Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 503

16/09/2020

Punde tu Mungu anapokuwa uzima katika watu, wanakuwa hawana uwezo wa kumwacha Mungu. Je, hili sio tukio la Mungu? Hakuna ushuhuda mkubwa kuliko huu! Mungu amefanya kazi hadi kiwango fulani; Amewataka watu kutoa huduma, na kuadibiwa, au kufa, na watu hawajarudi nyuma, ambalo linaonyesha kuwa watu hawa wameshindwa na Mungu. Watu ambao wana ukweli ni wale ambao, katika matukio wanayopitia ya kweli, wanaweza kusimama imara katika ushuhuda wao, kusimama imara katika nafasi zao, kusimama katika upande wa Mungu, bila kurudi nyuma, na ambao wanaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na watu wanaompenda Mungu, wale ambao, mambo yakishawatokea, wanaweza kumtii Mungu kabisa, na wanaweza kumtii Mungu hadi kifo. Matendo na ufunuo wako katika maisha halisi ndio ushuhuda wa Mungu, ni kuishi kwa kudhihirisha maisha ya mwanadamu na ushuhuda wa Mungu, na huku ni kufurahia upendo wa Mungu; unapopitia hadi kiwango hiki, matukio unayopitia yatakuwa yamekuwa na athari. Watu ambao wameuona upendo wa Mungu kwa kweli ni wale ambao wanaishi kwa kudhihirisha kwa kweli, ambao kila matendo yao yanapongezwa na wengine, ambao sura yao haipendezi lakini wanaoishi kwa kudhihirisha maisha ya utiifu wa hali ya juu, ambao wanawasiliana kwa karibu maneno ya Mungu na huelekezwa na Mungu, na kupata nuru kutoka kwa Mungu, ambao huweza kuongea mapenzi ya Mungu katika maneno yao, na wanawasiliana kwa karibu uhalisi, ambao huelewa zaidi kuhusu kuhudumu katika Roho, wanaongea kwa wazi, ambao ni wenye heshima na kuaminika, ambao hawakabiliki na wana tabia nzuri, ambao wanaweza kutii mipango ya Mungu na kusimama imara katika ushuhuda wakati mambo yanapowatokea, ambao wana utulivu bila kujali wanachokumbana nacho. Watu wengine wangali wachanga, lakini wanatenda kama mtu mzima; wamekomaa, wana ukweli, wanapendwa na wengine—na hawa ndio watu ambao wana ushuhuda, na ndio udhihirisho wa Mungu. Ni sawa na kusema, wanapopitia mambo na kufikia kiwango fulani, ndani yao watakuwa na ufahamu juu ya Mungu, tabia zao za ndani zitakuwa zimeimarika. Watu wengi hawaweki ukweli katika vitendo, na wengi hawasimami imara kwa ushuhuda wao. Ndani ya watu kama hao hakuna upendo wa Mungu, au ushuhuda kwa Mungu, na hawa ndio watu ambao wanachukiwa sana na Mungu. Wanakula na kunywa maneno ya Mungu, lakini wanachoonyesha ni Shetani, na wanaruhusu maneno ya Mungu kukashifiwa na Shetani. Ndani ya watu hawa hakuna dalili ya upendo wa Mungu, wanachokidhihirisha ni cha shetani. Kama moyo wako uko na amani na Mungu kila wakati, na huwa uko makini kwa watu na vitu vinavyokuzunguka, na kinachoendelea katika mazingira yako, na unafahamu mzigo wa Mungu, na kila mara una moyo unaomheshimu Mungu, basi Mungu atakupa nuru ndani yako. Kanisani kuna watu ambao ni “wasimamizi”, wanatazama makosa ya wengine, kisha kunakili na kuwa kama wao. Hawana uwezo wa kutofautisha, hawachukii dhambi, hawachukii au kughadhibishwa na vitu vya Shetani. Watu kama hao wamejawa na vitu vya Shetani, na hatimaye wataachwa na Mungu kabisa. Wale ambao wana maono kama msingi wao, na ambao huandama maendeleo, ni wale ambao mioyo yao daima inamheshimu Mungu, ambao ni wa wastani katika maneno na vitendo vyao, ambao wasingetaka kumpinga Mungu, kumkasirisha Mungu, au Kazi ya Mungu kwao isiwe na thamani, au shida walizozipitia ziwe bure, au yale yote ambayo wameweka katika vitendo yapite bure. Ni watu ambao wako tayari kutoa juhudi zaidi na upendo wa Mungu katika njia iliyo mbele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp