Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 479

10/09/2020

Kazi iliyofanywa na Paulo ilionyeshwa mbele ya mwanadamu, lakini upendo wake wa Mungu ulikuwa safi kiasi gani, upendo wake kwa Mungu ulikuwa ndani ya moyo wake kiasi gani—haya hayaonekani na mwanadamu. Mwanadamu anaweza tu kutazama kazi ambayo aliifanya, ambapo mwanadamu hujua kuwa kwa hakika alitumika na Roho Mtakatifu, na hivyo mwanadamu hudhani kwamba Paulo alikuwa bora kuliko Petro, ya kwamba kazi yake ilikuwa kubwa zaidi, kwa kuwa alikuwa na uwezo wa kutoa kwa makanisa. Petro alitazama tu matukio yake binafsi, na akapata watu wachache wakati wa kazi yake ya mara kwa mara. Kutoka kwake kunazo lakini nyaraka chache zinazojulikana, lakini ni nani anayejua jinsi upendo wa Mungu ulivyokuwa mkubwa kiasi gani moyoni mwake? Siku zote, usiku na mchana, Paulo alimfanyia Mungu kazi: alimradi kulikuwepo na kazi ya kufanywa, yeye aliifanya. Yeye alihisi kuwa kwa njia hii angeweza kulipata taji, na angemridhisha Mungu, lakini hakutafuta njia za kujibadilisha mwenyewe kupitia kazi hii. Chochote katika maisha ya Petro ambacho hakikukimu mapenzi ya Mungu kilimfanya kuhisi wasiwasi. Kama hakikukidhi mapenzi ya Mungu, basi angehisi kujuta, na angetafuta njia mwafaka ambayo angejitahidi kuridhisha moyo wa Mungu. Hata katika masuala madogo kabisa maishani mwake yasiyokuwa na maana, bado alijishurutisha mwenyewe kukidhi mapenzi ya Mungu. Alikuwa pia mkali ilipofikia tabia yake ya asili na alikuwa daima mkali katika masharti yake mwenyewe ili kuelekea ndani zaidi kwa ukweli. Paulo alitafuta tu sifa na hadhi ya kijuu juu. Alitafuta kuringa mwenyewe mbele za mwanadamu, na hakutafuta kufanya maendeleo zaidi katika kuingia kwa maisha. Kile alichojali kuhusu ni mafundisho ya kidini, si uhalisi. Baadhi ya watu husema, Paulo alimfanyia Mungu kazi nyingi, kwa nini yeye hakufanywa ukumbusho na Mungu? Petro alimfanyia Mungu kazi kidogo, na hakufanya mchango mkubwa katika makanisa, je, kwa nini yeye alifanywa mkamilifu? Petro alimpenda Mungu hadi kiwango fulani, ambacho kilitakiwa na Mungu; ni watu kama hawa pekee wana ushuhuda. Na kuhusu Paulo? Ni kiwango gani ambacho Paulo alimpenda Mungu, je, wewe wajua? Kazi ya Paulo ilikuwa kwa ajili ya nini? Na kazi ya Petro ilikuwa kwa ajili ya nini? Petro hakufanya kazi kubwa, lakini, je, wafahamu ni nini kilikuwa moyoni mwake? Kazi ya Paulo inahusiana na utoaji makanisani, na msaada wa makanisa. Kile ambacho Petro alishuhudia ni mabadiliko ya tabia ya maisha yake; alishuhudia upendo wa Mungu. Kwa kuwa sasa unajua tofauti katika kiini cha kila mmoja wao, unaweza kuona ni nani, hatimaye, kwa kweli alimwamini Mungu, na ni nani ambaye kwa kweli hakumwamini Mungu. Mmoja wao alimpenda Mungu kwa kweli, na mwingine hakumpenda Mungu kwa kweli; mmoja alipitia mabadiliko katika tabia yake, na mwingine hakupitia; mmoja aliabudiwa na watu, na alikuwa na picha nzuri, na mwingine alihudumu kwa unyenyekevu, na hakuonekana na watu kwa urahisi; mmoja alitafuta utakatifu, na mwingine hakuutafuta, na ingawa hakuwa najisi, hakuwa amemilikiwa na upendo safi; mmoja alimilikiwa na ubinadamu wa kweli, na mwingine hakuwa nao; mmoja alikuwa na hisia ya kiumbe wa Mungu, na mwingine hakuwa na hisia hiyo. Tofauti kama hizi ndizo zilizo katika kiini cha Paulo sawa na Petro. Njia ambayo Petro alitembea ni njia ya mafanikio, ambayo pia ni njia ya kutimiza kupatwa tena kwa ubinadamu wa kawaida na wajibu wa kiumbe wa Mungu. Petro anawakilisha wote hao waliofaulu. Njia ambayo Paulo aliitembea ni njia ya kushindwa, na anawakilisha wale wote ambao wanajisalimisha na kujipa matarajio yao wenyewe ya kijuu juu, na hawampendi Mungu kwa dhati. Paulo anawakilisha wote ambao hawana ukweli. Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na ukosefu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake wa Mungu. Je, huu si upendo mkamilifu wa Mungu? Je, hii si ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo wa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki. Fikiria kwamba wewe unaweza kumfanyia Mungu kazi, ilhali wewe humtii Mungu, na huna uwezo wa kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa njia hii, wewe hutakuwa tu umekosa kutimiza wajibu wa kiumbe cha Mungu, lakini pia utalaaniwa na Mungu, kwa kuwa wewe ni mtu ambaye hana ukweli, ambaye hana uwezo wa kumtii Mungu, na ambaye si mtiifu kwa Mungu. Wewe unajali tu kuhusu kumfanyia Mungu kazi, na hujali kuhusu kuweka ukweli katika vitendo, ama kujifahamu. Wewe humfahamu ama kumjua Muumba, na humtii ama kumpenda Muumba. Wewe ni mtu ambaye asilia si mtiifu kwa Mungu, na hivyo watu kama hawa hawapendwi na Muumba.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp