Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji wa Bwana Yesu kwa utukufu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na Anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunapowaza kuhusu haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa tulizaliwa siku za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya malipo ya “utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa”; hiyo ni baraka kweli! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja mara kwa mara zaidi. Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema zaidi wakati mwanadamu hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na ataonekana kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja wa wale watakaonyakuliwa kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine wameachana na familia zao, wengine wamekana ndoa zao, na baadhi yao hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe hata unashinda ule wa watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anampa neema yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, tunaamini, tayari yametazamika machoni Pake. Kwa hivyo, pia, sala zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi Zake kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Kuongezea, bila kusita hata kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye, tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu kinachotarajiwa.

Tunadharau wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; na mwishowe, wote wataangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni Mwokozi? Bila shaka, kuna nyakati ambapo tunajifunza kutoka kwa Bwana Yesu na tunakuwa na huruma kwa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na tunapaswa kuwa wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa maneno ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na Biblia ni uzushi, na madhehebu maovu. Imani kama hiyo imehifadhiwa ndani sana ya akili zetu. Bwana wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni hii, basi tutaokolewa. Sisi husaidiana na kuchochea kila mmoja wetu, na kila wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa kinaweza kukubaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkali ulioko kwenye mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi kukiacha? Je, kuna kitu ambacho hatuwezi kuvumilia kutengana nacho? Yote haya ni thabiti, na haya yote yanatazamwa na macho ya Mungu. Sisi, walio wachache wa maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa na wafuasi wa Bwana Yesu wa kawaida: Tunaota kuhusu kunyakuliwa, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo zinahukumiwa machoni pa Mungu. Bado, yote haya hutokea bila ajabu kabisa, yenye mantiki sana, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama hamu yetu ni ya haki, sembuse yeyote kati yetu ambaye anashuku usahihi wa yote yale ambayo sisi hushikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya Mungu? Hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, au hata kujishughulisha na njia ambayo mwanadamu hupitia. Kwa maana sisi hujali tu kuhusu kama tutaweza kunyakuliwa, kama tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa katika ufalme wa mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya mto wa uzima na matunda ya mti wa uzima. Je, sisi hatumwamini Bwana, na je, sisi sio wafuasi wake Bwana, kwa ajili ya kupata vitu hivi? Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeuweka msalaba migongoni mwetu. Nani anayeweza kusema kuwa gharama ambayo tumelipia haitakubalika na Bwana? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha? Hatutaki kuwa wale mabikira wapumbavu, ama mmoja wa wale ambao wameachwa. Aidha, tunaomba mara nyingi, na kumwomba Bwana atuepushe kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa kwenye Biblia kuwa “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya Biblia kwenye kumbukumbu, tunaijua vyema sana, na tunaiona kama hazina ya thamani, kama maisha, na kama vitambulisho vyetu vya wokovu wetu na kunyakuliwa kwetu …

Kwa maelfu ya miaka, wanaoishi wamefariki, wakichukua tamaa zao na ndoto zao, na hakuna anayejua kwa kweli iwapo wameenda kwa ufalme wa mbinguni. Wafu wanarudi, na wamesahau hadithi zote zilizowahi kutokea wakati mmoja, na bado wanafuata mafundisho na njia za babu zetu. Na kwa hivyo, miaka inavyopita na siku zinavyosonga, hakuna anayejua iwapo Bwana Yesu, Mungu wetu, kwa kweli hukubali yote tunayoyafanya. Tunangojea tu matokeo na kubashiri kuhusu yale yote ambayo yatatokea. Bado Mungu yu kimya siku zote, na hajawahi kutuonekania, wala kusema nasi. Na kwa hivyo, kwa hiari yetu tunahukumu mapenzi ya Mungu na tabia kwa mujibu wa Biblia na ishara. Sisi tumezoea kimya cha Mungu; tumekuwa na mazoea ya kupima usahihi na makosa ya tabia zetu kutumia njia zetu wenyewe za mawazo: tumekuwa na mazoea ya kutumia elimu yetu, dhana, na maadili yetu na kuyafanya yachukue nafasi ya matakwa ya Mungu kwetu sisi; tumekuwa na mazoea ya kufurahia neema ya Mungu; tumekuwa na mazoea ya Mungu kutoa msaada wakati sisi tunahitaji msaada huo; tumekuwa na mazoea ya kunyosha mikono yetu kwa Mungu ili tupate mambo yote, na kumuagiza Mungu; na pia tumekuwa na mazoea ya kufuata mafundisho ya dini, kutotilia maanani jinsi Roho Mtakatifu hutuongoza; zaidi ya hayo, tumekuwa na mazoea ya siku ambazo sisi ni bwana zetu wenyewe. Tunamwamini Mungu wa namna hii, ambaye hatujawahi kukutana naye. Maswali kama namna tabia Yake ilivyo, asili Yake na mali Zake ni zipi, mfano Wake ulivyo, kama tutamjua ama hatutamjua wakati Atakaporudi, na kadhalika—haya yote hayana umuhimu. Jambo muhimu ni kuwa Yeye yumo mioyoni mwetu, na kuwa tunamsubiri, na kuwa tunaweza kufikiria jinsi Alivyo. Tunathamini imani yetu, na kuthamini hali yetu ya kiroho. Tunaona kila kitu ni kama samadi, na kukanyaga vimbo vyote kwa nyayo zetu. Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Bwana mwenye utukufu, bila kujali jinsi safari yetu ilivyo ndefu na ngumu, bila kujali shida na hatari zinazotukumba, hakuna kitu kitakachosimamisha nyayo zetu tunapomfuata Bwana. “Mto safi wa maji ya uhai, ung’aao kama kioo, uliondoka katika kiti cha Mungu cha enzi na cha Mwanakondoo. Na katika kila upande wa ule mto, ulikuwapo ule mti wa uhai unaozaa matunda ya jinsi kumi na mbili, na kuyatoa hayo matunda yake kila mwezi: na majani yake mti huu yalikuwa ya ajili ya kuyaponya mataifa. Na laana haitakuwepo tena: ila kiti cha Mungu cha enzi na cha Mwanakondoo kitakuwa ndani yake; na watumishi wake watamhudumia: Na wao wataona uso wake; nayo mapaji ya nyuso zao yatakuwa na jina lake. Na hakutakuwa na usiku pale; wala hawahitaji mshumaa, wala mwanga wa jua; kwa sababu Bwana Mungu huwapa mwanga: na wao watatawala daima na milele” (Ufunuo 22:1-5). Kila wakati sisi hukariri maneno hayo, mioyo yetu hujawa na furaha isiyo na kifani na maridhio, na machozi hutiririka kutoka machoni mwetu. Shukrani ni kwa Bwana kwa kutuchagua, shukrani ni kwa Bwana kwa neema Yake. Ametupa mara mia sasa, Yeye ametupa uzima wa milele kwa ulimwengu ujao, na kama angetuomba tufe sasa, tungetii hiyo bila kusita hata kidogo. Bwana! Tafadhali njoo hivi karibuni! Usikawie hata dakika moja tena, kwa kuwa sisi tunakutamani sana na tumeacha kila kitu kwa ajili Yako.

Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi Wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango Wake. Usimamizi Wake huendelea kimya kimya, bila madhara ya kutia shauku, ilhali nyayo Zake, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti Chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima. Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho anawasili kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya akiwa na mamlaka na akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya mwanadamu yanabaki yalivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa kawaida, kama mfuasi asiye na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini asiye wa maana. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanawekwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye hutilia maanani uwepo Wake, hamna aliye na mawazo yoyote ya kazi Yake, na zaidi ya hayo, hakuna mtu aliye na tuhuma yoyote kuhusu Yeye ni nani. Sisi huendelea na kazi yetu tu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi …

Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa sana, tunatambua kuwa hilo ni tamko la Mungu, na tunaukubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hatuwezi kuyakana. Tamko linalofuata linaweza kuwa kupitia kwangu, au kwako, ama linaweza kupitia yeye. Bila kujali ni nani, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu huyo ni nani, hatufai kumwabudu, kwa kuwa bila kuzingatia chochote kingine, hawezi kuwa Mungu; hatuwezi kwa njia yoyote kumchagua mtu wa kawaida kama huyu kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika sana; Anawezaje kuwakilishwa na binadamu asiye na umuhimu hivyo? Zaidi ya hayo, sisi sote tunasubiri ujaji wa Mungu kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu hivyo anawezaje kustahili kufanya kazi ngumu na muhimu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, linaloonekana na wote. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itakuwaje Ajifiche kwa ukimya kati ya kundi la watu wa kawaida?

Na bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu, wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa na aibu na fedheha. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anatarajia kufanya. Labda tunaweza tu kunyakuliwa baada ya kuvumilia maumivu kama hayo? Vichwani mwetu tunafanya hesabu … kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili na hutenda kazi kati yetu. Japokuwa Amekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado hatuko tayari kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, wala hatuna nia ya kumwaminisha mtu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na hatima yetu. Kutoka Kwake, tunafurahia ugavi usioisha wa maji ya uhai, na kwa sababu Yake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Sisi tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Yeye bado, kwa unyenyekevu, hufanya kazi akiwa amefichwa ndani ya mwili, akionyesha sauti ya moyo Wake, akionekana kama hafahamu kukataliwa Kwake na binadamu, inavyoonekana yeye milele kusamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele kuvumilia mwanadamu kutomheshimu.

Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya kuzaliwa upya; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake na huba Yake; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, waliofanywa majivu na ghadhabu Yake katika macho Yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana, na Hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Ila, licha ya haya, majivuno yangali mioyoni mwetu, na sisi bado hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana nyingi sana, nyingi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambalo linaweza kunyakua nafasi ya Bwana katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum na hadhi ya huyu mwanadamu kwa kusita sana. Kama Yeye haneni kwa nguvu na kutufanya kukiri kwamba Yeye ni Mungu, basi sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu ambaye yuko karibu kuja ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu sana.

Matamshi ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya tutakachofanya na kuonyesha sauti ya moyo Wake. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na sauti ya moyo ya huyu mwanadamu asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu, anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu. Asili kama hii na mali Zake zimeshinda za binadamu wa kawaida, na haziwezi kumilikiwa au kupatwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, kutoka Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu, na kuonyesha sauti ya moyo ya Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu ambayo huelekezwa kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na Ametuletea matumaini, na akamaliza maisha yetu ambayo hayakuwa dhahiri, na Akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, si Yeye ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huo, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, wala hatupingi tena kazi na neno Lake, na tunasujudu, kabisa, mbele Yake. Hakuna tunachotaka ila kufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.

Kushindwa na Mungu ni kama mashindano ya kareti.

Kila neno la Mungu hugonga eneo letu la ubinadamu, na hutuacha tukiwa tumejawa na huzuni na hofu. Yeye hufichua fikra zetu, hufichua mawazo yetu, na hufichua tabia zetu potovu. Kupitia kwa yale yote sisi husema na kuyatenda, na kila wazo na fikra zetu, asili na kiini zinafichuliwa kwa neno Lake, na kutuacha na fedheha, tukitetemeka kwa hofu. Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, na hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa hadharani kabisa, na hata zaidi kuhisi tumeshawishika vikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba hatuna thamani machoni Pake, na kuwa sisi ni Shetani aishiye. Matumaini yetu yanavunjika, na kamwe hatuthubutu kumpa madai yoyote yasiyo na msingi au kumjaribu, na hata ndoto zetu hupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na ambao hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Kwa muda, akili zetu hukosa msimamo, na hatujui tutakavyoendelea kwa njia iliyo mbele wala hatujui jinsi ambavyo tutaendelea katika imani zetu. Inaonekana kama imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na ya kuwa hatujawahi kukutana na kufahamiana na Bwana Yesu. Kila kitu machoni petu hutushangaza, na kutufanya tuhisi ni kama tumetupwa mbali. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna hasira ambayo haiwezi kufichika na pia kuna aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, hali kadhalika, sisi hujaribu kuendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, na kujieleza kwa dhati mbele Yake. Ingawa kuna wakati mwingine ambao hatuna kiburi wala unyenyekevu kwa kutazamwa kwa nje, mioyoni mwetu tunateseka na hisia ya hasara kuliko ile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaweza kuonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, ndani yetu tunavumilia bahari ya mateso inayopanda na kushuka. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, na kutuacha bila tamaa zetu kuu na kutokuwa tayari kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu na anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kubwa kati yetu na Yeye na hakuna aliye tayari hata kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza ambapo sisi tunateseka kwa kupata pingamizi kubwa hivi na udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo. Hukumu na kuadibu Kwake zimetuwezesha kwa kweli kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia Kwake makosa ya binadamu, ambazo tukilinganishwa nazo, sisi ni watu wa hadhi ya chini na najisi sana. Hukumu Yake na kuadibu zimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hataweza kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi tena katika tabia potovu kama hiyo, na zimetufanya tutamani kuacha asili kama hiyo na kiini kama hicho haraka iwezekanavyo, na kutochukiwa tena Naye wala tusimchafue moyo. Hukumu na kuadibu kwake zimetufanya tufurahie kutii maneno Yake, na hatumo tayari tena kwenda kinyume na matayarisho na mipangilio Yake. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kutafuta uzima, na zimetuwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu…. Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, tumetoka kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti…. Mwenyezi Mungu ametupata, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui Zake zote!

Sisi ni kundi la watu wa kawaida tu waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, sisi ndio watu waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na sisi ndio maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, ila sasa tumeshindwa na Yeye. Tumepokea uzima na kupokea njia ya uzima wa milele kutoka kwa Mungu. Bila kujali mahali ambapo tupo hapa duniani, licha ya mateso na dhiki, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu pekee!

Upendo wa Mungu unaenea mbele kama maji ya chemichemi, na unapewa wewe, na mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu.

Kama vile mwezi hufuata jua daima, kazi ya Mungu haikomi kamwe, na inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata nyayo za Mungu na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu.

Machi 23, 2010

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp