Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kazi na Kuonekana kwa Mungu | Dondoo 73

Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi Wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango Wake. Usimamizi Wake huendelea kimya kimya, bila madhara ya kutia shauku, ilhali nyayo Zake, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti Chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima. Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho anawasili kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya akiwa na mamlaka na akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya mwanadamu yanabaki yalivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa kawaida, kama mfuasi asiye na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini asiye wa maana. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanawekwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye hutilia maanani uwepo Wake, hamna aliye na mawazo yoyote ya kazi Yake, na zaidi ya hayo, hakuna mtu aliye na tuhuma yoyote kuhusu Yeye ni nani. Sisi huendelea na kazi yetu tu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi …

Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa sana, tunatambua kuwa hilo ni tamko la Mungu, na tunaukubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hatuwezi kuyakana. Tamko linalofuata linaweza kuwa kupitia kwangu, au kwako, ama linaweza kupitia yeye. Bila kujali ni nani, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu huyo ni nani, hatufai kumwabudu, kwa kuwa bila kuzingatia chochote kingine, hawezi kuwa Mungu; hatuwezi kwa njia yoyote kumchagua mtu wa kawaida kama huyu kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika sana; Anawezaje kuwakilishwa na binadamu asiye na umuhimu hivyo? Zaidi ya hayo, sisi sote tunasubiri ujaji wa Mungu kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu hivyo anawezaje kustahili kufanya kazi ngumu na muhimu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, linaloonekana na wote. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itakuwaje Ajifiche kwa ukimya kati ya kundi la watu wa kawaida?

Na bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu, wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa na aibu na fedheha. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anatarajia kufanya. Labda tunaweza tu kunyakuliwa baada ya kuvumilia maumivu kama hayo? Vichwani mwetu tunafanya hesabu … kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili na hutenda kazi kati yetu. Japokuwa Amekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado hatuko tayari kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, wala hatuna nia ya kumwaminisha mtu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na hatima yetu. Kutoka Kwake, tunafurahia ugavi usioisha wa maji ya uhai, na kwa sababu Yake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Sisi tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Yeye bado, kwa unyenyekevu, hufanya kazi akiwa amefichwa ndani ya mwili, akionyesha sauti ya moyo Wake, akionekana kama hafahamu kukataliwa Kwake na binadamu, inavyoonekana yeye milele kusamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele kuvumilia mwanadamu kutomheshimu.

Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya kuzaliwa upya; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake na huba Yake; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, waliofanywa majivu na ghadhabu Yake katika macho Yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana, na Hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Ila, licha ya haya, majivuno yangali mioyoni mwetu, na sisi bado hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana nyingi sana, nyingi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambalo linaweza kunyakua nafasi ya Bwana katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum na hadhi ya huyu mwanadamu kwa kusita sana. Kama Yeye haneni kwa nguvu na kutufanya kukiri kwamba Yeye ni Mungu, basi sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu ambaye yuko karibu kuja ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu sana.

Matamshi ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya tutakachofanya na kuonyesha sauti ya moyo Wake. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na sauti ya moyo ya huyu mwanadamu asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu, anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu. Asili kama hii na mali Zake zimeshinda za binadamu wa kawaida, na haziwezi kumilikiwa au kupatwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, kutoka Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu, na kuonyesha sauti ya moyo ya Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu ambayo huelekezwa kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na Ametuletea matumaini, na akamaliza maisha yetu ambayo hayakuwa dhahiri, na Akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, si Yeye ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huo, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, wala hatupingi tena kazi na neno Lake, na tunasujudu, kabisa, mbele Yake. Hakuna tunachotaka ila kufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp