Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 151

Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu

Mienendo ya kijamii ilianza lini? Je, ni kitu kipya? (La.) Hivyo mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.) Katika akili zenu, ni kipengele kipi cha mienendo hii kinaweza kumpotosha mwanadamu? Ni mienendo ipi inawavutia sana? Watu wengine husema: “Sisi sote tumefikia umri fulani, tuko katika miaka ya arobaini, hamsini, sitini, sabini ama themanini ambapo hatuwezi kufaa katika mienendo hii na haituvutii tena.” Je, hii ni sahihi? Wengine husema: “Hatufuati watu mashuhuri, hicho ni kitu ambacho vijana walio katika umri wa ujana na ishirini wanafanya; pia hatuvai nguo za mitindo ya kisasa, hicho ni kitu ambacho watu wanaojali sura wanafanya.” Kwa hivyo ni ipi kati ya hii inaweza kuwapotosha? (Misemo maarufu.) Je, hii misemo maarufu inaweza kuwapotosha watu? Huu ni msemo mmoja, na mnaweza kuona iwapo unawapotosha watu au la, “Pesa inaifanya dunia izunguke”; huu ni mwenendo? Si hiki ni kitu kibaya zaidi kulinganishwa na mienendo ya mavazi na chakula mliyotaja? (Ndiyo.) “Pesa inaifanya dunia izunguke” ni filosofia ya Shetani na inaenea miongoni mwa wanadamu wote, katika kila jamii ya binadamu. Mnaweza kusema kwamba ni mwenendo kwa sababu umepatiwa kila mtu na sanasana uko katika mioyo yao. Watu walienda kutoka kutoukubali msemo huu hadi kuuzoea ili wanapokutana na maisha halisi, polepole waliukubali kwa kimya, kukiri uwepo wake na hatimaye, waliupa muhuri wao wa idhini. Je, hii si njia ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Pengine watu hawaelewi msemo huu kwa kiwango sawa, lakini kila mtu ana viwango tofauti vya tafsiri na kukiri kwa msemo huu kutokana na mambo ambayo yamefanyika karibu nao na uzoefu wao binafsi, siyo? Licha ya kiwango cha uzoefu mtu anao na msemo huu, ni nini athari mbaya unaweza kuwa nao katika moyo wa mtu? Kitu fulani kinafichuliwa kupitia tabia ya binadamu ya watu katika dunia hii, ikiwemo kila mmoja wenu. Hiki kinafasiriwa vipi? Ni ibada ya pesa. Ni vigumu kutoa hili kwa moyo wa mtu? Ni vigumu sana! Inaonekana kwamba upotovu wa Shetani kwa mwanadamu ni kamili kabisa! Hivyo baada ya Shetani kutumia mwenendo huu kuwapotosha watu, unaonyeshwa vipi kwao? Hamhisi kwamba hamtaishi katika dunia hii bila pesa yoyote, kwamba hata siku moja haiwezekani? Hadhi ya watu inatokana na kiasi cha pesa wako nayo na pia heshima yao. Migongo ya maskini imekunjwa kwa aibu, ilhali matajiri wanafurahia hadhi zao za juu. Wanatenda kwa njia ya kujigamba na wana majivuno, wakiongea kwa sauti kubwa na kuishi kwa kiburi. Msemo na mwenendo huu unaleta nini kwa watu? Si watu wengi wanaona kupata pesa kunastahili gharama yoyote? Si watu wengi hutoa Heshima na uadilifu wao wakitafuta pesa zaidi? Si watu wengi hupoteza fursa ya kufanya wajibu wao na kumfuata Mungu kwa sababu ya pesa? Si hii ni hasara kwa watu? (Ndiyo.) Si Shetani ni mbaya kutumia mbinu hii na msemo huu kumpotosha mwanadamu kwa kiwango kama hicho? Si hii ni hila yenye kijicho? Unaposonga kutoka kuukataa huu msemo maarufu hadi mwishowe kuukubali kama ukweli, moyo wako unaanguka kabisa chini ya mshiko wa Shetani, na hivyo unakuja kuishi naye bila kusudi. Msemo huu umekuathiri kwa kiwango kipi? Unaweza kujua njia ya ukweli, unaweza kujua ukweli, lakini huna nguvu ya kuufuatilia. Unaweza kujua kwa hakika neno la Mungu, lakini huko radhi kulipa gharama, huko radhi kuteseka kulipa gharama. Badala yake, kwako, ni afadhali utoe siku zako za baadaye na kudura yako kwenda kinyume na Mungu hadi mwisho kabisa. Licha ya kile Mungu anasema, licha ya kile Mungu anafanya, licha ya kiasi unagundua kwamba upendo wa Mungu kwako ni wa kina na mkubwa, bado ungeendelea kwa njia hiyo kwa ukaidi na kulipa gharama ya msemo huu. Hiyo ni kusema huu msemo tayari unadhibiti tabia na fikira zako, na unaona afadhali hatima yako idhibitiwe na msemo huu kuliko kuyatoa yote. Watu wanafanya hivi, wanadhibitiwa na msemo huu na kutawaliwa nao. Hii si athari ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Hii si filosofia na tabia potovu ya Shetani ikikita mizizi kwa moyo wako? Ukifanya hivyo, si Shetani amefikia lengo lake? (Ndiyo.) Unaona jinsi Shetani amempotosha mwanadamu kwa njia hii? Unaweza kumhisi? (La.) Hukumwona. Hukuihisi. Je, unaona uovu wa Shetani hapa? Shetani humpotosha mwanadamu wakati wote na pahali pote. Shetani anaifanya isiwezekane kwa mwanadamu kujilinda dhidi ya upotovu huu na anamfanya mwanadamu awe mnyonge kwake. Shetani anakufanya ukubali fikira zake, mitazamo yake na mambo maovu yanayotoka kwake katika hali ambapo huna kusudi na huna utambuzi wa kile kinachokufanyikia. Watu wanakubali kikamilifu vitu hivi na hawavibagui. Wanapenda sana vitu hivi na kuvishikilia kama hazina, wanaviacha vitu hivi viwatawale na kuwachezea, na hivi ndivyo upotovu wa Shetani kwa mwanadamu unakuwa wa kina na kina zaidi.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp