Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

Kazi na neno la Mungu vinanuiwa kusababisha badiliko katika tabia yenu; lengo Lake si tu kuwafanya muelewe ama mjue kazi na neno Lake. Hilo halitoshi. Wewe ni mtu aliye na uwezo wa kufahamu, kwa hivyo hupaswi kuona ugumu kuelewa neno la Mungu, kwa sababu maneno mengi ya Mungu yameandikwa katika lugha ya mwanadamu, na Anazungumza kwa uwazi sana. Kwa mfano, unaweza kabisa kujifunza ni nini ambacho Mungu angetaka uelewe na utende; hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida aliye na uwezo wa kufahamu anapaswa kuweza kufanya. Hasa, maneno ambayo Mungu anasema katika hatua ya sasa ni ya wazi na dhahiri zaidi, na Mungu anaonyesha mambo mengi ambayo watu hawajayazingatia, na vilvile kila aina ya hali za binadamu. Maneno Yake yanajumuisha yote na ni dhahiri kama mwanga wa mwezi kamili. Kwa hivyo sasa, watu wanaelewa masuala mengi, lakini bado kuna kitu kinachokosa—watu kuweka neno Lake katika vitendo. Ni lazima watu wapitie vipengele vyote vya ukweli kwa utondoti, na wauchunguze na kuutafuta kwa kina zaidi, badala ya kusubiri tu kufyonza chochote wanachopewa; vinginevyo wanakuwa kupe tu. Wanajua neno la Mungu, lakini hawaliweki katika vitendo. Mtu wa aina hii hapendi ukweli na mwishowe ataondolewa. Ili kuwa kama Petro wa miaka ya tisini, hili linamaanisha kwamba nyote mnapaswa kutenda neno la Mungu, muingie kwa kweli katika yale mnayoyapitia na mpate nuru hata zaidi na kubwa zaidi katika ushirikiano wenu na Mungu, ambao utakuwa wa msaada unaozidi daima kwa maisha yenu wenyewe. Ikiwa mmesoma maneno mengi ya Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandiko na hamna maarifa ya moja kwa moja ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu halisi, basi hutajua neno la Mungu. Kwa kadiri inavyokuhusu, neno la Mungu si uzima, bali tu nyaraka zisizovutia. Na ikiwa unaishi tu kwa kufuata nyaraka zisizovutia, basi huwezi kuelewa asili ya neno la Mungu wala hutaelewa mapenzi Yake. Ni wakati tu ambapo unapitia neno Lake katika matukio yako halisi ndipo maana ya kiroho ya neno la Mungu itafichuka kwako, na ni kupitia uzoefu tu ndiyo unaweza kuelewa maana ya kiroho ya ukweli mwingi na ufungue siri za neno la Mungu. Usipouweka katika vitendo, basi bila kujali jinsi neno Lake lilivyo dhahiri, yote uliyoelewa ni nyaraka na mafundisho matupu tu, ambayo yamekuwa kanuni za kidini kwako. Je, Mafarisayo hawakufanya hivi? Mkitenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa la utendaji kwenu; usipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwako ni hekaya ya mbinguni ya tatu tu. Kwa kweli, mchakato wa kumwamini Mungu ni mchakato wa ninyi kupitia neno Lake na vilevile kupatwa na Yeye, ama kuzungumza dhahiri zaidi, kumwamini Mungu ni kuwa na maarifa na ufahamu wa neno Lake na kupitia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake; huu ndio uhalisi wa ninyi kumwamini Mungu. Ikiwa mnamwamini Mungu na mnatumai kupata uzima wa milele bila kutafuta kutenda neno la Mungu kama kitu kilicho ndani yenu, basi ninyi ni wapumbavu. Hii itakuwa sawa na kwenda katika karamu na kuangalia tu chakula na kujua na kuweza kuvikariri vitu vitamu bila kuvionja kwa kweli. Je, mtu kama huyu si mpumbavu?

Ukweli ambao mwanadamu anahitaji kuwa nao unapatikana katika neno la Mungu, na ni ukweli wenye manufaa na usaidizi zaidi kwa wanadamu. Ni dawa na ruzuku ambayo miili yenu inahitaji, kitu kinachomsaidia mwanadamu kurejesha tena ubinadamu wake wa kawaida. Ni ukweli ambao mwanadamu anapaswa kujitayarisha nao. Kadiri mnavyotenda neno la Mungu, ndivyo maisha yenu yatakavyositawi haraka zaidi, na ndivyo ukweli utakavyokuwa dhahiri zaidi. Mnapozidi kukua katika kimo, mtaona vitu vya dunia ya kiroho kwa dhahiri zaidi, na ndivyo mtakavyokuwa na nguvu zaidi kumshinda Shetani. Ukweli mwingi ambao hamwelewi utafanywa kuwa dhahiri mtakapotenda neno la Mungu. Watu wengi wanaridhishwa kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na hawalengi kujitayarisha kwa mafundisho badala ya kuzidisha uzoefu wao kwa vitendo, lakini, je, hiyo si njia ya Mafarisayo? Kwa hivyo msemo “Neno la Mungu ni uzima” unawezaje kuwa wa kweli kwao? Maisha ya mtu hayawezi kukua kwa kusoma neno la Mungu tu, bali ni wakati tu neno la Mungu linawekwa katika vitendo. Ikiwa unaamini kwamba kuelewa neno la Mungu ndicho kitu pekee kinachohitajika kuwa na uzima na kimo, basi ufahamu wako umepotoka. Kuelewa neno la Mungu kwa kweli hutokea unapoweka ukweli katika vitendo, na ni lazima uelewe kwamba “ni kwa kutenda ukweli tu ndipo unaweza kueleweka.” Leo, baada ya kusoma neno la Mungu, unaweza tu kusema kwamba unajua neno la Mungu, lakini huwezi kusema kwamba unalielewa. Wengine husema kwamba njia ya pekee ya kutenda ukweli ni kuuelewa kwanza, lakini hii ni sahihi kwa kiwango fulani tu, na hakika si sahihi kikamilifu. Kabla uwe na maarifa ya ukweli fulani, hujapitia ukweli huo. Kuhisi kwamba unaelewa kitu unachosikia katika mahubiri si kuelewa kwa kweli—huku ni kuwa na maneno halisi ya ukweli tu, na si sawa na kuelewa maana ya kweli ndani yake. Kuwa tu na maarifa ya juujuu ya ukweli hakumaanishi kwamba kweli unauelewa ama una maarifa yoyote kuuhusu; maana ya kweli ya ukweli hutokana na kuupitia. Kwa hiyo, ni wakati tu unapopitia ukweli ndiyo unaweza kuuelewa, na ni hapo tu ndiyo unaweza kufahamu sehemu zake zilizofichika. Kukuza uzoefu wako ndiyo njia ya pekee ya kuelewa vidokezo, na kuelewa asili ya ukweli. Kwa hiyo, unaweza kuenda popote ukiwa na ukweli, lakini iwapo hakuna ukweli ndani yako, basi usifikirie kujaribu kuwashawishi hata wanafamilia wako sembuse watu wa kidini. Bila ukweli wewe ni kama vipande vidogo sana vya theluji vinavyopepea, lakini ukiwa na ukweli unaweza kuwa na furaha na uhuru, na hakuna anayeweza kukushambulia. Bila kujali jinsi nadharia fulani ilivyo thabiti, haiwezi kuushinda ukweli. Kukiwa na ukweli, dunia yenyewe haiwezi kuyumba na milima na bahari kusogezwa, wakati ukosefu wa ukweli unaweza kusababisha nyuta zenye nguvu za mji kuangushwa na mabuu. Huu ni ukweli dhahiri.

Katika hatua ya sasa, ni muhimu sana kujua ukweli kwanza, na kisha kuuweka katika vitendo na kujitayarisha zaidi na maana ya kweli ya ukweli. Mnapaswa kutafuta kupata hili. Badala ya kutafuta tu kuwafanya wengine wafuate maneno yako, unapaswa kuwasababisha wafuate vitendo vyako. Ni kwa njia hii pekee ndiyo unaweza kupata kitu cha maana. Bila kujali kitakachokukumba, bila kujali utakutana na nani, alimradi una ukweli, utaweza kusimama imara. Neno la Mungu ndicho kitu kimleteacho mwanadamu uzima, si kifo. Ikiwa baada ya kusoma neno la Mungu huchangamki, bali bado wewe ni mfu, basi una kasoro. Ikiwa baada ya muda fulani umesoma maneno mengi ya Mungu, na umesikiza mahubiri mengi ya vitendo, lakini bado uko katika hali ya kifo, basi hili ni thibitisho kwamba wewe si mtu anayethamini ukweli, wala wewe si mtu anayefuatilia ukweli. Ikiwa kweli mngetafuta kumpata Mungu, hamngelenga kujitayarisha na mafundisho na kutumia mafundisho ya juu sana kuwafunza wengine, lakini badala yake mngelenga kupitia neno la Mungu na kuweka ukweli katika vitendo. Je, hampaswi kutafuta kuingia katika hili sasa?

Mungu ana muda mdogo wa kufanya kazi Yake ndani ya mwanadamu, kwa hivyo kunaweza kuwa na matokeo yapi ikiwa hushirikiani na Yeye? Mbona Mungu daima anawataka mtende neno Lake punde mnapolielewa? Ni kwa sababu Mungu amewafichulia maneno Yake, na hatua yenu ifuatayo ni kuyatenda kwa kweli. Mnapotenda maneno haya, Mungu atatekeleza kazi ya nuru na mwongozo. Hivi ndivyo inavyopaswa kufanywa. Neno la Mungu linamwezesha mwanadamu asitawi maishani na asiwe na dalili zozote zinazoweza kumsababisha mwanadamu apotoke ama asionyeshe hisia. Unasema umesoma neno la Mungu na umelitenda, lakini bado hujapokea kazi yoyote kutoka kwa Roho Mtakatifu. Maneno yako yanaweza tu kumpumbaza mtoto. Huenda watu wengine wasijue ikiwa dhamira zako ni njema, lakini, je, unafikiri kwamba inawezekana Mungu asijue? Ni kwa nini wengine wanatenda neno la Mungu na kupokea nuru ya Roho Mtakatifu, lakini unatenda neno Lake na hupokei nuru ya Roho Mtakatifu? Je, Mungu ana mhemuko? Ikiwa dhamira zako kweli ni njema na wewe ni wa kushirikiana, basi Roho wa Mungu atakuwa nawe. Watu wengine daima hutaka kuonyesha utawala wao wenyewe, lakini kwa nini Mungu hawaruhusu wainuke na kuliongoza kanisa? Watu wengine wanatimiza kazi zao na kutenda wajibu wao tu, lakini kufumba na kufumbua, wamepata idhini ya Mungu. Hilo linawezekanaje? Mungu huchunguza moyo wa ndani sana wa mwanadamu, na watu wanaofuatilia ukweli lazima wafanye hivyo kwa dhamira njema. Watu wasio na dhamira njema hawawezi kusimama imara. Kimsingi kabisa, lengo lenu ni kuacha neno la Mungu lifanye kazi ndani yenu. Yaani, ni kuwa na ufahamu wa kweli wa neno la Mungu mnapolitenda. Pengine uwezo wenu wa kufahamu neno la Mungu ni duni, lakini unapotenda neno la Mungu, Anaweza kurekebisha dosari hii, kwa hivyo hampaswi tu kujua ukweli mwingi, lakini pia lazima muutende. Hili ni lengo kubwa zaidi ambalo haliwezi kupuuzwa. Yesu alivumilia fedheha nyingi na mateso mengi katika maisha Yake ya miaka thelathini na tatu na nusu. Aliteseka sana kwa sababu tu Alitenda ukweli, alifanya mapenzi ya Mungu katika vitu vyote, na alijali tu mapenzi ya Mungu. Haya yalikuwa mateso ambayo Hangepitia iwapo Angejua ukweli bila kuutenda. Ikiwa Yesu angefuata mafundisho ya Wayahudi na awafuate Mafarisayo, basi Hangeteseka. Unaweza kujifunza kutoka kwa matendo ya Yesu kwamba ufanisi wa kazi ya Mungu kwa mwanadamu hutokana na ushirikiano wa mwanadamu, na hili ni jambo ambalo lazima mtambue. Je, Yesu angeteseka jinsi Alivyoteseka msalabani ikiwa Hangetenda ukweli? Je, Angesali sala ya huzuni sana kama Hangetenda kulingana na mapenzi ya Mungu? Kwa hiyo, mnapaswa kuteseka kwa ajili ya kutenda ukweli; mtu anapaswa kupitia mateso ya aina hii.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp