Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 216

Kazi ya usimamizi wa Mungu ilianza Alipoumba ulimwengu, na mwanadamu ni kiini cha kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa kila kitu, unaweza kusemwa, ni kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu Kazi ya usimamizi Wake imesambaa katika maelfu ya miaka, na haijatekelezwa katika dakika na sekunde tu, ama kufumba na kufumbua, ama katika mwaka mmoja au miwili, ilimbidi Aumbe vitu vingine zaidi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, kama vile jua, mwezi, na aina zote za viumbe walio hai, na chakula na mazingira kwa ajili ya wanadamu. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa usimamizi wa Mungu.

Baada ya hapo, Mungu Alimkabidhi mwanadamu kwa Shetani, mwanadamu aliishi chini ya miliki ya Shetani, na hili taratibu lilisababisha kazi ya Mungu ya enzi ya kwanza: hadithi ya Enzi ya Sheria…. Kipindi cha miaka elfu kadhaa za Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wazoefu wa maelekezo ya Enzi ya Sheria, na wakaanza kupuuza, na taratibu wakaacha ulinzi wa Mungu. Na hivyo, pamoja na kushikilia sheria, walimwabudu Mungu na kutenda matendo maovu. Walikuwa bila ulinzi wa Yehova, na waliishi tu mbele ya madhabahu ndani ya hekalu. Kwa kweli, Kazi ya Mungu ilikuwa imejitenga nao kitambo sana, na hata kama Waisraeli walijikita katika sheria, na kulitaja jina la Yehova, na kwa majivuno kuamini kuwa wao pekee ndio walikuwa watu wa Yehova na walikuwa wamechaguliwa na Yehova, utukufu wa Mungu uliwaacha kimyakimya …

Mungu Anapofanya kazi Yake, huacha sehemu moja na taratibu hutekeleza kazi Yake katika sehemu nyingine mpya. Hii huonekana ya kiajabu sana kwa watu ambao wamepooza. Watu wameishi kuvithamini vya zamani na kuvirejelea vipya, vitu visivyofahamika kwa uhasama, au hata kuonekana kama bughudha. Aidha, kazi yoyote mpya Aifanyayo Mungu, kutoka mwanzo hadi mwisho, mwanadamu ndiye huwa wa mwisho kufahamu kuihusu miongoni mwa kila kitu.

Kama ilivyokuwa kawaida, baada ya kazi ya Yehova katika Enzi ya Sheria, Mungu Alianza kazi yake ya hatua ya pili: kwa kuutwaa mwili, kuwa na mwili kama binadamu kwa miaka kumi, ishirini, na kuongea na kufanya kazi Yake Kati ya waumini. Na bado bila mapendeleo, hakuna aliyejua, na ni idadi ndogo tu ya watu walitambua kuwa Alikuwa Mungu Aliyepata mwili baada ya Yesu Kristo kupigiliwa misumari msalabani na kufufuka. … Baada tu ya kazi ya Mungu katika hatua ya pili kukamilika—baada ya kusulubishwa—kazi ya Mungu ya kutoa mwanadamu kwenye dhambi (ambayo ni kusema, kumtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani) ilitimilika. Na hivyo, kutoka wakati huo kuendelea mbele, wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi. Na hivyo, baada ya kushikwa mateka na Shetani, mwanadamu alikuja hatua moja mbele karibu na kukubali wokovu mbele za Mungu. Kwa hakika, huu ulingo wa kazi ndio ulikuwa usimamizi wa Mungu ambao ulikuwa hatua moja mbali na Enzi ya sheria, na wa kiwango cha ndani kuliko Enzi ya Sheria.

Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili; na inaonekana inatatanisha. Watu wanahisi kwamba ni kama hadithi ya visasili, na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, hata hawajui ni hadithi ngapi ambazo zimetokea katika huu ulimwengu. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu. Katika kazi ya usimamizi wa Mungu wa wakati huu, wanadamu ndio chombo cha maovu ya Shetani, na kwa wakati uo huo ni chombo cha ukombozi wa Mungu, aidha ni sababu ya vita dhidi ya Mungu na Shetani. Wakati sawia na wakati wa kutekeleza kazi Yake, Mungu taratibu Humtoa mwanadamu kutoka mikononi mwa Shetani, na hivyo mwanadamu anakuja karibu zaidi na Mungu …

Baadaye kukaja Enzi ya Ufalme, ambayo ni hatua ya utendaji zaidi na bado ni ngumu zaidi kukubalika na mwanadamu. Hii ni kwa sababu jinsi mwanadamu ajavyo karibu na Mungu, ndivyo afikapo karibu na kiboko cha Mungu, na ndivyo uso wa Mungu unavyokuwa wazi mbele ya mwanadamu. Kwa kufuatia kukombolewa kwa wanadamu, mwanadamu kirasmi anarejelea familia ya Mungu. Mwanadamu alifikiria kuwa huu ndio wakati wa kufurahia, bado ameegemezwa kwa shambulizi la Mungu na mifano ya yale bado hayajaonekana na yeyote. Inavyokuwa, huu ni ubatizo ambao watu wa Mungu wanapaswa “kuufurahia.” Katika muktadha huo, watu hawana lingine ila kuacha na kujifikiria wao wenyewe, Mimi ndimi mwanakondoo, aliyepotea kwa miaka mingi, ambaye Mungu Amegharamika kumnunua, sasa kwa nini Mungu Ananitendea hivi? Ama ni njia ya Mungu kunicheka, na kunifichua? … Baada ya miaka mingi kupita, mwanadamu amedhoofika, kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu. Ijapokuwa mwanadamu amepoteza “utukufu” na “mapenzi” ya wakati uliopita, bila ya kufahamu amekuja kuelewa ukweli wa kuwa mwanadamu, na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu. Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe. Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu, na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake. Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma, matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu, na maneno na upendo wa Mungu vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya. Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku, nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza … ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu, na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua. Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba, na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni, lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka, na hatazami kando na uso wa Yehova. Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu, na kutazama uso Wake wenye tabasamu, na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu wanaomilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp