Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) (Sehemu ya Kwanza)

Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Je, “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Je, una ufahamu wowote wa juujuu kuhusu jambo hilo? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu. Ni kupitia tu kwa mawasiliano ya Mungu ya kipengele hiki cha ukweli ndipo nimehisi kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote na kuona kwamba uhai wa vitu vyote unapewa na Mungu, kwamba Mungu anatengeneza sheria hizi, na kwamba Anavilea vitu vyote. Kutokana na uumbaji Wake wa vitu vyote ninaona upendo wa Mungu.) Wakati uliopita, kimsingi tuliwasiliana kuhusu uumbaji wa Mungu wa vitu vyote na jinsi Aliunda sheria na kanuni kwa ajili ya vitu hivyo. Chini ya sheria hizi na chini ya kanuni hizi, vitu vyote huishi na kufa na mwanadamu na kuishi pamoja kwa amani na mwanadamu chini ya utawala wa Mungu na machoni pa Mungu. Tulizungumzia nini kwanza? Mungu aliumba vitu vyote na akatumia mbinu Zake kutunga sheria za ukuaji wa vitu vyote, na vilevile njia na mpangilio wa ukuaji wa vitu hivyo, na pia alitunga njia za kuwepo kwa vitu vyote duniani, ili viweze kuishi kwa kuendelea na kutegemeana. Kwa mbinu na sheria hizi, vitu vyote vinaweza kuwepo na kukua katika nchi hii kwa ufanisi na kwa amani. Ni kwa kuwa tu na mazingira kama haya ndipo wanadamu wanaweza kuwa na makao na mazingira ya kuishi yaliyo thabiti, na chini ya uongozi wa Mungu, waendelee kukua na kusonga mbele, kukua na kusonga mbele.

Wakati uliopita tulijadili kuhusu wazo la msingi la Mungu kupeana vitu vyote. Mungu kwanza huvipa vitu vyote kwa njia hii ili vitu vyote viwepo na kuishi kwa ajili ya wanadamu. Yaani, mazingira kama haya yapo kwa ajili ya sheria zilizotungwa na Mungu. Ni tu kwa Mungu kudumisha na kusimamia sheria kama hizi ndio wanadamu wana mazingira ya kuishi waliyonayo sasa. Tulichozungumzia wakati uliopita ni hatua kubwa kutoka kwa ufahamu wa Mungu tuliozungumzia awali. Kwa nini hatua kama hiyo ipo? Kwa sababu tulipozungumza hapo awali kuhusu kuanza kumjua Mungu, tulikuwa tunajadili katika eneo la Mungu kuwaokoa na kuwasimamia wanadamu—yaani, uokoaji na usimamizi wa watu waliochaguliwa na Mungu—kuhusu kumjua Mungu, matendo ya Mungu, tabia Yake, kile Anacho na Alicho, makusudi Yake, na vile Anampa mwanadamu ukweli na uhai. Lakini mada tuliyozungumza kuihusu wakati uliopita haikujikita tu katika mipaka ya Biblia na katika eneo la Mungu kuwaokoa watu Wake waliochaguliwa. Badala yake, ilitoka nje ya eneo hili, nje ya Biblia, na nje ya mipaka ya hatua tatu za kazi ambayo Mungu anafanya kwa watu Wake waliochaguliwa na kujadili Mungu Mwenyewe. Hivyo basi ukisikia sehemu hii ya mawasiliano Yangu, lazima usiwekee mipaka ufahamu wako wa Mungu kwa Biblia na hatua tatu za kazi ya Mungu. Badala yake, unahitaji kuuweka wazi mtazamo wako; unahitaji uone matendo ya Mungu na kile Anacho na alicho miongoni mwa vitu vyote, na vile Mungu anatawala na kusimamia vitu vyote. Kupitia kwa mbinu hii na juu ya msingi huu, unaweza kuona vile Mungu anapeana vitu vyote. Hii inawawezesha wanadamu kuelewa kwamba Mungu ni chanzo halisi cha uhai kwa vitu vyote na kwamba huu ni utambulisho halisi wa Mungu Mwenyewe. Hiyo ni kusema, utambulisho wa Mungu, hadhi na mamlaka na kila kitu Chake havilengwi tu kwa wale wanaomfuata Yeye wakati huu—havilengwi tu kwa kundi hili la watu—bali kwa vitu vyote. Basi ni nini eneo la vitu vyote? Eneo la vitu vyote ni pana sana. Ninatumia “vitu vyote” kueleza eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote kwa sababu Ninataka kuwaambia kwamba vitu vinavyotawaliwa na Mungu si vile mnavyoweza tu kuona kwa macho yenu, bali vinahusisha ulimwengu yakinifu ambao watu wote wanaweza kuuona, na vilevile ulimwengu mwingine usioweza kuonekana kwa macho ya binadamu nje ya ulimwengu yakinifu, na zaidi unahusisha anga na sayari nje ya mahali ambapo wanadamu wapo sasa. Hilo ni eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote ni pana zaidi. Kwenu ninyi, mnachopaswa kuelewa, mnachopaswa kuona, na kutoka kwa vitu mnavyopaswa kupata maarifa—hivi ndivyo kila mmoja wenu anahitaji na ni lazima aelewe, aone, na awe na hakika navyo. Ingawa eneo la hivi “vitu vyote” ni pana, Sitawaambia kuhusu eneo msiloweza kuona kabisa au msiloweza kukutana nalo. Nitawaambia tu kuhusu eneo ambalo binadamu wanaweza kukutana nalo, wanaweza kuelewa, na wanaweza kufahamu, ili kila mmoja aweze kuhisi maana halisi ya kirai hiki “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Hivyo, chochote Ninachowasilisha kwenu hakitakuwa maneno matupu.

Wakati uliopita, tulitumia mbinu ya kuhadithia ili kutoa maelezo rahisi ya jumla ya mada hii “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote,” ili muwe na ufahamu wa msingi wa jinsi Mungu huvipa vitu vyote. Ni nini kusudi la kuwafundisha kidogokidogo wazo hili la msingi? Ni kuwafanya mjue kwamba, nje ya Biblia na hatua tatu za kazi Yake, Mungu pia anafanya hata kazi nyingi zaidi ambayo wanadamu hawawezi kuiona au kukutana nayo. Kazi kama hiyo inatendwa binafsi na Mungu. Kama Mungu angekuwa anaongoza tu watu Wake waliochaguliwa kwenda mbele, bila hii kazi iliyo nje ya kazi Yake ya usimamizi, basi ingekuwa vigumu sana kwa binadamu hawa, ikiwemo pamoja na ninyi nyote, kuendelea kusonga mbele, na binadamu huu na ulimwengu huu haungeweza kuendelea kukua. Huo ndio umuhimu wa kirai hiki “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote” Ninachowasilisha kwenu siku hii.

Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu

Tumejadili mada nyingi na maudhui yanayohusiana na kirai hiki “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote,” lakini mnajua ndani ya mioyo yenu ni vitu vipi Mungu anatoa kwa wanadamu mbali na kuwapa ninyi neno Lake na kutenda kazi Yake ya kuadibu na hukumu kwenu? Watu wengine huenda wakasema, “Mungu hunipa neema na baraka, na kunipa nidhamu, faraja, na utunzaji na ulinzi kwa kila njia iwezekanayo.” Wengine watasema, “Mungu hunipa chakula cha kila siku na kinywaji,” ilhali wengine hata watasema, “Mungu hunipa kila kitu.” Kuhusu vitu hivi ambavyo watu wanaweza kukutana navyo katika maisha yao ya kila siku, nyote mnaweza kuwa na majibu yanayohusiana na matukio mnayopitia katika maisha yenu ya kimwili. Mungu humpa kila mtu vitu vingi, ingawa tunachojadili leo hakijajikita tu katika mipaka ya eneo la mahitaji ya watu ya kila siku, lakini kinamruhusu kila mmoja wenu kutazama mbali zaidi. Kutokana na mtazamo mkubwa, kwa vile Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, Anadumisha vipi uhai wa vitu vyote? Ili vitu vyote viweze kuendelea kuwepo, ni nini ambacho Mungu huleta kwa vitu vyote ili kudumisha kuwepo kwa vitu hivyo na kudumisha sheria za kuwepo kwa vitu hivyo? Hilo ndilo wazo kuu la kile tunachojadili leo. Je, mnaelewa Nilichosema? Mada hii huenda ikawa msiyoifahamu sana, lakini Sitazungumza kuhusu mafundisho ya dini yoyote ambayo ni ya kina sana. Nitajitahidi kuwafanya nyote muelewe baada ya kusikiliza. Hamhitaji kuhisi mzigo wowote—mnachotakiwa kufanya tu ni kusikiliza kwa makini. Kwa hali yoyote, bado Ninahitaji kuisisitiza zaidi kidogo: Ninazungumza juu ya mada gani? Niambieni. (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Basi ni vipi ambavyo Mungu huvipa vitu vyote? Ni nini ambacho Yeye huvipa vitu vyote ili isemwe kwamba “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? Je, mna dhana ama mawazo yoyote kuhusu hili? Inaonekana kwamba mada hii Ninayozungumzia kimsingi haileti kinachotumainiwa ndani ya mioyo yenu na ndani ya akili zenu. Lakini Natumai mtaweza kuunganisha mada hii pamoja na vitu Ninavyoenda kuzungumzia kwa matendo ya Mungu, na sio kuviunganisha kwa ufahamu wowote au kuvihusisha na desturi zozote za binadamu au uchunguzi. Ninazungumza tu kuhusu Mungu na kuhusu Mungu Mwenyewe. Hilo ni pendekezo Langu kwenu. Unaelewa, sivyo?

Mungu ametoa vitu vingi kwa wanadamu. Nitaanza kwa kuzungumza kuhusu kile ambacho watu wanaweza kuona, yaani, wanachoweza kuhisi. Hivi ni vitu ambavyo watu wanaweza kuvielewa na wanaweza kukubali. Hivyo basi kwanza tuanze na ulimwengu yakinifu kujadili kile ambacho Mungu amewapa wanadamu.

1. Hewa

Kwanza, Mungu aliumba hewa ili mwanadamu aweze kupumua. Je, “hewa” hii si hewa ya maisha ya kila siku ambayo wanadamu hukutana nayo kila mara? Je, hewa hii si kitu ambacho wanadamu hutegemea kila wakati, hata wanapolala? Hewa ambayo Mungu aliumba ina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu: ni kijenzi muhimu cha kila pumzi yao na cha uhai wenyewe. Kiini hiki, kinachoweza tu kuhisiwa lakini hakionekani, kilikuwa zawadi ya Mungu ya kwanza kwa vitu vyote. Baada ya kuumba hewa, je, Mungu aliacha kufanya kazi? Baada ya kuumba hewa, je, Mungu alizingatia uzito wa hewa? Je, Mungu alizingatia yaliyomo kwenye hewa? (Ndio.) Mungu alikuwa anafikiria nini alipoumba hewa? Kwa nini Mungu aliumba hewa, na fikira Yake ilikuwa gani? Wanadamu wanahitaji hewa, na wanahitaji kupumua. Kwanza kabisa, uzito wa hewa unapaswa kukubaliana na pafu la mwanadamu. Kuna yeyote anayejua uzito wa hewa? Hili si jambo ambalo watu wanahitaji kujua; hakuna haja ya kujua hili. Hatuhitaji idadi kamili kuhusiana na uzito wa hewa, na kuwa na wazo la jumla ni vizuri. Mungu aliumba hewa yenye uzito ambao ungefaa zaidi mapafu ya mwanadamu kupumua. Yaani, wanadamu wanafurahia na haiwezi kudhuru mwili wanapoivuta. Hili ndilo wazo kuhusu uzito wa hewa. Basi tutaongea kuhusu yaliyomo kwenye hewa. Kwanza, yaliyomo ndani ya hewa si sumu kwa wanadamu na hivyo hayatadhuru pafu na mwili. Mungu alihitaji kuzingatia haya yote. Mungu alihitaji kuzingatia kwamba hewa ambayo wanadamu wanapumua inapaswa kuingia na kutoka taratibu, na kwamba, baada ya kuvuta hewa, kadiri na kiasi cha hewa vinapaswa kuhakikisha damu pamoja na hewa chafu ndani ya mapafu na mwili vingejenga na kuvunjavunja kemikali mwilini vizuri, na pia kwamba hewa hiyo haipaswi kuwa na vijenzi vyovyote vya sumu. Kuhusu viwango hivi viwili, Sitaki kuwalisha mafungu ya maarifa, lakini badala yake nataka tu mjue kwamba Mungu alikuwa na mchakato maalum wa mawazo akilini mwake Alipoumba kila kitu—bora zaidi. Kuhusu kiasi cha vumbi katika hewa, kiasi cha vumbi, mchanga na uchafu duniani, na vilevile vumbi inayoelekea chini kutoka angani, Mungu alikuwa na mpango wa vitu hivi pia—njia ya kuondoa au kutatua vitu hivi. Huku kukiwa na vumbi kiasi, Mungu aliiumba ili vumbi isidhuru mwili na upumuaji wa mwanadamu, na kwamba vipande vya vumbi viwe na ukubwa usiokuwa na madhara kwa mwili. Je, uumbaji wa Mungu wa hewa haukuwa wa ajabu? Je, ulikuwa rahisi kama kupuliza pumzi ya hewa kutoka kinywani Mwake? (La.) Hata katika uumbaji wake wa vitu rahisi sana, maajabu ya Mungu, akili Zake, mawazo Yake, na hekima Yake vyote ni dhahiri. Je, Mungu ni mwenye uhalisi? (Ndiyo.) Hiyo ni kusema, hata katika kuumba kitu rahisi, Mungu alikuwa akifikiria kuhusu mwanadamu. Kwanza kabisa, hewa ambayo wanadamu hupumua ni safi, yaliyomo yanafaa kwa upumuaji wa mwanadamu, si sumu na hayasababishi madhara kwa wanadamu, na uzito huo umekadiriwa kwa upumuaji wa wanadamu. Hewa hii ambayo wanadamu huvuta pumzi na kutoa ni muhimu kwa mwili wao, umbo lao. Ili wanadamu waweze kupumua kwa uhuru, bila kizuizi au wasiwasi. Waweze kupumua kwa kawaida. Hewa ni kile ambacho Mungu aliumba mwanzo na ambacho ni cha lazima kwa upumuaji wa wanadamu.

2. Halijoto

Kitu cha pili ni halijoto. Kila mtu anajua halijoto ni nini. Halijoto ni kitu ambacho mazingira yanayofaa kuishi kwa wanadamu ni lazima yawe nacho. Ikiwa halijoto iko juu sana, tuseme ikiwa halijoto iko juu zaidi ya nyuzi Selisiasi 40, basi haingekuwa inachosha sana kwa wanadamu kuishi? Je, haitakuwa ya kumaliza sana? Je, na halijoto ikiwa chini sana, na kufikia nyuzi hasi Selisiasi 40? Wanadamu hawataweza pia kuistahimili. Kwa hiyo, Mungu alikuwa mwangalifu sana katika kuviweka vipimo hivi vya halijoto. Vipimo vya halijoto ambavyo mwili wa mwanadamu unaweza kufanya mabadiliko kimsingi ni nyuzi hasi Selisiasi 30 hadi nyuzi Selisiasi 40. Hiki ndicho kipimo cha halijoto cha msingi kutoka kaskazini mpaka kusini. Katika maeneo ya baridi, halijoto inaweza kuteremka mpaka nyuzi hasi 50 hadi 60 Selisiasi. Eneo kama hilo si mahali ambapo Mungu anamruhusu mwanadamu kuishi. Mbona kuna maeneo ya baridi hivyo? Katika hayo kuna hekima na makusudi ya Mungu. Hakuruhusu kusonga karibu na sehemu hizo. Mungu hulinda sehemu zilizo na joto sana na baridi sana, kumaanisha Hayuko tayari kumruhusu mwanadamu kuishi huko. Si kwa wanadamu. Kwa nini akaruhusu sehemu kama hizo kuwepo duniani? Ikiwa Mungu hangemruhusu mwanadamu kuishi au kuwepo huko, basi kwa nini akaziumba? Hekima ya Mungu imo humo. Yaani, halijoto ya msingi ya mazingira ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu pia imerekebishwa na Mungu vya kutosha. Kuna sheria hapa pia. Mungu aliumba vitu vingine kusaidia kudumisha halijoto kama hiyo, kudhibiti halijoto hiyo. Ni vitu gani vinatumiwa kudumisha halijoto hii? Kwanza kabisa, jua linaweza kuwaletea watu uvuguvugu, lakini watu wataweza kustahimili iwapo ni vuguvugu sana? Je, kuna yeyote anaweza thubutu kukaribia jua? Je, kuna kifaa chochote duniani kinachoweza kusonga karibu na jua? (La.) Mbona? Ni joto sana. Kitayeyuka. Kwa hiyo, Mungu ametengeneza kipimo maalum cha umbali wa jua kutoka kwa wanadamu: Amefanya kazi maalumu. Mungu ana kiwango cha umbali huu. Vilevile kuna Ncha ya kusini na Ncha ya Kaskazini za dunia. Kuna nini katika Ncha ya Kusini na Ncha ya Kaskazini? Kote kuna mito ya barafu. Wanadamu wanaweza kuishi juu ya mito ya barafu? Inafaa kuishi kwa wanadamu? (La.) La, hivyo hutaenda huko. Kwa vile huendi katika Ncha za Kusini na Kaskazini, mito ya barafu itahifadhiwa, na itaweza kufanya wajibu wake, ambao ni kudhibiti halijoto. Unaelewa? Ikiwa hakuna Ncha za Kusini na Kaskazini na jua linawaka juu ya dunia kila wakati, basi watu wote juu ya dunia watakufa kutokana na joto. Je, Mungu hutumia tu vitu hivi viwili kudhibiti halijoto? La, Hatumii tu vitu hivi viwili kudhibiti halijoto inayofaa kuishi kwa wanadamu. Pia kuna kila aina za viumbe vyenye uhai, kama vile nyasi juu ya mbuga za malisho, aina mbalimbali za miti na kila aina ya mimea iliyo ndani ya misitu. Vinafyonza joto la jua na kusanisi nishati ya joto ya jua kurekebisha halijoto ambayo wanadamu wanaishi ndani. Pia kuna vyanzo vya maji, kama vile mito na maziwa. Sehemu ya juu ya mito na maziwa si kitu kinachoweza kuamuliwa na yeyote. Hakuna yeyote anayeweza kudhibiti kiasi cha maji yaliyo juu ya dunia, wapi maji hayo yanatiririka, mwelekeo wa kutiririka huko, wingi wa maji hayo, au spidi ya mtiririko huo. Mungu pekee ndiye ajuaye. Vyanzo hivi mbalimbali vya maji, yakiwemo maji ya chini ya ardhi na mito na maziwa yaliyo juu ya ardhi ambayo watu wanaweza kuona, yanaweza pia kurekebisha halijoto ambayo wanadamu wanaishi ndani. Zaidi ya hayo, kuna kila aina ya uumbaji wa kijiografia, kama vile milima, tambarare, korongo kuu na ardhi ya majimaji wa uumbaji huu mbalimbali wa kijiografia na sehemu zao za juu na ukubwa vyote vina umuhimu katika kudhibiti halijoto. Kwa mfano, ikiwa mlima huu una nusu kipenyo cha kilomita 100, kilomita hizi 100 zitakuwa na athari ya kilomita 100. Lakini kuhusu safu za milima na korongo kuu ngapi kama hizo ambazo Mungu ameumba juu ya dunia, hili ni jambo ambalo Mungu amelifikiria kabisa. Kwa maneno mengine, nyuma ya kuwepo kwa kila kitu kilichoumbwa na Mungu kuna hadithi, na pia ina hekima na mipango ya Mungu. Tuseme, kwa mfano, misitu na kila aina ya mimea—sehemu ya juu na ukubwa wa sehemu ambamo vinakua haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu yeyote, wala mwanadamu yeyote hana usemi wa mwisho kuhusu vitu hivi. Kiasi cha maji ambayo vinafyonza, kiasi cha nishati ya joto ambayo vinafyonza kutoka kwa jua pia haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu yeyote. Vitu hivi vyote viko katika eneo la kile kilichopangwa na Mungu alipoumba vitu vyote.

Ni kwa sababu tu ya upangaji wa makini, fikira, na utaratibu wa Mungu katika vipengele vyote ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Kwa hiyo, kila kitu ambacho mwanadamu anakiona kwa macho yake, kama vile jua, Ncha za Kusini na Kaskazini ambazo watu mara nyingi husikia kuzihusu, vilevile viumbe mbalimbali vilivyo hai juu na chini ya ardhi na ndani ya maji, na sehemu za juu zenye misitu na aina zingine za mimea, na vyanzo vya maji, mikusanyiko mbalimbali ya maji, kuna kiasi gani cha maji chumvi na maji baridi, kuongezea mazingira mbalimbali ya kijiografia—Mungu hutumia vitu hivi kudumisha halijoto ya kawaida kwa kuishi kwa mwanadamu. Hii ni thabiti. Ni kwa sababu tu Mungu ana fikira kama hizi ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Haiwezi kuwa baridi zaidi wala joto zaidi: sehemu zenye joto zaidi na ambapo halijoto inazidi kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea bila shaka hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili yako. Sehemu zenye baridi zaidi na ambapo halijoto ni ya chini zaidi; sehemu ambazo, punde tu wanadamu wanapowasili, zitawafanya wagande sana baada ya dakika chache mpaka wasiweze kuzungumza, ubongo wao utaganda, wasiweze kufikiri, na hatimaye watakosa hewa—sehemu kama hizo pia hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Haijalishi ni aina gani ya uchunguzi wanadamu wanataka kufanya, au kama wanataka kuvumbua au wanataka kutengua mipaka hiyo—haijalishi watu wanafikiria nini, hawataweza kamwe kuzidi mipaka ya kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea. Hawataweza kuondoa mipaka hiyo ambayo Mungu alimuumbia mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu aliwaumba wanadamu, na Mungu anajua bora zaidi ni halijoto gani mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea. Je, wanadamu wenyewe wanajua? (La.) Mbona unasema wanadamu hawajui? Ni mambo gani ya upumbavu ambayo wanadamu wamefanya? Je, hakujakuwa na watu wachache ambao kila mara wanataka kushindana na Ncha za Kaskazini na Kusini? Kila mara wanataka kwenda huko kumiliki ardhi hiyo, ili waweze kukita mizizi na kuiendeleza. Je, hiki si kitendo cha kujiangamiza? Tuseme umechunguza kikamilifu Ncha za Kusini na Kaskazini. Lakini hata kama unaweza kuzoea halijoto hiyo, unaweza kuishi hapo, na unaweza “kuendeleza” mazingira ya kuishi na mazingira ya kuendelea kuishi ya Ncha za Kusini na Kaskazini, itamfaidi mwanadamu kwa njia yoyote? Je, utafurahi ikiwa barafu ya Ncha za Kusini na Kaskazini itayeyuka? Hili ni la kushangaza. Ni kitendo cha upuuzi. Wanadamu wana mazingira wanayoweza kuendelea kuishi ndani, lakini hawawezi tu kukaa hapa kimya na kwa uangalifu, na wanapaswa kwenda wasikoweza kuendelea. Kwa nini ni hivyo? Wamechoshwa na kuishi katika halijoto hii ya kufaa. Wamefurahia baraka nyingi sana. Mbali na hayo, haya mazingira ya kuishi ya kawaida yameharibiwa kiasi sana na wanadamu, hivyo wanaweza basi kwenda kwa Ncha ya Kusini na Ncha ya Kaskazini ili wafanye madhara mengi zaidi au kujihusisha katika “kusudi,” fulani ili waweze kuwa “watangulizi” wa aina fulani. Si huu ni upumbavu? Hivyo ni kusema, chini ya uongozi wa babu yao Shetani, wanadamu hawa wanaendelea kufanya kitu kimoja cha upuuzi baada ya kingine, wakiharibu bila hadhari na kwa utukutu makao mazuri ambayo Mungu aliwaumbia wanadamu. Hili ndilo Shetani alifanya. Zaidi ya hayo, kwa kuona kwamba kuendelea kuishi kwa wanadamu duniani kuko katika hatari kidogo, watu wengi sana wanataka kutafuta njia za kwenda kuishi juu ya mwezi, kutafuta njia ya kuondoka kwa kuona ikiwa wanaweza kuishi huko. Hatimaye, ni nini kinakosekana huko? (Oksijeni.) Je, wanadamu wanaweza kuendelea kuishi bila oksijeni? Kwa vile mwezi hauna oksijeni, si mahali ambapo mwanadamu anaweza kuishi huko, ilhali mwanadamu anaendelea kutaka kwenda huko. Hii ni nini? Ni kujiangamiza, sivyo? Ni mahali pasipo na hewa, na halijoto haifai kwa kuendelea kuishi kwa mwanadamu, hivyo hapajatayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu.

Halijoto ambayo tumezungumzia ni kitu ambacho watu wanaweza kukutana nacho katika maisha yao ya kila siku. Halijoto ni kitu ambacho miili yote ya wanadamu inaweza kuhisi, lakini hakuna anayefikiria vile halijoto hii iliumbwa, au ni nani anasimamia na kudhibiti halijoto ya kufaa kuishi kwa wanadamu. Hiki ndicho tunaanza kujua sasa. Je, kuna hekima ya Mungu katika hili? Je, kuna kitendo cha Mungu katika hili? (Ndiyo.) Ukifikiria kwamba Mungu aliumba mazingira yenye halijoto ya kufaa kuishi kwa wanadamu, je, hii ni njia moja ambayo Mungu huvipa vitu vyote? (Ndiyo.) Ni kweli.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp