Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

(Sehemu ya Tatu)

Kifuatacho tutaangalia mfano uliozungumziwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.

3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea

Mat 18:12-14 Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea? Na iwapo atampata, kweli nawaambia, anafurahi zaidi kwa sababu ya huyo kondoo, kuliko wao tisini na tisa ambao hawakupotea. Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.

Hii ni sitiari—watu wanapata hisia gani kutoka katika dondoo hii? Namna ambavyo sitiari hii inaelezwa inatumia mbinu za lugha katika lugha ya binadamu; ni kitu kilicho ndani ya mawanda ya maarifa ya binadamu. Kama Mungu angekuwa amesema kitu kinachofanana katika Enzi ya Sheria, watu wangehisi kwamba hakikuambatana na Alichokuwa Mungu, lakini Mwana wa Adamu alipoonyesha kifungu hiki katika Enzi ya Neema, kilionekana cha kufariji, chenye uzuri, na kilicho karibu kwa watu. Mungu alipokuwa mwili, Alipoonekana katika umbo la binadamu, Alitumia sitiari inayofaa sana kuonyesha sauti ya roho Yake katika ubinadamu. Sauti hii iliwakilisha sauti binafsi ya Mungu na kazi Aliyotaka kufanya katika enzi hiyo. Pia iliwakilisha mtazamo ambao Mungu alikuwa nao kwa watu katika Enzi ya Neema. Tukiangalia kutoka kwa mtazamo wa mwelekeo wa Mungu kwa watu, Alimfananisha kila mtu na kondoo. Kama kondoo amepotea, Atafanya kila awezalo ili kumpata. Hii inawakilisha kanuni ya kazi ya Mungu miongoni mwa binadamu wakati huu katika mwili. Mungu aliutumia mfano huu kufafanua uamuzi na mwelekeo Wake katika kazi hiyo. Haya ndiyo yaliyokuwa manufaa ya Mungu kuwa mwili: Angeweza kutumia vizuri maarifa ya binadamu na kutumia lugha ya binadamu kuongea na watu, kuonyesha mapenzi Yake. Aliewalezea au “kuwatafsiria” binadamu lugha Yake ya maana sana, ya kiungu ambayo watu walipata ugumu kuelewa kupitia lugha ya binadamu, kwa njia ya kibinadamu. Hii iliwasaidia watu kuelewa mapenzi Yake na kujua kile Alichotaka kufanya. Angeweza pia kuwa na mazungumzo na watu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kwa kutumia lugha ya kibinadamu, na kuwasiliana na watu kwa njia waliyoelewa. Aliweza pia kuongea na kufanya kazi kwa kutumia lugha na maarifa ya kibinadamu ili watu waweze kuhisi wema na ukaribu wa Mungu, ili wangeweza kuuona moyo Wake. Mnaona nini katika hili? Kwamba hakuna kuzuiliwa katika maneno na vitendo vya Mungu? Namna watu wanavyoona, hakuna njia ambayo Mungu angetumia maarifa ya kibinadamu, lugha, au njia za kuongea ili kuzungumza kuhusu kile ambacho Mungu Mwenyewe alitaka kusema, kazi Aliyotaka kufanya, au kuonyesha mapenzi Yake mwenyewe; huku ni kufikiria ambako si sahihi. Mungu alitumia aina hii ya sitiari ili watu waweze kuhisi ule uhalisi na uaminifu wa Mungu, na kuona mwelekeo Wake kwa watu katika kipindi hicho cha muda. Mfano huu uliwazindua watu waliokuwa wakiishi chini ya sheria kwa muda mrefu kutoka katika ndoto, na vilevile uliweza kuhemsha kizazi baada ya kizazi cha watu walioishi katika Enzi ya Neema. Kwa kukisoma kifungu cha mfano huu, watu wanajua uaminifu wa Mungu katika kuwaokoa binadamu na wanaelewa uzito wa mwanadamu katika moyo Wake.

Hebu tuangalie kwa mara nyingine sentensi ya mwisho katika dondoo hii: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Haya yalikuwa maneno binafsi ya Bwana Yesu, au yalikuwa maneno ya Baba Yake aliye mbinguni? Kwa juujuu, yaonekana alikuwa Bwana Yesu akiongea, lakini mapenzi Yake yanawakilisha mapenzi ya Mungu Mwenyewe, na ndiyo maana Akasema: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Watu wakati huo walimtambua tu Baba aliye mbinguni kama Mungu, na mtu huyu waliyeona mbele ya macho yao alikuwa ametumwa tu na Yeye, na hakuweza kuwakilisha Baba aliye mbinguni. Ndiyo maana Bwana Yesu alilazimika kusema hivyo vilevile, ili waweze kuhisi kwa kweli mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, na kuhisi ule uhalali na usahihi wa kile Alichosema. Hata ingawa jambo hili lilikuwa jepesi kusema, lilikuwa lenye utunzaji mwingi na lilifichua unyenyekevu na ufiche wa Bwana Yesu. Bila kujali kama Mungu alikuwa mwili au Alifanya kazi katika ulimwengu wa kiroho, Aliujua moyo wa binadamu kwa njia bora zaidi, na Alielewa kwa njia bora zaidi kile watu walichohitaji, Alijua ni nini watu walikuwa na wasiwasi kuhusu, na kile kilichowakanganya, hivyo Akaongeza mstari huu. Mstari huu uliangazia tatizo lililofichika ndani ya mwanadamu: Watu hawakuamini kile ambacho Mwana wa Adamu alisema, hivi ni kusema kwamba, Bwana Yesu alipokuwa akiongea Alilazimika kuongeza: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Ni katika kauli hii tu ndiyo maneno Yake yangezaa matunda, kuwafanya watu kuamini usahihi wao na kuboresha kiwango cha kuaminika kwa maneno hayo. Hii inaonyesha kwamba Mungu alipokuwa Mwana wa Adamu wa kawaida, Mungu na mwanadamu walikuwa na uhusiano mgumu sana, na kwamba hali ya Mwana wa Adamu ilikuwa ya kuaibisha mno. Inaonyesha pia namna ambavyo hadhi ya Bwana Yesu ilivyokuwa isiyo na maana miongoni mwa binadamu wakati huo. Aliposema haya, kwa hakika ilikuwa ni kuwaambia watu: Mnaweza kuwa na uhakika kwamba—haya hayawakilishi yale yaliyo moyoni Mwangu mwenyewe, lakini ni mapenzi ya Mungu aliye mioyoni mwenu. Kwa mwanadamu, jambo hili halikuwa la kejeli? Ingawa Mungu kufanya kazi katika mwili kulikuwa na manufaa mengi ambayo Hakuwa nayo katika nafsi Yake, Alilazimika kustahimili shaka na kukataliwa na wao pamoja na kutojali na kutochangamka kwao. Yaweza kusemekana kwamba mchakato wa kazi ya Mwana wa Adamu ulikuwa mchakato wa kupitia kukataliwa na mwanadamu, na mchakato wa kupitia mwanadamu akishindana dhidi Yake. Zaidi ya hayo, ulikuwa ni mchakato wa kufanya kazi ili kuendelea kushinda imani ya mwanadamu na kumshinda mwanadamu kupitia kile Alicho nacho na kile Alicho, kupitia kiini Chake binafsi halisi. Haikuwa sana kwamba Mungu mwenye mwili Alikuwa akipigana vita vikali dhidi ya Shetani; ilikuwa zaidi kwamba Mungu aligeuka na kuwa binadamu wa kawaida na kuanzisha mapambano pamoja na wale wanaomfuata Yeye, na katika mapambano haya Mwana wa Adamu alikamilisha kazi Yake kwa unyenyekevu Wake, pamoja na kile Alicho nacho na kile Alicho, na upendo na hekima Yake. Aliwapata watu Aliowataka, kushinda utambulisho na hadhi Aliyostahili, na kurudi kwa kiti Chake cha enzi.

Kifuatacho, hebu tuangalie dondoo mbili zifuatazo katika maandiko.

4. Samehe Sabini Mara Saba

Mat 18:21-22 Kisha Petro akakuja kwake, na kusema, Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atanikosea, nami nimsamehe? Hadi mara saba? Yesu akasema kwake, sikuambii, hadi mara saba: ila, hadi sabini mara saba.

5. Upendo wa Bwana

Mat 22:37-39 Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda.

Kati ya dondoo hizi mbili, moja yazungumzia msamaha na nyingine inazungumzia upendo. Mada hizi mbili zinaangazia kwa kweli kazi ambayo Bwana Yesu alitaka kutekeleza katika Enzi ya Neema.

Wakati Mungu alipokuwa mwili, Alileta pamoja naye hatua ya kazi Yake—Alileta pamoja naye kazi mahususi na tabia Aliyotaka kuonyesha katika enzi hii. Katika kipindi hicho, kila kitu ambacho Mwana wa Adamu alifanya kilizungukia kazi ambayo Mungu alitaka kutekeleza katika enzi hii. Asingeweza kufanya zaidi au kufanya kidogo zaidi. Kila kitu Alichosema na kila aina ya kazi Aliyotekeleza ilihusiana yote na enzi hii. Haijalishi kama Alionyesha kwa njia ya kibinadamu Akitumia lugha ya kibinadamu au kupitia kwa lugha ya kiungu—haijalishi ni njia gani, au kutoka kwa mtazamo gani—lengo Lake lilikuwa ni kuwasaidia watu kuelewa kile Alichotaka kufanya, mapenzi Yake yalikuwa nini, na mahitaji Yake yalikuwa yapi kutoka kwa watu. Anaweza kutumia mbinu mbalimbali kutoka mitazamo mbalimbali ili kuwasaidia watu kuelewa na kujua mapenzi Yake, kuelewa kazi Yake ya kuwaokoa binadamu. Hivyo basi katika Enzi ya Neema tunamwona Bwana Yesu akitumia lugha ya kibinadamu mara kwa mara kuonyesha kile Alichotaka kuwasilisha kwa mwanadamu. Hata zaidi, tunamwona kutoka katika mtazamo wa mwelekezi wa kawaida Akiongea na watu, Akiwaruzuku mahitaji yao, Akiwasaidia na kile walichoomba. Njia hii ya kufanya kazi haikuonekana katika Enzi ya Sheria iliyokuja kabla ya Enzi ya Neema. Aligeuka na kuwa karibu zaidi na mwenye huruma zaidi kwa binadamu, pamoja na kuweza kutimiza zaidi matokeo ya kimatendo katika umbo Lake na tabia Yake. Usemi kusamehe watu sabini mara saba unafafanua zaidi hoja hii. Kusudio lililotimizwa kupitia kwa nambari katika usemi huu ni kuwaruhusu watu kuelewa nia ya Bwana Yesu wakati huo aliposema hayo. Nia Yake ilikuwa kwamba watu wanafaa kuwasamehe wengine—si mara moja wala mara mbili na wala si hata mara saba, lakini sabini mara saba. Hili wazo la “sabini mara saba” ni la aina gani? Ni la kuwafanya watu kufanya msamaha kuwa wajibu wao wa kibinafsi, kitu ambacho lazima wajifunze, na njia ambayo lazima waendeleze. Hata ingawa huu ulikuwa usemi tu, ulikuwa hoja muhimu. Uliwasaidia watu kufahamu kwa kina kile Alichomaanisha na kugundua njia bora za kufanyia mazoezi na kanuni na viwango katika utendaji. Usemi huu uliwasaidia watu kuelewa waziwazi na ukawapa dhana sahihi kwamba wanafaa kujifunza kusamehe—kusamehe bila ya masharti na bila ya upungufu wowote, lakini kwa mtazamo wa uvumilivu na ufahamu kwa wengine. Bwana Yesu aliposema haya, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Alikuwa akifikiria kwa kweli kuhusu sabini mara saba? Hakuwa akifikiri kuhusu hilo. Ipo idadi ya mara ambazo Mungu atawasamehe binadamu? Kunao watu wengi walio na shauku katika “idadi” iliyotajwa, wanaotaka kwa kweli kuelewa asili na maana ya nambari hii. Wanataka kuelewa kwa nini nambari hii ilitoka kinywani mwa Bwana Yesu; wanaamini kwamba kuna uhusisho wa kina zaidi katika nambari hii. Kwa hakika, huu ulikuwa ni usemi tu wa Mungu katika ubinadamu. Uhusisho au maana yoyote lazima ichukuliwe pamoja na mahitaji ya Bwana Yesu kwa mwanadamu. Wakati Mungu alikuwa bado hajawa mwili, watu hawakuelewa mengi ya Alichosema kwa sababu kilitoka katika uungu kamilifu. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulionyeshwa kutoka katika ulimwengu wa kiroho ambayo watu wasingeweza kuiona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika ulimwengu wa kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa ubinadamu, na Alitoka kwa na, na akazidi mawanda ya ulimwengu wa kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya uungu, mapenzi, na mtazamo, kupitia mambo yale ambayo binadamu wangeweza kufikiria na mambo yale wangeweza kuona na kukumbana nayo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kukubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kuelewa, ili kuruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu nia Yake na viwango Vyake hitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao; hadi kufikia kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu kwa ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu. Kazi ya Mungu katika ubinadamu ilikuwa thabiti zaidi, halisi, na yenye malengo, mbinu zilikuwa zaweza kubadilika kwa urahisi zaidi, na kwa umbo iliweza kupita Enzi ya Sheria.

Hapa chini, hebu tuzungumzie kumpenda Bwana na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda. Je, hili ni jambo linaloelezewa moja kwa moja kupitia uungu? Bila shaka silo! Haya yalikuwa mambo yote ambayo Mwana wa Adamu alisema kwa ubinadamu; watu tu ndio wangeweza kusema kauli kama “Mpende jirani yako kama unavyojipenda. Kuwapenda wengine ni sawa na kuyatunza maisha yako binafsi,” na watu tu ndio wangeweza kuongea kwa njia hii. Mungu hajawahi kuongea kwa njia hiyo. Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu hana aina hii ya lugha katika uungu Wake kwa sababu Hahitaji aina hii ya imani, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda” ili kudhibiti upendo Wake kwa mwanadamu, kwa sababu upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni ufichuzi wa kiasili wa kile Alicho nacho na kile Alicho. Ni lini mmewahi kusikia kwamba Mungu alisema kitu kama “Nampenda binadamu kama Ninavyojipenda”? Kwa sababu upendo umo katika kiini cha Mungu, na ndani ya kile Alicho nacho na kile Alicho. Upendo wa Mungu kwa binadamu na jinsi Anavyowashughulikia watu na mtazamo Wake ni maonyesho ya kiasili na ufichuzi wa tabia Yake. Hahitaji kufanya hili kwa njia fulani kimakusudi, au kufuata mbinu fulani au mfumo wa maadili kimakusudi ili kutimiza kumpenda jirani Yake kama Anavyojipenda—tayari Anamiliki aina hii ya kiini. Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile walichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe. Hivyo ni kusema kwamba, Mwana wa Adamu kwa mwili Alionyesha tabia ya asili na kiini cha Mungu Mwenyewe kwa kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana na kwa usahihi zaidi unaowezekana. Ubinadamu wa Mwana wa Adamu haukuwa pingamizi au kizuizi cha mawasiliano na kuingiliana kwa binadamu na Mungu mbinguni tu, bali kwa hakika ilikuwa ndio njia ya pekee na daraja la pekee la mwanadamu kuungana na Bwana wa uumbaji. Wakati huu, je, hamhisi kwamba kunayo mifanano mingi kati ya asili na mbinu za kazi iliyofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na awamu ya sasa ya kazi? Hatua ya sasa ya kazi inatumia pia lugha nyingi za kibinadamu kueleza tabia ya Mungu, na inatumia lugha na mbinu nyingi kutoka katika maisha ya kila siku ya binadamu na maarifa ya kibinadamu ili kuonyesha mapenzi binafsi ya Mungu. Punde Mungu anapokuwa mwili, haijalishi kama Anaongea kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu au mtazamo wa kiungu, wingi wa lugha na mbinu Zake za maonyesho yote ni kupitia katika njia ya lugha na mbinu za kibinadamu. Yaani, wakati Mungu anapokuwa mwili, ndiyo fursa bora zaidi ya wewe kuweza kuona kudura ya Mungu na hekima Yake, na kujua kila kipengele halisi cha Mungu. Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati Alikuwa Akikua, Alipata kuelewa, kujifunza, na kuelewa baadhi ya maarifa ya binadamu, maarifa ya kawaida, lugha, na mbinu za maonyesho katika ubinadamu. Mungu mwenye mwili alimiliki mambo haya yaliyotokana na binadamu Aliyekuwa ameumba. Waligeuka na kuwa zana za Mungu katika mwili za kueleza tabia Yake na uungu Wake, na wakamruhusu kuifanya kazi Yake ya kufaa zaidi, halisi zaidi, na sahihi zaidi Alipokuwa akifanya kazi katikati ya mwanadamu, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu na kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Iliiwezesha kufikiwa zaidi na kueleweka kwa urahisi zaidi na watu, hivyo basi kutimiza matokeo ya kile Mungu Alichotaka. Je, si jambo la busara zaidi kwa Mungu kufanya kazi kupitia kwa mwili kwa njia hii? Je, hii sio hekima ya Mungu? Wakati Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi Aliyotaka kutekeleza, ndipo Angeonyesha tabia Yake na kazi Yake kwa utendaji, na huu ndio wakati pia ambao Angeanza rasmi huduma Yake kama Mwana wa Adamu. Hii ilimaanisha kwamba hakukuwepo tena na ghuba kati ya Mungu na binadamu, kwamba Mungu angesitisha karibuni kazi Yake ya kuwasiliana kupitia kwa wajumbe, na kwamba Mungu Mwenyewe binafsi angeweza kuonyesha maneno na kazi zote Alizotaka kufanya katika mwili. Hii ilimaanisha pia kwamba watu ambao Mungu huokoa walikuwa karibu na Yeye, na kwamba kazi Yake ya usimamizi ilikuwa imeingia eneo jipya, na kwamba binadamu wote walikuwa karibu kukumbwa na enzi mpya.

Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba mambo mengi yalifanyika Bwana Yesu alipozaliwa. Kubwa zaidi miongoni mwa hayo lilikuwa kutafutwa na mfalme wa ibilisi, hadi kufikia kiwango cha watoto wote wenye umri wa miaka miwili na chini katika eneo hilo kuchinjwa. Ni dhahiri kwamba Mungu alichukua hatari kubwa kwa kuwa mwili miongoni mwa binadamu; gharama kubwa Aliyolipia kwa ajili ya kukamilisha usimamizi Wake wa kumwokoa mwanadamu pia ni wazi. Matumaini makubwa ambayo Mungu alishikilia kwa ajili ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu katika mwili pia ni wazi. Wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi miongoni mwa wanadamu, Alikuwa anahisi vipi? Watu wanafaa kuweza kuelewa hilo kidogo, sivyo? Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu alifurahia kwa sababu Angeanza kuendeleza kazi Yake mpya miongoni mwa wanadamu. Bwana Yesu alipobatizwa na kuanza rasmi kazi Yake kukamilisha huduma Yake, moyo wa Mungu ulijawa na furaha kwa sababu baada ya miaka mingi sana ya kusubiri na matayarisho, hatimaye Angeweza kuuvaa mwili wa binadamu wa kawaida na kuanza kazi Yake mpya katika umbo la binadamu aliye na mwili na damu ambao watu wangeweza kuona na kugusa. Angeweza kuzungumza ana kwa ana na moyo kwa moyo na watu kupitia utambulisho wa binadamu. Mungu hatimaye angeweza kuwa ana kwa ana na mwanadamu katika lugha ya kibinadamu, kwa njia ya kibinadamu; Angeweza kumruzuku mwanadamu, kumwelimisha binadamu, na kumsaidia binadamu kwa kutumia lugha ya kibinadamu; angeweza kula kwenye meza moja na kuishi katika nafasi sawa na binadamu. Angeweza pia kuwaona binadamu, kuona vitu, na kuona kila kitu kwa njia ambayo binadamu walifanya hivyo na hata kupitia kwa macho yao. Kwake Mungu, huu ulikuwa tayari ushindi Wake wa kwanza wa kazi Yake katika mwili. Yaweza pia kusemekana kwamba yalikuwa ni ufanikishaji wa kazi kubwa—hili bila shaka ndilo ambalo Mungu alilifurahia zaidi. Kuanzia hapo ndiyo mara ya kwanza ambayo Mungu alihisi tulizo fulani katika kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Matukio haya yote yalikuwa ya kimatendo sana na ya asili sana, na tulizo ambalo Mungu alihisi lilikuwa halisi. Kwa mwanadamu, kila mara hatua mpya ya kazi ya Mungu inapokamilishwa, na kila mara Mungu anapohisi kuridhika, ndipo mwanadamu anapoweza kusogea karibu zaidi na Mungu, na ndipo watu wanapoweza kusonga karibu zaidi na wokovu. Kwa Mungu, huu pia ni uzinduzi wa kazi Yake mpya, wakati mpango Wake wa usimamizi unapoendelea hatua moja zaidi, na, aidha, wakati mapenzi Yake yanapokaribia mafanikio kamili. Kwa mwanadamu, kuwasili kwa fursa kama hiyo ni bahati, na nzuri sana; kwa wale wote wanaosubiria wokovu wa Mungu, ni habari za maana sana. Mungu anapotekeleza hatua mpya ya kazi, basi Anao mwanzo mpya na wakati ambapo kazi hii mpya na mwanzo mpya vinazinduliwa na kufahamishwa miongoni mwa binadamu, ni wakati ambao matokeo ya hatua hii ya kazi tayari yameamuliwa, na kufanikishwa, naye Mungu tayari ameona athari yake ya mwisho na tunda. Huu pia ndio wakati ambapo athari hizi zinamfanya Mungu aridhike, na moyo Wake, bila shaka una furaha. Kwa sababu katika macho ya Mungu, tayari ameona na kuamua watu anaowatafuta, na tayari Amelipata kundi hili, kundi ambalo linaweza kufanya kazi Yake kufanikiwa na kumpa utoshelevu, Mungu anahisi Akiwa ameondolewa shaka, Anaweka pembeni wasiwasi Wake, na Anahisi mwenye furaha. Kwa maneno mengine, wakati mwili wa Mungu unaweza kuanza kazi mpya miongoni mwa binadamu, na Anaanza kufanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kizuizi, na wakati Anapohisi kwamba yote yamefanikishwa, tayari Ameuona mwisho. Na kwa sababu ya mwisho huu Anatosheka, na kuwa mwenye moyo wa furaha. Furaha ya Mungu inaonyeshwa vipi? Unaweza kufikiria hayo? Je, Mungu Angeweza kulia? Mungu Anaweza kulia? Mungu Anaweza kupiga makofi? Mungu Anaweza kucheza? Mungu Anaweza kuimba? Na wimbo huo ungekuwa upi? Bila shaka Mungu Angeweza kuimba wimbo mzuri, wa kusisimua, wimbo ambao unaweza kuonyesha shangwe na furaha katika moyo Wake. Angeweza kuwaimbia binadamu, kujiimbia Mwenyewe, na kuuimba kwa viumbe vyote. Furaha ya Mungu inaweza kuonyeshwa kwa njia yoyote—yote haya ni kawaida kwa sababu Mungu ana shangwe na huzuni, na hisia Zake mbalimbali zinaweza kuonyeshwa kwa njia mbalimbali. Hii ndiyo haki Yake na ndilo jambo la kawaida zaidi. Hufai kufikiria chochote kingine kuhusu hili, na hufai kupisha vizuizi vyako binafsi kwa Mungu, huku ukimwambia kwamba Yeye hafai kufanya hiki wala kile, Hafai kutenda kwa njia hii au ile, kuwekea mipaka shangwe Yake au hisia yoyote ile Aliyo nayo. Katika mioyo ya watu Mungu hawezi kuwa na furaha, Hawezi kutokwa na machozi, Hawezi kulia—Hawezi kuonyesha hisia zozote. Kupitia yale tuliyowasiliana katika nyakati hizi mbili, Naamini hamtamwona tena Mungu kwa njia hii, lakini mtamruhusu Mungu kuwa na uhuru na uachiliaji fulani. Hiki ni kitu kizuri. Katika siku za usoni kama mtaweza kuhisi kwa kweli huzuni ya Mungu mnaposikia kwamba Yeye ana huzuni, na mnaweza kuhisi kwa kweli shangwe Yake mnaposikia kuhusu Yeye kuwa na furaha—angalau, mnaweza kujua na kuelewa waziwazi kile kinachomfanya Mungu kuwa na furaha na kile kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni—unapoweza kuhisi huzuni kwa sababu Mungu ana huzuni na kuhisi furaha kwa sababu Mungu ana furaha, Atakuwa ameupata moyo wako na hakutakuwa tena na kizuizi chochote na Yeye. Hamtajaribu tena kumzuilia Mungu na fikira na maarifa ya binadamu. Wakati huo, Mungu atakuwa hai na dhahiri moyoni mwako. Atakuwa Mungu wa maisha yako na Bwana wa kila kitu chako. Je, mnalo tamanio kama hili? Je, mnayo imani kuwa mnaweza kutimiza haya?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp