Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 264

Ni viumbe wangapi wanaoishi na kuzaana katika ulimwengu mpana, wakifuata sheria ya maisha tena na tena, wakifuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani muumbaji wa mwanadamu? Je, kweli wanadamu waliumbwa na mazingira asilia? Je, kweli wanadamu wana uamuzi juu ya hatima yao? … Kwa maelfu ya miaka wanadamu wameyauliza haya maswali, tena na tena. Kwa bahati mbaya, jinsi wanadamu wanavyopagawa na haya maswali, ndivyo kiu yao ya sayansi huendelea kukua. Sayansi hupatiana kutosheleza kwa muda na raha ya muda ya mwili, ila haitoshi kumpa mwanadamu uhuru kutokana na upweke, ukiwa, na hofu isiyodhihirika na kutosaidika ndani ya moyo wake. Wanadamu hutumia ujuzi wa kisayansi unaoweza kuonekana kwa macho na ambao akili zaweza kuufahamu kutuliza moyo wake. Na bado ujuzi wa kisayansi kama huu hauwezi kuwazuia wanadamu kutafiti yasiyofahamika. Wanadamu hawajui ni nani Mkuu wa kila kitu katika ulimwengu huu, aidha hajui mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyomo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha. Wanadamu huishi na hufa chini ya macho yake Mungu. Wanadamu huishi kwa usimamizi wa Mungu, na wakati macho Yake yatafumbika kwa mara ya mwisho, hio pia ni kwa usimamizi Wake. Tena na tena, mwanadamu huja na kwenda, nyuma na mbele. Bila mapendeleo, yote ni sehemu ya ukuu na michoro ya Mungu. Usimamizi wa Mungu ungali unaendelea mbele na haujawahi kusimama. Atawafanya wanadamu wafahamu uwepo Wake, waamini katika ukuu Wake, watazame matendo Yake, na warudi katika ufalme Wake. Huu ni mpango Wake, na kazi ambayo Amekuwa Akiitekeleza kwa maelfu ya miaka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp