Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 259

Mungu aliumba dunia hii na kuleta mwanadamu, kiumbe hai ambacho alitia uhai ndani yake. Baadaye, mwanadamu akaja kuwa na wazazi na jamaa na hakuwa mpweke tena. Tangu mwanadamu alipotua macho kwa mara ya kwanza katika dunia hii tunayoishi, ilibainika kuwa angeishi ndani ya utaratibu wa Mungu. Ni pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ndiyo hustawisha kila kiumbe hai katika ukuaji wake hadi kinapokomaa. Wakati wa mchakato huu, hakuna hata mmoja anayeamini kwamba mwanadamu huishi na kukua chini ya uangalizi wa Mungu. Badala yake, anashikilia kwamba mwanadamu hukua chini ya upendo na utunzaji wa wazazi wake, na kwamba ukuaji wake unaongozwa na silika ya maisha. Hii ni kwa sababu mwanadamu hajui aliyeleta maisha au kulikotoka maisha hayo, pia hafahamu jinsi silika ya maisha husababisha miujiza. Mwanadamu anajua tu kwamba chakula ndicho msingi wa kuendelea kwa maisha, kwamba uvumilivu ni chanzo cha kuwepo kwa maisha, na kwamba imani iliyomo akilini mwake ni utajiri wa maisha yake. Mwanadamu haihisi neema na riziki itokayo kwa Mungu. Mwanadamu huyatumia kwa uharibifu maisha aliyopewa na Mungu…. Hapana hata mwanadamu mmoja ambaye Mungu Anamwangazia usiku na mchana amechukua jukumu la kuanza Kumwabudu. Mungu Anaendelea kufanya kazi kama Alivyopanga juu ya mwanadamu Akiwa hana matarajio yoyote kutoka kwa mwanadamu. Anafanya hivyo kwa matumaini kwamba siku moja, mwanadamu ataamka kutoka katika ndoto yake na ghafla kuelewa thamani na madhumuni ya maisha, kuelewa gharama Aliyopitia Mungu ili Ampe mwanadamu kila kitu alicho nacho, na kujua jinsi Mungu anavyotamani kwa ari mwanadamu ageuke na Kumrudia. Hakuna yeyote amewahi kufikiria juu ya siri ya asili na endelezo la maisha ya mwanadamu. Na bila shaka, Mungu tu Ambaye Anaelewa yote haya na kwa kimya huvumilia mapigo na maumivu kutoka kwa binadamu, ambaye alipokea kila kitu kutoka kwa Mungu bila shukurani. Binadamu huchukulia kila kitu kinacholetwa na maisha kimzaha, na tena kama “kama jambo lisilo na shaka,” Mungu amesalitiwa, amesahaulika, na kukataliwa na binadamu. Je, mpango wa Mungu ni wa maana namna hii? Je mwanadamu, kiumbe hai ambaye alitoka katika mkono wa Mungu, ni wa maana namna hiyo? Mpango wa Mungu ni wa umuhimu kabisa; hata hivyo, maisha ya viumbe vya mkono wa Mungu vipo kwa ajili ya mpango Wake. Kwa hivyo, Mungu hawezi kuuharibu mpango wake kwa sababu ya chuki Yake kwa mwanadamu. Ni kwa ajili ya mpango Wake na pumzi aliyotoa ndiyo maana Mungu Hustahimili mateso yote, siyo kwa ajili ya mwili wa mwanadamu ila ni kwa sababu ya uhai wa mwanadamu. Mungu ana hamu ya kuchukua pumzi aliyopuliza ndani mwa mwanadamu, wala sio nyama za mwili. Huu ndio mpango wake.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

No One Understands God’s Earnest Wish to Save Man

I

God created this world and brought man into it, a living being to whom God gave life. Then man had parents and kin, no longer alone, destined to live in God’s ordainment. It’s the life breath from God that supports each living being throughout their growth into adulthood. During all this process, they believe that it is just thanks to their parents’ love and care. Not one single man whom God cares for day and night takes initiative to worship Him. God continues to work just as He’s planned on man, who seems to be beyond any hope. And He hopes that one day, man will wake from his dream, see the value and purpose of life, understand what it cost God to give man everything, how He longs for man’s return to Him. Yes, He longs for man’s return to Him.

II

None believes that man lives and grows up under God’s care. They think man’s growth is from life’s instinct. For they don’t know who gave life or from whence it came, how life’s instinct creates miracles. Oh, they think that the food that they eat sustains life, that man lives because he perseveres, that man exists by beliefs; they are blind to God’s providence. They then squander the God-given life. Not one single man whom God cares for day and night takes initiative to worship Him. God continues to work just as He’s planned on man, who seems to be beyond any hope. And He hopes that one day, man will wake from his dream, see the value and purpose of life, understand what it cost God to give man everything, how He longs for man’s return to Him. Yes, He longs for man’s return to Him. Not one single man whom God cares for day and night takes initiative to worship Him. God continues to work just as He’s planned on man, who seems to be beyond any hope. And He hopes that one day, man will wake from his dream, see the value and purpose of life, understand what it cost God to give man everything, how He longs for man’s return to Him. Yes, He longs for man’s return to Him.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp