Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 120

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo

Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa Kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na hali halisi hii. Kwa nini tuzungumzie mamlaka ya Mungu? Mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanatofautiana vipi na mamlaka yaliyomo kwenye akili ya binadamu? Ni nini maalum sana kuyahusu? Na kunao umuhimu gani haswa kuyazungumzia hapa? Kila mmoja wenu lazima aweze kutilia maanani kwa umakinifu suala hili. Kwa watu wengi zaidi, “Mamlaka ya Mungu” ni fikira isiyoeleweka, ile ambayo ni ngumu sana kupata kuielewa, na mazungumzo yoyote kuihusu huenda yasizae matunda mazuri. Kwa hivyo lazima kutakuwepo na pengo kati ya maarifa ya mamlaka ya Mungu ambayo binadamu anaweza kumiliki, na hali halisi ya mamlaka ya Mungu. Ili kuliziba pengo hili, mtu lazima kwa utaratibu aweze kuelewa mamlaka ya Mungu kwa njia ya watu halisi-maishani, matukio, vitu au mambo muhimu yanayopatikana katika uwezo wa binadamu, na ambayo binadamu wanaweza kuyaelewa. Ingawaje kauli hii “Mamlaka ya Mungu” inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni ithibati tosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na unakuruhusu kabisa kutambua na kuelewa hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya.

Mungu aliumba kila kitu, na baada ya kukiumba, Anao utawala juu ya kila kitu. Kuongezea kuwa na utawala juu ya kila kitu, pia anadhibiti kila kitu. Wazo hili linamaanisha nini “Mungu anadhibiti kila kitu”? Hali hii inaweza kuelezewa vipi? Hali hii inatumika vipi katika maisha halisi? Mnawezaje kuyajua mamlaka ya Mungu kwa kuelewa hoja hii kwamba “Mungu Anadhibiti kila kitu”? Kutoka kwenye kauli ile ile “Mungu anadhibiti kila kitu” tunafaa kuona kwamba kile ambacho Mungu anadhibiti si sehemu ya sayari, sehemu ya uumbaji, wala sehemu ya mwanadamu, lakini kila kitu: kuanzia kwa viumbe vile vikubwa hadi vile vidogovidogo, kuanzia kwa vile vinavyoonekana hadi visivyoonekana, kuanzia kwa nyota ulimwenguni hadi kwenye vitu vilivyo na uhai ulimwenguni, pamoja na viumbe vidogovidogo visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida au viumbe vilivyo katika maumbo mengine. Huu ndio ufafanuzi hakika wa “kila kitu” ambacho Mungu “anadhibiti,” na ndio upana ambao Mungu anaonyesha ukuu Wake, urefu wa utawala na kanuni Yake.

Kabla ya binadamu hawa kujitokeza, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa uwepo wavyo wote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata ruwaza maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data yenye uhakika; njia ambazo zinasafiria, kasi na ruwaza ya mizingo yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa hakika na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kupotoka hata chembe. Hakuna nguvu inaweza kubadilisha au kutatiza mizingo yazo au ruwaza zao ambazo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum zinazotawala mzunguko wazo na data yenye uhakika inayozifafanua iliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu ruwaza fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na ruwaza zinazoonyesha mzunguko wavyo, vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Hoja hii inampa binadamu mshawasha wa kukubaliana na kutambua kwamba kunaye Mwenyezi aliye miongoni mwa ruwaza hizi za mzunguko, anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei-kimaumbile lakini zinaamrishwa na Bwana na Mungu. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.

Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi. Kwa nini hali iko hivi? Jibu la pekee tu ni, kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Au, nikijibu kwa njia nyingine, kwa sababu ya fikira za Mungu na matamshi ya Mungu; kwa sababu Mungu Mwenyewe hufanya haya yote. Hivi ni kusema, ni mamlaka ya Mungu na ni akili ya Mungu ambayo iliunda sheria hizi; zitasonga na kubadilika kulingana na fikira Zake, na kusonga huku na mabadiliko haya yote yanafanyika au kutoweka kwa minajili ya mpango Wake. Hebu tuchukulie magonjwa ya mlipuko, kwa mfano. Yanazuka tu bila onyo, hakuna anayejua asili yake, au sababu maalum zinazoelezea ni kwa nini huwa yanafanyika, na kila wakati magonjwa ya mlipuko yanapofika mahali fulani, wale walio na bahati mbaya hawawezi kukwepa maafa. Sayansi ya binadamu inafafanua na kutuelewesha kwamba magonjwa ya mlipuko yanasababishwa na kuenea kwa vijiumbe maradhi vibaya au haribifu, na kasi yao, eneo lao, na mbinu ya kuenea kwake haiwezi kutabiriwa au kudhibitiwa na sayansi ya binadamu. Ingawaje binadamu huvipinga vijiumbe maradhi hivi kwa kila namna inayowezekana, huwa hauwezi kudhibiti ni watu gani au wanyama gani ambao wanaathiriwa kwa vyovyote vile wakati kunapokuwa na mkurupuko wa magonjwa mlipuko. Kitu cha pekee ambacho binadamu wanaweza kufanya ni kujaribu kuyazuia, kuyapinga, na kuyafanyia utafiti. Lakini hakuna anayejua chanzo asilia kinachoelezea mwanzo au mwisho wa magonjwa mlipuko yoyote ya kibinafsi, na hakuna anayeweza kuyadhibiti. Wakiwa wamekabiliwa na ongezeko na kuenea kwa magonjwa mlipuko, suala la kwanza ambalo binadamu hufanya ni kuunda chanjo, lakini mara nyingi magojwa mlipuko hayo hutoweka kabisa kabla ya hata chanjo kuwa tayari. Kwa nini magonjwa mlipuko hutoweka kabisa? Wengine husema kwamba viini vimeweza kudhibitiwa, wengine husema kwamba vimetoweka kabisa kwa sababu ya mabadiliko katika misimu…. Kuhusiana na ikiwa makisio haya ya kuchanganyikiwa ni kweli au la, sayansi haiwezi kutupa ufafanuzi wowote, na wala haitoi jibu lolote lenye uhakika. Kile ambacho binadamu wanakabiliwa nacho si makisio haya tu lakini pia ukosefu wa mwanadamu katika kuelewa na woga wa magonjwa mlipuko haya. Hakuna anayejua, baada ya kila kitu kuchambuliwa, ni kwa nini magonjwa mlipuko haya huanza au ni kwa nini huisha. Kwa sababu binadamu wanayo imani tu katika sayansi, unategemea pakubwa kwa sayansi hiyo, lakini hautambui mamlaka ya Muumba au kuukubali ukuu Wake, hautawahi kuwa na jibu.

Katika ukuu wa Mungu, mambo yote yapo na huangamia kwa sababu ya mamlaka Yake, kwa sababu ya usimamizi Wake. Baadhi ya mambo huja na kwenda polepole, na binadamu hawezi kutambua ni wapi yalitokea au kung’amua sheria ambazo mambo haya hufuata, sisemi hata kuelewa sababu za mambo haya kuja na kwenda. Ingawaje binadamu anaweza kushuhudia, kusikia, au kupitia yote yanayokuja na kuisha miongoni mwa mambo yote; ingawaje mambo haya yanao mwelekeo kwa binadamu, na ingawaje binadamu hung’amua kupitia kwa yaliyofichika akilini mwake, hali isiyokuwa ya kawaida, hali ya mara kwa mara au hata hali ya ajabu ya mambo mbalimbali, bado hajui chochote kuhusu mapenzi ya Muumba na akili Yake ambavyo vinaelezea mambo hayo. Kunazo hadithi nyingi zinazotokana na haya mambo yote, ukweli mwingi uliofichwa. Kwa sababu binadamu amepotoka na kwenda mbali na Muumba, kwa sababu hakubali hoja hii kwamba Mamlaka ya Muumba ndiyo hutawala mambo yote, hatawahi kujua kila kitu kinachofanyika katika ukuu Wake. Kwa sehemu nyingi zaidi, udhibiti na ukuu wa Mungu huzidi mipaka ya fikra ya binadamu, maarifa ya binadamu, kuelewa kwa binadamu, kuhusu kile ambacho sayansi ya binadamu inaweza kutimiza; uwezo wa binadamu walioundwa hauwezi kushindana nao. Baadhi ya watu husema “Kwa sababu hujashuhudia ukuu wa Mungu wewe mwenyewe, unawezaje kusadiki kwamba kila kitu kinatokana na mamlaka Yake?” Kuona si kuamini kila mara; kuona si kutambua na kuelewa kila mara. Kwa hivyo sadiki hutokea wapi? Ninaweza kusema kwa uhakika, “Sadiki inatokana na kiwango na kina cha kuelewa kwa watu kwa, na hali wanayopitia wao, uhalisi na chanzo kikuu cha mambo.” Kama unasadiki kwamba Mungu yupo, lakini huwezi kutambua, na wala huwezi kuelewa, hoja ya udhibiti wa Mungu na ukuu wa Mungu katika mambo yote, basi katika moyo wako hutawahi kukubali kwamba Mungu anayo mamlaka kama haya na kwamba mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Hutawahi kukubali kwa kweli Muumba kuwa Bwana wako, Mungu wako.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp