Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 365

Duniani, kila aina ya pepo wanazungukazunguka bila mwisho wakitafuta mahali pa kupumzika, bila kusita wanatafuta maiti za watu wazile. Watu Wangu! Lazima mbaki ndani ya utunzaji Wangu na ulinzi. Kamwe msiwahi kuishi katika hali ya upotovu! Msiwahi tenda mambo kiholela! Badala yake, salimisha uaminifu wako katika nyumba Yangu, na ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kupinga hila ya Shetani. Katika hali yoyote usiishi kama ilivyokuwa katika siku za awali, kufanya jambo moja mbele Yangu na jingine nyuma Yangu—ukifanya hivyo umeshapita kiwango cha kukombolewa. Hakika Nimetamka zaidi ya kiasi cha kutosha maneno ya aina hii, sivyo? Ni kwa sababu asili ya mwanadamu ya zamani hairekebiki ndiyo maana Nimemkumbusha tena na tena. Usichoke! Haya yote Niyasemayo ni kwa mujibu wa kuhakikisha hatima yako! Kile Shetani anahitaji kwa hakika ni uchafu na pahali pabaya; na kadri unavyokosa kuokoleka kabisa, na kadri unavyokuwa mpotovu, ukikataa kujiwasilisha kwa hali ya kujizuia, ndivyo roho wachafu watakavyotumia nafasi yoyote ya kupenyeza. Mara unapowasili katika hii nafasi, uaminifu wako utakuwa kelele tupu, bila uhalisi wowote, na azimio lako litaliwa na pepo wachafu, kugeuzwa kuwa uasi au hila za Shetani, na kutumiwa kuzuia kazi Yangu. Papo hapo Nitakupiga mpaka ufe wakati wowote na popote Nitakavyotaka. Hakuna mtu anayejua uzito wa hali hii; wote wanachukulia mambo wanayosikia kuwa hali ya maneno matupu na hawachukui tahadhari kwa lolote. Sikumbuki kile kilichofanywa katika siku za nyuma. Je, bado unasubiri Niwe mpole kwako Nisahau kwa mara nyingine tena? Ingawa binadamu umenipinga Mimi, Sitashikilia lolote dhidi yake, kwa maana kimo cha mwanadamu ni kidogo mno, na kwa hiyo Sihitaji makubwa kwake. Yote Ninayotaka ni kwamba yeye asijitumie mwenyewe kwa ubadhirifu, na ajiwasilishe kwa kujizuia. Hakika si zaidi ya uwezo wako kufikia sharti hili moja? Wengi wa watu wanasubiri Nifichue mafumbo zaidi ili walishe macho yao. Ilhali, iwapo utakuja kuelewa siri zote za mbinguni, je, ni nini utakalofanya na hayo maarifa? Je, yataweza kuongeza upendo wako Kwangu? Je, yatachochea upendo wako Kwangu? Mimi Simdharau mwanadamu, wala kukata kauli kwa wepesi juu yake. Kama hizi hazingekuwa hali halisi za mwanadamu, Mimi kamwe Singewahi kamwe kuwavisha watu taji na vitambulisho hivi kwa kawaida. Fikiria kuhusu siku za nyuma: Kumekuwepo na nyakati zozote ambazo Nimewahi kuwakashifu nyinyi? Nyakati zozote ambazo Niliwadharau nyinyi? Nyakati zozote ambazo Nimekutazama bila kuzingatia hali zako halisi? Nyakati zozote ambazo Nilichosema kilishindwa kujaza moyo wako na kinywa chako na kusadiki? Nyakati zozote ambazo Nimenena bila ya kuwa na sauti ya undani ndani yenu? Ni nani kati yenu ambaye amesoma maneno Yangu bila hofu na kutetemeka, akiwa na hofu sana kwamba Nitampiga na kumwingiza kuzimu? Ni nani asiyeweza kuvumilia majaribio ndani ya maneno Yangu? Ndani ya maneno Yangu kuna mamlaka, lakini haya si ya kupitisha hukumu ya kawaida juu ya mtu; Badala yake, kwa kujali hali halisi za mwanadamu, daima Namwonyesha mwanadamu maana iliyopo katika maneno Yangu. Kwa kweli, yupo aliye na uwezo wa kutambua nguvu za kudura katika maneno Yangu? Yupo ambaye anaweza kupokea ndani ya nafsi yake dhahabu safi zaidi ambayo maneno Yangu yanaundwa nayo? Nimezungumza maneno mangapi, lakini kuna yeyote ambaye amewahi kuyathamini?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp