Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 433

Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Kadiri watu wanavyoujua uhalisi zaidi, kadiri wanavyoweza kugundua ikiwa maneno ya wengine ni halisi; kadiri watu wanavyojua uhalisi, ndivyo wanavyokuwa na dhana kidogo zaidi; kadiri watu wanavyopitia uhalisi zaidi, kadiri wanavyojua zaidi matendo ya Mungu wa uhalisi, na ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kuacha nyuma tabia zao potovu na za kishetani; kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyomjua Mungu zaidi na kuuchukia mwili zaidi na kupenda ukweli; na kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyofika karibu na ubora wa mahitaji ya Mungu. Watu waliopatikana na Mungu ni wale walio na uhalisi, na wanaojua uhalisi; wale ambao wamepatikana na Mungu wamepata kuyajua matendo halisi ya Mungu kutokana na kupitia katika uhalisi. Kadiri hasa unavyoshirikiana zaidi na Mungu na kuudhibiti mwili wako, ndivyo utakavyopokea zaidi kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo utakavyopata uhalisi zaidi, na ndivyo utapatiwa nuru zaidi na Mungu—na hivyo ukubwa wa ufahamu wako wa matendo halisi ya Mungu. Ikiwa unaweza kuishi katika mwangaza wa sasa wa Roho Mtakatifu, njia ya sasa ya kutenda itakuwa wazi kwako, na utaweza kujitenga zaidi na dhana za kidini na vitendo vilivyopita zamani. Leo tunalenga uhalisi: Kadiri watu walivyo na uhalisi zaidi, ndivyo ufahamu wao wa ukweli unavyokuwa wazi, na ufahamu wao wa mapenzi ya Mungu unaongezeka. Uhalisi unaweza kuzishinda nyaraka zote na mafundisho yote ya kidini, unaweza kushinda nadharia na utaalamu wote, na kadiri watu wanavyoangazia uhalisi zaidi, ndivyo wanavyompenda Mungu kwa dhati zaidi na kuyatamani maneno Yake. Ikiwa daima unalenga uhalisi, falsafa yako ya maisha, dhana za kidini, na tabia asilia zitafutwa kutokana na kazi ya Mungu. Wale wasiouandama uhalisi, na hawafahamu uhalisi, wanaelekea kutafuta kile kilicho na nguvu za juu, na watalaghaiwa kwa urahisi. Roho Mtakatifu hana namna ya kufanya kazi ndani ya watu kama hao, na kwa hivyo wanajisikia watupu, na kwamba maisha yao hayana maana.

Roho Mtakatifu anaweza tu kufanya kazi ndani yako ukijifunza kweli, ukitafuta kweli, ukiomba kweli, na ukiwa radhi kuteseka kwa ajili ya kuutafuta ukweli. Wale ambao hawautafuti ukweli hawana chochote ila tu nyaraka na mafundisho ya kidini, na nadharia tupu, na wale wasio na ukweli kiasili wana dhana nyingi kuhusu Mungu. Watu kama hawa hutamani tu Mungu aibadilishe miili yao ya nyama kuwa miili ya kiroho ili kwamba waweze kurudi katika mbingu ya tatu. Hawa watu ni wapumbavu kiasi gani? Wote wasemao mambo sampuli hii hawana ufahamu wa Mungu, au uhalisi; watu kama hawa hawawezi kushirikiana na Mungu, na wanaweza tu kusubiri bila kufanya chochote. Ikiwa watu wanataka kuelewa ukweli, na kuuona ukweli wazi wazi, na ikiwa, aidha, wanataka kuingia ndani ya ukweli, na kuuweka katika vitendo, ni sharti wajifunze kweli, watafute kweli, na wawe na hitaji la kweli. Unapotamani, na unaposhirikiana na Mungu kweli, Roho wa Mungu kwa hakika atakugusa na kufanya kazi ndani yako, jambo ambalo litakuletea nuru zaidi na kukupa ufahamu zaidi kuhusu uhalisi na kuwa wa msaada mkubwa kwa maisha yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kujua Uhalisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp