Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu | Dondoo 486

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu | Dondoo 486

89 |07/09/2020

Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa kwa awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wanatii Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima kwa utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haijakubaliwa na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na kuendelea kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Katika kazi ya Mungu, Anakuletea kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja. Natoa mwangaza mpya ili muweze kuona na kuwaleta kwa mwangaza wa sasa. Unapotembea katika mwangaza huu, Roho Mtakatifu ataanza kazi ndani yako mara moja. Wengine wanaweza kuwa waasi na kusema, “Sitafanya tu usemavyo,” Basi Nakwambia kwamba sasa ni mwisho wa njia. Umenyauka na huna maisha zaidi. Hivyo, kwa kupitia mabadiliko ya tabia yako, ni muhimu kabisa kwenda sambamba na mwangaza wa sasa. Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi kwa mtu mwingine ajaye. Fuata kwa makini; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndipo maisha yako yanaweza kuzidi kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua ndani uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Ukifanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu wa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui kupitia mtu wa aina gani Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, hii inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza. Unapotembea kwenye njia sawa, utapewa ufunuo kwa mambo yote. Bila kujali yale Roho Mtakatifu atafichua kwa wengine, ukiendelea kwa uzoefu wako kwa msingi wa maarifa yao, kupitia mambo wewe mwenyewe, basi uzoefu huu utakuwa sehemu ya maisha yako, na utaweza kuwasambazia wengine kwa sababu ya huu uzoefu. Wale wanaosambazia wengine kwa kuyarudia maneno ni wale wasio na uzoefu; itakulazimu kujifunza kupata, kupitia mwangaza na kupatiwa nuru ya wengine, njia ya kutenda kabla ya kuzungumza kuhusu uzoefu na maarifa yako halisi. Hii itakuwa ya manufaa zaidi kwa maisha yako binafsi. Unapaswa kuwa na uzoefu kwa njia hii, kutii yote yatokayo kwa Mungu. Unapaswa kutafuta akili ya Mungu kwa vitu vyote na kujifunza masomo kwa vitu vyote, ukijenga ukuaji kwa maisha yako. Vitendo hivyo vitamudu ukuaji wa haraka zaidi.

Roho Mtakatifu Anakupatia nuru kupitia uzoefu wa vitendo vyako na Anakukamilisha kupitia imani yako. Uko tayari kweli kukamilishwa? Kama kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu, basi utakuwa na ujasiri kuweka kando mwili wako, na kuweza kufanya asemavyo Mungu na kutokuwa mtu mtulivu ama mnyonge. Utaweza kutii yote yatokayo kwa Mungu, na vitendo vyako vyote, viwe vimefanywa hadharani au faraghani, vitastahiki kwa Mungu. Kuwa mtu mwaminifu na fanya mazoezi ya ukweli kwa mambo yote, na utakamilishwa. Wale wanadamu wadanganyifu wanaotenda njia moja mbele ya wengine na nyingine nyuma yao hawako tayari kukamilishwa. Wote ni wana wa laana na uharibifu; si wa Mungu lakini wa Shetani. Hao si aina ya wanadamu waliochaguliwa na Mungu! Kama vitendo na tabia yako haiwezi kustahiki mbele ya Mungu ama kufikiriwa na Roho wa Mungu, basi hii inaonyesha wewe una shida. Ukikubali tu hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kuweka umuhimu katika mabadiliko ya tabia yako ndipo utawekwa kwa njia ya kukamilishwa. Ikiwa kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu na kufanya mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kutii kazi yote ya Mungu na kutotoa neno la malalamiko, wala hupaswi kutathmini ama kuhukumu kazi ya Mungu utakavyo. Haya ni masharti ya msingi kabisa ya kukamilisha na Mungu. Mahitaji ya wale wanaotaka kukamilishwa na Mungu ni haya: fanya mambo yote kwa moyo unaompenda Mungu. Inamaanisha nini “kufanya mambo kwa moyo unaompenda Mungu”? Inamaanisha kwamba vitendo na tabia yako yote inaweza kuletwa mbele ya Mungu. Kwa sababu una nia sawa, iwapo vitendo vyako ni sawa ama vibaya, huogopi vikionyeshwa kwa Mungu ama kwa ndugu na dada zako; unathubutu kuapa kwa Mungu. Kwamba kila nia, fikra, na wazo lako linaweza kufaa kuchunguzwa mbele ya Mungu: ukitenda na kuingia kwa njia hii, basi maendeleo katika maisha yako yatakuwa mepesi.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi