Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 19

20/05/2020

Wale Watu Wasiotambuliwa na Mungu

Kunao baadhi ya watu ambao imani yao haijawahi kutambuliwa katika moyo wa Mungu. Kwa maneno mengine, Mungu hatambui kwamba watu hawa ni wafuasi Wake, kwa sababu Mungu haisifu imani yao. Kwa watu hawa, haijalishi wamemfuata Mungu kwa miaka mingapi, mawazo na mitazamo yao haijawahi kubadilika. Wao ni kama wasioamini, wanatii kanuni na njia ambayo wasioamini wanafanya mambo yao, kutii sheria zao za kusalia na imani. Hawakuwahi kukubali neno la Mungu kama maisha yao, hawakuwahi kusadiki kwamba neno la Mungu ni ukweli, hawakuwahi kunuia kukubali wokovu wa Mungu, na hawakuwahi kutambua Mungu kama Mungu wao. Wanachukulia kusadiki Mungu kuwa uraibu fulani wa wanagenzi, wakishughulikia Mungu kama riziki ya kiroho, hivyo basi hawafikirii kwamba ipo thamani ya kujaribu na kuelewa tabia ya Mungu, au kiini halisi cha Mungu. Unaweza kusema kwamba kila kitu kinacholingana na Mungu wa kweli hakihusiani kwa vyovyote vile na watu hawa. Hawana hamu yoyote, na hawawezi kusumbuliwa ili kuitikia. Hii ni kwa sababu ndani kabisa ya mioyo yao kunayo sauti ya nguvu ambayo siku zote inawaambia: Mungu haonekani na hagusiki, na Mungu hayupo. Wanasadiki kwamba kujaribu kumwelewa Mungu wa aina hii hakutastahili jitihada zao; itakuwa sawa na wao kujidanganya. Wanamtambua Mungu kwa maneno tu, na hawachukui msimamo wowote halisi. Pia hawafanyi chochote katika hali ya kimatendo, wakifikiri kwamba wao ni werevu sana. Mungu anachukulia vipi watu kama hawa? Anawachukulia kuwa wasioamini. Baadhi ya watu huuliza: “Je, wasioamini wanaweza kulisoma neno la Mungu? Je, wanaweza kutekeleza wajibu wao? Je, wanaweza kuyasema maneno haya: ‘Nitaishi kwa ajili ya Mungu’?” Kile ambacho binadamu huona mara nyingi ni maonyesho ya juujuu tu ya watu, na wala si kiini chao halisi. Ilhali Mungu haangalii maonyesho haya ya juujuu; Yeye huona tu kiini chao halisi cha ndani. Hivyo basi, Mungu anao mwelekeo wa aina hii, ufafanuzi wa aina hii, kwa watu kama hawa. Kuhusiana na kile ambacho watu hawa husema: “Kwa nini Mungu hufanya hivi? Kwa nini Mungu hufanya vile? Siwezi kuelewa haya; siwezi kuelewa yale; haya hayaingiliani na fikira za binadamu; Lazima unielezee haya; …” Jibu langu ni: Inahitajika kuelezea suala hili kwako? Je, suala hili lina chochote kuhusiana na wewe? Unafikiria wewe ni nani? Ulitokea wapi? Umefuzu kumwelekeza Mungu? Je, unamwamini Yeye? Je, Anatambua imani yako? Kwa sababu imani yako haina chochote kuhusiana na Mungu, matendo Yake yana uhusiano gani na wewe? Hujui pale ulipo katika moyo wa Mungu, ilhali umefuzu kuzungumza na Mungu?

Maneno ya Maonyo

Hamhisi vibaya baada ya kusikia matamshi haya? Ingawa huenda msiwe radhi kusikiliza maneno haya, au msiwe radhi kuyakubali, yote ni uhakika. Kwa sababu awamu hii ya kazi ni ya Mungu kutenda, kama hujali nia za Mungu, hujali mwelekeo wa Mungu na huelewi kiini halisi na tabia ya Mungu, basi hatimaye wewe ndiwe utakayekosa kufaidi. Msiyalaumu maneno yangu kwa kuwa magumu kusikiliza, na msiyalaumu kwa kupunguza majivuno ya shauku yenu. Mimi naongea ukweli; na wala Sinuii kuwavunja moyo. Haijalishi ni nini Ninachowauliza ninyi, na haijalishi ni vipi mnavyohitajika kukifanya, Ninatumai kwamba mtatembelea njia sahihi, na ninatumai kwamba mtafuata njia ya Mungu na wala msipotoke katika njia hii. Kama hutaendelea kulingana na neno la Mungu, na hufuati njia Yake, basi hakutakuwa na shaka kwamba unaasi dhidi ya Mungu na umepotea kutoka kwa njia sahihi. Hivyo basi Nahisi kwamba yapo masuala fulani ambayo lazima Niwabainishie, na kuwafanya kusadiki dhahiri shairi, waziwazi, bila ya tone la mashaka na kuwasaidia waziwazi kujua mwelekeo wa Mungu, nia za Mungu, namna Mungu anavyomfanya binadamu kuwa mtimilifu, na ni kwa njia gani Yeye Hupanga matokeo ya binadamu. Endapo kutakuwa na siku ambayo hutaweza kuanza katika njia hii, basi Sitahitajika kuwajibika kwa vyovyote vile kwa sababu maneno haya tayari yamezungumzwa kwako waziwazi. Na kuhusu vile unavyoshughulikia matokeo yako binafsi—suala hili lote umeachiwa wewe. Mungu Anayo mielekeo tofauti kuhusiana na matokeo ya watu aina tofauti. Anazo njia Zake binafsi za kuwapima binadamu, na kiwango Chake binafsi cha mahitaji. Kiwango chake cha kuwapima watu ni kile ambacho ni cha haki kwa kila mmoja—hakuna shaka kuhusu hilo. Hivyo basi, woga wa watu fulani hauhitajiki. Je, umepata tulizo la moyo sasa?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp