Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 37

Mungu anafanya kazi Yake katika ulimwengu mzima. Wote wanaoamini katika Yeye lazima walikubali neno Lake, na kula na kunywa neno Lake; hakuna atakayepatwa na Mungu kwa kuona ishara na maajabu yanayoonyeshwa na Mungu. Katika enzi zote, Mungu ametumia neno kila wakati kumfanya mwanadamu mkamilifu, hivyo hampaswi kuweka mawazo yenu yote kwa ishara na maajabu, ila unapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu. Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Mungu alinena baadhi ya maneno, na katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena maneno mengi. Baada ya Yesu kumaliza kunena maneno haya mengi, mitume na manabii ambao walikuja baadaye walifanya watu watende kulingana na sheria na amri zilizowekwa na Yesu, na wakawafanya waishi kulingana na kanuni zilizonenwa na Yesu. Mungu wa siku za mwisho hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kumfanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu. Hili ndilo lengo la kazi Anayofanya na maneno Anenayo. Mungu hatumii mbinu ya kuonyesha ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kamili—Anatumia maneno, na Anatumia mbinu nyingi za kazi kumfanya mwanadamu kamili. Iwe ni usafishaji, kushughulikia, upogoaji, ama kupewa maneno, Mungu hunena kutoka taswira nyingi tofauti kumfanya mwanadamu kamili, na kumpa mwanadamu maarifa kuu ya kazi, hekima na ajabu ya Mungu. Mwanadamu anapofanywa mkamilifu katika wakati ambao Mungu Anamaliza enzi katika siku za mwisho, atakuwa amehitimu kuona ishara na maajabu. Unapokuwa na maarifa ya Mungu na unaweza kumtii Mungu bila kujali Anachofanya, utaona ishara na maajabu, kwani hautakuwa na dhana kuhusu ukweli wa Mungu. Kwa sasa, wewe ni mpotovu na huwezi kuwa na utiifu kamili kwa Mungu—je umehitimu kuona ishara na maajabu? Wakati ambao Mungu anaonyesha ishara na maajabu ndio wakati ambao Mungu anamwadhibu mwanadamu, na pia wakati ambao enzi inabadilika, na zaidi, wakati ambao enzi inatamatika. Wakati ambao kazi ya Mungu inatekelezwa kama kawaida, Haonyeshi ishara na maajabu. Kuonyesha ishara na maajabu ni jambo rahisi mno, lakini hiyo si kanuni ya kazi ya Mungu, wala si lengo la usimamizi wa Mungu wa mwanadamu. Iwapo mwanadamu angeona ishara na maajabu, na kama mwili wa kiroho wa Mungu ungemtokea mwanadamu, je watu wote hawangeweza “kuamini” katika Mungu? Nimesema hapo awali kuwa kikundi cha washindi wanapatwa kutoka Mashariki, washindi ambao wanatoka katika mashaka makubwa. Je maneno haya yana maana gani? Yanamaanisha kuwa watu hao ambao wamepatwa waliamini kwa kweli tu baada ya kupitia hukumu na kuadibu, na kushughulikiwa na kupogolewa, na aina yote ya usafishaji. Imani ya watu kama hao sio isiodhahiri na dhahania, bali ni ya kweli. Hawajaona ishara na maajabu yoyote, ama miujiza yoyote; hawazungumzi kuhusu barua ngumu kueleweka na kanuni, ama mitazamo ya muhimu sana; badala yake, wana ukweli, na maneno ya Mungu, na maarifa ya kweli kuhusu ukweli wa Mungu. Je kikundi hiki hakina uwezo wa kuweka wazi nguvu za Mungu? Kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni ya uhakika. Katika enzi ya Yesu, hakuja kumfanya mwanadamu awe kamili, ila kumkomboa mwanadamu, na hivyo Alionyesha miujiza kadhaa ili kufanya watu wamfuate. Kwani Yeye hasa Alikuja kukamilisha kazi ya kusulubiwa, na kuonyesha ishara haikuwa sehemu ya huduma Yake. Ishara na maajabu hayo yalikuwa ni kazi ambayo yalifanyika ili kufanya kazi Yake iwe na matokeo ya kufaa; hayo yalikuwa tu kazi ya ziada, na hayakuwakilisha kazi ya enzi nzima. Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Mungu pia Alionyesha ishara na maajabu kadhaa—lakini kazi Anayofanya Mungu leo ni kazi halisi, na kwa uhakika hawezi kuonyesha ishara na maajabu sasa. Punde alipoonyesha tu onyesha ishara na maajabu, kazi Yake halisi ingetupwa nje ya mpangilio wake, na hataweza kufanya kazi nyingine zaidi. Iwapo Mungu angesema neno litumiwe kumfanya mwanadamu kuwa kamili, lakini pia Aonyeshe ishara na maajabu, basi mwanadamu kumwamini ama kutomwamini kweli kungeweza kuwekwa wazi? Hivyo, Mungu hafanyi vitu vya aina hiyo. Kuna udini mwingi sana katika mwanadamu; Mungu amekuja katika nyakati za mwisho ili kutoa dhana zote za kidini na vitu visivyo vya kidunia ndani ya mwanadamu, na kumfanya mwanadamu ajue ukweli wa Mungu. Amekuja kutoa picha ya Mungu ambayo ni ya dhahania na bunifu—picha ya Mungu ambaye, kwa maneno mengine, hayupo hata kidogo. Na hivyo, sasa kitu cha pekee kilicho cha thamani ni wewe kuwa na ufahamu kuhusu hali halisi! Ukweli unashinda kila kitu. Unamiliki ukweli kiasi gani leo? Je, kila kitu kinachoonyesha ishara na maajabu ni Mungu? Roho wabaya pia wanaweza kuonyesha ishara na maajabu; je, hawa wote ni Mungu? Katika imani yake kwa Mungu, kile anachotafuta mwanadamu ni ukweli, anachotafuta ni uzima, na sio ishara na maajabu. Hivi ndivyo linavyopaswa kuwa lengo la wote wanaoamini katika Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp