumu vikiondoka kutoka kwangu, sitakuwa na njia ya kuendelea kuishi. Kama ningekuwa bila adabu Yako na hukumu, ningepoteza upendo Wako, upendo ambao ni mkuu sana mpaka sina maneno ya kuueleza. Bila Upendo wako, ningeishi chini ya himaya ya Shetani, na singeweza kuuona uso wako mtukufu. Jinsi gani, Nieleze, ningeweza kuendelea kuishi? Giza kama hili, maisha kama haya, singeweza kuvumilia. Mimi kuwa na wewe ni kama kukuona Wewe, hivyo ni jinsi gani ningeweza kukuacha? Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu, hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho. Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe; jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe? Nimemwaga machozi mengi ya huzuni kwa sababu ya upendo Wako, ilhali daima nimehisi kuwa maisha kama haya ni ya maana zaidi, yenye uwezo mwingi wa kuniimarisha, yenye uwezo zaidi wa kunibadilisha, na yenye uwezo zaidi wa kunifanya nifikie ukweli ambao lazima viumbe wawe nao.”

Tanbihi:

a. Maandishi ya asilia yanasema “ya-”.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp