Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

(Sehemu ya Kwanza)

Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo. Tukizungumzia umuhimu, ni nini kitu muhimu zaidi kwa kila muumini katika Mungu? Baadhi ya watu wanafikiri kwamba kitu muhimu zaidi ni kuyaelewa mapenzi ya Mungu; baadhi wanasadiki ni muhimu zaidi kula na kunywa maneno ya Mungu; baadhi wanahisi kitu muhimu zaidi ni kujijua wenyewe; wengine wanayo maoni kwamba kitu muhimu zaidi ni kujua namna ya kupata wokovu kupitia kwa Mungu, namna ya kumfuata Mungu, na namna ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Tutayaweka masuala haya yote pembeni kwa leo. Hivyo basi ni nini tunachozungumzia? Tunazungumzia mada kuhusu Mungu. Je, hii ndiyo mada muhimu zaidi kwa kila mtu? Maudhui ya mada kuhusu Mungu ni yapi? Bila shaka, mada hii haiwezi kamwe kutenganishwa na tabia ya Mungu, kiini cha Mungu na kazi ya Mungu. Hivyo leo, hebu tuzungumzie “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe.”

Tangu wakati binadamu walipoanza kumsadiki Mungu, wamekuwa wakikutana na mada kama vile kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Inapokuja kwa kazi ya Mungu, baadhi ya watu watasema: “Sisi ndio tunaofanyiwa kazi ya Mungu; tunaipitia kila siku, na hivyo basi tumezoeana nayo.” Na kuhusiana na tabia ya Mungu, baadhi ya watu watasema: “Tabia ya Mungu ni mada tunayoisoma, kuchunguza, na kuzingatia katika maisha yetu yote, hivyo basi tunafaa kuzoeana nayo.” Na kama ni Mungu Mwenyewe, baadhi ya watu watasema: “Mungu Mwenyewe ndiye tunayemfuata, tuliye na imani Kwake, na ndiye tunayemfuata, hivyo tumejuzwa pia kuhusu Yeye.” Mungu hajawahi kukomesha kazi Yake tangu uumbaji, wakati wote huu Ameendelea kuonyesha tabia Yake na kutumia njia mbalimbali kuonyesha neno Lake. Wakati huohuo, hajawahi kusita kujionyesha Yeye Mwenyewe na kiini Chake kwa mwanadamu, akionyesha mapenzi Yake kwa binadamu na kile Anachohitaji kutoka kwa huyo binadamu. Hivyo kutoka katika mtazamo wa moja kwa moja, mada hizi hazifai kuwa za kigeni kwa yeyote yule. Kwa watu wanaomfuata Mungu leo, hata hivyo, Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe kwa hakika ni mambo ambayo hayajulikani kwao. Kwa nini hali iko hivi? Kwa kadri binadamu anapopitia kazi ya Mungu, anawasiliana pia na Mungu, na kuwafanya kuhisi ni kana kwamba wanaelewa tabia ya Mungu au wanajua sehemu kidogo kuhusu vile inavyofanana. Hivyo basi, binadamu hafikiri kuwa yeye ni mgeni katika kazi ya Mungu au tabia ya Mungu. Badala yake, binadamu anafikiri ni mwenyeji kabisa na Mungu na anaelewa mengi kuhusu Mungu. Lakini kulingana na hali ya sasa, uelewa wa watu wengi kumhusu Mungu umezuiliwa katika kile walichosoma vitabuni, na upana mfinyu wa kile walichopitia wao binafsi, wakiwa wamezuiliwa na kufikiria kwao, na zaidi ya yote, ukiwa umewekewa mipaka ya ukweli wanaoweza kuona kwa macho yao binafsi. Haya yote yapo mbali sana na Mungu Mwenyewe wa kweli. Sasa huu umbali upo “mbali” vipi? Pengine binadamu mwenyewe hana hakika, au pengine binadamu anayo dhana, ana fununu kiasi—lakini kwake Mungu Mwenyewe, uelewa wa binadamu kumhusu Yeye u mbali sana na kiini cha Mungu Mwenyewe wa kweli. Hii ndiyo maana tunahitajika kutumia mada kama “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” ili kuwasilisha ujumbe huu hatua kwa hatua na kwa njia mahususi.

Kwa hakika, tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haijafichika, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi kimakusudi kujaribu kujificha Mwenyewe ili watu wasiweze kumjua Yeye au kumwelewa Yeye. Tabia ya Mungu siku zote imekuwa wazi na siku zote imekuwa ikitazama kila mtu kwa njia ya uwazi. Katika usimamizi wa Mungu, Mungu hufanya kazi Yake akitazama kila mmoja; na kazi Yake ndiyo inafanywa kwa kila mtu. Anapofanya kazi hii, Anafichua bila kusita tabia Yake, huku Akitumia bila kusita kiini Chake na kile Anacho na alicho kuongoza na kukimu kila mmoja. Katika kila enzi na kila awamu, licha ya kama hali ni nzuri au mbaya, tabia ya Mungu siku zote iko wazi kwa kila mtu binafsi, na vile vitu Anavyomiliki na uwepo Wake siku zote viko wazi kwa kila mtu binafsi, kwa njia sawa kwamba maisha Yake yanamtoshelezea mwanadamu kila wakati na bila kusita na kumsaidia mwanadamu. Licha ya haya yote, tabia ya Mungu inabakia fiche kwa baadhi ya watu. Kwa nini iko hivyo? Ni kwa sababu ingawaje watu hawa wanaishi ndani ya kazi ya Mungu na wanamfuata Mungu, hawajawahi kutafuta kuelewa Mungu au kutaka kumjua Mungu, sikwambii hata kumkaribia Mungu. Kwa watu hawa, kuelewa tabia ya Mungu kunamaanisha mwisho wao wawadia; kwa maanisha karibu wanahukumiwa na kushtakiwa na tabia ya Mungu. Hivyo basi, watu hawa hawajawahi kutamani kuelewa Mungu au tabia Yake, na hawatamani uelewa au maarifa ya kina ya mapenzi ya Mungu. Hawanuii kufahamu mapenzi ya Mungu kupitia ushirikiano wa kimakusudi—wanafurahia tu milele na hawachoki kufanya mambo wanayotaka kuyafanya; kusadiki kwa Mungu wanayetaka kusadiki Kwake; kusadiki kwa Mungu aliyepo tu katika fikira zao, Mungu aliyepo tu katika dhana zao; na kusadiki kwa Mungu asiyeweza kutenganishwa na wao katika maisha yao ya kila siku. Na kwake Mungu Mwenyewe wa kweli, wanapuuza kabisa, hawataki kusikia mambo ya Mungu na hawana tamanio la kumwelewa Yeye, kumtilia maanani Yeye, na hata hawana nia kidogo ya kuwa karibu zaidi na Yeye. Wanayatumia tu maneno ambayo Mungu anayaonyesha ili kuweza kujipamba, kujiandaa upya. Kwa wao, hilo tayari linawafanya kuwa waumini wenye mafanikio na watu walio na imani kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Ndani ya mioyo yao, wanaongozwa na kufikiria kwao, dhana zao, na hata ufasili wao binafsi wa Mungu. Mungu Mwenyewe wa kweli, kwa mkono mwingine, hana chochote kuhusiana na wao. Kwa sababu pindi wanapomwelewa Mungu Mwenyewe wa kweli, kuelewa tabia ya Mungu ya kweli, na kuelewa kile Mungu anacho na alicho, hii inamaanisha kwamba vitendo vyao, imani yao, na yale yote wanayoyafuatilia yatashutumiwa. Na ndiyo maana hawako radhi kukielewa kiini cha Mungu, na ndiyo maana wanasitasita na hawako radhi kutafuta kwa bidii au kuomba kumwelewa zaidi Mungu, kupata kujua zaidi kuhusu mapenzi Yake Mungu, na kuelewa kwa njia bora zaidi tabia ya Mungu. Afadhali Mungu kwao awe kitu kilichotungwa, kisicho na chochote na kibaya. Afadhali kwao Mungu awe mtu ambaye yupo hasa vile ambavyo wamemfikiria Yeye, Anayeweza kunyenyekea mbele zao, Asiyeishiwa na ujazo na Anayepatikana siku zote. Wanapotaka kufurahia neema ya Mungu, wanamuomba Mungu kuwa hiyo neema. Wanapohitaji baraka za Mungu, wanamuomba Mungu kuwa baraka hizo. Wanapokabiliwa na dhiki, wanamwomba Mungu kuwatia wao moyo, na kuwa usalama wao. Maarifa ya watu hawa kumhusu Mungu imebakia palepale pa mipaka ya neema na baraka. Uelewa wao wa kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu umezuiliwa pia na kufikiria kwao na vilevile barua na mafundisho ya kidini tu. Lakini wapo baadhi ya watu walio na hamu ya kuielewa tabia ya Mungu, wanaotaka kumwona Mungu Mwenyewe kwa kweli, na kuielewa tabia ya Mungu kwa kweli na kile Anacho na alicho. Watu hawa wanautafuta uhalisia wa ukweli na wokovu wa Mungu na wanatafuta kupokea ushindi, wokovu, na utimilifu wa Mungu. Watu hawa wanaitumia mioyo yao kulisoma neno la Mungu, wanaitumia mioyo yao kuthamini hali na kila mtu, tukio, au kitu ambacho Mungu amewapangia, na kuomba na kutafuta kwa uaminifu. Kile wanachotaka zaidi ni kuyajua mapenzi ya Mungu na kuielewa tabia ya kweli na kiini cha Mungu. Hivi ndivyo ilivyo ili wasiweze tena kumkosea Mungu, na kupitia kwa mambo waliyoyapitia, waweze kuona upendo zaidi wa Mungu na upande Wake wa kweli. Iko hivyo pia ili Mungu halisi na wa kweli ataweza kuwepo ndani ya mioyo yao, na ili Mungu atakuwa na nafasi katika mioyo yao, kiasi cha kwamba hawatakuwa wakiishi tena miongoni mwa kufikiria, dhana, au hali ya kuyaepuka mambo. Kwa watu hawa, sababu inayowafanya kuwa na tamanio kuu la kuielewa tabia ya Mungu na kiini Chake ni kwa sababu tabia ya Mungu na kiini Chake ni mambo ambayo mwanadamu anaweza kuyahitaji wakati wowote katika uzoefu wao, mambo yanayojaza uhai katika maisha yao yote walioishi. Pindi wanapoielewa tabia ya Mungu, wataweza kumheshimu sana kwa njia bora zaidi, kushirikiana kwa njia bora zaidi na kazi ya Mungu, na kuyaweka zaidi katika fikira mapenzi ya Mungu na kutekeleza wajibu wao kwa njia bora zaidi wakitumia uwezo wao. Hawa ndio watu wa aina mbili inapokuja katika mielekeo yao kwa tabia ya Mungu. Watu wa aina ya kwanza hawataki kuielewa tabia ya Mungu. Ingawaje wanasema wanataka kuielewa tabia ya Mungu, kupata kumjua Mungu Mwenyewe, kuona kile Mungu anacho na alicho, na kushukuru kwa dhati mapenzi ya Mungu, ndani yao kabisa wanaona afadhali Mungu asikuwepo. Ni kwa sababu watu wa aina hii wanakosa kumtii Mungu kila wakati na wanampinga; wanapigana na Mungu kwa sababu ya vyeo vilivyo ndani ya mioyo yao na mara nyingi wanashuku na hata kukataa uwepo wa Mungu. Hawataki kuruhusu tabia ya Mungu au kuacha Mungu mwenyewe wa kweli kumiliki mioyo yao. Wanataka tu kutosheleza matamanio, kufikiria, na maono yao binafsi. Hivyo basi, watu hawa wanaweza kumsadiki Mungu, kumfuata Mungu, na hata wanaweza kutupilia mbali familia na kazi zao kwa sababu Yake Yeye, lakini hawasitishi njia zao za maovu. Baadhi yao hata huiba au kubadhiri sadaka au kumlaani Mungu kisirisiri, huku wengine wakiweza kutumia vyeo vyao kushuhudia mara kwa mara kuhusu wao wenyewe, kujiongezea zaidi umaarufu wao, na kushindana na Mungu kwa ajili ya watu na hadhi. Wanatumia mbinu na njia mbalimbali kuwafanya watu kuwaabudu, kujaribu mara kwa mara kuwa na ufuasi mkubwa wa watu na kutaka kuwadhibiti watu hao. Baadhi hata hupotosha kimakusudi watu na kuwafanya kufikiria kwamba wao ni Mungu ili waweze kuchukuliwa kama Mungu. Hawawezi katu kuwaambia watu kwamba wamepotoshwa, kwamba pia wao wamepotoka na wana kiburi, na hivyo basi hawafai kuwaabudu, na kwamba haijalishi watafanya vyema kiasi kipi, haya yote ni kutokana na utukuzaji wa Mungu na kile wanachostahili kufanya kwa kweli. Kwa nini hawasemi mambo haya? Kwa sababu wana hofu kuu ya kupoteza nafasi yao ndani ya mioyo ya watu. Hii ndiyo maana watu kama hao hawamtukuzi Mungu katu na katu hawamshuhudii Mungu, kwani hawajawahi kujaribu kumwelewa Mungu. Wanaweza kumjua Mungu kama hawamwelewi? Haiwezekani! Hivyo, ingawa maneno katika mada “kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu mwenyewe” yanaweza kuwa rahisi, maana yao ni tofauti kwa kila mmoja. Kwa mtu anayekosa kumtii Mungu mara kwa mara, na anampinga Mungu na ni mkatili kwa Mungu, yanamaanisha shutuma; huku kwa mtu anayefuatilia uhalisia wa kweli na mara nyingi anakuja mbele ya Mungu kutafuta mapenzi ya Mungu, maneno hayo bila shaka ni kama samaki na maji. Hivyo miongoni mwenu, wakati baadhi yenu mnaposikiza mazungumzo ya tabia ya Mungu na kazi ya Mungu, wanaanza kuumwa na kichwa, mioyo yao inajaa upinzani, na wanakuwa katika hali isiyo na utulivu kabisa. Lakini kuna wengine miongoni mwenu wanaofikiria: Mada hii ndiyo hasa Ninayohitaji, kwa sababu mada hii ni yenye manufaa sana kwangu. Ni sehemu ambayo haiwezi kukosekana katika uzoefu wangu wa maisha; ni swali ambalo halijapata jibu bado, msingi wa imani kwa Mungu, na jambo ambalo mwanadamu hawezi kufikiria kuliacha. Kwenu nyote, mada hii inaweza kuonekana kuwa karibu na mbali, isiyojulikana ilhali inayozoeleka. Lakini haijalishi ni nini, hii ni mada ambayo kila mmoja aliyeketi hapa, lazima aisikilize, aijue, na lazima aielewe. Haijalishi ni vipi utakavyoishughulikia, haijalishi ni vipi utakavyoiangalia au utakavyoipokea, lakini umuhimu wa mada hii huwezi kupuuzwa.

Mungu amekuwa akifanya kazi Yake tangu Alipomuumba mwanadamu. Mwanzoni, kazi ilikuwa rahisi sana, lakini hata hivyo, ingali ilikuwa na maonyesho ya kiini na tabia ya Mungu. Ingawa kazi ya Mungu sasa imepandishwa daraja, na Yeye akitia kiwango kikubwa mno cha kazi thabiti kwa kila mmoja anayemfuata Yeye, na kuonyesha kiwango kikubwa cha neno Lake, kuanzia mwanzo hadi sasa, nafsi ya Mungu imekuwa ikifichwa kutoka kwa mwanadamu. Ingawaje amekuwa mwili mara mbili, kuanzia wakati wa simulizi za biblia hadi kwa siku za kisasa, nani amewahi kuona nafsi halisi ya Mungu? Kutokana na uelewa wenu, yupo mtu amewahi kuona nafsi halisi ya Mungu? La. Hakuna aliyewahi kuona nafsi halisi ya Mungu, kumaanisha hakuna aliyewahi kuona nafsi ya kweli ya Mungu. Hili ni jambo ambalo kila mmoja anakubaliana nalo. Hivi ni kusema, nafsi halisi ya Mungu, au Roho wa Mungu, amefichwa kutoka kwa binadamu wote, wakiwemo Adamu na hawa, ambao Aliwaumba, na akiwemo Ayubu mwenye haki, ambaye alikuwa Amemkubali. Hata wao hawakuona nafsi halisi ya Mungu. Lakini kwa nini Mungu anaficha kimakusudi nafsi Yake halisi? Baadhi ya watu husema: “Mungu anaogopa kuwaogofya watu.” Wengine husema: “Mungu huficha nafsi Yake halisi kwa sababu binadamu ni mdogo sana na Mungu ni mkubwa sana; wanadamu hawaruhusiwi kumwona Yeye, la sivyo watakufa.” Wapo pia wale wanaosema: “Mungu ameshughulika sana akisimamia kazi Yake kila siku, huenda Asiwe na muda wa kuonekana na kuruhusu watu kumwona Yeye.” Haijalishi ni nini mnachosadiki, Ninayo hitimisho hapa. Hitimisho hilo ni nini? Ni kwamba Mungu hataki hata watu kuona nafsi Yake halisi. Akiwa amefichwa kutoka kwa binadamu ni kitu ambacho Mungu anafanya kimakusudi. Kwa maneno mengine, ni nia ya Mungu kwa watu kutoona nafsi Yake halisi. Hili linafaa kuwa wazi kwa wote sasa. Kama Mungu hajawahi kuonyesha nafsi Yake kwa yeyote, basi mnafikiria nafsi ya Mungu ipo? (Ipo.) Bila shaka ipo. Uwepo wa nafsi ya Mungu haupingiki. Lakini kuhusu nafsi ya Mungu ni kubwa vipi au inafanana vipi, haya ni maswali ambayo mwanadamu anafaa kuchunguza? La. Jibu ni la. Kama nafsi ya Mungu si mada ambayo tunafaa kuchunguza, basi ni swali lipi ambalo tunafaa kuchunguza? (Tabia ya Mungu.) (Kazi ya Mungu.) Kabla hatujaanza kuwasiliana mada hii rasmi, hata hivyo, hebu turudi katika kile tulichokuwa tukikizungumzia muda mfupi uliopita: Kwa nini Mungu hajawahi kuonyesha nafsi Yake kwa mwanadamu? Kwa nini Mungu anaficha kimakusudi nafsi Yake kutoka kwa mwanadamu? Kunayo sababu moja tu, nayo ni: Ingawaje binadamu aliyeumbwa amepitia miaka elfu na elfu ya kazi ya Mungu, hakuna hata mtu mmoja anayejua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na kiini cha Mungu. Watu kama hao, mbele ya macho ya Mungu, ni upinzani kwake Yeye, na Mungu hatajionyesha kwa watu walio wakatili kwake Yeye. Hii ndiyo sababu ya pekee mbona Mungu hajawahi kumwonyesha binadamu nafsi Yake na ndiyo sababu anaikinga yeye kimakusudi nafsi Yake dhidi yao. Sasa mnaelewa kuhusu umuhimu wa kujua tabia ya Mungu?

Tangu kuwepo kwa usimamizi wa Mungu, siku zote amejitolea kabisa katika kutekeleza kazi Yake. Licha ya kuficha nafsi Yake kutoka kwao, siku zote Amekuwa katika upande wa binadamu, akiwafanyia kazi, akionyesha tabia Yake, akiongoza binadamu wote na kiini Chake, na kufanya kazi Yake kwa kila mmoja kupitia nguvu Zake, hekima Yake, na mamlaka Yake, hivyo akiileta Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na sasa Enzi ya Ufalme katika uwepo. Ingawaje Mungu huificha nafsi Yake kutoka kwa binadamu, tabia Yake, uwepo Wake na miliki Yake, na mapenzi Yake kwa binadamu yanafichuliwa bila wasiwasi wowote kwa binadamu kwa minajili ya kuona na kupitia hali hiyo. Kwa maneno mengine, ingawaje binadamu hawawezi kumwona au kumgusa Mungu, tabia na kiini cha Mungu ambacho binadamu wamekuwa wakigusana nacho ni maonyesho kabisa ya Mungu Mwenyewe. Je, hayo si kweli? Licha ya ni mbinu gani au ni kutoka katika mtazamo gani Mungu hufanya kazi Yake, siku zote Anawakaribisha watu kulingana na utambulisho Wake wa kweli, akifanya kile ambacho Anafaa kufanya na kusema kile Anachofaa kusema. Haijalishi ni nafasi gani Mungu anazungumzia kutoka—Anaweza kuwa amesimama kwenye mbingu ya tatu, au amesimama akiwa mwili Wake, au hata kama mtu wa kawaida—siku zote Anaongea kwa binadamu kwa moyo Wake wote na kwa akili Zake zote, bila uongo na bila ufichaji wowote. Wakati Anapotekeleza kazi Yake, Mungu huonyesha neno Lake na tabia Yake, na huonyesha kile Anacho na alicho, bila kuficha chochote. Anamwongoza mwanadamu na maisha Yake na uwepo Wake na miliki yake. Hivi ndivyo binadamu alivyoishi katika Enzi ya Sheria—enzi asilia ya binadamu—akiongozwa na Mungu asiyeonekana na asiyegusika.

Mungu alipata mwili kwa mara ya kwanza baada ya Enzi ya Sheria, hali ya kupata mwili iliyodumu kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Kwa mwanadamu, miaka thelathini na mitatu na nusu ni muda mrefu? (Si mrefu sana.) Kwa sababu urefu wa maisha ya mwanadamu ni mirefu kuliko miaka thelathini na fulani, huu si muda mrefu kwa mwanadamu. Lakini kwa Mungu mwenye mwili, miaka hii thelathini na mitatu na nusu ilikuwa mirefu mno. Aligeuka na kuwa mtu—mtu wa kawaida aliyetekeleza kazi na agizo la Mungu. Hii ilimaanisha kwamba lazima angefanya kazi ambayo mtu wa kawaida asingeweza kufanya, huku akivumilia mateso ambayo binadamu wa kawaida hawezi kuvumilia. Kiwango cha mateso aliyovumilia Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, kuanzia mwanzo wa kazi Yake hadi wakati Aliposulubishwa kwenye msalaba, huenda kisiwe ni kitu watu wa leo wangeweza kushuhudia wao binafsi, lakini mnaweza angaa kutambua kiasi kupitia hadithi zilizo kwenye Biblia? Licha ya ni maelezo mangapi yaliyopo kwenye ukweli huu uliorekodiwa, kwa ujumla, kazi ya Mungu katika kipindi hiki kilijaa ugumu na mateso. Kwa mwanadamu aliyepotoka muda wa miaka thelathini na mitatu na nusu si mrefu; mateso kidogo si jambo la kutisha. Lakini kwa Mungu mtakatifu asiye na doa, ambaye lazima avumilie dhambi zote za binadamu, na kula, kulala na kuishi na watenda dhambi, maumivu haya ni mengi mno. Yeye ndiye Muumba, Bwana wa viumbe vyote na Mtawala wa vitu vyote, lakini Alipokuja duniani alilazimika kuvumilia unyanyasaji na ukatili wa wanadamu waliopotoka. Ili kuikamilisha kazi Yake na kuokoa binadamu kutoka kwa taabu, Alilazimika kushutumiwa na binadamu, na kuvumilia dhambi za wanadamu wote. Kiwango cha mateso aliyopitia hakiwezi kwa kweli kueleweka au kutambulika na watu wa kawaida. Mateso haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Yanasimamia udhalilishaji Alioteseka na gharama Aliyolipia kwa sababu ya wokovu wa binadamu, kukomboa dhambi zake, na kukamilisha awamu hii ya kazi Yake. Yanamaanisha binadamu angekombolewa kutoka katika msalaba na Mungu. Hii ndiyo gharama iliyolipwa kwa damu, kwa maisha, gharama ambayo viumbe walioumbwa hawawezi kumudu. Ni kwa sababu Anacho kiini cha Mungu na Amejihami na kile Mungu anacho na alicho, ndiyo maana Anaweza kuvumilia aina hii ya mateso na aina hii ya kazi. Hili ni jambo ambalo hakuna kiumbe aliyeumbwa anaweza kufanya badala Yake. Hii ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema na ufunuo wa tabia Yake. Je, hii inafichua chochote kuhusu kile Mungu anacho na alicho? Je, wanadamu wanastahili kuijua?

Katika enzi hiyo, japokuwa mwanadamu hakuiona nafsi ya Mungu, alipokea sadaka ya Mungu dhidi ya dhambi zake na akakombolewa kutoka kwenye msalaba na Mungu. Huenda mwanadamu awe amezoeana na kazi aliyofanya Mungu katika Enzi ya Neema, lakini yupo yeyote aliyezoeana na tabia na mapenzi yalionyeshwa na Mungu katika kipindi hiki? Binadamu anajua tu kuhusu maudhui ya kazi ya Mungu katika enzi tofauti katika vipindi mbalimbali, au anajua hadithi zinazohusiana na Mungu zilizofanyika kwa wakati mmoja na ule Mungu alikuwa akitekeleza kazi Yake. Maelezo haya na hadithi ni kwa ukweli zaidi taarifa fulani tu au hadithi za kumbukumbu kuhusu Mungu, na vyote hivi havina chochote kuhusiana na tabia na kiini cha Mungu. Hivyo haijalishi ni hadithi ngapi watu wanajua kuhusu Mungu, haimaanishi kwamba wanao uelewa wa kina na maarifa kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake. Kama hali ilivyokuwa katika Enzi ya Sheria, ingawaje watu kutoka Enzi ya Neema walikuwa wamepitia mtagusano wa karibu sana na wa kikweli na Mungu wa mwili, maarifa yao kuhusu Mungu na kiini cha Mungu yalikuwa kweli mambo yasiyokuwepo.

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu akawa mwili tena, kwa njia sawa na ile Aliyotumia mara ya kwanza. Katika kipindi hiki cha kazi, Mungu angali anaonyesha bila kusita neno Lake, anafanya kazi anayofaa kufanya na kuonyesha kile Anacho na alicho. Wakati huohuo, Anaendelea kuvumilia na kustahili na kutotii na kutojua kwa binadamu. Je, Mungu hafichui kila wakati tabia Yake na kuonyesha mapenzi yake katika kipindi hiki cha kazi pia? Hivyo basi, kuanzia uumbaji wa binadamu hadi sasa, tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki Zake, na mapenzi Yake, siku zote yamekuwa wazi kwa kila mmoja. Mungu hajawahi kuficha kimakusudi kiini Chake, tabia Yake au mapenzi Yake. Ni vile tu mwanadamu hajali kuhusu kile ambacho Mungu anafanya, mapenzi Yake ni yapi—ndio maana uelewa wa binadamu kumhusu Mungu ni finyu mno. Kwa maneno mengine, wakati Mungu anaficha nafsi Yake, Yeye pia Anasimama kando ya mwanadamu kila wakati, akionyesha waziwazi mapenzi Yake, tabia Yake na kiini chake halisi siku zote. Kimsingi, nafsi ya Mungu pia iko wazi kwa watu, lakini kutokana na upofu na kutotii kwa binadamu, siku zote hawawezi kuuona kuonekana kwa Mungu. Hivyo kama hali iko hivyo, basi si kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe kunafaa kuwa rahisi mno kwa kila mmoja? Hili ni swali gumu sana kujibu, sivyo? Mnaweza kusema ni rahisi, lakini wakati watu wengine wanatafuta kumjua Mungu, hatimaye hawamjui Yeye au kupata uelewa wa wazi kumhusu Yeye—siku zote ni jambo lililojaa ukungu na lisiloeleweka. Lakini mkisema si rahisi, hilo si sahihi vilevile. Baada ya kuwa mlengwa wa kazi ya Mungu kwa muda mrefu, kila mmoja anafaa, kupitia uzoefu wake, kuwa amepitia kwa kweli mambo mbalimbali na Mungu. Anafaa kuwa amehisi Mungu angaa kwa kiwango fulani katika moyo wake au awali amegongana na Mungu katika kiwango cha kiroho, hivyo anafaa angalau kuwa na ufahamu kiasi tambuzi kuhusu tabia ya Mungu au kupata uelewa fulani kumhusu Yeye. Kuanzia wakati binadamu alianza kumfuata Mungu hadi sasa, mwanadamu amepokea mengi mno, lakini kutokana na sababu za aina zote—uhodari wa kimasikini ya kibinadamu, kutojua, uasi, na nia mbalimbali—wanadamu wamepoteza mambo mengi mno. Je, Mungu hajampatia mwanadamu mali ya kutosha? Ingawaje Mungu huficha nafsi Yake kutoka kwa wanadamu, Anawatosheleza mahitaji yao kwa kile Anacho na alicho, na hata maisha Yake; maarifa ya binadamu ya Mungu hayafai kuwa vile yalivyo tu sasa. Ndiyo maana Nafikiri inahitajika kuwa na ushirika zaidi na nyinyi kuhusu mada ya kazi ya Mungu, kuhusu tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Kusudio ni ili miaka elfu ya utunzaji na fikira ambayo Mungu amemwagia binadamu isije ikaisha bure bilashi, na ili mwanadamu aweze kuelewa kwa dhati na kutambua mapenzi ya Mungu kwake. Ni ili watu waweze kusonga mbele kwenye hatua mpya ya maarifa yao kumhusu Mungu. Itaweza pia kumrudisha Mungu katika nafasi Yake inayofaa kwenye mioyo ya watu yaani kumfanyia Yeye haki.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp