Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, wewe unalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je umeona umuhimu ulioko humu? Je, unajua juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yako? Je, unaweza thubutu kuweka wazi kila ulichofanya mbele Yangu? Na mna ujasiri wa kujiita watu Wangu usoni Mwangu—hamna hisia za aibu, pia, bila mantiki yoyote! Wakati mmoja au mwingine, watu kama hawa watafukuzwa kutoka katika nyumba Yangu. Usithubutu kunidanganya, ukifikiri kwamba umesimama kwa ajili ya ushuhuda Wangu! Je, hili ni jambo ambalo binadamu ana uwezo wa kufanya? Iwapo hakungekuwa na kitu kilichobakia katika nia na malengo yako, ungekuwa tayari umeshika njia tofauti. Je, unafikiri kuwa Sijui ni kiasi gani moyo wa binadamu unaweza kustahimili? Kuanzia wakati huu kuendelea, katika mambo yote lazima ujiweke katika ukweli wa mazoezi; kupiga tu domo, kama ulivyokuwa ukifanya, hakutakusaidia. Katika siku zilizopita, wengi wenu mlifaulu kudoea chini ya paa Langu; Kwa sababu ya ukali wa maneno Yangu, wewe umeweza kusimama imara mpaka leo. Je, unafikiri kwamba maneno Yangu huzungumzwa tu kiholela bila sababu? Haiwezekani! Mimi huangalia chini juu ya mambo yote kutoka juu, na Ninatoa mamlaka juu ya mambo yote kutoka juu. Kwa njia iyo hiyo, Nimeutuma wokovu Wangu juu ya dunia. Kamwe hakuna wakati ambapo Mimi Sitazami, kutoka mahali Pangu pa siri, kila hatua ya binadamu, kila wanachosema na kutenda. Binadamu Kwangu ni kama kitabu kilicho wazi: Mimi Nawaona na kuwajua kila mmoja. Mahali hapo pa siri ni makaazi Yangu, na mbingu ndiyo kitanda ambamo Mimi hujilaza. Jeshi la shetani haliwezi kunifikia, kwa maana Mimi nimejawa na ukuu, haki na hukumu. Siri isiyoelezeka imo katika maneno Yangu. Wakati Naongea, unakuwa kama ndege waliotupwa majini, wakazidiwa na kuchanganyikiwa, au watoto ambao wamepatwa na hofu hivi karibuni, wakionekana kutojua lolote, kwa sababu roho yako imeingia katika hali ya mshangao. Kwa nini Nasema kwamba mahali pa siri ni makaazi Yangu? Je, unajua maana ya ndani ya yale Ninayosema? Ni nani katika binadamu wote ana uwezo wa kunijua Mimi? Nani ana uwezo wa kunijua Mimi kama vile anavyomjua baba yake na mama yake? Ninapopumzika katika makaazi Yangu, Mimi huchunguza kwa karibu: Watu wote duniani wamo katika pilka pilka, "kusafiri duniani kote" na kukimbia huku na kule, yote kwa ajili ya hatima yao, maisha yao ya baadaye. Lakini hakuna hata mmoja anayeweka nguvu yake kwa ajili ya kujenga ufalme Wangu, hata nguvu kiasi cha ile mtu anayotumia kuvuta pumzi. Mimi Niliumba wanadamu, na Nimewaokoa mara nyingi kutoka katika dhiki, lakini hawa binadamu ni wasio na shukrani wote: Hakuna hata mmoja miongoni mwao anayeweza kuhesabu matukio yote ya wokovu Wangu. Imekuwa miaka mingapi, zimekuwa karne ngapi tangu kuumbwa kwa dunia mpaka wa leo, na ni miujiza ngapi Niliyofanya, mara ngapi Nimeweka wazi hekima Yangu? Lakini mwanadamu, kama mwendawazimu anayeteseka na shida ya akili na kiwewe au, wakati mwingine kama kongoni anayeputa huku na kule katika msitu, hana nia hata kidogo ya kuyajali mambo Yangu. Mara nyingi Nimempa mwanadamu hukumu ya kifo na kumhukumu afe, lakini mpango wa usimamizi wa kazi Yangu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote. Kwa hivyo mwanadamu bado yuko katika mikono Yangu, akiegemea vile vitu vya kale alivyokwamilia. Kwa sababu ya hatua za kazi zangu, mimi, kwa mara nyingine tena, Nimewaokoeni, ninyi viumbe mliozaliwa katika familia kubwa zenye ufisadi, uozo, uchafu, na aibu.

Kazi Niliyopanga inaendelea kusonga mbele bila kukoma hata kwa muda kidogo. Baada ya kuingia katika Enzi ya Ufalme, na baada ya kukuweka katika ufalme Wangu kama watu Wangu, Nitakuwa na madai mengine ya kuweka dhidi yako; Hiyo ni kusema, Nitaanza kutangaza rasmi na kueneza mbele yako katiba ambayo Nitatumia kuongoza enzi hii:

Kwa sababu mnaitwa watu Wangu, mnapaswa kuwa na uwezo wa kulitukuza jina Langu, kumaanisha, kusimama katika ushuhuda wakati wa majaribio. Mtu yeyote akijaribu kunidanganya na kunificha ukweli, au kushiriki katika shughuli zisizo za heshima nyuma Yangu, bila ubaguzi Nitamfukuza nje, aondolewe kutoka kwa nyumba Yangu awe akisubiri hukumu. Wale ambao hawajakuwa waaminifu na watiifu Kwangu katika siku za mbeleni, na leo hii wanainuka na kunihukumu hadharani, wao pia watafukuzwa kutoka kwa nyumba Yangu. Wale ambao ni watu Wangu lazima wajali kuhusu mizigo Yangu kila mara na vile vile kutafuta kujua maneno Yangu. Ni watu kama hawa tu ndio Nitakaowapa nuru, na wao kwa hakika wataishi chini ya uongozi Wangu na kupata nuru, na kamwe hawatakutana na kuadibu. Wale ambao, kwa kutojali mizigo Yangu, wanamakinika na mipango ya hatima yao wenyewe, yaani, wale ambao hawalengi kwa matendo yao kukidhi Moyo Wangu bali wanataka kuomba omba vya bure, viumbe hawa wanaofanana na waombaji, Ninakataa kata kata kuwatumia, kwa sababu tangu walipozaliwa hawajui chochote kuhusu maana ya kujali mizigo Yangu. Wao ni watu wenye akili isiyokuwa ya kawaida; watu kama hawa wanaugua kutokana na "utapiamlo" wa ubongo, na wanastahili kwenda nyumbani wapate "lishe." Siwahitaji watu wa aina hii. Miongoni mwa watu Wangu, kila mtu atatakiwa kuzingatia kuwa kunijua ni wajibu unaotakiwa kutekelezwa mpaka mwisho, kama kula, kuvaa, na kulala, mambo ambayo mtu kamwe hawezi kusahau hata kwa muda mfupi, ili kwamba mwishowe kunijua litakuwa jambo la kawaida kama vile kula, jambo ambalo wewe hufanya bila jitihada yoyote, kwa mkono uliozoea. Kuhusu maneno Ninayoyanena, Kila neno lazima lichukuliwe kwa uhakika mkubwa na lichukuliwe kikamilifu; hakuwezi kuwa na hatua nusu za uzembe katika kutimiliza haya. Mtu asiyekuwa makini na maneno Yangu ataonekana kama ananipinga Mimi kwa uwazi; mtu yeyote asiyeyala maneno Yangu, au hatafuti kuyajua, ataonekana kama ambaye hanizingatii, na bila kusita atafagiliwa nje ya mlango wa nyumba Yangu. Kwa maana, kama Nilivyosema zamani, Ninachotaka sio watu wengi ila wateule wachache. Kati ya watu mia, kama mmoja tu ataweza kunijua kupitia maneno Yangu, basi bila kusita Ningewatupilia mbali wengine wote ili Nizingatie kumpa nuru na kumweka katika mwanga mmoja huyu. Kutokana na hili unaweza kuona kuwa si mbali na ukweli kwamba idadi kubwa pekee ndio inaweza kunidhihirisha, kuishi kwa maisha ya Kimungu. Ninachotaka ni ngano (hata ingawa viini vya mbegu havijajaa) na sio vigugu mwitu (hata kama viini vyake vimejaa vya kutosha na ni vya kutamanika). Na kwa wale wasiojali kuhusu kutafuta lakini badala yake kuwa na tabia za kuzembea, wanapaswa kuondoka kwa hiari yao wenyewe; Mimi sitaki kuwaona tena, wasije wakaleta aibu kwa jina Langu. Kuhusu yale Ninayohitaji kutoka kwa watu Wangu, Nitakomea katika maagizo hayo kwa sasa, na Nitasubiri kuweka vikwazo zaidi kulingana na jinsi mabadiliko ya hali yatakavyokuwa.

Katika siku zilizopita, idadi kubwa ya watu walifikiri Mimi ni Mungu Mwenyewe mwenye hekima, kwamba mimi ndiye Nilikuwa Mungu aliyeona ndani kwa kina ya mioyo ya watu; lakini yote yalikuwa maneno ya juu juu tu. Kama mwanadamu angenijua kwa kweli, hangedhania na kurukia mambo bila kuzingatia kikamilifu, ila angezidi kujaribu kuendelea kunijua kupitia maneno Yangu. Wakati tu alifika katika hatua ambapo kweli angepata kuona matendo Yangu, ndipo angestahili kusema kwamba Nilikuwa mwenye busara, kwamba Mimi ni wa ajabu. Ufahamu wako kunihusu ni mdogo mno. Katika enzi zote, ni watu wangapi wamenihudumia na kwa miaka mingapi, baada ya kuona matendo Yangu, wakaja kujua kwa hakika kitu kunihusu; na basi daima wakawa na moyo wa unyenyekevu Kwangu, na kutokuwa na nia hata kidogo ya upinzani Kwangu, kwa sababu ni vigumu jinsi gani kutafuta nyayo Zangu. Kama uongozi Wangu ungekosekana miongoni mwa watu hawa, hawangethubutu kutenda bila kufikiria, na hivyo, baada ya kuishi kwa uzoefu wa miaka mingi, hatimaye walijumlisha sehemu ya ufahamu kunihusu, wakisema kwamba Mimi ni wa Hekima, wa Ajabu na Mshauri, kwamba maneno Yangu ni kama upanga wenye makali pande mbili, kwamba matendo Yangu ni makuu, ya kustaajabisha, na kupendeza, kwamba Mimi Nimevikwa adhama, kwamba hekima Yangu inafika juu kuliko anga, na ufahamu mwingine. Lakini leo wewe unanijua tu kwa misingi ambayo wao walitengeneza, kwa hivyo idadi kubwa kati yenu, kama walivyo kasuku, mnayarudia tu maneno waliyosema. Ni kwa sababu Mimi huzingatia jinsi ufahamu wako Kwangu ni mdogo na udogo wa "elimu" yako ndio maana Nimekusamehe kuadibu kwingi. Lakini hata hivyo, idadi kubwa kati yenu bado hawajijui wenyewe, au unafikiri tayari ushayafikia mapenzi Yangu katika matendo yako, na kwa sababu hii umeepuka hukumu. Au unafikiri kwamba, baada ya kuwa na mwili, Nimekosa kujua kabisa mwelekeo wa matendo ya mwanadamu, na kwa sababu hii pia umeepuka kuadibu. Ama unafikiri kwamba Mungu unayemwamini hayuko katika maeneo yote ya ulimwengu, na kwa hivyo umeweka kumjua Mungu kama shughuli ya kufanya wakati huna shughuli nyingine badala ya kuweka kumjua Mungu katika moyo wako kama wajibu ambao lazima utekelezwe, na kutumia imani katika Mungu kama njia ya kuchangamsha wakati ambao labda ungetumiwa kwa kuzembea. Kama Singeuonea huruma ukosefu wako wa sifa za kustahili, mantiki, na ufahamu, basi nyote mngeangamia katika kuadibu Kwangu, na kutoweka kabisa ulimwenguni. Lakini hadi wakati Kazi Yangu hapa duniani itamalizika, Mimi Nitabaki mwenye huruma kwa mwanadamu. Hili ni jambo ambalo lazima nyote mlijue. Komeni kuyachanganya mazuri na mabaya.

Februari 25, 1992

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Kumi Na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa Waovu Lazima Waadhibiwe Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu Jinsi ya Kuujua Uhalisi Amri za Enzi Mpya Ufalme wa Milenia Umewasili Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe Kuijua Kazi ya Mungu Leo Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania? Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika" Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne Je, Umekuwa Hai Tena? Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili) Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili Je, Utatu Mtakatifu Upo? Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza) Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili) Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali? Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi? Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi Unajua Nini Kuhusu Imani? Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe” Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia Kazi katika Enzi ya Sheria Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza) Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili) Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu? Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza) Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili) Kiini cha Mwili Ulio na Mungu Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza) Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili) Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu? Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako Wewe U Mwaminifu kwa Nani? Maonyo Matatu Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu Kutanafusi kwa Mwenye Uweza Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji