Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili)

Wanaopeleka watoto na jamaa zao wasioamini kabisa kanisani ni wachoyo sana na wanaonyesha ukarimu wao. Watu hawa wanasisitiza tu upendo, bila kujali iwapo wanaamini ama iwapo ni matakwa ya Mungu. Wengine wanaleta wake zao mbele ya Mungu, ama kuleta wazazi wao mbele ya Mungu, na bila kujali iwapo Roho Mtakatifu anakubali ama anafanya kazi Yake, kwa upofu “wanawachukua watu wenye vipaji” kwa ajili ya Mungu. Kuna faida gani inayoweza kupatikana kutokana na kueneza ukarimu huu kwa watu hawa wasioamini? Hata kama hawa wasioamini wasio na uwepo wa Roho Mtakatifu wanapambana kumfuata Mungu, bado hawawezi kuokolewa kama mtu anavyodhani wanaweza. Wanaopokea wokovu kwa kweli si rahisi hivyo kuwapata. Wale ambao hawajapitia kazi ya Roho Mtakatifu na majaribio na hawajakamilishwa na Mungu aliyepata mwili hawawezi kukamilika kabisa. Kwa hivyo, watu hawa hawana uwepo wa Roho Mtakatifu kutoka wakati wanaanza kumfuata Mungu kwa jina. Kulingana na hali yao halisi, hawawezi tu kufanywa kamili. Hivyo, Roho Mtakatifu Haamui kutumia nguvu nyingi kwao, wala Hawapatii nuru yoyote ama kuwaongoza kwa njia yoyote; Anawaruhusu tu kufuata na hatimaye kufichua matokeo yao—haya yametosha. Shauku na nia za mwanadamu zinatoka kwa Shetani, na hakuna vile zinaweza kukamilisha kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali mtu ni mtu wa aina gani, mtu lazima awe na kazi ya Roho Mtakatifu—je, mtu anaweza kumkamilisha mtu? Mbona mume anampenda mke wake? Na mbona mke anampenda mume wake? Mbona watoto ni watiifu kwa wazazi wao? Na mbona wazazi wanawapenda sana watoto wao? Watu kweli wana nia za aina gani? Je, si kuweza kukidhi mipango na tamaa zao za ubinafsi? Kweli ni ya mpango wa usimamizi wa Mungu? Ni ya kazi ya Mungu? Ni ya kutimiza wajibu wa kiumbe? Waliomwamini Mungu kwanza na hawangepata uwepo wa Roho Mtakatifu hawawezi kupata kazi ya Roho Mtakatifu; imeamuliwa kwamba watu hawa wataangamizwa. Bila kujali kiasi cha upendo ambao mtu anao kwao, hauwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Shauku na upendo wa mwanadamu unawakilisha nia za mwanadamu, lakini haviwezi kuwakilisha nia za Mungu na haviwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Hata mtu akieneza kiasi kikubwa zaidi cha upendo ama huruma kwa hao watu wanaomwamini Mungu kwa jina na kujifanya kumfuata Yeye lakini hawajui ni nini maana ya kumwamini Mungu, bado hawatapata huruma ya Mungu ama kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hata kama watu wanaomfuata Mungu kwa dhati ni wenye akili ndogo na hawawezi kuelewa kweli nyingi, bado wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu mara kwa mara, lakini wale walio wa akili nzuri kidogo, lakini hawaamini kwa dhati hawawezi kabisa kupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Hakuna kabisa uwezekano wowote wa wokovu na watu hawa. Hata wakisoma na kusikiza ujumbe mara kwa mara ama kuimba sifa kwa Mungu, mwishowe hawataweza kubaki mpaka wakati wa pumziko. Iwapo mtu anatafuta kwa dhati hakuamuliwi na jinsi wengine wanamhukumu ama jinsi wengine karibu wanamwona, lakini kunaamuliwa na iwapo Roho Mtakatifu anamfanyia kazi na iwapo ana uwepo wa Roho Mtakatifu, na kunaamuliwa zaidi na iwapo tabia yake inabadilika na iwapo ana maarifa ya Mungu baada ya kupitia kazi ya Roho Mtakatifu kwa muda fulani; ikiwa Roho Mtakatifu anamfanyia mtu kazi, tabia ya mtu huyu itabadilika polepole, na mtazamo wake wa kumwamini Mungu utakua safi polepole. Bila kujali muda gani mtu anamfuata Mungu, kama wamebadilika, hii inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kwake. Kama hawajabadilika, inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwake. Hata kama hawa watu wanatoa huduma fulani, wanachochewa na nia zao za kupata bahati nzuri. Huduma ya mara kwa mara haiwezi kuchukua nafasi ya mabadiliko katika tabia yao. Hatimaye, bado wataangamizwa, kwani hakuna haja ya wale wanaotoa Huduma ndani ya ufalme, wala hakuna haja ya yeyote ambaye tabia yake haijabadilika kuwahudumia wale watu ambao wamekamilishwa na walio waaminifu kwa Mungu. Hayo maneno kutoka zamani, “Wakati mtu anamwamini Bwana, bahati inatabasamu kwa familia yake nzima,” yanafaa kwa Enzi ya Neema lakini hayana uhusiano na hatima ya mwanadamu. Yalifaa tu kwa hatua ya wakati wa Enzi ya Neema. Maana iliyokusudiwa ya maneno haya inaelekezwa kwa amani na baraka yakinifu ambazo watu wanafurahia; hayamaanishi kwamba familia nzima ya anayemwamini Bwana itaokolewa, wala hayamaanishi kwamba wakati mtu anapata bahati nzuri, familia yake nzima pia itaingia rahani. Iwapo mtu anapokea baraka ama kupata bahati mbaya inaamuliwa kulingana na kiini cha mtu, na haiamuliwi kulingana na asili ya kawaida ambayo mtu anashiriki na wengine. Ufalme hauna kabisa usemi kama huu ama kanuni kama hii. Kama mtu anaweza kusalimika hatimaye, ni kwa sababu amefikia mahitaji ya Mungu, na kama mtu hawezi hatimaye kubaki katika kipindi cha pumziko, ni kwa sababu mtu huyu hamtii Mungu na hajakidhi mahitaji ya Mungu. Kila mtu ana hatima inayofaa. Hatima hizi zinaamuliwa kulingana na asili ya kila mtu na hazihusiani kabisa. Mwenendo ovu wa mtoto hauwezi kuhamishwa kwa wazazi wake, na haki ya mtoto haiwezi kushirikishwa wazazi wake. Mwenendo ovu wa mzazi huwezi kuhamishwa kwa watoto wake, na haki ya mzazi haiwezi kushirikishwa watoto wake. Kila mtu anabeba dhambi zake husika, na kila mtu anafurahia bahati yake husika. Hakuna anayeweza kuchukua ya mwengine. Hii ni haki. Kwa mtazamo wa mwanadamu, iwapo wazazi wanapata bahati nzuri, watoto wao pia wanaweza, na watoto wakifanya maovu, wazazi wao lazima walipie dhambi zao. Huu ni mtazamo wa mwanadamu na njia ya mwanadamu ya kufanya vitu. Si mtazamo wa Mungu. Matokeo ya kila mtu yanaamuliwa kulingana na asili inayotoka kwa mwenendo wao, na daima yanaamuliwa inavyofaa. Hakuna awezaye kubeba dhambi za mwengine; hata zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kupokea adhabu badala ya mwengine. Hii ni thabiti. Malezi ya upendo ya mzazi kwa watoto wake hayamaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya watoto wake, wala upendo wenye utiifu wa mtoto kwa wazazi wake haumaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya wazazi wake. Hiyo ndiyo maana ya kweli ya maneno haya, “Basi kutakuwa na watu wawili shambani; mmoja wao atachukuliwa, na mwingine kuachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga katika kisiagi; mmoja atachukuliwa, na mwingine kuachwa.” Hakuna anayeweza kuwaingiza watoto wake watenda maovu rahani kwa msingi wa upendo wao wa kina kwa watoto wao, wala hakuna anayeweza kumwingiza mke wake (ama mume) rahani kwa sababu ya mwenendo wao wa haki. Hii ni kanuni ya utawala; hakuwezi kuwa na ubaguzi kwa mtu yeyote. Wanaotenda haki ni wanaotenda haki, na watenda maovu ni watenda maovu. Watenda haki watasalimika, na watenda maovu wataangamizwa. Watakatifu ni watakatifu; wao si wachafu. Wachafu ni wachafu, na hawana sehemu yoyote takatifu. Watu wote waovu wataangamizwa, na watu wote wa haki watasalimika, hata kama watoto wa watenda maovu wanafanya matendo ya haki, na hata kama wazazi wa mtu wa haki wanafanya matendo ya haki. Hakuna uhusiano kati ya mume anayeamini na mke asiyeamini, na hakuna uhusiano kati ya watoto wanaoamini na wazazi wasioamini. Ni aina mbili zisizolingana. Kabla ya kuingia rahani, mtu ana jamaa wa kimwili, lakini baada ya mtu kuingia rahani, mtu hana jamaa wa kimwili tena wa kuzungumzia. Wanaofanya wajibu wao na wasiofanya ni adui, wanaompenda Mungu na wanaomchukia Mungu ni wapinzani. Wanaoingia rahani na wale ambao wameangamizwa ni aina mbili ya viumbe wasiolingana. Viumbe wanaotimiza wajibu wao watasalimika, na viumbe wasiotimiza wajibu wao wataangamizwa; zaidi ya hayo, hii itadumu milele. Je, unampenda mume wako ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Je, unampenda mke wako ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Je, wewe ni mtiifu kwa wazazi wako wasioamini ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Mtazamo wa mwanadamu wa kumwamini Mungu ni sahihi ama la? Mbona unamwamini Mungu? Unataka kupata nini? Unampenda Mungu jinsi gani? Wasioweza kutimiza wajibu wao kama viumbe na hawawezi kufanya juhudi nzima wataangamizwa. Watu leo wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao, na pia ushirikiano wa damu, lakini baadaye hii yote itavunjwa. Waumini na wasioamini hawalingani ila wanapingana. Walio rahani wanaamini kwamba kuna Mungu na wanamtii Mungu. Wasiomtii Mungu wote watakuwa wameangamizwa. Familia hazitakuwa tena duniani; kunawezaje kuwa na wazazi na watoto ama mahusiano kati ya waume na wake? Kutoambatana kati ya imani na kutoamini kutakuwa kumevunja haya mahusiano ya kimwili!

Awali hakukuwa na familia miongoni mwa binadamu, ila mwanamume na mwanamke tu, watu wa aina mbili. Hakukuwa na nchi, sembuse familia, lakini kwa sababu ya upotovu wa mwanadamu, watu wa aina yote walijipanga katika koo binafsi, baadaye kukua kwa nchi na mataifa. Nchi na mataifa haya yalikuwa na familia ndogo binafsi, na kwa namna hii watu wa aina yote walisambazwa miongoni mwa jamii mbalimbali kulingana na tofauti ya lugha na mipaka igawayo. Kwa kweli, bila kujali idadi ya jamii zilizo duniani, binadamu wana babu mmoja pekee. Mwanzoni, kulikuwa na watu wa aina mbili tu, na aina hizi mbili zilikuwa mwanamume na mwanamke. Hata hivyo, kwa sababu ya maendeleo ya kazi ya Mungu, kupita kwa historia na mabadiliko ya kijiografia, kwa viwango mbalimbali aina hizi mbili za watu ziliendelezwa kuwa watu wa aina nyingine zaidi. Mwishowe, bila kujali idadi ya jamii zilizo katika binadamu, binadamu wote bado ni viumbe wa Mungu. Bila kujali jamii ambayo watu wako ndani, wote ni viumbe Wake; wote ni vizazi vya Adamu na Hawa. Hata kama hawajatengenezwa na mikono ya Mungu, ni vizazi vya Adamu na Hawa, ambao Mungu Mwenyewe aliumba. Bila kujali aina ambayo watu wako ndani, wote ni viumbe Wake; kwa sababu ni wa binadamu, ambao uliumbwa na Mungu, hatima yao ni hiyo ambayo binadamu wanapaswa kuwa nayo, na wamegawanywa kulingana na kanuni zinazopanga binadamu. Hiyo ni kusema kwamba, watenda maovu na wenye haki, hata hivyo, ni viumbe. Viumbe wafanyao maovu wataangamizwa hatimaye, na viumbe wafanyao matendo ya haki watasalimika. Huu ni mpangilio unaofaa sana wa viumbe wa aina hizi mbili. Watenda maovu hawawezi, kwa sababu ya kutotii kwao, kukataa kwamba ni viumbe wa Mungu lakini wameporwa na Shetani na hivyo hawawezi kuokolewa. Viumbe wa mwenendo wa haki hawawezi kutegemea ukweli kwamba watasalimika kukataa kwamba wameumbwa na Mungu na bado wamepokea wokovu baada ya kupotoshwa na Shetani. Watenda maovu ni viumbe wasiomtii Mungu; ni viumbe ambao hawawezi kuokolewa na tayari wameporwa na Shetani. Watu wanaotenda maovu ni watu pia; ni watu waliopotoshwa mno na watu wasioweza kuokolewa. Jinsi walivyo viumbe pia, watu wa mwenendo wa haki pia wamepotoshwa, lakini ni watu walio tayari kuacha tabia yao potovu na wanaweza kumtii Mungu. Watu wa mwenendo wa haki hawajajaa haki; badala yake, wamepokea wokovu na kuacha tabia yao potovu kumtii Mungu; watashikilia msimamo huo mwishowe, lakini hii si kusema kwamba hawajapotoshwa na Shetani. Baada ya kazi ya Mungu kuisha, miongoni mwa viumbe Wake wote, kutakuwa na wale watakaoangamizwa na wale watakaosalimika. Huu ni mwelekeo usioepukika wa kazi Yake ya usimamizi. Hakuna anayeweza kuyakataa haya. Watenda maovu hawawezi kusalimika; wanaomtii na kumfuata Mungu hadi mwishowe hakika watasalimika. Kwa sababu kazi hii ni ya usimamizi wa binadamu, kutakuwa na wale watakaobaki na wale watakaoondolewa. Haya ni matokeo tofauti ya watu wa aina tofauti, na hii ndiyo mipango inayofaa zaidi ya viumbe Wake. Mpango wa mwisho wa Mungu kwa mwanadamu ni kugawa kwa kuzivunja familia, kuyavunja mataifa na kuivunja mipaka ya kitaifa. Ni moja isiyo na familia na mipaka ya kitaifa, kwani mwanadamu, hata hivyo, ni wa babu mmoja na ni kiumbe wa Mungu. Kwa ufupi, viumbe wafanyao maovu wataangamizwa, na viumbe wanaomtii Mungu watasalimika. Kwa njia hii, hakutakuwa na familia, hakutakuwa na nchi na hasa hakutakuwa na mataifa katika pumziko la baadaye; binadamu wa aina hii ni aina takatifu kabisa ya binadamu. Adamu na Hawa waliumbwa awali ili mwanadamu aweze kutunza mambo yote duniani; mwanadamu awali alikuwa bwana wa vitu vyote. Nia ya Yehova ya kumuumba mwanadamu ilikuwa kumruhusu mwanadamu kuwa duniani na pia kutunza vitu vyote duniani, kwani mwanadamu awali hakuwa amepotoshwa na pia hakuweza kutenda maovu. Hata hivyo, baada ya mwanadamu kupotoshwa, hakuwa mtunzaji wa vitu vyote tena, na madhumuni ya wokovu wa Mungu ni kurejesha kazi hii ya mwanadamu, kurejesha ufahamu wa awali wa mwanadamu na utii wake wa awali; binadamu rahani watakuwa picha halisi ya matokeo ambayo kazi ya Mungu ya wokovu inatarajia kufikia. Ingawa hayatakuwa tena maisha kama yale ya bustani ya Edeni, kiini chake kitakuwa sawa; binadamu hawatakuwa tu nafsi yake ya awali isiyo potovu, lakini badala yake binadamu waliopotoshwa na kisha kupata wokovu. Watu hawa waliopata wokovu hatimaye (yaani, baada ya kazi Yake kuisha) wataingia rahani. Vivyo hivyo, matokeo ya wale walioadhibiwa pia yote yatafichuliwa mwishowe, na wataangamizwa tu baada ya kazi Yake kuisha. Hii ni kusema kwamba baada ya kazi Yake kuisha, watendao maovu na wale waliookolewa wote watafichuliwa, kwani kazi ya kufichua watu wa aina zote (bila kujali iwapo ni watenda maovu ama waliookolewa) itatekelezwa kwa watu wote wakati huo huo. Watenda maovu wataondolewa, na wale wanaoweza kubaki watafichuliwa wakati huo huo. Kwa hivyo, matokeo ya watu wa aina zote yatafichuliwa wakati huo huo. Hataliruhusu kwanza kundi la watu waliookolewa kuingia rahani kabla ya kuweka kando watenda maovu na kuwahukumu au kuwaadhibu kidogo kidogo; ukweli kwa kweli si hivyo. Wakati watenda maovu wanaangamizwa na waliosalimika wanaingia rahani, kazi Yake katika ulimwengu mzima itakuwa imemalizika. Hakutakuwa na utaratibu wa kipaumbele miongoni mwa wale wanaopata baraka na wale wanaopata taabu; wanaopokea baraka wataishi milele, na wanaopata taabu wataangamia milele. Hizi hatua mbili za kazi zitakamilika wakati huo huo. Ni hasa kwa sababu kuna watu wasiotii ndiyo maana haki ya watu wanaotii itafichuliwa, na ni hasa kwa sababu kuna wale waliopokea baraka ndiyo maana taabu ya wale wanaotenda maovu kwa sababu ya mwenendo wao mbovu itafichuliwa. Kama Mungu hakufichua watenda maovu, hao watu wanaomtii Mungu kwa dhati hawangeona jua; kama Mungu hangewapelekea wanaomtii katika hatima inayofaa, wasiomtii Mungu hawangeweza kupata adhabu wanayostahili. Huu ndio mwendo wa kazi Yake. Kama hangefanya kazi hii ya kuadhibu maovu na kutuza mazuri, viumbe Wake hawangeweza kuingia hatima zao husika. Mwanadamu aingiapo rahani, watenda maovu wataangamizwa, binadamu wote wataingia katika njia sahihi, na watu wa kila aina watakuwa na aina yao kulingana na kazi wanayopaswa kufanya. Hii tu ndiyo itakuwa siku ya binadamu kupumzika na mwenendo usioepukika wa maendeleo ya binadamu, na wakati tu binadamu wataingia rahani ndipo utimilifu mkubwa na wa mwisho wa Mungu utamalizika; hii itakuwa tamati ya kazi Yake. Hii kazi itamaliza maisha ya uharibifu ya kimwili ya binadamu, na itamaliza maisha ya binadamu potovu. Kutoka hapa binadamu wataingia katika ulimwengu mpya. Ingawa mwanadamu anaishi kimwili, kuna tofauti kubwa kati ya kiini cha maisha yake na kiini cha maisha ya binadamu wapotovu. Maana ya kuwepo kwake na maana ya kuwepo kwa binadamu wapotovu pia ni tofauti. Ingawa haya si maisha ya mtu wa aina mpya, inaweza kusemwa kuwa maisha ya binadamu ambao wamepata wokovu na maisha yenye ubinadamu na busara kurejeshwa. Hawa ni watu ambao hawakumtii Mungu wakati mmoja, na ambao walishindwa na Mungu wakati mmoja na baadaye kuokolewa na Yeye; hawa ni watu waliomwaibisha Mungu na baadaye wakamshuhudia. Uwepo wao, baada ya kupitia na kuendelea kuishi baada ya jaribio Lake, ni uwepo wa maana kubwa zaidi; ni watu waliomshuhudia Mungu mbele ya Shetani; ni watu wanaofaa kuishi. Watakaoangamizwa ni watu wasioweza kumshuhudia Mungu na hawafai kuishi. Uangamizi wao utakuwa kwa sababu ya mwenendo wao mwovu, na uangamizi ni hatima yao bora zaidi. Mwanadamu aingiapo baadaye katika ulimwengu mzuri, hakutakuwa na mahusiano kati ya mume na mke, kati ya baba na binti ama kati ya mama na mwana wa kiume ambayo mwanadamu anafikiria atapata. Wakati huo, mwanadamu atafuata aina yake, na familia itakuwa tayari imevunjwa. Baada ya kushindwa kabisa, Shetani hatawasumbua binadamu tena, na mwanadamu hatakuwa tena na tabia potovu ya kishetani. Wale watu wasiotii watakuwa wameangamizwa tayari, na wale watu wanaotii pekee ndio wataishi. Na basi familia chache sana zitasalimika bila kuharibika; mahusiano ya kimwili yatawezaje kuweko? Maisha ya kimwili ya zamani ya mwanadamu yatapigwa marufuku kabisa; mahusiano ya kimwili yatawezaje kuweko kati ya watu? Bila tabia potovu ya kishetani, maisha ya watu hayatakuwa tena maisha ya zamani ya siku zilizopita, lakini badala yake maisha mapya. Wazazi watapoteza watoto, na watoto watapoteza wazazi. Waume watapoteza wake, na wake watapoteza waume. Watu sasa wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao. Wakati wote watakuwa wameingia rahani hakutakuwa na mahusiano ya kimwili tena. Binadamu kama hawa tu ndio watakuwa wa haki na watakatifu, binadamu kama hawa tu ndio watamwabudu Mungu.

Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote, Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Uangamizi wa mwisho wa wale wana wa kutotii pia utafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp