Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 23

Licha ya Yesu, kwa kuwa Mungu mwenye mwili, na kuwa bila hisia kabisa, Yeye daima Aliwafariji wanafunzi Wake, Aliwapa mahitaji yao, Akawasaidia, na Akawaendeleza. Bila kujali kiwango cha kazi Aliyofanya au kiasi gani cha mateso Alivumilia, Yeye kamwe hakuwa na matarajio kupita kiasi kwa mwanadamu, lakini kila mara Alikuwa mwenye subira na kuvumilia dhambi zao, kiasi kwamba katika Enzi ya Neema Alijulikana kwa upendo kama “Mpendwa Mwokozi Yesu.” Kwa watu wa wakati huo—na kwa watu wote. Kile Yesu Alikuwa nacho na kile Alichokuwa, ilikuwa huruma na fadhili. Yeye kamwe hakukumbuka makosa ya watu au kuruhusu makosa yao kuathiri jinsi Yeye Alivyowachukulia. Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, mara nyingi Alitoa chakula na vinywaji kwa watu ili waweze kula hadi washibe. Yeye Aliwatendea wafuasi Wake wote kwa ukarimu, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kufufua wafu. Ili kwamba watu waweze kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanyika kwa bidii na kwa dhati, Yeye Alifanya mpaka kiwango cha kufufua maiti iliyooza, kuwaonyesha kwamba mikononi Mwake hata wafu wanaweza kuwa hai tena. Kwa njia hii Alivumilia kwa kimya kati yao na Alifanya kazi Yake ya ukombozi. Hata kabla Asulubiwe msalabani, Yesu Alikuwa tayari Amebeba dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu. Alikuwa tayari Amefungua njia ya msalaba ili kumkomboa mwanadamu kabla hajasulubiwa. Mwishowe Aligongwa misumari msalabani, Alijitoa sadaka yeye mwenyewe kwa ajili ya msalaba, na Aliweka huruma Yake yote, fadhili Zake, na utakatifu juu ya mwanadamu. Aliendelea kuvumilia wanadamu, kamwe Hakutafuta kulipiza kisasi, lakini kuwasamehe hao dhambi zao, Akiwasihi watubu, na kuwafundisha kuwa na subira, uvumilivu na upendo, kufuata nyayo Zake na kujitoa wenyewe kwa ajili ya msalaba. Upendo wake kwa ndugu na dada uilizidi upendo wake kwa Maria. Kanuni ya kazi Aliyofanya ilikuwa kuwaponya watu na kutoa mapepo, yote kwa ajili ya ukombozi Wake. Haijalishi Alikoenda, Yeye Aliwachukua wote waliomfuata kwa wema. Aliwafanya maskini kuwa tajiri, viwete wakatembea, vipofu wakaona, viziwi wakasikia; Yeye Aliwaalika mpaka watu wasiofaa machoni pa wanadamu na maskini zaidi, wenye dhambi, wakala pamoja Naye, Hakuepukana nao ila daima Alikuwa na subira, hata Akasema, “Wakati mchungaji anapoteza kondoo mmoja kati ya mia, yeye huondoka na kuwaacha nyuma wale tisini na tisa ili amtafute kondoo mmoja aliyepotea, na anapompata yeye hufurahia kwa shangwe.” Yeye Aliwapenda wafuasi wake kama kondoo anavyopenda wanakondoo wake. Ingawa walikuwa wajinga na wasio na ufahamu, na wenye dhambi katika macho Yake, na zaidi walikuwa washirika wa chini zaidi katika jamii, Aliona hawa wenye dhambi—waliodharauliwa na wengine—kama vipenzi Vyake. Kwa kuwa Alikuwa na fadhila kwao, Alitoa uhai Wake kwa ajili yao, kama mwana kondoo aliyetolewa madhabahuni. Alitembea kati yao kama mtumishi wao, Akawaruhusu kumtumia na kumchinja, Alijiwasilisha kwao bila masharti. Kwa wafuasi Wake Alikuwa Mpendwa Mwokozi Yesu, lakini kwa Mafarisayo, ambao waliwahubiria watu kutoka viweko vya mnara, Hakuwaonyesha huruma na wema, bali Yeye Aliwachukia na kuchukizwa nao. Hakufanya kazi sana miongoni mwa Mafarisayo, mara chache tu Aliwahubiria na kuwakemea; Yeye hakuwakomboa, au kufanya ishara na miujiza kati yao. Alihifadhi huruma Yake na upendo kwa wafuasi Wake, kuvumilia kwa ajili ya hawa wenye dhambi mpaka mwisho wakati Alipigwa misumari msalabani, kustahimili kila udhalilishaji mpaka Alivyowakomboa wanadamu wote kikamilifu. Hii ndio ilikuwa jumla ya kazi Yake.

Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, Shetani angechukua makazi duniani, na dunia nzima ingekuwa makao yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji huruma na fadhili kwa wanadamu; kupitia kwa kazi hiyo tu ndio mwanadamu angeweza kupokea msamaha na mwishowe afuzu kufanywa kuwa mkamilifu na kupatwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alifanya kazi Yake hapa duniani ilikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa na mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaanzisha hatima ya mwanadamu. Baada ya Yesu kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo mwanadamu alikombolewa. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Alidhihakiwa, Akatukanwa, na Akaachwa pweke, Aliachwa hata bila mahali pa kulaza kichwa chake, Hakuwa hata na mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, nafsi Yake yote—mwili safi na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani, na kupitia kila namna ya mateso. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na askari hata wakamtemea mate usoni; ila Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea na kujitoa bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa binadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ya Yesu inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria na si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo binadamu amepitia—Enzi ya Ukombozi.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp