Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 24

Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote. Enzi nzee ikipita, itabadilishwa na enzi mpya, na mara tu kazi nzee imekamilika, kazi mpya itaendeleza usimamizi wa Mungu. Kupata mwili huku ni kupata mwili kwa Mungu mara ya pili kufuatia kukamilika kwa kazi ya Yesu. Bila shaka, kupata mwili huku hakufanyiki kivyake, bali ni hatua ya tatu ya kazi baada ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kila hatua mpya ya kazi ya Mungu kila mara huleta mwanzo mpya na enzi mpya. Vivyo hivyo kuna mabadiliko yanayokubaliana katika tabia ya Mungu, katika njia Yake ya kufanya kazi, katika sehemu Yake ya kufanya kazi, na katika jina Lake. Ndiyo maana basi ni vigumu kwa mwanadamu kukubali kazi ya Mungu katika enzi mpya. Lakini licha ya jinsi anapingwa na mwanadamu, Mungu huendelea kufanya kazi Yake, na daima Yeye huwa Akiongoza wanadamu wote kuendelea mbele. Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp