Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 352

13/08/2020

Tayari Nimeshasema kuwa wale wanaonifuata ni wengi lakini wanaonipenda kwa moyo wa kweli ni wachache. Huenda ikawa wengine wanasema, “Ningeweza kujinyima mengi kiasi hicho ikiwa sikupendi Wewe? Ningeendelea bado kukufuata ikiwa sikupendi?” Unazo sababu nyingi kwa hakika. Kwa hakika, upendo wako ni mkubwa, lakini nini umuhimu wa mapenzi yako Kwangu? “Upendo,” kama unavyoitwa, unaashiria hisia safi isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi, na kuwa na mawazo. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi na hakuna kutenga. Katika upendo hakuna shaka, hakuna uongo na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna kukaa mbali na hakuna kitu kisicho safi. Ukipenda, basi hudanganyi, hulalamiki, huasi na hupeani au kuchukua rushwa. Ukipenda, basi unajinyima bila kusononeka, unavumilia hali ngumu, na unaambatana na Mimi. Ungeacha vitu vyako vyote kwa sababu Yangu: familia yako, siku zako za baadaye, ujana wako, na ndoa yako. La sivyo, basi upendo wako si upendo hata kidogo, bali ni uongo na usaliti! Upendo wako ni upendo wa aina gani? Je, ni upendo wa kweli? Je, ni wa uongo? Umejinyima kiasi gani? Umejitolea kiasi gani? Je, Nimepata upendo kiasi gani kutoka kwako? Je, unajua? Moyo wenu umejaa maovu, usaliti na uongo. Kwa hivyo kiwango kipi cha upendo wenu ni kichafu? Mnaamini kuwa mmewacha kila kitu kwa ajili Yangu; Mnaamini kuwa upendo wenu Kwangu tayari umetosha, ila ni kwa nini maneno yenu na matendo yenu huambatana na uasi na uongo? Mnanifuata, ilhali hamkubali neno Langu. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, kisha mnanitenga na kuniweka kando. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali mko na shaka na Mimi. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, ilhali hamkubali kuwepo Kwangu. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali hamnitendei vile Ninavyopaswa kutendewa na mnafanya mambo yawe magumu Kwangu katika kila hatua. Je, hii inachukuliwa kama mapenzi? Mnanifuata, ilhali mnanichukua kama mjinga na kunidanganya Mimi katika kila jambo. Je, haya ni mapenzi? Mnanihudumia, ilhali hamnichi. Je, huu ni upendo? Mnanipinga katika kila hali na kila jambo. Je, yote haya yanachukuliwa kama upendo? Mmejinyima mengi, huu ni ukweli, ilhali hamjawahi kuyafanya Ninayowaagiza mfanye. Je, huu unaweza kuwa upendo? Uchunguzi wa makini unaashiria kuwa hamna upendo Kwangu ndani yenu. Baada ya miaka hii mingi ya kazi na maneno mengi Niliyosambaza, ni kiasi kipi mlichopokea kwa hakika? Je, hii haistahili mtazamo mwangalifu wa nyuma? Ninawaonya: Wale Niwaitao sio wale ambao hawajapotoshwa, bali wale Ninaowachagua ni wale wanaonipenda kwa ukweli. Kwa hivyo, mnapaswa kuwa makini na maneno na matendo yenu, na muichunguze azma na mawazo yenu ili vitu hivi visije vikavuka mipaka. Wakati wa mwisho, fanyeni jitihada ili muonyeshe mapenzi yenu Kwangu, isije ghadhabu yangu ikabaki kwenu milele!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Upendo Safi Bila Dosari

I

Upendo ni hisia safi, safi bila dosari. Tumia moyo, tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki, hutazamii kupata kitu, cha malipo. Ukipenda utajitolea, ukubali taabu, kuwa kimoja, Mungu katika mapatano.

II

Upendo hauna shauku, ujanja wala uongo. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Upendo haujitengi, upendo hauna dosari. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki, hutazamii kupata kitu cha malipo. Ukipenda utajitolea, ukubali taabu, kuwa kimoja, Mungu katika mapatano.

III

Utatoa familia, ujana wako na siku za usoni. Utoe ndoa yako kwa Mungu, toa vyote kwake. Utatoa familia, ujana na siku za usoni. Utoe ndoa yako kwa Mungu, toa vyote kwake. Ama upendo wako si upendo kabisa, bali uongo, usaliti kwa Mungu.

IV

Upendo ni hisia safi, safi bila dosari. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp