Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Ni shughuli sahihi ya mwanadamu kuchukua maneno Yangu kama msingi wa maisha yake. Mwanadamu lazima aanzishe fungu lake binafsi katika kila sehemu ya maneno Yangu; kutofanya hivyo kutakuwa kuuliza matata, kutafuta maangamizo yake mwenyewe. Binadamu haunijui, na kwa sababu ya hili, badala ya kuleta maisha yake Kwangu badala, anachofanya ni kujipanga tu mbele Yangu na takataka mikononi mwake, na hivyo kujaribu kuniridhisha. Lakini, mbali na kuridhishwa na mambo yalivyo, Naendelea kutoa matakwa kwa binadamu. Napenda sifa za mwanadamu, lakini Nachukia wizi wake. Wanadamu wote wana mioyo iliyojaa ulafi; ni kama moyo wa binadamu unadhibitiwa na Shetani, na mwanadamu hawezi kuponyoka na kutoa moyo wake Kwangu. Ninapozungumza, mwanadamu husikiza sauti Yangu kwa makini; lakini Ninapokoma kuzungumza, anaaza tena “biashara” yake na kusitisha kabisa kuyajali maneno Yangu, ni kama maneno Yangu ni duni kwa biashara yake. Sijawahi kuwa mzembe kwa binadamu, na bado Nimekuwa pia mvumilivu na mkarimu kwa binadamu. Na hivyo, kwa sababu ya huruma Yangu, binadamu wote wamekuwa wenye kiburi, wasio na maarifa na tafakari ya binafsi, na wanatumia vibaya uvumilivu Wangu ili kunidanganya. Hakuna mmoja kati yao anayenijali kwa dhati, na hakuna mmoja kweli ananithamini kama kitu apendacho moyoni mwake; ni wakati tu walipo na wakati wa ziada ndipo wanaponitambua kwa kiwango duni. Juhudi ambazo Nimetumia kwa mwanadamu tayari ni zaidi ya kipimo. Ninamfanyia mwanadamu aina ya pekee ya kazi, na mbali na haya, Nimempaa mzigo wa ziada, ili, ndani ya kile Ninacho na kile Nilicho, mwanadamu anaweza kupata maarifa na kupitia mabadiliko. Simtaki mwanadamu awe mtumiaji tu, lakini Namtaka awe mzalishaji anayeweza kumshinda Shetani. Ingawa Sidai chochote kutoka kwa mwanadamu, hata hivyo Nina viwango vya matakwa Ninayoyatoa, kwani kuna madhumuni kwa yale Ninayoyafanya, na pia Ninatenda kulingana na kanuni: Sichezi kiholela, anavyodhani mwanadamu, wala Siundi mbingu na dunia na mambo mengi ya uumbaji kwa ghafla na bila mpango. Kwa kazi Zangu, mwanadamu anapaswa kuwa na uwezo wa kuona kitu, kupata kitu. Hapaswi kutumia vibaya uchangamfu wa ujana wake, ama kutunza maisha yake kama vazi ambalo linakusanya vumbi; badala yake, anapaswa kujilinda vikali, kuchukua kutoka kwa fadhila Yangu kwa ajili ya starehe yake mwenyewe, hadi, kwa sababu Yangu, hawezi kumrudia Shetani, na kwa sababu Yangu anamshambulia Shetani. Si Ninachomwulizia mwanadamu ni rahisi hivi?

Mwangaza hafifu unapoanza kuonekana Mashariki, watu wote ulimwenguni kwa sababu hii wanaupa kipaumbele mwangaza ulio Mashariki. Bila kujawa na usingizi, wanadamu huenda kuchunguza chanzo cha mwangaza wa mashariki, lakini kwa sababu ya vikwazo vya uwezo wa binadamu, hakuna anayeweza kuona mahali unapotokea mwangaza. Wakati yote yaliyo ulimwenguni yameangaziwa kabisa, mwanadamu atazinduka kutoka usingizi na ndoto, na hapo tu ndipo atakapotambua kwamba siku Yangu inawadia polepole duniani. Binadamu wote wanasherehekea kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu ya haya hawalali tena, na si wapumbavu tena. Chini ya mng’aro wa mwangaza Wangu, binadamu wote wanakuwa na uwazi wa akili na mtazamo, na ghafla wanakuwa na furaha ya maisha. Chini ya kifuniko cha ukungu, Nawalinda wanadamu. Wanyama wote wako katika mapumziko; kwa sababu ya ujio wa mwangaza hafifu, kila kitu katika uumbaji kinafahamu kwamba maisha mapya yanakaribia. Kwa sababu hii, wanyama pia wanatoka nje ya mapango yao, kutafuta chakula. Mimea, bila shaka, si tofauti, na kwa mng’aro wa mwangaza majani yao ya kijani yanang’aa, yakisubiri kutakasa sehemu yao binafsi Kwangu wakati Niko duniani. Wanadamu wote wanataka ujio wa mwangaza, lakini bado wanahofia ujio wake, na wasiwasi kwamba ubaya wao hutafichika tena, kwani mwanadamu yu uchi kabisa, na hajafunikwa. Watu wangapi wanahofia, kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu mwangaza umetokea, wako katika hali ya mshtuko? Watu wangapi, baada ya kuuona mwangaza, wamejawa majuto yasiyo na mipaka, wakichukia uchafu wao, lakini, bila uwezo wa kubadilisha ukweli uliotimia, wanaweza tu kunisubiri kutamka hukumu. Watu wangapi, wakisafishwa na mateso gizani, wanapoona mwangaza wanapigwa ghafla na umuhimu wake mkubwa, na hatimaye kukumbatia mwangaza karibu na vifua vyao, wakiogopa kuupoteza tena? Watu wangapi, badala ya kutupwa nje ya uzingo na kutoka kwa ghafla kwa mwanga, wanaendelea tu na kazi ya kila siku, kwa sababu wamekuwa vipofu kwa miaka mingi, na hivyo hawana habari kwamba mwangaza umekuja, wala hawaridhishwi nao. Katika mioyo ya wanadamu, Mimi siko juu, wala chini. Wanadamu hawajali iwapo Nipo au la, kama kwamba maisha ya mwanadamu hayawezi kuwa na upweke zaidi iwapo Sipo, na iwapo Nipo, hayatafaidika na furaha. Kwa sababu wanadamu hawanithamini, raha Ninayowapa ni chache. Lakini punde tu binadamu unaponiabudu kidogo, basi pia Nitafanya mabadiliko kwa mtazamo Wangu kwa binadamu. Kwa sababu hii, wakati tu binadamu unapofahamu sheria hii, ndipo tu wanadamu watakapokuwa na bahati ya kujitolea Kwangu na kudai vitu vilivyo mikononi Mwangu. Hakika pendo la mwanadamu Kwangu halifungwi tu na maslahi yake mwenyewe? Hakika imani yake Kwangu haifungwi tu kwa mambo Ninayompa? Inaweza kuwa kwamba, isipokuwa tu yeye kuona mwangaza Wangu, mwanadamu hawezi kunipenda kwa dhati kwa njia ya imani yake? Hakika nguvu za mwanadamu na afya hazizuiliwi na hali ya leo? Inaweza kuwa kwamba mwanadamu anahitaji ujasiri ili anipende?

Kutegemea kuwepo Kwangu, mambo mengi ya uumbaji yanakubali kwa utiifu mahali yanamoishi, na katu, bila ya nidhamu Yangu, hayajihusishi na uasherati bila kujali. Kwa hivyo, milima inakuwa mipaka kati ya mataifa ulimwenguni, maji yanakuwa vikwazo vya kuwatenga watu kati ya nchi, na hewa inapuliza kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi mwingine katika uwanda wa dunia. Binadamu tu huwezi kweli kutii matakwa ya mapenzi Yangu; hii ndiyo maana Nasema kwamba, kwa viumbe vyote, mwanadamu pekee ni ndiye wa kundi la wasiotii. Mwanadamu hajawahi kweli kunitii, na kwa sababu hii wakati wote Nimemweka chini ya nidhamu kali. Iwapo katikati ya binadamu, itakuja kuwa kwamba utukufu Wangu umetandaa ulimwengu nzima, basi hakika Nitachukua utukufu Wangu wote na kuufanya uwe wazi mbele ya mwanadamu. Kwa sababu katika uchafu wake mwanadamu hafai kutazama utukufu Wangu, kwa maelfu ya miaka Sijawahi kujitokeza hadharani, lakini Nimebakia mafichoni; kwa sababu hii utukufu Wangu hujawahi kuwa wazi mbele ya mwanadamu, na mwanadamu daima amezama kwa shimo la kina la dhambi. Nimeusamehe udhalimu wa binadamu, lakini wanadamu hawajui jinsi ya kujihifadhi, na badala yake daima wanajiweka wazi kwa dhambi, kuruhusu dhambi kuwajeruhi. Huu si ukosefu wa mwanadamu wa kujiheshimu na kujipenda? Katikati ya binadamu, kuna kweli yeyote anayeweza kupenda? Ibada ya mwanadamu inaweza kuwa na uzito wa wakia ngapi? Hakuna bidhaa safi zilizochanganywa na kinachoitwa uhalisi wake? Si ibada yake imeungana kabisa na mkanganyiko? Ninachohitaji ni upendo wa mwanadamu usiogawanyika. Mwanadamu hanijui, na ingawa anaweza kupata kunijua, hatanipa moyo wake wa ukweli na dhati. Kwa mwanadamu, Sidai kile asichotaka kupeana. Akinipa ibada yake, Nitaikubali bila pingamizi; lakini asiponiamini, na kukataa kujitoa hata kidogo Kwangu, badala ya kukasirika juu ya hayo, Nitamwondoa tu kwa njia ingine na kumtuma kwa nyumba inayomfaa. Radi, inayovingirika angani, inamwangusha chini mwanadamu, milima ya juu, inapoanguka, inamzika; wanyama pori kwa njaa yao wanamla kwa ulafi; na bahari, zinapobingirika, zinazingira kichwa chake. Binadamu wanapojishughulisha na migogoro ya mauaji ya jamii, wanadamu wote watatafuta maangamizo yao katika majanga yatokayo katikati ya binadamu.

Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu yu nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; binadamu utaguswa vipi? Mmeona na macho yenu hali ya mwanadamu; hakika bado hamna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii? Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawaadhimisha, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu.

Machi 19, 1992

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Kumi Na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa Waovu Lazima Waadhibiwe Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu Jinsi ya Kuujua Uhalisi Amri za Enzi Mpya Ufalme wa Milenia Umewasili Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe Kuijua Kazi ya Mungu Leo Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania? Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika" Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne Je, Umekuwa Hai Tena? Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili) Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili Je, Utatu Mtakatifu Upo? Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza) Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili) Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali? Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi? Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi Unajua Nini Kuhusu Imani? Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe” Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia Kazi katika Enzi ya Sheria Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza) Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili) Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu? Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza) Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili) Kiini cha Mwili Ulio na Mungu Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza) Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili) Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu? Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako Wewe U Mwaminifu kwa Nani? Maonyo Matatu Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu Kutanafusi kwa Mwenye Uweza Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji