Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 72

Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba mambo mengi yalifanyika Bwana Yesu alipozaliwa. Kubwa zaidi miongoni mwa hayo lilikuwa kutafutwa na mfalme wa ibilisi, hadi kufikia kiwango cha watoto wote wenye umri wa miaka miwili na chini katika eneo hilo kuchinjwa. Ni dhahiri kwamba Mungu alichukua hatari kubwa kwa kuwa mwili miongoni mwa binadamu; gharama kubwa Aliyolipia kwa ajili ya kukamilisha usimamizi Wake wa kumwokoa mwanadamu pia ni wazi. Matumaini makubwa ambayo Mungu alishikilia kwa ajili ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu katika mwili pia ni wazi. Wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi miongoni mwa wanadamu, Alikuwa anahisi vipi? Watu wanafaa kuweza kuelewa hilo kidogo, sivyo? Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu alifurahia kwa sababu Angeanza kuendeleza kazi Yake mpya miongoni mwa wanadamu. Bwana Yesu alipobatizwa na kuanza rasmi kazi Yake kukamilisha huduma Yake, moyo wa Mungu ulijawa na furaha kwa sababu baada ya miaka mingi sana ya kusubiri na matayarisho, hatimaye Angeweza kuuvaa mwili wa binadamu wa kawaida na kuanza kazi Yake mpya katika umbo la binadamu aliye na mwili na damu ambao watu wangeweza kuona na kugusa. Angeweza kuzungumza ana kwa ana na moyo kwa moyo na watu kupitia utambulisho wa binadamu. Mungu hatimaye angeweza kuwa ana kwa ana na mwanadamu katika lugha ya kibinadamu, kwa njia ya kibinadamu; Angeweza kumruzuku mwanadamu, kumwelimisha binadamu, na kumsaidia binadamu kwa kutumia lugha ya kibinadamu; angeweza kula kwenye meza moja na kuishi katika nafasi sawa na binadamu. Angeweza pia kuwaona binadamu, kuona vitu, na kuona kila kitu kwa njia ambayo binadamu walifanya hivyo na hata kupitia kwa macho yao. Kwake Mungu, huu ulikuwa tayari ushindi Wake wa kwanza wa kazi Yake katika mwili. Yaweza pia kusemekana kwamba yalikuwa ni ufanikishaji wa kazi kubwa—hili bila shaka ndilo ambalo Mungu alilifurahia zaidi. Kuanzia hapo ndiyo mara ya kwanza ambayo Mungu alihisi tulizo fulani katika kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Matukio haya yote yalikuwa ya kimatendo sana na ya asili sana, na tulizo ambalo Mungu alihisi lilikuwa halisi. Kwa mwanadamu, kila mara hatua mpya ya kazi ya Mungu inapokamilishwa, na kila mara Mungu anapohisi kuridhika, ndipo mwanadamu anapoweza kusogea karibu zaidi na Mungu, na ndipo watu wanapoweza kusonga karibu zaidi na wokovu. Kwa Mungu, huu pia ni uzinduzi wa kazi Yake mpya, wakati mpango Wake wa usimamizi unapoendelea hatua moja zaidi, na, aidha, wakati mapenzi Yake yanapokaribia mafanikio kamili. Kwa mwanadamu, kuwasili kwa fursa kama hiyo ni bahati, na nzuri sana; kwa wale wote wanaosubiria wokovu wa Mungu, ni habari za maana sana. Mungu anapotekeleza hatua mpya ya kazi, basi Anao mwanzo mpya na wakati ambapo kazi hii mpya na mwanzo mpya vinazinduliwa na kufahamishwa miongoni mwa binadamu, ni wakati ambao matokeo ya hatua hii ya kazi tayari yameamuliwa, na kufanikishwa, naye Mungu tayari ameona athari yake ya mwisho na tunda. Huu pia ndio wakati ambapo athari hizi zinamfanya Mungu aridhike, na moyo Wake, bila shaka una furaha. Kwa sababu katika macho ya Mungu, tayari ameona na kuamua watu anaowatafuta, na tayari Amelipata kundi hili, kundi ambalo linaweza kufanya kazi Yake kufanikiwa na kumpa utoshelevu, Mungu anahisi Akiwa ameondolewa shaka, Anaweka pembeni wasiwasi Wake, na Anahisi mwenye furaha. Kwa maneno mengine, wakati mwili wa Mungu unaweza kuanza kazi mpya miongoni mwa binadamu, na Anaanza kufanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kizuizi, na wakati Anapohisi kwamba yote yamefanikishwa, tayari Ameuona mwisho. Na kwa sababu ya mwisho huu Anatosheka, na kuwa mwenye moyo wa furaha. Furaha ya Mungu inaonyeshwa vipi? Unaweza kufikiria hayo? Je, Mungu Angeweza kulia? Mungu Anaweza kulia? Mungu Anaweza kupiga makofi? Mungu Anaweza kucheza? Mungu Anaweza kuimba? Na wimbo huo ungekuwa upi? Bila shaka Mungu Angeweza kuimba wimbo mzuri, wa kusisimua, wimbo ambao unaweza kuonyesha shangwe na furaha katika moyo Wake. Angeweza kuwaimbia binadamu, kujiimbia Mwenyewe, na kuuimba kwa viumbe vyote. Furaha ya Mungu inaweza kuonyeshwa kwa njia yoyote—yote haya ni kawaida kwa sababu Mungu ana shangwe na huzuni, na hisia Zake mbalimbali zinaweza kuonyeshwa kwa njia mbalimbali. Hii ndiyo haki Yake na ndilo jambo la kawaida zaidi. Hufai kufikiria chochote kingine kuhusu hili, na hufai kupisha vizuizi vyako binafsi kwa Mungu, huku ukimwambia kwamba Yeye hafai kufanya hiki wala kile, Hafai kutenda kwa njia hii au ile, kuwekea mipaka shangwe Yake au hisia yoyote ile Aliyo nayo. Katika mioyo ya watu Mungu hawezi kuwa na furaha, Hawezi kutokwa na machozi, Hawezi kulia—Hawezi kuonyesha hisia zozote. Kupitia yale tuliyowasiliana katika nyakati hizi mbili, Naamini hamtamwona tena Mungu kwa njia hii, lakini mtamruhusu Mungu kuwa na uhuru na uachiliaji fulani. Hiki ni kitu kizuri. Katika siku za usoni kama mtaweza kuhisi kwa kweli huzuni ya Mungu mnaposikia kwamba Yeye ana huzuni, na mnaweza kuhisi kwa kweli shangwe Yake mnaposikia kuhusu Yeye kuwa na furaha—angalau, mnaweza kujua na kuelewa waziwazi kile kinachomfanya Mungu kuwa na furaha na kile kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni—unapoweza kuhisi huzuni kwa sababu Mungu ana huzuni na kuhisi furaha kwa sababu Mungu ana furaha, Atakuwa ameupata moyo wako na hakutakuwa tena na kizuizi chochote na Yeye. Hamtajaribu tena kumzuilia Mungu na fikira na maarifa ya binadamu. Wakati huo, Mungu atakuwa hai na dhahiri moyoni mwako. Atakuwa Mungu wa maisha yako na Bwana wa kila kitu chako. Je, mnalo tamanio kama hili? Je, mnayo imani kuwa mnaweza kutimiza haya?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp