Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 107
05/08/2020
Ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake. Ingawa yuko katika mwili, ubinadamu Wake si kama ule wa binadamu wa mwili kabisa. Anao upekee wa tabia Yake Mwenyewe, na hii pia huongozwa na uungu Wake. Uungu Wake hauna udhaifu; udhaifu wa Kristo unaelezea ule wa ubinadamu Wake. Kwa kiasi fulani, udhaifu huu huzuia uungu Wake, lakini mipaka hiyo ipo tu kati ya wigo fulani na wakati, na sio zisizo na mipaka. Linapokuja suala la muda wa kufanya kazi ya uungu Wake, hufanyika bila kujali ubinadamu Wake. Ubinadamu wa Kristo kabisa huongozwa na uungu Wake. Mbali na maisha ya kawaida ya ubinadamu Wake, matendo mengine yote ya ubinadamu Wake ni ya kushawishiwa, inayoathirika na kuelekezwa na uungu Wake. Ingawa Kristo Anao ubinadamu, haukatizi kazi ya uungu Wake. Hii hasa ni kwa sababu ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake; ingawa ubinadamu Wake haujakomaa katika mwenendo Wake mbele ya wengine, hauathiri kazi ya kawaida ya uungu Wake. Ninaposema kwamba ubinadamu Wake haujapotoshwa, Ninamaanisha kwamba ubinadamu wa Kristo unaweza moja kwa moja kuongozwa na uungu Wake, na kwamba Yeye ni mwenye hisia kubwa kuliko ile ya mwanadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake unafaa zaidi kwa kuongozwa na uungu katika kazi Yake; ubinadamu Wake una uwezo wa kuonyesha kazi ya uungu, kama vile unao uwezo wa kutii kazi kama hiyo. Mungu Anapofanya kazi katika mwili, hajawahi kamwe kupoteza maono ya wajibu wa mwanadamu katika mwili Anaopaswa kutimiza; Anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli. Anayo dutu ya Mungu, na utambulisho Wake ni mfano wa Mungu Mwenyewe. Ni kwamba tu Amekuja duniani na kuwa kiumbe aliyeumbwa, na ganda la nje la kiumbe, na sasa Amemiliki ubinadamu ambao hakuwa nao mwanzo; Yeye anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni. Hiki ni kiumbe cha Mungu Mwenyewe na hakiigwi na binadamu. Utambulisho Wake ni Mungu Mwenyewe. Ni kutokana na mtazamo wa mwili ndio Yeye huabudu Mungu; Kwa hivyo, maneno “Kristo huabudu Mungu mbinguni” si kwa makosa. Kile Anachouliza binadamu hasa ni nafsi Yake Mwenyewe; Yeye tayari Ameshafanikisha yote Anayotarajia kutoka kwa binadamu kabla ya kuwauliza wafanye hayo. Asingeweza kudai wengine wakati Yeye Mwenyewe Anapata kwao bure, kwa kuwa haya yote yanayotengeneza nafsi Yake. Bila kujali jinsi Yeye hufanya kazi Yake, wala Naye hangewahi kutenda kwa namna inayomuasi Mungu. Haijalishi Analomuuliza mwanadamu, hakuna mahitaji Yake yanayozidi uwezo wa mwanadamu kupata. Yote Afanyayo ni kufanya mapenzi ya Mungu na ni kwa ajili ya usimamizi Wake. Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake. Kwa hiyo, haijalishi jinsi ubinadamu Wake ni wa kawaida ni wazi kuwa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe; haijalishi upande Anaosimama Akiongea na kwa vyovyote vile Yeye hutii mapenzi ya Mungu, haiwezi kusemwa kwamba Yeye si Mungu Mwenyewe. Wanadamu wajinga na wapumbavu mara nyingi huchukua ubinadamu wa kawaida wa Kristo kama dosari. Haijalishi jinsi Anavyofichua na kuonyesha nafsi ya uungu Wake, mwanadamu bado hawezi kukiri kwamba Yeye ni Kristo. Na zaidi kwamba Kristo Anaonyesha utii Wake na unyenyekevu, ndivyo wanadamu wengi wajinga humchukua Kristo kwa mzaha. Kuna hata wale ambao huelekeza Kwake mtizamo wa kutengwa na dharau, ilhali kuweka wale “wanadamu wakubwa” wa picha ya kujidai juu ya meza na kuwaabudu. Upinzani wa binadamu dhidi ya, na uasi wa Mungu huja kutokana na ukweli kwamba kiini cha Mungu mwenye mwili hutii mapenzi ya Mungu, vili vile kutokana ubinadamu wa kawaida wa Kristo; hapa ndipo kuna chanzo cha upinzani wa binadamu na uasi wake kwa Mungu. Kama Kristo hangekuwa mwenye umbo la ubinadamu wala nia ya kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe aliyeumbwa, lakini badala yake kumiliki ubinadamu mkuu, basi kuna uwezekano hakungekuwa na uasi katika mwanadamu yeyote. Sababu ya binadamu kuwa tayari kuamini katika Mungu Asiyeonekana mbinguni ni kwa sababu Mungu mbinguni hana ubinadamu na Yeye hana sifa ya kiumbe hata moja. Hivyo binadamu siku zote humchukua Yeye kwa heshima kubwa, lakini anayo tabia ya dharau kwa Kristo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video