Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 106

Dutu ya Mungu yenyewe hushika na kutumia mamlaka, lakini Yeye Anao uwezo wa kuwasilisha kwa ukamilifu mamlaka ambayo hutoka Kwake. Iwe ni kazi ya Roho au kazi ya mwili, hakuna ambayo itazozana na nyingine. Roho wa Mungu ndiyo mamlaka juu ya viumbe vyote. Mwili na dutu ya Mungu pia inayo mamlaka, bali Mungu katika mwili Anaweza kufanya kazi yote inayotii mapenzi ya Baba wa mbinguni. Hii haiwezi kupatikana au kufanyika na binadamu yeyote. Mungu Mwenyewe ni mamlaka, lakini mwili Wake unaweza kunyenyekea kwa mamlaka Yake. Hii ndiyo maana ya ndani ya maneno: “Kristo hutii mapenzi ya Mungu Baba.” Mungu ni Roho na Anaweza kufanya kazi ya wokovu, kama vile Mungu Anavyoweza kuwa mwanadamu. Hata hivyo, Mungu Mwenyewe Anafanya kazi Yake Mwenyewe; Yeye wala hazuii wala kuathiri, wala kufanya kazi inayozipinganisha pande zote mbili, kwa kuwa kiini cha kazi iliyofanywa na Roho na mwili yote ni sawa. Iwe ni Roho au mwili, vyote hufanya kazi kutimiza nia moja na kusimamia kazi sawa. Ingawa Roho na mwili huwa na sifa mbili tofauti, dutu yao ni sawa; zote zina dutu ya Mungu Mwenyewe, na utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Mungu Mwenyewe hana mambo ya kuasi; dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote. Hata katika mwili, Mungu hafanyi lolote linalomuasi Mungu Baba. Hata kwa gharama ya kutoa sadaka maisha Yake, Angekuwa kwa ukamilifu tayari na kutofanya uchaguzi mwingine. Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelagaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani. Haijalishi ugumu wa kazi, au udhaifu wa mwili, Mungu, wakati Anapoishi katika mwili, kamwe hatafanya kitu chochote kitakachopinga kazi ya Mungu Mwenyewe, wala kuacha mapenzi ya Mungu Baba kwa njia ya uasi. Ni afadhali Ateseke maumivu ya mwili kuliko kwenda kinyume na matakwa ya Mungu Baba; ni kama vile Yesu Alisema katika sala, “Baba, kama inawezekana, kikombe hiki kiniondokee; hata hivyo, si kama Mimi Nipendavyo, bali kama Wewe upendavyo.” Wanadamu watachagua, bali Kristo hawezi. Ingawa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe, bado Yeye Anatafuta mapenzi ya Mungu Baba, na Anatimiza kile Alichokabidhiwa na Mungu Baba, kutoka kwa mtazamo wa mwili. Hili ni jambo ambalo haliwezi kupatikana kwa binadamu. Hilo ambalo huja kutoka kwa Shetani haliwezi kuwa na dutu ya Mungu, bali mojawapo ya yale ambayo hukosa kutii na kumpinga Mungu. Haliwezi kumtii Mungu kikamilifu, wala kutii mapenzi ya Mungu kwa hiari. Wanadamu wote isipokuwa Kristo wanaweza kufanya yaliyo ya kumpinga Mungu, na hakuna anayeweza moja kwa moja kufanya kazi aliyoaminiwa na Mungu; hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuzingatia usimamizi wa Mungu kama wajibu wake wenyewe kutekeleza. Kuwasilisha mapenzi ya Mungu Baba ni kiini cha Kristo; uasi dhidi ya Mungu ni tabia ya shetani. Sifa hizo mbili hazipatani, na yeyote aliye na sifa za shetani hawezi kuitwa Kristo. Sababu ambayo binadamu hawezi kufanya kazi ya Mungu kwa niaba Yake ni kwa sababu mwanadamu hana kiini chochote cha Mungu. Binadamu humfanyia Mungu kazi kwa ajili ya maslahi binafsi ya binadamu na ya matarajio Yake ya baadaye, lakini Kristo Anafanya kazi ya kufanya mapenzi ya Mungu Baba.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp