Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 311
22/10/2020
Kutoka juu hadi chini na kuanzia mwanzo hadi mwisho, Shetani amekuwa akiisumbua kazi ya Mungu na kutenda kinyume na Yeye. Mazungumzo yote ya urithi wa utamaduni wa kale, maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale, mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius, na maandiko bora ya Confucius na ibada ya kishirikina vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, na vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekani popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na “masokwe” wa kale kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu kwa makusudi. Hajamtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wako tayari kumpokea Mungu na kuukaribisha ujio wa Mungu kwa furaha. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kila mara kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi inayoungua na ubani, ni harufu nzito sana inayosababisha kukosa hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo lazima mwanadamu hawezi kujizuia kutapika. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti hii inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii sanamu zimetapakaa, zikiwa na rangi zote za upinde wa mvua, ambazo zinaibadilisha nchi kuwa ulimwengu unaometameta, na mfalme wa mashetani anakenua, kana kwamba njama yake mbovu imefanikiwa. Wakati ule ule, mwanadamu hana habari kumhusu, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwisha mharibu kiasi kwamba hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani kumfutilia mbali Mungu mara moja, kumtukana na kumwangamiza tena, naye anajaribu kuharibu na kuvuruga kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu “kuingilia kati” kazi yake miongoni mwa wanadamu wa duniani? Anawezaje kumruhusu Mungu kuufichua uso wake wa chuki? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kati kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu, aliyejawa kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kutawala nguvu yake duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? Akiwa na roho mbaya, bado anaamini kwamba yeye ni mzuri kupita kiasi. Genge hili la washiriki jinai! Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemharibu mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu anafanana na wanyama wabaya wasioweza kuvumilika, wala hana tena hata chembe ya mwanadamu asilia mtakatifu. Hata wanatamani kutawala kama madikteta duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu ili kwamba isiweze kusonga mbele hata kidogo na kumfunga mwanadamu kana kwamba wapo nyuma ya kuta za shaba na chuma cha pua. Baada ya kufanya dhambi nyingi sana na kusababisha shida nyingi sana, wanawezaje kutarajia kitu chochote tofauti na kusubiri kuadibu? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanaupinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, kwa kuwa mfalme wao amepanda kwenye kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakiwaongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi ili watikise vichwa vyao na kuchochea vurugu. Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu wa wafalme wote, bila kutambua kwamba wao si chochote zaidi ya nzi juu ya kitu kilichooza. Si hivyo tu, wanatoa maoni ya kashfa dhidi ya uwepo wa Mungu kwa kuwategemea wazazi wao nguruwe na mbwa. Nzi wadogo wanadhani wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi mwenye meno. Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, ilhali wazazi wao ni nguruwe na mbwa wachafu mara bilioni kuliko wao wenyewe? Bila kutambua hali yao wenyewe ya kuwa duni, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na kiburi na wanajiinua kila mahali kuhusu uzuri wao na mvuto wao wenyewe, wanamtupia mwanadamu uchafu wao kwa siri. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao wenyewe, na hivyo wanautesa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea kisa cha ndani cha ulimwengu wa kidini). Mwanadamu hajui kwamba, ingawa mbawa za nzi ni nzuri na za kupendeza, hata hivyo ni nzi mdogo tu aliyejaa uchafu na kujawa na vijidudu. Kwa kutegemea uwezo wa wazazi wao nguruwe na mbwa, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya kuungwa mkono kabisa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliozidi. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza tena kazi yao ya utesaji, wakiendeleza kazi yao ya muda wa maelfu kadhaa ya miaka. Kikundi hiki cha waliopotoka hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu hata zaidi. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Wao ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani inamfanya Mungu atoe sauti kuu, na Hawezi kujizuia kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize. Ili mwanadamu ampende Mungu ni lazima aelewe mapenzi Yake na furaha na huzuni Yake, vilevile na kile Anachokichukia zaidi. Hii itakuza zaidi kuingia kwa mwanadamu. Kadiri mwanadamu anavyoingia kwa haraka, ndivyo moyo wa Mungu unavyoridhika zaidi; kadiri mwanadamu anavyomtambua kwa uwazi mfalme wa mashetani, ndivyo mwanadamu anavyosogea karibu zaidi na Mungu, ili kwamba matamanio Yake yaweze kutimia.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video