Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 609

26/09/2020

Watu ambao wanamwamini Mungu kwa muda mrefu sasa wametumainia hatima iliyo nzuri, watu wote ambao wanamwamini Mungu wanatumai kwamba bahati nzuri itawajia ghafla, na wote wanatumai kwamba bila kujua, watajikuta wameketi kwa amani pahali pamoja au pengine mbinguni. Lakini Ninasema watu hawa kwa mawazo yao mazuri hawajawahi kujua kama wana sifa ya kupokea bahati nzuri kama hiyo inayoanguka kutoka mbinguni, au kukaa juu ya kiti huko mbinguni. Kwa sasa nyinyi mna maarifa mazuri kujihusu, lakini bado mnatarajia kwamba mnaweza kuepuka maafa ya siku za mwisho na mkono wa mwenye Uweza ukiwaadhibu wale waovu. Inaonekana kana kwamba kuwa na ndoto tamu na kutaka vitu kama tu wanavyopenda ni jambo la kawaida la watu wote ambao Shetani amewapotosha, si kipaji cha ajabu cha mtu fulani binafsi. Hata hivyo, bado Nataka kukomesha tamaa zenu badhirifu na hamu zenu za kupata baraka. Kwa kuwa dhambi zenu ni nyingi na ukweli wa kutotii kwenu ni mwingi na unaongezeka kila wakati, haya yanawezaje kupatana na ramani zenu nzuri za baadaye? Kama unataka kuendelea unavyopenda kuwa mwenye makosa, bila chochote kinachokuzuia, lakini bado unataka ndoto zitimie, basi Nakusihi uendelee katika usingizi wako na usiamke kamwe, kwa sababu unaota ndoto isiyoweza kutimia, na haitatumika kukufanya uwe mtu usiye wa kawaida mbele ya Mungu mwenye haki. Kama unataka tu ndoto zitimie, basi usiote kamwe, lakini kabiliana na ukweli milele, kabiliana na mambo ya hakika. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kukuokoa. Je, kwa maneno thabiti, hatua za taratibu hizi ni zipi?

Kwanza, fanya uchunguzi wa dhambi zako zote, na kuchunguza mwenendo na mawazo yako yote ambayo hayafuati ukweli.

Hiki ni kipengee ambacho mnaweza kukifanya kwa urahisi, na Ninaamini kwamba watu wanaofikiri wanaweza kufanya hivi. Hata hivyo, wale watu ambao hawajui kamwe ni nini maana ya dhambi na ukweli ni tofauti, kwa sababu kimsingi wao si watu wa kufikiri. Mimi nazungumza na watu ambao wamethibitishwa na Mungu, ni waaminifu, hawajazikosea vibaya amri za utawala, na wanaweza kupata dhambi zao wenyewe kwa urahisi. Ingawa hiki ni kipengee ambacho Ninahitaji kwenu ambacho ni rahisi kwenu, sicho kipengee cha pekee Ninachohitaji kwenu. Lolote litokealo, Ninatumai kwamba hamtalicheka hitaji hili kwa siri, au hata zaidi, kwamba hamtaliangalia kwa dharau au kulichukulia kimzaha. Lichukulieni kwa umakini, na msilipuuze.

Pili, kwa kila moja ya dhambi na kutotii kwako tafuta ukweli unaoambatana na utumie ukweli huu kuzitatua, kisha badilisha vitendo vyako vya dhambi na mawazo yako na vitendo vya kutotii na kutenda ukweli.

Tatu, kuwa mtu mwaminifu, si mtu ambaye siku zote anakuwa mjanja, mwenye hila daima. (Hapa Ninakusihi tena uwe mtu mwaminifu.)

Kama unaweza kutimiza vipengee hivi vyote vitatu basi una bahati, wewe ni mtu ambaye ndoto zake zinatimia na ambaye hupata bahati nzuri. Labda mtayachukulia maombi haya matatu yasiyovutia kwa umakini, au labda mtayachukulia bila kuwajibika. Kwa vyovyote vile, azma Yangu ni kutimiza ndoto zenu, kuweka mawazo yenu katika matendo, si kuwadhihaki au kuwadanganya.

Madai Yangu yanaweza kuwa rahisi, lakini kile Ninachowaambia si rahisi hivyo kama kujumlisha moja na moja upate mbili. Kama mnazungumzia tu mambo haya bila kufikiria, mkiongea sana kwa kuparaganya kwa maneno matupu ya majivuno yanayopita kiasi, basi ramani zenu na matakwa yenu yatakuwa ukurasa mtupu milele. Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale kati yenu ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Kinyume cha hayo, Mimi Huwatendea wale ambao hawajatosheleza madai Yangu kwa adhabu, siyo zawadi, sembuse huruma yoyote. Labda mnawaza kwamba kwa kuwa wafuasi kwa miaka mingi mnaweka bidii bila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote mnaweza kupata bakuli la wali katika nyumba ya Mungu kwa kuwa watendaji huduma. Ningesema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu siku zote hadi sasa mmekuwa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani na kutokuwa na manufaa kwa wengine. Hivyo Mimi nawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kusifiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile ambacho Nimedai, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia madai Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu, na hali ikiwa bora zaidi Niigeuze miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwa utupu, kwa sababu Siwezi kuwaleta katika ufalme Wangu maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani, katika enzi ijayo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp