Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

(Sehemu ya Nne)

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)

Kusudi la mjadala wetu wa haya mambo ni nini? Je, ni ili kwamba watu waweze kutafiti kanuni zilizopo kwenye uumbaji wa Mungu wa ulimwengu? Je, ni ili kwamba watu wavutiwe na falaki na jiografia? (Hapana.) Sasa ni nini? Ni ili kwamba watu wataelewa matendo ya Mungu. Katika matendo ya Mungu, watu wanaweza kukubali na kuthibitisha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kama unaweza kuielewa hoja hii, basi utaweza kuthibitisha kweli nafasi ya moyoni mwako na utaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni Mungu Mwenyewe wa kipekee, Muumbaji wa mbingu na nchi na vitu vyote. Hivyo, je, inasaidia katika uelewa wako juu ya Mungu kujua kanuni za vitu vyote na kujua matendo ya Mungu? (Ndiyo.) Inasaidiaje? Kwanza, utakapojua matendo haya ya Mungu, bado utavutiwa na falaki na jiografia? Bado utakuwa na moyo wa kushuku na mashaka kwamba Mungu ni Muumbaji wa vitu vyote? Bado utakuwa na moyo wa mtafiti na mashaka kwamba Mungu ni Muumbaji wa vitu vyote? (Hapana.) Utakapothibitisha kwamba Mungu ni Muumbaji wa ulimwengu na zaidi ujue kanuni zilizopo katika uumbaji Wake, moyoni mwako kweli utaamini kwamba Mungu anakimu ulimwengu? (Ndiyo.) Je, “kukimu” limesemwa tu kwa aina yoyote ya maana au limesemwa katika mazingira maalumu? Kwamba Mungu anakimu ulimwengu ina maana na matumizi mapana sana. Mungu hawakimu tu watu kwa kuwapatia mahitaji yao ya kila siku ya chakula na kinywaji, Anawapatia wanadamu kila kitu wanachohitaji, ikiwa ni pamoja na kila kitu ambacho watu wanakiona na vitu ambavyo haviwezi kuonekana. Mungu anatetea, anasimamia na anatawala mazingira ya kuishi ambayo binadamu anahitaji. Mazingira yoyote ambayo binadamu anayataka katika msimu wowote, Mungu ameyaandaa. Angahewa au halijoto yoyote ambayo inafaa kwa ajili ya uwepo wa binadamu pia ipo chini ya udhibiti wa Mungu na hakuna kati ya kanuni hizi ambayo inatokea yenyewe tu au bila utaratibu; ni matokeo ya kanuni ya Mungu na matendo Yake. Mungu Mwenyewe ni chanzo cha kanuni zote hizi na ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Huu ni ukweli uliothibitishwa na usioweza kushambuliwa na haijalishi unauamini au huuamini, haijalishi unaweza kuuona au huwezi kuuona, au haijalishi unaweza kuuelewa au huwezi kuuelewa.

Ninajua kwamba watu wengi wanaamini tu kile ambacho Mungu alisema na kufanya katika Biblia na kwamba Mungu alifichua matendo Yake kwa idadi ndogo ya watu ili kwamba watu waweze kuona thamani ya uwepo Wake, na waelewe hadhi Yake na kujua kwamba ni kweli Anaishi. Hata hivyo, kwa watu wengi sana ukweli kwamba Mungu Aliuumba ulimwengu na kwamba Anasimamia na kukimu vitu vyote unaonekana kuwa usio dhahiri au wenye utata na hata wanakuwa na mtazamo wa mashaka. Aina hii ya mtazamo inawafanya watu kuendelea kuamini kwamba sheria za ulimwengu asilia zilijitengeneza zenyewe, kwamba mabadiliko, mageuzi na ajabu ya ulimwengu asilia na sheria ambazo zinaongoza asili ziliibuka kwa hiari yao. Maana yake hii ni kwamba katika akili za watu, hawawezi kufikiri jinsi ambavyo Mungu alitengeneza kanuni juu ya vitu vyote, hawawezi kuelewa jinsi ambavyo Mungu anasimamia na kuvihudumia vitu vyote. Kwa sababu ya mipaka ya kigezo hiki, watu hawaamini katika uumbaji wa Mungu na utawala juu ya vitu vyote na kwamba ni Mpaji; na hata waumini wamejikita katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme, yaani, matendo ya Mungu na vile vile kuwakimu Kwake binadamu kwa namna fulani yapo tu kwa wateule wake. Hiki ni kitu ambacho Nachukia kukiona na kinaleta maumivu makali sana, kwa sababu binadamu hufurahia yote ambayo Mungu huleta, halafu wakati huohuo wanakana yote ambayo Anafanya na yote ambayo Anawapatia. Watu wanaamini tu kwamba mbingu na nchi na vitu vyote vinaongozwa na kanuni zao za asili na kwa sheria zao za asili na kwamba hazina mtawala wa kuvidhibiti au mtawala yeyote wa kuzikimu na kuzilinda. Hata kama unamwamini Mungu, unaweza usiamini yote haya kuwa ni maneno Yake; hili ni eneo kati ya maeneo ambayo hayajapewa uzito kwa kila anayemwamini Mungu, kwa kila mtu ambaye anakubali neno la Mungu, na kila mtu anayemfuata Mungu. Hivyo, Ninapoanza tu kujadili kitu fulani ambacho hakihusiani na Biblia au kile kinachodaiwa kuwa istilahi ya kiroho, baadhi ya watu wanasumbuliwa au wanachoshwa au hata kutofurahia. Inaonekana kwamba imefarakishwa kutoka kwa watu wa kiroho na mambo ya kiroho. Hicho ni kitu kibaya. Linapokuja suala la kujua matendo ya Mungu, hata kama hatutaji falaki, jiografia, au biolojia, tunajua utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, tunajua kukimu Kwake vitu vyote, na kwamba Yeye ni chanzo cha vitu vyote. Hii ni kazi muhimu sana na ambayo inapaswa kuchunguzwa, mmeelewa?

Kuhusu hadithi mbili ambazo Nimezisema, ingawa zinaweza kuwa na maudhui ambayo si ya kawaida na zinaweza kuwa zimesimuliwa na kuwasilishwa kwako kwa mtindo wa kipekee, hata hivyo Nilitaka kutumia lugha ya moja kwa moja na njia rahisi ili kwamba ungeweza kukubali na kuelewa kitu ambacho ni cha kina zaidi. Hili ndilo lilikuwa lengo langu tu. Nilitaka mwone na kuamini kuwa Mungu ni Mtawala wa vitu vyote kutokana na hadithi hizi ndogo na matukio. Lengo la kusimulia hadithi hizi ni kuwafanya mwone na kujua matendo ya Mungu yasiyokuwa na kikomo ndani ya hadithi yenye kikomo. Kuhusu ni lini mtafikia kikamilifu matokeo haya ndani yenu inategemea uzoefu wako binafsi na maendeleo yako binafsi. Ukifuatilia ukweli na ikiwa unatafuta kumjua Mungu, basi mambo haya yatafanya kazi kama kumbusho lenye nguvu na imara kwako; yatakufanya uwe na utambuzi wa kina sana, ubayana katika uelewa wako, na polepole utasogea karibu na matendo ya kweli ya Mungu, ukaribu ambao utakuwepo bila umbali na bila hitilafu. Hata hivyo, kama hutafuti kumjua Mungu, basi hadithi hizo ulizozisikia haziwezi kukudhuru. Mnaweza kuzichukulia kama hadithi za kweli.

Je, mlielewa kitu chochote kwenye hadithi hizi mbili? Kwanza, je, hadithi hizi mbili zinajitenga na mjadala wetu wa awali kuhusu Mungu kumjali binadamu? Je, kuna uhusiano usioepukika? (Ndiyo.) Uhusiano huo ni upi? Je, ni kwamba ndani ya hadithi hizi mbili tunaona matendo ya Mungu na jinsi ambavyo Anapanga na kushughulika na kila kitu kwa ajili ya binadamu? Je, ni kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya na mawazo Yake yote yanaelekezwa kwa uwepo wa binadamu? (Ndiyo.) Je, sio kwamba fikra makini za Mungu na kujali kwake binadamu kuko dhahiri? Binadamu hana haja ya kufanya chochote. Mungu amewaandaliwa watu hewa hiyo hiyo wanayoivuta. Mboga na matunda wanayokula vinapatikana kwa urahisi. Kutoka kaskazini hadi kusini, kutoka mashariki hadi magharibi, kila kanda ina rasilimali zake asili na mazao na matunda tofauti na mboga zimeandaliwa na Mungu. Tukizungumza juu ya mazingira mapana, Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili. Kama kusingekuwa na udhibiti na ukuu wa Mungu, hakuna mwanadamu ambaye angeweza kudumisha na kuweka wiano katika mazingira, hata kama yaliumbwa na Mungu kwanza. Katika baadhi ya maeneo hakuna hewa, hivyo watu hawawezi kuishi hapo na hawapaswi kutoka nje ya mipaka, hii ni kwa ajili ya usalama wa binadamu na mambo haya ni ya siri sana. Kila pembe ya mazingira, urefu na upana wa dunia, na kila kiumbe hai duniani—vilivyo hai na vilivyokufa—viliandaliwa na Mungu na Alivifikiria: Kwa nini kitu hiki kinahitajika? Kwa nini sio cha lazima? Lengo la kuwa na kitu hiki hapa ni nini na kwa nini kiende hapo? Mungu alikuwa amekwishafikiria hii yote na hakuna haja ya watu kuyafikiria. Kuna baadhi ya watu wapumbavu ambao siku zote wanafikiri juu ya kuhamisha milima, lakini badala ya kufanya hivyo, kwa nini wasihamie kwenye tambarare? Kama huipendi milima, kwa nini unakwenda kuishi karibu nayo? Huu si upumbavu? Nini hutokea ikiwa utauhamisha mlima huo? Kimbunga kikali kitavuma au wimbi kubwa litapiga na makazi ya watu yataharibiwa. Je, hicho kisingekuwa kitu cha kipumbavu kufanya? Sio? Watu wanaweza tu kuharibu. Hawawezi hata kudumisha pahali pa pekee waliponapo pa kuishi, na ilhali wanataka kukimu vitu vyote. Hili haliwezekani.

Mungu anamwacha mwanadamu kusimamia vitu vyote na kuwa na utawala juu yao, lakini mwanadamu anafanya kazi nzuri? (Hapana.) Ni kwa jinsi gani mwanadamu anafanya kazi mbaya? Mwanadamu ana tabia ya uharibifu; mwanadamu sio kwamba tu hawezi kutunza vitu kama Mungu alivyoviumba, kwa kweli ameviharibu. Binadamu ameifanya milima kuwa vifusi, ameijaza bahari kwa mchanga, na amezibadilisha tambarare kuwa majangwa ambapo hakuna kinachoweza kuishi. Halafu katika majangwa hayo mwanadamu amejenga viwanda na kujenga vinu vya nyuklia na uharibifu unaendelea katika pande zote. Mito si mito tena, bahari si bahari tena…. Binadamu anapovunja uwiano na kanuni za maumbile, siku yao ya maafa na kifo haipo mbali na haiepukiki. Maafa yanapokuja, watajua viumbe vya Mungu ni vya thamani kiasi gani jinsi vyote ni muhimu kwa binadamu. Mwanadamu kuishi katika mazingira yenye hali ya hewa nzuri ni sawa na kuwa peponi. Watu hawatambui baraka hii, lakini wakati ambapo wataipoteza yote ndipo watatambua ni jinsi gani yote ni adimu na ya thamani. Ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuirudisha hii yote? Watu wangefanyaje ikiwa Mungu Asingekuwa tayari kuitengeneza tena? Mngefanyaje? (Tusingeweza kufanya chochote.) Kwa kweli, kuna kitu mnachoweza kufanya na ni rahisi sana na Nitakapowaambia ni nini, mara moja mtajua kwamba hiyo inawezekana. Kwa nini mwanadamu amejikuta katika mashaka yake ya kimazingira ya sasa? Je, ni kwa sababu ya tamaa na uharibifu wa mwanadamu? Ikiwa mwanadamu atasitisha uharibifu huu, je, mazingira ya kuishi hayatakuwa sawa taratibu yenyewe? Ikiwa Mungu hafanyi chochote, ikiwa Mungu hatamani tena kufanya kitu chochote kwa ajili ya binadamu—yaani, hataki kuingilia—njia bora zaidi ingekuwa ni binadamu kusitisha uharibifu huu na kurudisha vitu kuwa vile vilivyokuwa. Kusitisha uharibifu huu wote humaanisha kusitisha uporaji na uharibifu wa vitu ambavyo Mungu ameviumba. Hii itaruhusu mazingira ambamo mwanadamu anaishi kuboreka taratibu. Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha uharibifu zaidi wa mazingira na hali itakuwa mbaya zaidi. Je, mbinu Yangu ni rahisi? (Ndiyo, ni rahisi.) Ni rahisi na inawezekana, siyo? Ni rahisi kweli, na inawezekana kwa baadhi ya watu, lakini je, hii inawezekana kwa watu walio wengi duniani? (Haiwezekani.) Kwenu nyinyi, angalau inawezekana? (Ndiyo.) Chanzo cha “ndiyo” yenu ni nini? Je, mtu anaweza kusema kuwa inahusisha kuanzisha msingi wa uelewa kuhusu matendo ya Mungu? Je, mtu anaweza kusema inahusisha kushikilia kanuni na mpango wa Mungu? (Ndiyo.) Kuna njia ya kubadilisha haya yote, lakini hiyo siyo mada tunayoijadili sasa. Mungu anawajibika kwa kila uhai wa binadamu na anawajibika hadi mwisho. Mungu Anawakimu, hata kama umeugua kutokana na mazingira yaliyoharibiwa na Shetani, au kuathiriwa na uchafuzi au kupata madhara mengine, haijalishi; Mungu Anakukimu na Atakuacha uendelee kuishi. Je, una imani katika hili? (Ndiyo.) Mungu hachukulii upotevu wa maisha ya binadamu kwa urahisi.

Mmehisi umuhimu wa kumtambua Mungu kama chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo, tumehisi.) Mna hisia gani? Endelea, nitasikiliza. (Hapo awali, hatukufikiria kamwe kuhusisha milima, bahari na maziwa na matendo ya Mungu. Leo, kupitia ushirika wa Mungu, sasa tunaelewa kwamba haya yote siku zote yalikuwa ni matendo ya Mungu na yanatoka kwa hekima Yake, hivyo tunaona kwamba uumbaji wa Mungu wa vitu vyote ulioamuliwa kabla kuanzia mwanzoni kabisa na vyote vinakuwa na mapenzi mema ya Mungu. Vitu vyote vinahusiana na binadamu ndiye anayenufaika mwishowe. Tulichokisikia leo kinaonekana ni kipya na kigeni, na tumehisi jinsi ambavyo matendo ya Mungu ni halisi. Katika uhalisia na katika maisha yetu ya kila siku tunaona kwa kweli vitu kama vilivyo tunapokutana na viumbe hai.) Unaiona kabisa, sio? Mungu kumkimu binadamu sio bila msingi imara, hatamki tu maneno machache na kuishia hapo tu. Mungu anafanya mambo mengi, hata vitu ambavyo huvioni anafanya kwa manufaa yako. Mwanadamu anaishi katika mazingira haya, ulimwengu huu ambao Mungu Aliutengeneza, na ndani yake watu na vitu vingine vinategemeana, kama tu ambavyo gesi inayotoka kwenye mimea inaitakasa hewa na kuwanufaisha watu wanaoivuta. Hata hivyo, baadhi ya mimea ni sumu kwa watu, lakini hakuna mimea mingine ambayo ni kiuasumu kwao? Hili ni moja ya maajabu ya uumbaji wa Mungu! Hatukujadili mada hii leo, badala yake tumejadili kimsingi hali ya kutegemeana ya mwanadamu na vitu vingine, jinsi ambavyo mwanadamu hawezi kuishi bila vitu vingine. Ni nini umuhimu wa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote? Mwanadamu hawezi kuishi bila vitu vingine, kama ambavyo mwanadamu anahitaji hewa kuweza kuishi na namna ambavyo kama ungewekwa kwenye ombwe ungekufa upesi. Hii ni kanuni ya msingi sana kukufanya kuona kwamba mwanadamu anahitaji vitu vingine. Hivyo ni aina gani ya mtazamo ambao mwanadamu anapaswa kuwa nao kwa vitu vyote? (Kuvithamini sana.) Vithamini sana, vitunze, vitumie kwa ufanisi, usiviharibu, usivipoteze, na usivibadilishe kwa ghafula, maana vitu vyote vinatoka kwa Mungu na vinatolewa kwa binadamu na binadamu anapaswa kuvichukulia kwa uangalifu. Leo tumejadili mada hizi mbili, na mtarudi na kuzitafakari kwa kina. Wakati ujao tutajadili vitu vingi zaidi kwa kina. Ushirika wetu utaishia hapa kwa leo. Kwa heri! (Kwa heri!)

Januari 18, 2014

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp