Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 241

09/08/2020

Duniani, Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe katika mioyo ya watu; mbinguni, Mimi Ndiye Mkuu wa viumbe vyote. Nimepanda milima na kuvuka mito, na Nimeingia na kutoka katikati ya binadamu. Nani anathubutu kwa uwazi kumpinga Mungu wa vitendo Mwenyewe? Nani anathubutu kutoka kati ya ukuu wa Mwenyezi? Nani anayethubutu kudai kuwa Mimi, bila shaka, Niko mbinguni? Tena, nani ambaye anathubutu kudai kuwa Mimi, bila kukosea, Niko duniani? Hakuna binadamu kati ya wote anayeweza kujieleza kwa ufasaha na undani mahali ambapo Mimi Naishi. Inawezekana kuwa kwamba, wakati Mimi niko mbinguni, Mimi ni Mungu Mwenyewe asiye wa kawaida? Inawezekana kuwa kwamba, wakati Mimi niko hapa duniani, Ninakuwa Mungu wa vitendo Mwenyewe? Kwamba Mimi ni Mtawala wa viumbe vyote, au kwamba Mimi ninapitia mateso ya ulimwengu wa mwanadamu—hakika hivi haviwezi kuamua iwapo Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe? Kama mwanadamu anadhani hivyo, si yeye ni mpumbavu asiye na matumaini ya kubadilika? Mimi niko mbinguni; Mimi pia Niko duniani; Niko miongoni mwa mambo idadi kubwa ya viumbe, na pia katikati ya idadi kubwa ya watu. Mwanadamu anaweza kunigusa kila siku; zaidi ya hayo, anaweza kuniona kila siku. Kulingana na binadamu, Mimi huonekana kuwa wakati mwingine Nimejificha na wakati mwingine Naonekana; Mimi Naonekana kuwa na maisha halisi, na hata hivyo Naonekana pia kutokuwa na nafsi. Ndani Mwangu kuna siri kubwa sana zisizoweza kufahamika na binadamu. Ni kana kwamba watu wote wananitazama kwa njia ya hadubini ili kugundua siri hata zaidi ndani Mwangu, wakiwa na matumaini ya kuondoa hisia za wasiwasi katika nyoyo zao. Lakini hata watumie darubini ya nguvu kivipi, binadamu watawezaje kuziweka wazi siri zilizo ndani Mwangu?

Wakati watu Wangu, kupitia kwa kazi Yangu, wanatukuzwa pamoja na Mimi, wakati huo maficho ya joka kubwa jekundu yatafichuliwa, matope yote na uchafu kufagiliwa mbali, na maji machafu, yaliyokusanyika kwa miaka mingi, kukaushwa na moto Wangu unaochoma, yasikuwepo tena. Hapo joka kubwa jekundu litaangamia katika ziwa la moto wa jehanamu. Je, kweli unayo nia ya kusalia chini ya ulinzi Wangu ili usinyakuliwe na joka? Je, kweli unachukia mbinu yake ya udanganyifu? Nani ambaye anaweza kuwa shahidi Wangu wa dhati? Kwa ajili ya jina Langu, kwa ajili ya Roho Wangu, kwa ajili ya mpango Wangu mzima wa usimamizi—nani ambaye anaweza kutoa nguvu zake zote katika mwili wake? Leo, wakati ufalme uko katika ulimwengu wa watu, ndio wakati ambao Nimekuja binafsi katika ulimwengu wa wanadamu. Kama haingekuwa hivyo, je, yupo ambaye angeweza, kwa ujasiri, kwenda katika uwanja wa vita kwa niaba Yangu? Ndipo ufalme uweze kuchukua mkondo, ili moyo Wangu uweze kuridhika, na tena, ili siku Yangu iweze kuja, ili wakati uweze kuja ambapo mambo mengiya uumbaji yamezaliwa upya na kukua kwa wingi, ili kwamba mwanadamu aweze kuokolewa kutoka kwenye bahari ya mateso, ili siku inayofuata iweze kuja, na ili iwe ni ya ajabu, yenye kutoa maua na kushamiri, na tena, ili starehe ya siku za usoni itimizwe, binadamu wote wanajitahidi kwa nguvu zao zote, bila kuwacha chochote katika kujitoa sadaka wenyewe kwa ajili Yangu. Je, hii si ishara kwamba ushindi tayari ni Wangu, na alama ya kukamilika kwa mpango Wangu?

Wanadamu wanavyozidi kukaa katika siku za mwisho, ndivyo watakavyozidi kuhisi utupu wa dunia na ndivyo watakavyopungukiwa na ujasiri wa jinsi ya kuishi. Kwa sababu hii, watu wasiohesabika wamekufa katika hali ya kuvunja matumaini, wengine wengi wamevunjwa matumaini katika jitihada zao, na wengine wengi kuteseka wenyewe kuwa kunyanyaswa katika mikono ya shetani. Mimi Nimewaokoa watu wengi, Nimewapa wengi msaada, na mara nyingi, wakati binadamu wamepoteza mwanga, Mimi Nimewaongoza kurudi katika nafasi ya mwanga, ili wapate kunijua wakiwa kwenye mwanga, na kunifurahia katika furaha. Kwa sababu ya ujio wa mwanga Wangu, kuabudu hukuzwa katika mioyo ya watu wanaokaa katika ufalme Wangu, kwa maana Mimi ni Mungu wa kupendwa na binadamu, Mungu ambaye binadamu unajishika katika hali ya upendo, na mwanadamu anajazwa na maono ya kudumu ya umbo Langu. Lakini, hatimaye, hakuna yeyote ambaye anaelewa kama hii ni kazi ya Roho, au ni kutokana na mwili. Hili jambo moja pekee linatosha kumfanya mwanadamu kupitia mwendo wa maisha kwa undani. Mwanadamu hajawahi kunichukia katika undani wa moyo wake kabisa; badala yake, yeye huambatana na Mimi katika kina cha roho yake. Hekima yangu inaibua upendezewaji wake, maajabu Ninayotenda ni ukuu machoni pake, maneno Yangu yanastaajabisha akili yake, na bado yeye ana mapenzi tele kwayo. Ukweli Wangu humfanya mwanadamu asijue la kusema, aduwae na kushtuka, na bado yeye yuko tayari kukubali hayo yote. Je, hiki si kipimo cha mwanadamu jinsi alivyo hasa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 15

God Is in Heaven and Also on Earth

I

When on earth, God is a practical God in the hearts of man. In heaven He’s the Master, ruling over everything. He’s climbed the mountains and waded through the rivers. He has drifted in and out through the place where people live. God is up in heaven, and on earth He resides. He’s among all creation, amidst the myriads of mankind. Man can touch God every day, man can see Him every day.

II

Who dares to oppose practical God and break out from His reign? Who dares to assert that He’s in heaven, beyond the shadow of doubt? Who dares assert that God for certain exists on earth? In all humanity, none can say or describe where God dwells. God is up in heaven, and on earth He resides. He’s among all creation, amidst the myriads of mankind. Man can touch God every day, man can see Him every day.

III

Could it be when in heaven, He’s a supernatural God? Could it be when God’s on earth, He is practical God Himself? Ruling all creation or tasting human suffering, can these determine He’s practical God Himself? God is up in heaven (God is in heaven), and on earth He resides (and on earth He resides). He’s among all creation (all creation), amidst the myriads of mankind. Man can touch God every day (man can touch Him every day), man can see Him every day (every day). God is in heaven, and on earth He resides.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp