Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 160

Baada ya uumbaji wa mwanadamu hapo mwanzoni, Waisraeli ndio waliokuwa kielelezo cha kazi, na Israeli nzima ilikuwa ngome ya kazi ya Yehova duniani. Kazi ya Yehova ilikuwa imwongoze mwanadamu moja kwa moja na kumchunga kwa kuweka wazi sheria ili kwamba mwanadamu aweze kuishi maisha ya kawaida na kumwabudu Yehova kwa njia ya kawaida duniani. Katika Enzi ya Sheria Mungu alikuwa Asiyeonekana wala kuguswa na mwanadamu. Alikuwa tu Anawaongoza wanadamu waliokuwa mwanzo wamepotoshwa na Shetani, na Alikuwepo kuwaagiza na kuwaongoza wanadamu, kwa hivyo maneno yote Aliyoyanena yalikuwa ya kisheria, amri na uelewa wa kawaida wa kuishi maisha kama mwanadamu, na wala sio kuhusu ukweli unaomruzuku mwanadamu. Waisraeli chini ya uongozi Wake hawakuwa wale waliopotoshwa zaidi na Shetani. Kazi yake ya kisheria ilikuwa tu hatua ya kwanza kabisa katika kazi ya ukombozi, mwanzo hasa wa kazi ya wokovu, na haikuwa inahusiana kamwe na mabadiliko katika tabia za kimaisha za mwanadamu. Kwa hivyo, mwanzoni mwa kazi ya ukombozi hapakuwa na haja Kwake kuwa katika mwili kwa ajili ya kazi Yake katika Israeli. Ndiyo maana Alihitaji kiungo, yaani, chombo ambacho kwacho Angemfikia mwanadamu. Kwa hivyo kukazuka miongoni mwa viumbe waliozungumza na kufanya kazi kwa niaba ya Yehova, na hivi ndivyo wana wa wanadamu na manabii walikuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu. Wana wa wanadamu walifanya kazi miongoni mwa wanadamu kwa niaba ya Yehova. Ili waitwe na Yeye inamaanisha kuwa hao watu walipanga sheria kwa niaba ya Yehova na walikuwa miongoni mwa watu wa Israeli; na watu kama hao walikuwa makasisi walioangaliwa na kulindwa na Yehova, na Roho wa Yehova alifanya kazi ndani yao; walikuwa viongozi miongoni mwa wanadamu na wahudumu wa Yehova wa moja kwa moja. Manabii kwa upande mwingine ndio waliokuwa na jukumu la kunena na mataifa na makabila yote kwa niaba ya Yehova. Ndio vilevile waliotoa unabii kuhusu kazi ya Yehova. Wote wanadamu na manabii walikuzwa na Roho wa Yehova Mwenyewe na walikuwa na kazi ya Yehova ndani yao. Miongoni mwa wanadamu, walikuwa ndio wale waliomwakilisha Yehova moja kwa moja; walifanya kazi tu kwa kuwa waliinuliwa na Yehova wala si kwa kuwa walikuwa miili ambamo Roho mtakatifu Mwenyewe alikuwa kapata mwili. Kwa hivyo, ingawa wao walifanya kazi na kuongea kwa niaba ya Mungu, hao wana wa mwanadamu na manabii wa Enzi ya Sheria hawakuwa mwili wa Mungu mwenye mwili. Hii ilikuwa kinyume kabisa katika Enzi ya Neema na hatua ya mwisho, kwani kazi ya ukombozi na hukumu ya mwanadamu vilifanywa na Mungu katika mwili Mwenyewe, na hapakuwa na haja ya kukuza manabii na wanadamu kufanya kazi kwa niaba Yake. Machoni pa mwanadamu, hamna tofauti kubwa kati ya kiini na mbinu za kazi zao. Ni kwa sababu hii mwanadamu anachanganya kati ya kazi ya Mungu kuwa mwili na ile ya manabii na wanadamu. Kimsingi, umbo la Mungu mwenye mwili lilikuwa sawa na lile la manabii na wanadamu. Mungu kuwa mwili alikuwa wa kawaida na halisi zaidi kuliko manabii. Kwa hivyo mwanadamu anashindwa kabisa kuwatofautisha. Mwanadamu huangazia umbile peke yake bila kugundua kuwa japo wote hufanya kazi na kuongea, kuna tofauti kubwa kati yao. Kwa sababu uwezo wa mwanadamu wa kung’amua ni duni, mwanadamu anashindwa kung’amua mambo ya kimsingi na hata zaidi hawezi kubainisha kitu changamano. Maneno na kazi za manabii na za wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu zote zilikuwa zinafanya wajibu wa mwanadamu, kufanya jukumu lake kama kiumbe na kufanya ambacho mwanadamu anapaswa kufanya. Hata hivyo, maneno na kazi za Mungu mwenye mwili ilikuwa ni kuendeleza huduma Yake. Japo umbile Lake lilikuwa lile la kiumbe, kazi Yake haikuwa kutimiza majukumu Yake bali Huduma Yake. Dhana “wajibu” inarejelea viumbe ilhali “huduma” inarejelea mwili wa Mungu mwenye mwili. Kuna tofauti kubwa kati ya haya mawili, na haya mawili hayabadilishani nafasi. Kazi ya mwanadamu ni kufanya wajibu wake, ilhali kazi ya Mungu ni kusimamia, na kuendeleza huduma Yake. Kwa hivyo, japo mitume wengi walitumiwa na Roho Mtakatifu na manabii wengi wakajazwa Naye, kazi zao na maneno yao yalikuwa tu kutimiza wajibu wao kama viumbe. Japo unabii wao ungeweza kuwa mkubwa kuliko maisha kama yanavyozungumziwa na Mungu mwenye mwili, na hata ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu kuliko wa Mungu kuwa mwenye mwili, walikuwa bado wanafanya wajibu wao na wala si kutimiza huduma yao. Wajibu wa mwanadamu unarejelea majukumu yake, na ni kitu kinachoweza kupatwa kwa mwanadamu. Hata hivyo, huduma ifanywayo na Mungu mwenye mwili inahusiana na usimamizi Wake, na haiwezi kupatikana kwa mwanadamu. Hata kama Mungu mwenye mwili hunena, kufanya kazi, au kutenda miujiza, Anafanya kazi kubwa katika usimamizi Wake, kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya mwanadamu ni kufanya tu wajibu wake kama kiumbe katika hatua fulani ya usimamizi wa Mungu. Bila usimamizi kama huo, yaani, ikiwa huduma ya Mungu kuwa mwili itapotea, pia wajibu wa viumbe utapotea. Kazi ya Mungu kuendeleza huduma Yake ni kumsimamia mwanadamu, ilhali mwanadamu afanyapo wajibu wake ni kutimiza wajibu wake ili kuafikia masharti ya Muumba na haiwezi kwa vyovyote vile kuchukuliwa kwamba ameendeleza huduma ya mtu yeyote. Kwa nafsi asili ya Mungu, yaani, Roho, kazi ya Mungu ni usimamizi wake, bali kwa Mungu kuwa mwili akiwa na umbile la nje la kiumbe, kazi yake ni kuendeleza huduma Yake. Kazi yoyote Aifanyayo Mungu ni ya kuendeleza huduma Yake, na mwanadamu anaweza tu kufanya awezalo ndani ya upeo Wake wa usimamizi na chini ya uongozi Wake.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp