Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 136

Kazi ya Mungu katika mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na kumsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, si mwanadamu ni adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa amehitimu kumshuhudia Mungu? Kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu—je, huu si udanganyifu? Kama unayatoa maisha yako kwa haya mambo yasiyokuwa na uhalisia, yasiyoweza kutekelezeka, huoni kama unafanya kazi bure? Unawezaje kuwa mwandani wa Mungu wakati hujui Mungu ni nani? Kufuatilia huko si kusio dhahiri na kwa dhahania? Je, sio kwa udanganyifu? Mtu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Kuna maana gani kivitendo kuwa mwandani wa Mungu? Je, unaweza kuwa mwandani wa Roho wa Mungu? Huwezi kuona jinsi Roho alivyo mkubwa na alivyoinuliwa? Kuwa mwandani wa Mungu asiyeonekana, asiyeshikika—hii sio dhana isiyoeleweka na dhahania? Maana tendaji ya kufuatilia huku ni gani? Je, sio udanganyifu mtupu tu? Kile unachokitafuta ni kuwa mwandani wa Mungu, lakini bado ni mtumwa wa Shetani, maana humfahamu Mungu, na kumtafuta “Mungu wa vitu vyote,” asiye kuwepo ambaye haonekani, hashikiki, na mitazamo yako mwenyewe. Kwa maana isiyo dhahiri, huyo “Mungu” ni Shetani, na kwa uhalisia, ni wewe mwenyewe. Unatafuta kuwa mwandani wako mwenyewe halafu bado unasema unatafuta kuwa mwandani wa Mungu—huko si ni kukufuru? Thamani ya ufukuziaji wako huu ni nini? Ikiwa Roho wa Mungu hawezi kuwa mwili, basi kiini cha Mungu ni kitu kisichoonekana, Roho wa uzima asiyeshikika, asiyekuwa na umbo, hana vitu vya kushikika, hafikiki na mwanadamu hawezi kumtambua. Mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Roho asiyekuwa na mwili, wa ajabu na asiyeweza kueleweka kama huyu? Huu sio utani? Fikra ya kipuuzi kama hiyo ni batili na haitekelezeki. Mwanadamu aliyeumbwa kwa asili yuko tofauti na Roho wa Mungu, sasa inawezekanaje wawili hawa kuwa wandani? Ikiwa Roho wa Mungu hakutambuliwa katika mwili, ikiwa Mungu hakuwa mwili na kujishusha Mwenyewe kwa kufanyika kiumbe, basi mwanadamu aliyeumbwa asingekuwa na sifa na kuwa na uwezo wa kuwa mwandani Wake, na licha ya wachamungu ambao wanaweza kuwa na nafasi ya kuwa wandani wa Mungu baada ya Roho zao kuingia mbinguni, watu wengi wasingeweza kuwa wandani wa Roho wa Mungu. Na ikiwa mwanadamu anataka kuwa mwandani wa Mungu mbinguni chini ya uongozi wa Mungu mwenye mwili, je, yeye si mwanadamu mpumbavu kupindukia? Mwanadamu anakuwa tu “mwaminifu” kwa Mungu asiyeonekana, na wala hamzingatii Mungu ambaye hawezi kuonekana, kwa maana ni rahisi sana kumfuata Mungu asiyeonekana—mwanadamu anaweza kufanya hivyo kwa vyovyote apendavyo. Lakini njia ya Mungu anayeonekana si rahisi. Mwanadamu ambaye anamtafuta Mungu asiye dhahiri hakika hawezi kumpata Mungu, maana vitu ambavyo si dhahiri na ni vya dhahania vyote vinafikiriwa na mwanadamu, na ambavyo mwanadamu hawezi kuvipata. Ikiwa Mungu ambaye alikuja kwenu angekuwa Mungu wa kifahari na aliyeinuliwa ambaye angekuwa hafikiki kwenu, sasa mngewezaje kutafuta mapenzi Yake? Na mngewezaje kumfahamu na kumwelewa? Ikiwa angefanya kazi Yake tu, na wala hakuwa na uhusiano na mwanadamu, au hakuwa na ubinadamu wa kawaida na hakuweza kufikiwa na mwanadamu mwenye mwili wa kufa, basi, hata kama Alifanya kazi kubwa kwa ajili yako, lakini hukuweza kuhusiana naye, na hukuweza kumwona, utawezaje kumfahamu? Kama isingekuwa kwa kuchukua mwili wa ubinadamu, mwanadamu asingeweza kumjua Mungu; ni kwa sababu tu ya Mungu mwenye mwili ndiyo mwanadamu amefuzu kuwa mwandani wa Mungu katika mwili. Mwanadamu huwa mwandani wa Mungu kwa sababu mwanadamu huhusiana naye, kwa sababu mwanadamu huishi naye na kuambatana naye, na kwa hivyo huja kumjua. Isingekuwa hivyo mwanadamu kumtafuta Mungu si kungekuwa ni bure? Hii ni kusema, si kwa sababu ya kazi ya Mungu ndiyo mwanadamu anaweza kuwa mwandani wa Mungu, bali ni kwa sababu ya uhalisi na ukawaida wa Mungu katika mwili. Ni kwa sababu tu Mungu huwa mwili ndiyo mwanadamu huwa na nafasi ya kufanya wajibu wake, na nafasi ya kumwabudu Mungu wa kweli. Je, si huu ni ukweli halisi na unaoweza kutekelezeka? Sasa, bado unatamani kuwa mwandani wa Mungu mbinguni? Ni pale tu ambapo Mungu anajinyenyekeza kwa kiwango fulani, ambavyo ni sawa na kusema, ni pale tu ambapo Mungu anafanyika kuwa mwili, ndipo mwanadamu anaweza kuwa mwandani na msiri Wake. Mungu ni wa Roho: Mwanadamu anawezaje kuwa na sifa ya kuwa mwandani wa Roho huyu, ambaye ameinuliwa sana na asiyeweza kueleweka? Ni pale tu ambapo Roho wa Mungu anaposhuka na kuwa mwili, anakuwa kiumbe anayefanana na mwanadamu, ndipo mwanadamu huweza kuelewa mapenzi Yake na kimsingi kumilikiwa naye. Yeye huzungumza na kufanya kazi katika mwili, hushiriki katika furaha, huzuni, na mateso ya mwanadamu, huishi katika dunia ile ile kama mwanadamu, humlinda mwanadamu, na kumwongoza, na kupitia katika hili humsafisha mwanadamu na kumruhusu mwanadamu kupata wokovu Wake na baraka Zake. Baada ya kuvipata vitu hivi, mwanadamu hupata kuyaelewa mapenzi ya Mungu kwa kweli, na ni hapo tu ndipo anaweza kuwa mwandani wa Mungu. Hii ndiyo inaweza kutekelezeka. Kama Mungu angekuwa haonekani na hashikiki, mwanadamu angewezaje kuwa mwandani Wake? Je, si hili ni fundisho lililo tupu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp