Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Siri Kuhusu Biblia | Dondoo 269

Biblia ni kitabu cha kihistoria, na ikiwa ungekula na kunywa Agano la Kale wakati wa Enzi ya Neema—ikiwa ungeweka katika vitendo kile kilichokuwa kinatakiwa katika wakati wa Agano la Kale wakati wa Enzi ya Neema—Yesu angekukataa, na kukuhukumu; ikiwa ungetumia Agano la Kale katika kazi ya Yesu, basi ungekuwa Farisayo. Ikiwa, leo, utaweka pamoja Agano Jipya na la Kale kula na kunywa, na kuliweka katika vitendo, basi Mungu wa leo Atakuhukumu; utakuwa umetanga mbali na kazi ya Roho Mtakatifu leo! Ikiwa unakula Agano la Kale, na kula Agano Jipya, basi upo nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu! Wakati wa kipindi cha Yesu, Yesu aliwaongoza Wayahudi na wale wote ambao walimfuata Yeye kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu katika Yeye wakati huo. Hakuichukulia Biblia kama msingi wa kile Alichofanya, bali Alizungumza kulingana na kazi Yake; Hakutilia maanani kile ambacho Biblia ilisema, wala hakutafuta katika Biblia njia ya kuongoza wafuasi Wake. Kuanzia pale Alipoanza kufanya kazi, Aliongoza njia ya toba—neno ambalo halikutajwa kabisa katika unabii wa Agano la Kale. Sio kwamba tu Hakutenda kulingana na Biblia, lakini pia Aliongoza njia mpya, na Akafanya kazi mpya. Na wala Hakurejelea kabisa Biblia Alipohubiri. Wakati wa Enzi ya Sheria, hakuna ambaye aliweza kufanya miujiza Yake ya kuponya wagonjwa na kutoa mapepo. Kazi Yake, mafundisho Yake, mamlaka Yake—hakuna mtu aliyefanya hivi wakati wa Enzi ya Sheria. Yesu alifanya tu kazi Yake mpya, na ingawa watu wengi walimhukumu kwa kutumia Biblia—na hata wakatumia Agano la Kale kumsulubisha—kazi Yake ilipitiliza Agano la Kale; kama hii haikuwa hivyo, kwa nini watu walimwangika msalabani? Ilikuwa ni kwa sababu haikusema kitu katika Agano la Kale la mafundisho Yake, na uwezo Wake wa kuponya wagonjwa na kutoa mapepo? Kazi Yake ilikuwa ni kwa ajili ya kuongoza katika njia mpya, haikuwa ni kwa makusudi ya kufanya ugomvi dhidi ya Biblia, au kwa makusudi kujitenga na Agano la Kale. Alikuja tu kufanya huduma Yake, kuleta kazi mpya kwa wale waliomtamani sana na kumtafuta. Hakuja kufafanua Agano la Kale au kutetea kazi yake. Kazi Yake bado haikuwa ni kwa ajili ya kuruhusu Enzi ya Sheria kuendelea kukua, maana kazi Yake haikuzingatia Biblia kama msingi wake; Yesu alikuja kufanya tu kazi ambayo Alipaswa kufanya. Hivyo, Hakufafanua unabii wa Agano la Kale, wala Hakufanya kazi kulingana na maneno ya Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Alipuuzia kile ambacho Agano la Kale lilisema, Hakujalia kama lilikubaliana na kazi Yake au la, na Hakujali kile ambacho watu wengine walijua kuhusu kazi Yake, au namna walivyokuwa wakiihukumu. Aliendelea tu kufanya kazi ambayo Alipaswa kufanya, ingawa watu wengi walitumia unabii waliousema manabii wa Agano la Kale kumhukumu. Ilionekana kwa watu kana kwamba kazi Yake haikuwa na msingi, na kulikuwa na mengi ambayo yalikuwa hayapatani na rekodi za Agano la Kale. Je, huu sio upuuzi? Je, kuna ulazima wa kutumia mafundisho ya dini katika kazi ya Mungu? Je, ni lazima iwe kulingana na maneno ya unabii waliyosema manabii? Hata hivyo, kipi ni kikubwa? Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Alivunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp