Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu (Sehemu ya Tatu)

Binadamu Hupata Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya Dhati

Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya “Wokovu wa Mungu kwa Ninawi.”

Yona 1:1-2 Sasa neno la Yehova likaja kwa Yona mwana wa Amitai, likisema, Amka, nenda Ninawi, mji mkuu, na uipigie kelele, kwani uovu wao umeenda juu mbele yangu.

Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa. Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. Nani anayejua iwapo Mungu atabadili na kughairi, na kuiacha ghadhabu yake iliyo kali, ili tusiangamie? Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo alikuwa amesema angeliwafanyia; na hakulifanya.

Yona 4 Lakini lilimwudhi Yona mno, naye alikuwa na hasira sana. Na akaomba kwa Yehova, na kusema, Nakuomba, Ee Yehova, hivi sivyo nilivyonena, nilipokuwa bado katika nchi yangu? Kwa hivyo nilitorokea Tarshishi kabla: kwa sababu nilijua kwamba wewe ni Mungu wa neema, na mwenye huruma, asiyekasirika haraka, na wa rehema kubwa, na wewe unaghairi maovu. Kwa hivyo sasa, Ee Yehova, chukua, nakusihi, uhai wangu kutoka kwangu; kwa sababu ni heri nikufe kuliko kuishi. Kisha Yehova akasema, Je, unafanya vizuri kukasirika? Hivyo Yona akatoka nje ya mji, na kuketi katika upande wa mashariki wa mji, na huko akajitengenezea kibanda, na akaketi chini yake katika kivuli, mpaka aweze kuona kile kingefanyikia mji huo. Naye Yehova Mungu akatayarisha mtango, na akaufanya ukuje juu yake Yona, ili uweze kuwa kivuli juu ya kichwa chake, na kumwokoa kutoka katika huzuni yake. Kwa hivyo Yona akawa na furaha sana juu ya ule mtango. Lakini Mungu akatayarisha buu siku iliyofuata wakati kulipopambazuka, nalo likaula ule mtango hadi ukanyauka. Na hivyo ikatimia, wakati jua lilipopanda, kwamba Mungu akautayarisha upepo mkali wa mashariki; na jua likapiga kichwa chake Yona, kiasi kwamba alizimia, naye akatamani afe, na akasema, Ni heri mimi nife kuliko niishi. Mungu akasema kwa Yona, Je, unafanya vizuri kukasirika kwa sababu ya mtango? Na yeye akasema, naam, nafanya vizuri kukasirika, hata mpaka kufa. Kisha Yehova akasema, Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?

Muhtasari wa Hadithi ya Ninawi

Ingawaje hadithi ya “wokovu wa Mungu wa Ninawi” ni fupi kwa urefu, inaruhusu mtu kuweza kuona kidogo tu ule upande mwingine wa tabia ya haki ya Mungu. Ili kuweza kuelewa haswa upande huo unajumuisha nini, lazima turudi kwenye Maandiko na kuangalia nyuma katika mojawapo ya matendo ya Mungu.

Hebu kwanza tuangalie mwanzo wa hadithi hii: “Sasa neno la Yehova likaja kwa Yona mwana wa Amitai, likisema, Amka, nenda Ninawi, mji mkuu, na uipigie kelele, kwani uovu wao umeenda juu mbele yangu” (Yona 1:1-2). Katika fungu hili kutoka kwenye Maandiko, tunajua kwamba Yehova Mungu alimwamuru Yona kwenda katika mji wa Ninawi. Kwa nini alimwamuru Yona kwenda katika mji huo? Biblia iko wazi kabisa kuhusu suala hili: Maovu ya watu walio ndani ya mji huo yalikuwa yamefikia macho ya Yehova Mungu, na hivyo basi Alimtuma Yona ili kuwatangazia kile Alichonuia kufanya. Ingawa hakuna kitu kilichorekodiwa kinachotwambia Yona alikuwa nani, jambo hili, bila shaka, halina uhusiano wowote na kumjua Mungu. Hivyo basi, huhitaji kumwelewa mwanamume huyu. Unahitaji kujua tu kile ambacho Mungu alimwamuru Yona kufanya na kwa nini Alifanya kitu hicho.

Onyo la Yehova Mungu Lawafikia Waninawi

Hebu tuendelee hadi kwenye fungu la pili, sura ya tatu ya kitabu cha Yona: “Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa.” Haya ndiyo maneno ambayo Mungu alipitisha moja kwa moja kwake Yona ili aweze kuwaambia Waninawi. Ndiyo pia, kwa kawaida, maneno ambayo Yehova Mungu alipenda kusema kwa Waninawi. Maneno haya yanatwambia kwamba Mungu alianza kukerwa na kuchukia watu wa mji huu kwa sababu ya maovu yao yaliyokuwa yamefika machoni pa Mungu, na hivyo basi, Alipenda kuuangamiza mji huo. Hata hivyo, kabla ya Mungu kuangamiza mji, Aliwatangazia Waninawi, na hapo kwa hapo Akawapa fursa ya kutubu maovu yao na kuanza upya. Fursa hii ingedumu kwa siku arubaini. Kwa maneno mengine, kama watu waliokuwa ndani ya mji huu wasingetubu, na kukubali dhambi au maovu yao wenyewe mbele ya Yehova Mungu ndani ya siku arubaini, Mungu angeangamiza mji huu kama Alivyoangamiza Sodoma. Hivi ndivyo ambavyo Yehova Mungu alipenda kuwaambia watu wa Ninawi. Ni wazi kwamba, hili halikuwa tangazo rahisi. Halikuweza tu kuonyesha hasira ya Yehova Mungu, lakini pia lilionyesha mtazamo Wake kwa wale Waninawi; wakati uo huo tangazo hili rahisi lilitumika kama onyo kali kwa watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huo. Onyo hili liliwaambia kwamba matendo yao maovu yalikuwa yamewafanya kuchukiwa na Yehova Mungu na liliwaambia kwamba matendo yao maovu yangewaletea hivi karibuni fedheha kutokana na maangamizo yao wenyewe; kwa hivyo, maisha ya kila mmoja kule Ninawi yalikuwa karibu kuangamia.

Utofautishaji Mkavu Katika Mwitikio wa Ninawi na Sodoma kwa Onyo la Yehova Mungu

Kupinduliwa kunamaanisha nini? Kwa muktadha wa mazungumzo, kunamaanisha kutoweka. Lakini kwa njia gani? Ni nani angefanya mji mzima kupinduliwa? Haiwezekani kwa binadamu kufanya kitendo kama hicho, bila shaka. Watu hawa hawakuwa wajinga; mara tu waliposikia matangazo haya, walipata wazo hilo. Walijua kwamba yalikuwa yametoka kwa Mungu; walijua kwamba Mungu angetekeleza kazi Yake; walijua kwamba maovu yao yalikuwa yamemkasirisha Yehova Mungu na kumfanya kuwa na hasira kali kwao, ili waweze kuangamizwa pamoja na mji wao. Je, watu wa mji huo walichukulia vipi suala hilo baada ya kusikiliza onyo la Yehova Mungu? Biblia inafafanua kwa maelezo fafanuzi namna ambavyo watu hawa walivyoitikia, kuanzia kwa mfalme wao hadi kwa binadamu wa kawaida. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. …”

Baada ya kusikia tangazo la Yehova Mungu, watu wa Ninawi walionyesha mtazamo uliokuwa kinyume kabisa na ule wa watu wa Sodoma—watu wa Sodoma walimpinga Mungu waziwazi, huku wakiendelea kutoka kwa maovu hadi maovu, lakini baada ya kusikia maneno haya, Waninawi hawakupuuza suala hilo, wala hawakuweza kulipinga; badala yake walimsadiki Mungu na kutangaza kufunga. “Walisadiki” inarejelea nini hapa? Neno lenyewe linapendekeza imani na unyenyekevu. Kama tutatumia tabia halisi ya Waninawi kuelezea neno hili, inamaanisha kwamba walisadiki Mungu anaweza na angeweza kufanya vile Alivyosema, na kwamba walikuwa radhi kutubu. Je, watu wa Ninawi walihisi woga mbele ya janga lililokuwa karibu kutokea? Imani yao ndiyo iliyotia woga katika mioyo yao. Kwa kweli, ni nini tunachoweza kutumia kuthibitisha Imani na woga wa Waninawi? Ni sawa na vile Biblia inavyosema: “na wao wakatangaza kufunga, na wakavalia nguo ya gunia, kuanzia wale walio wakubwa zaidi na hata kwa wale walio wadogo zaidi.” Hivi ni kusema kwamba Waninawi walisadiki kweli, na kwamba kutoka kwenye imani hii woga uliibuka, ambao sasa ulisababisha kufunga na kuvaliwa kwa nguo ya gunia. Hivi ndivyo walivyoonyesha mwanzo wa toba yao. Tofauti kabisa na watu wa Sodoma, Waninawi hawakumpinga Mungu tu, bali walionyesha pia waziwazi toba yao kupitia kwa tabia na matendo yao. Bila shaka, hii haikutumika tu kwa watu wa kawaida wa Ninawi; hata mfalme wao hakubakizwa.

Toba ya Mfalme wa Ninawi Inapata Sifa ya Yehova Mungu

Wakati mfalme wa Ninawi alipozisikia habari hizi, aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua nguo zake, akavalia nguo ya gunia na kukalia jivu. Kisha akatangaza kwamba hakuna mtu kwenye mji huo ambaye angeruhusiwa kuonja chochote, na kuwa hakuna mifugo, wanakondoo na ng’ombe ambao wangekunywa maji na kula nyasi. Binadamu na mifugo kwa pamoja walitakikana kujifunika nguo ya gunia; nao watu wangemsihi Mungu kwa uaminifu. Mfalme pia alitangaza kwamba watu wote wangetupilia mbali njia zao za maovu na kukataa udhalimu ulioko mikononi mwao. Tukifanya uamuzi kutoka kwenye misururu ya vitendo hivi, mfalme wa Ninawi alionyesha toba yake ya dhati. Misururu ya vitendo alivyofanya—kutoka kwenye kiti chake cha ufalme, kulitupa joho lake la kifalme, kuvalia nguo ya gunia na kukalia majivu—kulionyesha watu kwamba mfalme wa Ninawi aliweka kando hadhi yake ya kifalme na kuvalia nguo ya gunia pamoja na watu wa kawaida wa nchi. Hii ni kusema kwamba mfalme wa Ninawi hakuweza kushikilia wadhifa wake wa kifalme ili aendelee na njia zake za maovu au udhalimu katika mikono yake baada ya kikao cha tangazo kutoka kwa Yehova Mungu; badala yake, aliweka pembeni mamlaka aliyoyashikilia na kutubu mbele ya Yehova Mungu. Kwenye kipindi hiki cha muda, mfalme wa Ninawi hakuwa akitubu akiwa mfalme; alikuwa amekuja mbele ya Mungu kuungama na kutubu dhambi zake akiwa binadamu wa kawaida wa Mungu. Aidha, aliuambia mji mzima kuungama na kutubu dhambi zao mbele ya Yehova Mungu kwa njia sawa na yeye; vilevile, alikuwa na mpango mahususi wa namna ya kufanya hivyo kama inavyoonekana kwenye Maandiko: “Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: … na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao.” Kama kiongozi wa mji, mfalme wa Ninawi alimiliki hadhi na nguvu za kimamlaka na angefanya chochote alichopenda. Alipokabiliwa na tangazo la Yehova Mungu, angeweza kupuuza suala hilo au kutubu na kuungama tu dhambi zake pekee; kuhusiana na kama watu wa mji wangechagua kutubu au la, angepuuza suala hili kabisa. Hata hivyo, mfalme wa Ninawi hakufanya hivyo kamwe. Mbali na kuinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, kuvalia nguo ya gunia na kujipaka jivu na kuungama na kutubu dhambi zake mbele ya Yehova Mungu, aliweza pia kuwaamuru watu na mifugo ndani ya mji huo kufanya hivyo. Aliweza hata kuamuru watu “kumlilia Mungu kwa nguvu.” Kupitia misururu hii ya vitendo, mfalme wa Ninawi aliweza kukamilisha kwa kweli kile ambacho kiongozi anafaa kufanya; misururu ya vitendo vyake ndiyo iliyokuwa migumu kwa mfalme yeyote katika historia ya binadamu kutimiza, hatua na pia hatua ambayo hakuna aliyewahi kutimiza. Matendo haya yanaweza kuitwa shughuli isiyo na kifani katika historia ya binadamu; yanastahili kukumbukwa na kuigwa na binadamu. Tangu enzi ya mwanadamu, kila mfalme alikuwa amewaongoza wafuasi wake kukinzana na kumpinga Mungu. Hakuna yule aliyewahi kuwaongoza wafuasi wake kusihi Mungu kutafuta ukombozi kwa ajili ya maovu yao, kupokea msamaha wa Yehova Mungu na kuepuka adhabu kali. Mfalme wa Ninawi, hata hivyo, aliweza kuwaongoza raia wake kumlilia Mungu, kuacha njia zao mbalimbali za maovu na kutupilia mbali udhalimu ulio mikononi mwao. Aidha, aliweza pia kuweka kando kiti chake cha enzi, na badala yake, Yehova Mungu alibadilisha na kughairi na kugeuza hasira Yake, na kuruhusu watu wa mji huu kuishi na kuwalinda dhidi ya kuangamia. Matendo ya mfalme yanaweza kuitwa tu muujiza wa nadra katika historia ya binadamu; yanaweza hata kuitwa kielelezo cha binadamu waliopotoka wanaoungama na kutubu dhambi zake mbele ya Mungu.

Mungu Aona Kutubu kwa Dhati katika Vina vya Mioyo ya Waninawi

Baada ya kusikiliza tangazo la Mungu, mfalme wa Ninawi na raia Wake walitekeleza misururu ya vitendo. Je, ni nini asili ya tabia na matendo yao? Kwa maneno mengine, ni nini kiini cha uzima wa mwenendo wao? Kwa nini walifanya kile walichofanya? Katika macho ya Mungu walikuwa wametubu kwa dhati, si tu kwa sababu walikuwa wamemsihi Mungu kwa dhati na kuungama dhambi zao mbele Yake, lakini pia kwa sababu walikuwa wameacha mwenendo wao wenye maovu. Walichukua hatua namna hii kwa sababu baada ya kusikia matamshi ya Mungu, walitishika pakubwa na kusadiki kwamba angefanya vile ambavyo alikuwa amesema. Kwa kufunga, kuvalia nguo ya gunia na kukalia jivu, walipenda kuonyesha namna walivyokuwa radhi kubadilisha njia zao na kujizuia na maovu, kumwomba Yehova Mungu kuzuia hasira Yake, kusihi Yehova Mungu kutupilia mbali uamuzi Wake, pamoja na msiba mkuu ambao ulikuwa karibu kuwasibu. Kupitia uchunguzi wa tabia yao yote, tunaona ya kwamba tayari walielewa kwamba vitendo vyao vya awali vilimchukiza Yehova Mungu na kwamba walielewa sababu iliyomfanya kutaka kuwaangamiza hivi karibuni. Kwa sababu hizi, wote walipenda kutubu kabisa, kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, pindi tu walipotambua tangazo la Yehova Mungu, kila mmoja wao alihisi woga katika mioyo yao; hawakuendelea tena na mwenendo wao wa maovu wala kuendelea kutenda vitendo ambavyo Yehova Mungu alichukia. Vilevile, walimsihi Yehova Mungu kusamehe dhambi zao za kale na kutowatendea kulingana na vitendo vyao vya kale. Walikuwa radhi kutowahi kujihusisha tena katika maovu na kutenda kulingana na maagizo ya Yehova Mungu, kama tu wasingewahi kumkasirisha Yehova Mungu. Toba yao ilikuwa ya dhati na ya kweli. Ilitoka kwenye kina cha mioyo yao na haikuwa ya kujidanganya, wala haikuwa ya muda.

Baada ya watu wa Ninawi, kutoka kwa mfalme mwenye mamlaka hadi kwa raia wake, kujua kwamba Yehova Mungu alikuwa amewakasirikia, kila mojawapo ya vitendo vyao, tabia yao nzima, pamoja na kila mojawapo ya uamuzi na machaguo yao vilikuwa wazi na dhahiri mbele ya Mungu. Moyo wa Mungu ulibadilika kulingana na tabia yao. Akili Zake Mungu zilikuwa zinafikiria nini wakati huo? Biblia inaweza kukujibia swali hili. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo alikuwa amesema angeliwafanyia; na hakulifanya.” Ingawaje Mungu alibadilisha fikira Yake, hakukuwa na chochote kigumu kuhusu mtazamo wa fikira Yake. Aliweza kubadilika kutoka katika kuonyesha hasira Yake hadi kutuliza hasira Yake, na kisha kuamua kutouleta msiba mkuu katika mji wa Ninawi. Sababu ya uamuzi wa Mungu wa—kuwaokoa Waninawi dhidi ya msiba wao mkuu—ilikuwa ya haraka mno, ni kwa sababu Mungu aliangalia moyo wa kila mmoja wa wale Waninawi. Aliona kwamba katika kina cha mioyo yao waliweza: kuungama na kutubu kwa dhati dhambi zao, imani yao ya dhati kwake Yeye, mtazamo wao wa kina kuhusu vile vitendo vyao vya maovu vilikuwa vimeipa tabia Yake hasira kali, na woga uliotokana na adhabu ya Yehova Mungu iliyokuwa inakaribia. Wakati uo huo, Yehova Mungu aliweza kusikia maombi kutoka kwenye kina cha mioyo yao wakimsihi kusitisha hasira Yake dhidi yao ili waweze kuepuka msiba huu mkuu. Wakati Mungu alipoangalia hoja hizi zote, kwa utaratibu hasira yake ilitoweka. Licha ya vile hasira yake ilivyokuwa kuu hapo awali, alipoona kutubu kwao kwa dhati ndani ya kina cha mioyo ya watu hawa, moyo Wake uliguswa na hili, na kwa hivyo Hakuweza kuvumilia kuwaletea msiba mkuu, na Alisitisha hasira yake kwao. Badala yake Aliendelea kuwaonyesha huruma Yake na uvumilivu kwao na akaendelea kuwaongoza na kuwakimu.

Kama Imani Yako kwa Mungu ni ya Kweli, Utapokea Utunzaji Wake Mara Nyingi

Kubadilisha kwa nia zake Mungu kwa watu wa Ninawi hakukuhusisha kusitasita au kutoeleweka kokote. Badala yake kulikuwa ni mabadiliko kutoka kwa hasira tupu hadi uvumilivu mtupu. Huu ni ufunuo wa kweli kuhusu hali halisi ya Mungu. Mungu hajawahi kusitasita au kufikiria mara mbili kuhusu hatua Zake; kanuni na makusudio yaliyo katika matendo Yake ni wazi na dhahiri yasiyo na kasoro wala hatia, yasiyo na njama yoyote kamwe ama mifumo iliyoingiliana. Kwa maneno mengine, hali halisi ya Mungu haina giza wala maovu mengine. Mungu alikasirikia Waninawi kwa sababu ya vitendo vya maovu ambavyo vilikuwa vimefikia macho Yake; wakati ule hasira Yake ilitokana na hali Yake halisi. Hata hivyo, wakati hasira ya Mungu ilipotoweka na akatoa uvumilivu Wake kwa watu wa Ninawi kwa mara nyingine tena, kila kitu Alichofichua kilikuwa bado ni hali Yake halisi. Uzima wa badiliko hili ulitokana na badiliko katika mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu. Kwenye kipindi hiki chote cha muda, tabia ya Mungu isiyoweza kukosewa haikubadilika; hali halisi ya uvumilivu wa Mungu haikubadilika; hali halisi ya upendo na huruma ya Mungu haikubadilika. Wakati watu wanapotekeleza vitendo vya maovu na kumkosea Mungu atawashushia ghadhabu Yake. Wakati watu wanatubu kwa kweli, moyo wa Mungu utabadilika, na hasira Yake itasita. Wakati watu wanapoendelea kumpinga Mungu kwa usumbufu, hasira Yake kali haitasita; hasira Yake itaendelea kuwa kwao hatua kwa hatua mpaka watakapoangamizwa. Hii ndiyo hali halisi ya tabia ya Mungu. Haijalishi kama Mungu anaonyesha hasira au huruma na upole, mwenendo wa binadamu, tabia na mtazamo wake kwa Mungu ndani ya kina cha moyo wake vinatoa masharti ya kile ambacho kinaonyeshwa kupitia kwa ufunuo wa tabia ya Mungu. Kama Mungu anaendelea kuonyesha mtu hasira Yake, moyo wa mtu huyu bila shaka humpinga Mungu. Kwa sababu hajawahi kutubu kwa kweli, kuinamisha kichwa chake mbele ya Mungu au kumiliki imani ya kweli kwa Mungu, hajawahi kupata huruma na uvumilivu wa Mungu. Kama mtu anapokea utunzaji wa Mungu na mara nyingi hupokea huruma na uvumilivu wake, basi mtu huyo bila shaka anaamini Mungu kwa kweli ndani ya moyo wake, na moyo wake haumpingi Mungu. Yeye kwa mara nyingi anatubu kwa kweli mbele ya Mungu; kwa hivyo, hata kama nidhamu ya Mungu mara nyingi humshukia mtu huyu, hasira Yake haitamshukia.

Ufafanuzi huu mfupi unaruhusu watu kuuona moyo wa Mungu, kuona uhalisia wa hali Yake halisi ili kuona kwamba ghadhabu ya Mungu na mabadiliko katika moyo Wake yana sababu. Licha ya Utofautishaji mkavu ambao Mungu alionyesha Alipoghadhabishwa na pale Alipobadilisha moyo Wake, jambo ambalo linafanya watu kusadiki kwamba utofautishaji mkavu au nafasi kubwa yaonekana kuwepo kati ya dhana hizi mbili za hali halisi ya Mungu—ghadhabu Yake na Uvumilivu Wake—Mtazamo wa Mungu kwa kule kutubu kwa Waninawi kwa mara nyingine kunaruhusu watu kuweza kuona ule upande mwingine wa tabia halisi ya Mungu. Mabadiliko katika moyo wa Mungu yanaruhusu kwa kweli binadamu kwa mara nyingine kuuona ukweli wa huruma na upole wenye upendo wa Mungu na kuona ufunuo wa kweli wa hali halisi ya Mungu. Binadamu hawana budi kutambua kwamba rehema ya Mungu na upole wenye upendo si hadithi za uwongo tu, wala si ughushi. Hii ni kwa sababu hisia za Mungu kwa wakati huo zilikuwa kweli; Mabadiliko ya Mungu yalikuwa kweli; Mungu kwa kweli aliwapa binadamu kwa mara nyingine tena rehema na uvumilivu Wake.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp