Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa urejesho Wangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulikane waliko na gharika hili la urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya ya maji; na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao basi wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini yeye hajawahi kunitambua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utajiri uliofichika ndani Mwangu. Ingawa Mimi humruzuku mwanadamu na kumpa kila siku, hana uwezo wa kukubali kwa kweli, hana uwezo wa kupokea utajiri wote niliompa. Hakuna jambo lolote kuhusu upotovu wa mwanadamu ambalo huniepuka; Kwangu, ulimwengu wake wa ndani ni kama mwezi unaong’aa juu ya maji. Mimi Sifanyi mchezo na mwanadamu wala kufanya mambo kwake kwa namna isiyo ya dhati; ni kwamba tu mwanadamu hawezi kujiwajibikia, na hivyo wanadamu wote daima wamepotoka, na hata wa leo bado hawana uwezo wa kujitoa wenyewe kutoka upotovu huo. Ole wao, maskini wanadamu! Kwa nini mwanadamu ananipenda lakini hawezi kufuata nia za Roho Wangu? Je, Mimi Sijajifichua kwa wanadamu kwa kweli? Wanadamu kwa kweli hawajapata kuuona uso Wangu kamwe? Je, inawezekana kwamba Nimeonyesha huruma kiasi kidogo sana kwa wanadamu? Enyi waasi wa wanadamu wote! Lazima waharibiwe chini ya miguu Yangu, ni lazima watokomee kabisa katikati ya kuadibu Kwangu, na lazima, siku ambayo mpango Wangu mkubwa utakamilika, watatupiliwa mbali kutoka kati ya wanadamu, ili wanadamu wote wazijue nyuso zao mbaya. Sababu ya mwanadamu kuona uso Wangu na kusikia sauti Yangu mara chache ni kwamba dunia nzima imejawa na machafuko sana, na kelele zake ni kubwa mno, na hivyo mwanadamu ni mvivu mno kutafuta uso Wangu na kujaribu kuelewa Moyo Wangu. Je, hii si sababu ya kupotoshwa kwa mwanadamu? Je, hii si ndiyo sababu mwanadamu yuko na mahitaji? Wanadamu wote daima wamekuwa katikati ya utoaji Wangu; kama isingekuwa hivyo, Nisingekuwa mwenye huruma, nani angenusurika mpaka leo? Utajiri Nilio nao hauna wa kulingana nao, na bado maafa yote yamo mikononi Mwangu—na ni nani awezaye kuepuka maafa wakati wowote apendapo? Je, maombi ya mwanadamu yanaweza kumruhusu afanye hivyo? Au machozi yaliyo moyoni mwa mwanadamu? Mwanadamu hajawahi kuniomba Mimi kwa kweli, na hivyo miongoni mwa wanadamu wote hakuna mwanadamu aliyewahi kuishi maisha yake yote kwenye mwanga wa ukweli, na watu wanaishi katikati ya mwanga unaooneka kwa kipindi pekee. Hii ndiyo imesababisha mahitaji ya mwanadamu leo.

Kila mwanadamu ana hamu kubwa, tayari kufanya jambo lolote kwa sababu Yangu ili apate kitu kutoka Kwangu, na hivyo, nikizingatia saikolojia ya mwanadamu, Mimi humpa ahadi za kuhamasisha upendo wa kweli ndani yake. Je, ni upendo wa kweli wa mwanadamu unaompa nguvu? Je, ni uaminifu wa mwanadamu Kwangu ndio umegusa Roho Wangu mbinguni? Mbingu haijawahi kuathiriwa na matendo ya mwanadamu hata kidogo, na iwapo kumtendea Kwangu mwanadamu kungetegemea matendo yake yote, basi wanadamu wote wangeishi katikati ya kuadibu Kwangu. Nimewaona watu wengi wakitiririkwa na machozi, na Nimewaona watu wengi wakitoa nyoyo zao ili wapate utajiri Wangu. Licha ya “uchaji Mungu” kama huu, Sijawahi kujitoa kwa mwanadamu kikamilifu kwa sababu ya hisia zake za ghafla, kwa sababu mwanadamu hajawahi kuwa radhi kujitoa kwa furaha mbele Yangu. Nimeng’oa barakoa za watu wote na kutupa barakoa hizo katika ziwa la moto, na kama matokeo, unaodaiwa kuwa uaminifu wa mwanadamu na maombi yake hayajawahi kuwa imara mbele Zangu. Mwanadamu ni kama wingu angani: Wakati upepo unavuma, anahofia uwezo mkubwa wa nguvu yake na hivyo huelea kwa haraka kufuata upepo, akiwa na woga sana kuwa ataangamizwa kwa sababu ya uasi wake. Je, huu sio uso mbaya wa mwanadamu? Je, hili silo linalodaiwa kuwa utiifu wa mwanadamu? Je, hii siyo “hisia ya kweli” na nia njema bandia ya mwanadamu? Watu wengi hukataa kushawishiwa na maneno yote yatokayo kwenye kinywa Changu, na wengi hawakubali tathmini Yangu, na hivyo maneno na matendo yao hufichua nia zao za kuasi. Nisemacho ni kinyume cha asili ya zamani ya mwanadamu? Je, si Nimepeana ufafanuzi wa kufaa kwa binadamu kulingana na “sheria za asili”? Mwanadamu hanitii kwa kweli; angenitafuta kwa kweli, haingenibidi kusema mengi. Mwanadamu ni takataka isiyo na maana, na ni lazima Nitumie kuadibu Kwangu kumlazimisha kuendelea mbele; Nisingefanya hivyo,—ingawa ahadi Ninazompa ni za kutosha starehe yake—moyo wake ungeweza kushawishiwa vipi? Mwanadamu ameishi na mapambano machungu kwa miaka mingi; inaweza kusemekana, siku zote ameishi kwa kukata tamaa. Matokeo yake ni kuwa ameachwa kama amekufa moyo, na amechoka kimawazo na kimwili, na hivyo hapokei utajiri Ninaompa kwa furaha. Hata leo, hakuna mwanadamu aliye na uwezo wa kukubali utamu wote wa roho kutoka Kwangu. Watu wanaweza tu kubaki maskini, na kusubiri siku ya mwisho.

Watu wengi wangependa kunipenda kwa kweli, lakini kwa sababu mioyo yao si yao wenyewe, hawawezi kujidhibiti wenyewe; watu wengi hunipenda kwa kweli katika majaribio Ninayotoa, lakini hawana uwezo wa kuelewa kwamba Mimi kwa kweli Nipo, na wananipenda tu katikati ya utupu; na si kwa sababu ya kuwepo Kwangu halisi; watu wengi, baada ya kuweka nyoyo zao mbele Zangu, hawazijali, na hivyo nyoyo zao zinanyakuliwa na Shetani wakati wowote anapopata nafasi, na baada yake huniacha; watu wengi hunipenda kwa dhati Ninapotoa maneno Yangu, lakini hawathamini maneno Yangu katika roho zao, badala yake wakiyatumia kwa kawaida kama mali ya umma na kuyatupa yalipotoka wakati wowote wanapotaka. Mwanadamu hunitafuta akiwa na maumivu, na hunitazamia akiwa na majaribu. Wakati kuna amani yeye hunifurahia, wakati wa hatari yeye hunikana, wakati ana kazi nyingi yeye hunisahau, na asipokuwa na kitu cha kufanya yeye hufanya vitu kwa namna isiyo ya dhati—lakini kamwe hakuna yeyote ambaye amenipenda katika maisha yake yote. Ningependa mwanadamu awe mwenye bidii mbele Zangu: Mimi Simuombi chochote, ila tu watu wote wanichukulie kwa umakini, kwamba, badala ya kunihadaa, waniruhusu kurudisha uaminifu wa mwanadamu. Nuru Yangu, mwangaza na gharama ya juhudi Zangu huenea kwa watu wote, ilhali hivyo pia ukweli halisi wa kila tendo la mwanadamu huenea kwa watu wote, kama ufanyavyo wao kunidanganya. Ni kama kwamba viungo vya udanganyifu wa mwanadamu vimekuwa naye tangu tumboni mwa mamake, kama kwamba amekuwa na mbinu hizi maalum za kuhadaa tangu kuzaliwa kwake. Kuzidisha, hajawahi kufichua siri yake; hakuna mwanadamu aliyewahi kutambua chanzo cha ujuzi huu wa udanganyifu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu anaishi katika udanganyifu bila kujua, na ni kana kwamba yeye hujisamehe mwenyewe, kana kwamba ni mipango ya Mungu na sio yeye kunidanganya. Je, hiki sicho chanzo halisi cha mwanadamu kunidanganya? Je, huu sio mpango wake wa ujanja? Sijawahi kuchanganywa na ushawishi na hila za mwanadamu, kwa maana Mimi Nilishatambua kiini chake muda mrefu uliopita. Nani anayejua kiasi cha uchafu ulio katika damu yake, na kiasi gani cha sumu ya Shetani kimo ndani ya mafupa yake? Mwanadamu anapata uzoefu wa sumu hii kila uchao, hata anakosa busara ya kufahamu maafa ya Shetani na hivyo hana nia ya kutambua “sanaa ya uwepo wa afya.”

Wakati mwanadamu yuko mbali nami, na wakati ananijaribu, Mimi hujificha kutoka kwake kati ya mawingu. Na hivyo, hawezi kunipata hata kidogo, na huishi tu mikononi mwa waovu, akifanya yote watakayo. Mwanadamu anaponikaribia, Mimi hujitokeza kwake na sifichi uso Wangu kutoka kwake, na kwa wakati huu, mwanadamu huona hisia ya ukarimu usoni Mwangu. Yeye ghafla hupata fahamu na ingawa hatambui, ndani yake kunazaliwa upendo Kwangu. Katika moyo wake, yeye ghafla huhisi utamu usio na kifani, na hustaajabu jinsi gani hakuweza kutambua kuwepo Kwangu ulimwenguni. Hivyo basi mwanadamu ana hisia kubwa ya uzuri Wangu, na zaidi, ya thamani Yangu kubwa. Matokeo yake ni kuwa yeye hatamani kamwe kuniacha tena, Ananiona kama mwanga wa maisha yake, na akiwa na woga sana kuwa Naweza kumwacha, hunikumbatia kwa nguvu. Mimi siguswi na bidii ya mwanadamu, lakini ni mwenye rehema kwake kwa sababu ya upendo wake. Kwa wakati huu, mwanadamu mara moja huishi katikati ya majaribio Yangu. Uso Wangu hutoweka kutoka moyo wake, na yeye mara moja huona kuwa maisha yake ni matupu na anafikiria kukimbia. Wakati huu, moyo wa mwanadamu huwekwa wazi. Yeye hanikumbatii kwa sababu ya tabia Yangu, lakini ananiomba Nimlinde kwa sababu ya upendo Wangu. Hata hivyo, upendo Wangu unapomgeukia mwanadamu, yeye mara moja hubadili mawazo yake; yeye hukiuka agano lake nami na hujiweka mbali na hukumu Yangu, asiwe na nia ya kutazamia uso Wangu wa rehema tena, na hivyo hubadilisha mtazamo wake Kwangu na husema kuwa Sijawahi kumwokoa mwanadamu. Je, upendo wa kweli unahusisha huruma pekee? Je, mwanadamu ananipenda tu akiishi chini ya mwanga Wangu unaong’aa? Yeye anaangalia ya jana lakini anaishi katika wakati huu—si hizi ni hali za mwanadamu? Je, kesho mtakuwa jinsi mlivyo bado? Ninachotaka ni mwanadamu awe na moyo unaonitamani kwa kina na sio moyo unaoridhishwa na vitu vya juu juu.

Machi 21, 1992

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Kumi Na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa Waovu Lazima Waadhibiwe Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu Jinsi ya Kuujua Uhalisi Amri za Enzi Mpya Ufalme wa Milenia Umewasili Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe Kuijua Kazi ya Mungu Leo Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania? Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika" Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne Je, Umekuwa Hai Tena? Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili) Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili Je, Utatu Mtakatifu Upo? Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza) Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili) Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali? Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi? Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi Unajua Nini Kuhusu Imani? Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe” Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia Kazi katika Enzi ya Sheria Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza) Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili) Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu? Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza) Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili) Kiini cha Mwili Ulio na Mungu Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza) Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili) Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu? Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako Wewe U Mwaminifu kwa Nani? Maonyo Matatu Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu Kutanafusi kwa Mwenye Uweza Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji