Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 33

Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli

Ukiangalia Mwanzo 22:2, Mungu alimtolea Ibrahimu amri ifuatayo: “Umchukue mwana wako sasa, mwana wako wa pekee Isaka, unayempenda, na uende hadi nchi ya Moria; na huko umtoe kwa sadaka ya kuteketezwa juu ya mojawapo ya milima ambayo nitakuambia.” Maana ya Mungu ilikuwa wazi: Alikuwa akimwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake wa pekee Isaka, ambaye alimpenda, kwa minajili ya sadaka ya kuteketezwa. Tukiiangalia amri ya Mungu leo, je ingali inakinzana na dhana za binadamu? Ndiyo! Kile alichokifanya Mungu wakati huo ni kinyume sana na dhana za binadamu na hakieleweki kwa binadamu. Katika dhana zao, watu husadiki yafuatayo: Wakati binadamu hakusadiki, na akafikiria ni jambo lisilowezekana, Mungu Alimpa mwana, na baada ya kupata mtoto, Mungu alimwomba amtoe mwana wake—haiwezekani! Mungu kwa hakika alinuia kufanya nini? Kusudio halisi la Mungu lilikuwa nini? Alimpa Ibrahimu mtoto bila masharti yoyote, ilhali pia Alimwomba Ibrahimu aweze kutoa bila masharti. Maji yalikuwa yamezidi unga? Katika mtazamo wa mtu wa pembeni, hapa maji hayakuwa tu yamezidi unga lakini pia ilikuwa kwa kiasi fulani hali ya “kuunda tatizo pasipo na tatizo.” Lakini Ibrahimu mwenyewe hakusadiki kwamba Mungu alikuwa akihitaji mengi sana. Ingawaje alikuwa na wasiwasi fulani, na alimshuku kidogo Mungu, alikuwa tayari bado kumtoa mtoto wake. Wakati huu, ni nini unachoona ambacho kinathibitisha kuwa Ibrahimu alikuwa radhi kumtoa mtoto wake? Ni nini kinazungumzwa kwenye sentensi hizi? Maandishi asilia yanaelezea yafuatayo: “Naye Ibrahimu akaamka asubuhi mapema, na kuweka tandiko kwa punda wake, akawachukua vijana wake wawili pamoja naye, naye Isaka mwana wake, na akapasua kuni kwa sababu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, na akaondoka, na kuenda pahali ambapo alikuwa ameambiwa na Mungu” (Mwa 22:3). “Na wakafika pahali hapo ambapo Mungu alikuwa amemwambia; naye Ibrahimu akajenga madhabahu hapo, na kuziweka kuni kwa mpango, na kumfunga Isaka mwana wake, naye akamlaza juu ya madhabahu kwa zile kuni. Na Ibrahimu akanyosha mbele mkono wake, na kukichukua kisu ili amchinje mwana wake” (Mwa 22:9-10). Wakati Ibrahimu alipounyosha mkono wake, na kukichukua kisu ili kumwua mtoto wake, Mungu aliviona vitendo vyake? Naam aliviona. Mchakato wote—kuanzia mwanzo, wakati Mungu alipomwomba Ibrahimu kumtoa Isaka, hadi pale ambapo Ibrahimu alikiinua kisu chake ili kumwua mtoto wake—hilo lilionyesha Mungu moyo wa Ibrahimu, na haijalishi kuhusu ujinga wake wa awali, kutojua kwake, na kutomwelewa Mungu kwake, wakati huo moyo wa Ibrahimu kwa Mungu ulikuwa kweli, na wenye uaminifu, na kwa kweli alikuwa akienda kumrudisha Isaka, mtoto aliyepewa yeye na Mungu, ili arudi kwa Mungu. Ndani yake, Mungu aliuona utiifu—utiifu uleule ambao Yeye Alitamani.

Kwa binadamu, Mungu hufanya mengi yasiyoeleweka na yaliyo ya ajabu. Wakati Mungu anapotaka kupangilia mtu, mpango huu mara nyingi unakinzana na dhana za binadamu, na huwa haueleweki kwa binadamu huyo, ilhali ni ukosefu wa mwafaka huu na kutofahamu ndiyo majaribio ya Mungu na mtihani wake kwa binadamu. Ibrahimu, huku haya yakiendelea, aliweza kuonyesha utiifu kwa Mungu uliokuwa ndani yake, jambo ambalo ndilo lililokuwa sharti muhimu zaidi la yeye kuweza kushibisha mahitaji ya Mungu. Hapo tu, wakati Ibrahimu alipoweza kutii mahitaji ya Mungu, alipomtoa Isaka ndipo Mungu Alipohisi kwa kweli utulivu na kukubaliwa na wanadamu—kwa Ibrahimu, ambaye Alikuwa amemchagua. Hapo tu ndipo Mungu alipokuwa na hakika kwamba mtu huyu Aliyekuwa amemchagua Yeye alikuwa kiongozi muhimu ambaye angetekeleza ahadi Yake na mpango Wake wa usimamizi wa baadaye. Ingawaje lilikuwa tu jaribio na mtihani, Mungu alihisi furaha, Alihisi upendo wa binadamu kwake Yeye, na Alihisi akiwa ametulizwa na binadamu kwa mara ya kwanza. Wakati huu ambao Ibrahimu alipokiinua kisu chake ili kumwua Isaka, Mungu alimsimamisha? Mungu hakumruhusu Ibrahimu kumpa Isaka, kwani Mungu hakuwa na nia yoyote ya kumtoa uhai Isaka. Hivyo, Mungu alimsimamisha Ibrahimu kwa wakati mwafaka. Kwake Mungu, utiifu wa Ibrahimu ulikuwa tayari umepita mtihani, kile alichofanya kilitosha, naye Mungu tayari alikuwa ameona matokeo ya kile Alichokuwa amenuia kufanya. Je, matokeo haya yalimtosheleza Mungu? Yaweza kusemekana kwamba matokeo haya yalimtosheleza Mungu na kwamba ndiyo ambayo Mungu alitaka, na ndiyo ambayo Mungu alikuwa ametamani kuyaona. Je, hili ni kweli? Ingawaje, katika miktadha tofauti, Mungu anatumia njia tofauti za kupima kila mtu. Kwa Ibrahimu Mungu aliona kile Alichotaka, Aliona kwamba moyo wa Ibrahimu ulikuwa wa kweli, na kwamba utiifu wake haukuwa na masharti na ilikuwa hali hii hasa ya “kutokuwa na masharti” ambayo Mungu alitamani. Watu mara nyingi husema, tayari nimetoa hii, tayari nimeachana na ile—kwa nini bado Mungu hajatosheka na mimi? Kwa nini Anaendelea kuniweka katika majaribio? Kwa nini Anaendelea kunijaribu? Hii yaonyesha ukweli mmoja: Mungu bado hajauona moyo wako, na bado hajapata moyo wako. Hivi ni kusema, Hajauona uaminifu kama wakati ule ambao Ibrahimu aliweza kukiinua kisu chake ili kumuua mtoto wake kwa mkono wake mwenyewe na kumtoa kwa Mungu. Bado Hajauona utiifu wako usio na masharti, na hajatulizwa na wewe. Ni jambo la kiasili, hivyo basi, kwamba Mungu anaendelea kukujaribu. Je, haya si kweli?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp