Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kazi na Kuonekana kwa Mungu | Dondoo 68

Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika wanadamu yakitawanyika hapa na pale, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Niliporudi katika “nchi Yangu,” Nilianza sehemu nyingine tena ya kazi katika mpango Wangu wa asili, ili mwanadamu aje kunijua zaidi. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba ni wakati muafaka wa kazi Yangu, kwa hiyo Naharakisha mbele na nyuma, kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Hii ni enzi mpya, hata hivyo, na Nimeleta kazi mpya ili Niwachukue watu wapya wengi zaidi katika enzi mpya na kuachana na wengi wa wale Nitakaowaondoa. Katika taifa la joka kubwa jekundu, Nimetekeleza hatua ya kazi isiyoeleweka kwa wanadamu, kuwafanya kuyumba katika upepo, ambapo baadaye wengi wanabebwa kwa siri na upepo unaovuma. Kweli, huu ni “uwanja wa kupura” Ninaotaka kuusafisha; ni kile Ninachotamani na pia ni mpango Wangu. Kwa maana wengi waovu wameingia ndani kimya wakati Niko kazini, lakini Sina haraka ya kuwafukuza. Badala yake, Nitawatawanya wakati utakapofika. Ni baada ya hapo tu ndipo Nitakuwa chemchemi ya uzima, kuwakubalia wanaonipenda kweli wapokee kutoka Kwangu tunda la mtini na harufu ya yungiyungi. Katika nchi ambako Shetani huishi, nchi ya vumbi, hakuna dhahabu safi iliyobaki, ila ni mchanga tu, na kwa hiyo, Nikikabiliwa na hali hizi, Nafanya hatua hiyo ya kazi. Lazima ujue kwamba Ninachopata ni dhahabu safi, iliyosafishwa, wala si mchanga. Ni jinsi gani waovu wanaweza kubaki katika nyumba Yangu? Ninawezaje kuruhusu Mbweha kuwa vimelea ndani ya paradiso Yangu? Natumia kila mbinu inayoweza kufikiriwa kuvifukuza vitu hivi. Kabla ya mapenzi Yangu kufichuliwa, hakuna anayefahamu Ninachotaka kufanya. Nikichukua fursa hii, Ninawafukuza wale waovu, na wanalazimika kuondoka machoni Pangu. Hili ndilo Mimi huwawafanyia waovu, lakini bado kutakuwa na siku ya wao kunifanyia huduma. Hamu ya watu kupata baraka ni kubwa mno; Kwa hivyo Ninageuza mwili Wangu na kuonyesha uso Wangu wa utukufu kwa nchi za Mataifa, ili watu wote waishi katika dunia yao wenyewe na kujihukumu, huku Naendelea kusema maneno ambayo Napaswa kuyasema na kuwaruzuku wanadamu wanachohitaji. Wakati wanadamu wanapata fahamu, Nitakuwa Nimeeneza kazi Yangu kitambo. Kisha Nitawaonyesha wanadamu mapenzi Yangu, na kuanza sehemu ya pili ya kazi Yangu juu ya wanadamu, kuwaruhusu watu wote wanifuate kwa karibu ili waambatane na kazi Yangu, na kuwaruhusu watu kufanya kila wawezalo kutekeleza nami kazi Ninayopaswa kufanya.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp