Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 11

Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu

Kabla ya kuwa na mitazamo au hitimisho zako binafsi, unafaa kwanza kuelewa mwelekeo wa Mungu kwako, kile ambacho Mungu anafikiria, na kuamua kama kufikiria kwako ni sahihi au la. Mungu hajawahi kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya mtu, na Hajawahi kutumia kiwango cha mateso yaliyovumiliwa na mtu katika kuasisi matokeo yake. Basi Mungu hutumia kiwango gani katika kuasisi matokeo ya binadamu? Kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya binadamu—hii ndiyo inaingiliana zaidi na dhana za watu. Na pia kuna hao watu binafsi ambao mara nyingi mnawaona, wale ambao katika wakati fulani walijitolea kabisa, wakatumia muda mwingi kabisa, wakagharamika kabisa, wakateseka kabisa. Hawa ndio, kwa maoni yenu, wanaweza kuokolewa na Mungu. Kile tu ambacho watu hawa wanaonyesha, yote wanayoishi kwa kudhihirisha, ndiyo hasa dhana ya wanadamu kuhusu kiwango ambacho Mungu anaanzisha kuhusiana na matokeo ya binadamu. Bila kujali ni nini unachosadiki, Sitaorodhesha mifano hii mmoja baada ya mwingine. Nikiongea kwa ujumla, mradi tu si kiwango cha kufikiria binafsi kwa Mungu, basi kinakuja kutoka kwenye kufikiria kwa binadamu na ni dhana tu ya binadamu. Ni nini athari za kusisitiza bila mwelekeo dhana na kufikiria kwako binafsi? Bila shaka, athari inaweza kuwa tu Mungu akikusukuma mbali. Hii ni kwa sababu siku zote unaringa kuhusu sifa zako mbele ya Mungu, unashindana na Mungu, na kuleta mzozo dhidi ya Mungu, na hujaribu hata kufahamu kwa kweli kufikiria kwa Mungu, wala hujaribu kuzifahamu nia za Mungu na mwelekeo wa Mungu kwa binadamu. Kuendelea mbele hivi ni kujiheshimu kuliko yote na wala si kumheshimu Mungu. Unajisadiki; husadiki Mungu. Mungu hataki mtu wa aina hii, na Mungu hatamwokoa mtu wa aina hii. Kama huwezi kuachilia aina hii ya mtazamo, na kisha kuirekebisha mitazamo hii ya kale isiyokuwa sahihi; kama ungeweza kuendelea mbele kulingana na maagizo ya Mungu; anza kutenda njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa sasa na kusonga mbele; kuweza kuheshimu Mungu na kumwona kuwa mkubwa katika mambo yote; usitumie ndoto zako za kibinafsi, mitazamo au imani katika kujifafanua, kumfafanua Mungu. Na badala yake, unazitafuta nia za Mungu kwa hali zote, unatimiza utambuzi na uelewa wa mwelekeo wa Mungu kwa binadamu, na unatumia kiwango cha Mungu kutosheleza Mungu—kufanya hivi kungependeza! Huku kungemaanisha karibu unaanza katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Kwa sababu Mungu hatumii namna ambavyo watu hufikiria kwa njia hii au njia ile mawazo na mitazamo yao, kama kiwango cha kuanzisha matokeo ya binadamu, basi ni aina ipi ya kiwango Anayoitumia? Mungu hutumia majaribio kuanzisha matokeo ya binadamu. Kunavyo viwango viwili vya kutumia katika majaribio yanayoasisi matokeo ya binadamu: Kiwango cha kwanza ni idadi ya majaribio ambayo watu hao wanapitia, na kiwango cha pili ni matokeo ya watu hawa katika majaribu haya. Ni viashirio hivi viwili vinavyoasisi matokeo ya binadamu. Sasa tutaweza kufafanua viwango hivi viwili.

Kwanza kabisa, unapokabiliwa na jaribio kutoka kwa Mungu (kidokezo: Inawezekana kwamba katika macho yako jaribio hili ni dogo sana na halifai kutajwa), Mungu atakufanya kuwa na ufahamu kabisa kwamba huu ni mkono wa Mungu juu yako, na kwamba ni Mungu ambaye amepangilia hali hizi zote kwako. Wakati kimo chako hakijakomaa, Mungu atapanga majaribio ili kuweza kukupima. Majaribio haya yatalingana na kimo chako, yale ambayo unaweza kuelewa, na yale ambayo unaweza kustahimili. Kujaribu sehemu yako gani? Kujaribu mwelekeo wako kwa Mungu. Je, mwelekeo huu ni muhimu sana? Bila shaka ni muhimu! Zaidi ya hayo, ni muhimu hasa! Kwa sababu mwelekeo huu wa binadamu ndiyo matokeo anayotaka Mungu, ndicho kitu muhimu zaidi kulingana na Mungu. Ama sivyo Mungu asingetumia jitihada Zake kwa watu kwa kujihusisha na aina hizi za kazi. Mungu hutaka kuuona mwelekeo wako kwake Yeye, kupitia kwa majaribio haya; Anataka kujua kama uko kwenye njia sahihi na Anataka kujua kama unamcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo basi, bila kujali kama unaelewa ukweli mwingi au kidogo wakati huo, bado utakabiliwa na majaribio ya Mungu, na kufuatia ongezeko lolote katika kiwango chochote cha ukweli unaouelewa, Mungu ataendelea kupangilia majaribio sawa na hayo kwako. Wakati unapokabiliwa kwa mara nyingine tena na jaribio, Mungu anataka kuona iwapo mtazamo wako, mawazo yako, na mwelekeo wako kwa Mungu umekuwa na ukuaji wowote mpaka sasa. Baadhi ya watu husema: “Kwa nini siku zote Mungu anataka kuiona mielekeo ya watu? Kwani Mungu hajaona namna wanavyouweka ukweli katika matendo? Kwa nini Atake tena kuiona mielekeo ya watu?” Huku ni kupayuka kwa upuuzi! Kwa sababu Mungu anaendelea hivi, basi nia za Mungu lazima ziwe mumohumo. Siku zote Mungu huwaangalia watu kutoka pembeni mwao, akiangalia kila neno na tendo lao, kila kitendo na kusonga kwao, na hata kila fikira na wazo lao. Kila kitu kinachowafanyikia watu: vitendo vyao vizuri, makosa yao, dhambi zao, na hata kuasi na kusaliti kwao, Mungu atazirekodi zote kama ithibati katika kuasisi matokeo yao. Kwa kadri kazi ya Mungu inavyoendelea kuimarika hatua kwa hatua, unasikia ukweli zaidi na zaidi, unakubali mambo mazuri zaidi na zaidi, taarifa nzuri, na uhalisia wa kweli. Kwenye mkondo wa mchakato huu, mahitaji ya Mungu kwako wewe yataongezeka pia. Wakati uo huo, Mungu atapanga majaribio makubwa zaidi kwako. Shabaha yake ni kuchunguza kama mwelekeo wako kwa Mungu umekomaa mpaka sasa. Bila shaka, kwenye kipindi hiki, mtazamo ambao Mungu anahitaji kwako unaingiliana na uelewa wako wa uhalisia wako wa ukweli.

Huku kimo chako kinapoendelea kuimarika kwa utaratibu, kile kiwango ambacho Mungu anahitaji kutoka kwako wewe kitaendelea kuimarika kwa utaratibu pia. Kama utakuwa hujakomaa, Mungu atakupa kiwango kidogo sana; wakati kimo chako kitakapokuwa kikubwa kidogo, Mungu atakupa kiwango cha juu zaidi kidogo. Lakini Mungu atakuwa vipi baada ya wewe kuuelewa ukweli wote? Mungu atahakikisha kuwa unakabiliana na hata majaribio makubwa zaidi. Katikati ya majaribio haya, kile Mungu anachotaka kupata, kile Mungu anachotaka kuona, ni maarifa yako ya kina zaidi ya Mungu na kumcha kwako Kwake kwa njia ya kweli. Wakati huu, mahitaji ya Mungu kwako wewe yatakuwa ya juu zaidi “makali zaidi” kuliko wakati ambapo kimo chako kilikuwa kidogo zaidi (kidokezo: Watu huona kwamba hali hii ni kali, lakini Mungu kwa hakika Huiona kuwa ya kustahimilika). Wakati Mungu anawapa watu majaribio, ni uhalisia gani ambao Mungu anataka kuunda? Mungu anauliza kila mara kwamba watu wampe Yeye moyo wao. Baadhi ya watu watasema: “Mtu anawezaje kufanya hivyo? Natekeleza wajibu wangu, niliacha nyumba yangu na riziki yangu, niligharamika kwa sababu ya Mungu. Hii yote si mifano ya kuutoa moyo wangu kwa Mungu? Ni vipi vingine nitakavyoutoa moyo wangu kwa Mungu? Yaweza kuwa kwamba, hii si mifano ya kuutoa moyo wangu kwa Mungu? Mahitaji mahususi ya Mungu ni yapi?” Mahitaji haya ni mepesi mno. Kwa hakika, kunao baadhi ya watu ambao tayari wameitoa mioyo yao kwa Mungu katika viwango tofauti na awamu mbalimbali za majaribio yao. Lakini wengi wa watu huwa hawapi Mungu mioyo yao. Wakati Mungu anapokupa jaribio, Mungu hutaka kujua kama moyo wako uko pamoja Naye, pamoja na mwili au pamoja na Shetani. Wakati Mungu anapokupa jaribio, Mungu anataka kujua kama unasimama katika upinzani na Yeye au kama unasimama katika hali ambayo inalingana na Yeye, na kutaka kuona moyo wako kama uko na Yeye. Wakati hujakomaa na wakati wa kukabiliwa na majaribio, kiwango cha imani yako kiko chini, na huwezi kujua hasa ni nini unachohitaji ili kutosheleza nia za Mungu kwa sababu unao uelewa finyu wa ukweli. Licha ya haya yote, bado unaweza kumwomba Mungu kwa dhati na uaminifu, kuwa radhi kuutoa moyo wako kwa Mungu, kumfanya Mungu kuwa mkuu wako, na kuwa radhi kumpa Mungu yale mambo unayosadiki kuwa yenye thamani zaidi. Hii ndiyo maana ya wewe kuwa tayari umempa Mungu moyo wako. Unaposikiliza mahubiri mengi zaidi na zaidi, na kuelewa ukweli zaidi na zaidi kimo chako kitaanza kukomaa kwa utaratibu. Kiwango ambacho Mungu huhitaji kutoka kwako si sawa na kile ambacho ulikuwemo wakati ulikuwa hujakomaa; Anahitaji kiwango cha juu zaidi kuliko hicho. Wakati moyo wa binadamu unapewa Mungu kwa utaratibu, unaanza kuwa karibu zaidi na karibu zaidi na Mungu; wakati binadamu anaweza kuwa karibu na Mungu kweli, wanaanza kuwa na moyo ambao sanasana unamcha Yeye. Mungu anataka aina hii ya moyo.

Wakati Mungu anataka kuumiliki moyo wa mtu, Atawapa majaribio mengi. Kwenye majaribio haya, kama Mungu hatauchukua moyo wa mtu huyu, wala Haoni kama mtu huyu anao mwelekeo wowote—hivi ni kusema Havioni vitu ambavyo mtu huyu anapitia au anafanya mambo kwa njia ambayo ni ya kumcha Mungu, na Haoni mwelekeo au suluhisho ambalo linajiepusha na maovu kutoka kwa mtu huyu. Kama hivi ndivyo ilivyo, basi baada ya majaribio mengi, subira ya Mungu kwa mtu huyu binafsi itaondolewa, na Hatamvumilia mtu huyu tena. Hataweza kuwapa watu kama hawa majaribio, na Hataweza tena kuwashughulikia. Basi hiyo inamaanisha kwamba matokeo ya mtu huyu ni yapi? Inamaanisha kwamba hawatakuwa na matokeo. Yawezekana kwamba mtu huyu hajafanya maovu yoyote. Yawezekana pia kwamba watu hawa hawajafanya chochote cha kukatiza au kutatiza. Yawezekana kuwa watu hawa hawajampinga Mungu waziwazi. Hata hivyo, moyo wa mtu huyu umefichwa kutoka kwa Mungu. Hawajawahi kuwa na mwelekeo na mtazamo wazi kwa Mungu, na Mungu hawezi kuona waziwazi kwamba moyo wake amekabidhiwa Yeye, na Yeye Hawezi kuona waziwazi kwamba mtu huyu anatafuta kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu hana subira tena kwa watu hawa, Hatawagharamia tena, Hatatoa tena rehema Yake kwao, na Hatawafanyia kazi wao tena. Maisha ya imani ya mtu huyu katika Mungu tayari hayapo tena. Hii ni kwa sababu katika majaribio yote mengi ambayo Mungu amempa mtu huyu, Mungu hajapata matokeo Anayotaka. Hivyo basi, kunayo idadi ya watu ambao ndani yao Sijawahi kuuona mwangaza na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu. Inawezekanaje kuona haya? Mtu wa aina hii huenda aliamini katika Mungu kwa miaka mingi, na kwenye sehemu ya juujuu wamekuwa amilifu. Wamevisoma vitabu vingi, wameyashughulikia masuala mengi, wameandika nakala nyingi, wamekuwa na ujuzi wa barua na falsafa nyingi. Hata hivyo, hakuna ukuaji wowote unaonekana kamwe, na wala kuwa na mtazamo wowote wa kuonekana kwa Mungu kutoka kwa mtu huyu, wala hakuna mwelekeo wowote wazi. Hivi ni kusema kwamba huwezi kuona moyo wa mtu huyu. Moyo wao siku zote umesetiriwa, moyo wao umefumikwa—Umefunikwa kutoka kwa Mungu, hivyo basi Mungu hajauona moyo wa kweli wa mtu huyu, Hajaona kumcha Mungu kwa mtu huyu, na hata zaidi Hajaona namna ambayo mtu huyu anatembea katika njia za Mungu. Kama mpaka sasa Mungu hajampata mtu wa aina hii, Anaweza kuwapata katika siku za usoni? Hawezi! Je, Mungu ataendelea kusukumiza mbele mambo ambayo hayawezi kupatikana? Hatafanya hivyo! Mwelekeo wa Mungu kwa watu kama hawa, hivyo basi ni nini? (Anawasukumia mbali, Hawasikilizi.) Yeye hawasikilizi! Mungu hasikilizi mtu wa aina hii; Anawasukumia mbali. Mmetia kwenye kumbukumbu maneno haya kwa haraka sana, kwa usahihi sana. Inaonekana mmeelewa kile mlichosikia!

Kunao baadhi ya watu ambao, punde wanapoanza kumfuata Mungu wao hawana ukomavu na hawajui chochote; hawaelewi nia za Mungu; hawajui pia maana ya kusadiki Mungu, kuchukua njia iliyoundwa na binadamu na inayokosewa na wengi ya kusadiki Mungu, kufuata Mungu. Wakati mtu wa aina hii anakabiliwa na majaribio hawana habari na hawajali kuhusu mwongozo na nuru ya Mungu. Hawajui maana ya kuutoa moyo wao kwa Mungu na maana ya kusimama imara wakati wa jaribio. Mungu atampa mtu huyu kiwango finyu cha muda na katika kipindi hiki, Atawaacha kuelewa jaribio la Mungu ni nini, na nia za Mungu ni nini. Baadaye mtu huyu atahitaji kuonyesha mtazamo wao. Kuhusiana na watu wale walio katika awamu hii, Mungu angali anasubiri. Kuhusiana na watu wale ambao mitazamo yao ingali inayumbayumba, wale wanaotaka kumpa Mungu mioyo yao lakini hawajawa na maridhiano ya kufanya hivyo, ambao, ingawa wameweza kutenda ukweli fulani, wakati wanapokumbwa na jaribio kuu, wanaokwepa na wanataka kukata tamaa—mwelekeo wa Mungu kwa watu kama hawa ni upi? Mungu angali bado ana matarajio kidogo kwa watu kama hawa. Matokeo yanategemea na mielekeo na utendakazi wao. Mungu anaitikia vipi kama watu si amilifu katika kuwa na maendeleo? Yeye hukata tamaa. Hii ni kwa sababu kabla Mungu hajakata tamaa kwako, tayari wewe mwenyewe umekata tamaa. Kwa hivyo, huwezi kumlaumu Mungu kwa kufanya hivyo, je, unaweza? Je, hiyo ni haki? (Ni haki.)

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp