Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hukumu Katika Siku za Mwisho | Dondoo 91

10/09/2020

Kuna tofauti kubwa kati ya kazi iliyofanywa Israeli na kazi ya leo. Yehova aliyaongoza maisha ya Waisraeli, na hakukuwa na kuadibu na hukumu nyingi, kwa sababu wakati huo, watu walielewa kidogo sana kuhusu ulimwengu na walikuwa na tabia chache zilizokuwa potovu. Hapo zamani, Waisraeli walimtii Yehova kabisa. Alipowaambia wajenge madhabahu, walijenga madhabahu haraka; Alipowaambia wavae mavazi rasmi ya makuhani, walitii. Katika siku hizo, Yehova alikuwa kama mchungaji akilichunga kundi la kondoo, na kondoo wakifuata mwongozo wa mchungaji na kula nyasi katika malisho; Yehova aliyaongoza maisha yao, Akiwaongoza katika jinsi walivyokula, kuvalia, kuishi, na kusafiri. Huo haukuwa wakati wa kuweka wazi tabia ya Mungu, kwa kuwa wanadamu wa wakati huo walikuwa waliozaliwa karibuni; kulikuwa na wachache waliokuwa waasi na wapinzani, hakukuwa na uchafu mwingi kati ya wanadamu, na kwa hivyo watu hawangeweza kutenda kama foili kwa tabia ya Mungu. Ni kupitia watu ambao wanatoka katika nchi ya uchafu ndipo utakatifu wa Mungu unaonyeshwa; leo, Yeye hutumia uchafu ulioonyeshwa katika watu hawa wa nchi ya uchafu, naye Anahukumu, na kwa kufanya hivyo, kile Alicho kinafichuliwa katika hukumu Yake. Kwa nini Anahukumu? Anaweza kunena maneno ya hukumu kwa sababu Anadharau dhambi; Je, Angewezaje kukasirika sana hivyo ikiwa hakuchukia uasi wa wanadamu? Kusingekuwa na karaha ndani Yake, kusingekuwa na machukio, Asingejali uasi wa watu, basi hiyo ingethibitisha Yeye kuwa mchafu kama mwanadamu. Kwamba Yeye anaweza kumhukumu na kumwadibu mwanadamu ni kwa sababu Yeye huchukia uchafu, na Anachokichukia hakimo ndani Yake. Kama pia kungekuwa na upinzani na uasi ndani Yake, Asingewadharau wale ambao ni wapinzani na waasi. Kazi ya siku za mwisho ingekuwa ikifanywa Israeli, hakungekuwa na maana yoyote kwayo. Mbona kazi ya siku za mwisho inafanywa nchini China, mahali paovu na palipo nyuma kabisa kimaendeleo kuliko sehemu zote? Ni ili kuonyesha utakatifu na haki Yake. Kwa kifupi, kadri mahali palivyo paovu, ndivyo utakatifu wa Mungu unavyoweza kuonyeshwa wazi zaidi. Kwa kweli, yote haya ni kwa ajili ya kazi ya Mungu. Ni leo tu ndipo mnatambua kuwa Mungu ameshuka kutoka mbinguni ili Asimame kati yenu, Ameonyeshwa kupitia uchafu na uasi wenu, na ni wakati huu tu ndipo mnamjua Mungu. Je, hii siyo sifa kubwa zaidi? Kwa kweli, ninyi ni kikundi cha watu nchini China waliochaguliwa. Na kwa sababu mlichaguliwa na mmefurahia neema ya Mungu, na kwa sababu hamfai kufurahia neema kubwa kama hiyo, hii inathibitisha kwamba haya yote ni kuwapa sifa kubwa kabisa. Mungu amewatokea, na kuwaonyesha tabia Yake nzima iliyo takatifu, na Amewapa yote hayo, na kuwasababisha mfurahie baraka zote ambazo mnaweza kufurahia. Hamjaionja tu tabia ya Mungu yenye haki, lakini, zaidi ya hayo, mmeuonja wokovu wa Mungu, ukombozi wa Mungu na upendo wa Mungu usio na kikomo. Ninyi, wachafu zaidi ya wote, mmefurahia neema kubwa kama hii—je, hamjabarikiwa? Je, huku si Mungu kuwainua? Ninyi ni wa chini zaidi ya wote, kwa asili hamstahili kufurahia baraka kubwa kama hiyo, lakini Mungu anang’ang’ania kukuinua. Je, huoni aibu? Ikiwa huwezi kutekeleza wajibu wako, basi mwishowe utaaibika, nawe utajiadhibu. Leo, hufundishwi nidhamu, wala huadhibiwi; mwili wako uko salama salimini—lakini mwishowe, maneno haya yatakuaibisha. Hadi leo, bado Sijamwadibu mtu yeyote waziwazi; maneno Yangu yanaweza kuwa makali, lakini Ninawatendeaje watu? Ninawafariji, na kuwashawishi, na kuwakumbusha. Ninafanya hivi ili kuwaokoa tu. Je, kwa kweli hamwelewi mapenzi Yangu? Mnapaswa kuelewa Ninachosema, na kutiwa moyo nacho. Ni sasa tu ndipo kunao watu wengi wanaoelewa. Je, hii si baraka ya kuwa foili? Je, kuwa foili si jambo la kubarikiwa zaidi? Mwishowe, mnapoenda kueneza injili, mtasema hivi: “Sisi ni foili wa kawaida.” Watawauliza, “Inamaanisha nini kwamba ninyi ni foili wa kawaida?” Nanyi mtasema: “Sisi ni foili kwa kazi ya Mungu, na kwa nguvu Zake kuu. Tabia nzima ya Mungu yenye haki imefunuliwa kupitia uasi wetu; sisi ni vyombo vya kutumikia kwa kazi ya Mungu ya siku za mwisho, sisi ni viambatisho vya kazi Yake, na pia vifaa vya kazi hiyo.” Wanaposikia hivyo, watavutiwa sana. Baadaye, utasema: “Sisi ni vielelezo na mifano ya Mungu kukamilisha kazi ya ulimwengu wote, na ya ushindi Wake wa wanadamu wote. Iwe sisi ni watakatifu au wachafu, kwa jumla, bado tumebarikiwa zaidi kuliko ninyi, kwa maana tumemwona Mungu, na kupitia fursa ya Yeye kutushinda, nguvu kuu za Mungu zimeonyeshwa; ni kwa sababu tu sisi ni wachafu na waovu ndiyo tabia Yake yenye haki imetokea. Je, hivyo mnaweza kuishuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Hamstahili! Hii ni Mungu kutuinua tu! Ingawa tunaweza kukosa kuwa wenye kiburi, tunaweza kumsifu Mungu kwa kujivunia, kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kurithi ahadi kubwa kama hiyo, na hakuna mtu anayeweza kufurahia baraka kubwa kama hiyo. Tunashukuru sana kwamba sisi, ambao ni wachafu sana, tunaweza kufanya kazi kama foili wakati wa usimamizi wa Mungu.” Na wanapouliza, “Vielelezo na mifano ni nini?” unasema, “Sisi ni wanadamu waasi zaidi na wachafu zaidi; tumepotoshwa kwa kina kabisa na Shetani, nasi ni viumbe tulio nyuma kimaendeleo na duni zaidi kimwili. Sisi ni mifano bora ya wale ambao wametumiwa na Shetani. Leo, tumechaguliwa na Mungu kama wa kwanza kati ya wanadamu walioshindwa, na tumeona tabia ya Mungu yenye haki na kurithi ahadi Yake; tunatumiwa kuwashinda watu zaidi, kwa hiyo sisi ndio vielelezo na mifano ya wale wanaoshindwa kati ya wanadamu.” Hakuna ushuhuda bora zaidi kuliko maneno haya, na huu ndio uzoefu wako bora kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp