Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 610

06/09/2020

Nina matamanio mengi. Natamani muweze kutenda kwa njia inayofaa na yenye mwenendo mzuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, muwe na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu na kutotii kwenu. Kama kila mojawapo ya mazungumzo ambayo Nimekuwa nayo na nyinyi hayajatosha kuvuta nadhari yenu, basi huenda Sitasema mengine. Hata hivyo, nyinyi mnaelewa matokeo ya hayo. Sipumziki kamwe, kwa hiyo Nisiponena, Nitafanya kitu ili watu wakitazame. Ningeweza kuufanya ulimi wa mtu uoze, au mtu afe na viungo vyake kutolewa, au kumpa mtu kasoro za neva na kumfanya atende kama mwendawazimu. Au, basi tena, Ningeweza kufanya baadhi ya watu wavumilie maumivu makali Ninayowasababishia. Kwa njia hii Ningejihisi mwenye furaha, mwenye furaha sana na kufurahishwa sana. Imesemwa daima kwamba “Mema hulipizwa kwa mema, na maovu kwa maovu,” mbona isiwe hivyo sasa? Kama unataka kunipinga Mimi na unataka kutoa hukumu fulani kunihusu, basi Nitauozesha mdomo wako, na hilo litanipendeza Mimi sana. Hii ni kwa sababu mwishowe hujafanya lolote linalohusiana na ukweli, sembuse na maisha, ilhali kila kitu Ninachofanya ni ukweli, kila kitu kinahusiana na kanuni za kazi Yangu na amri za utawala Ninazoeleza rasmi. Kwa hiyo, Namsihi sana kila mmoja wenu kujilimbikiza wema kiasi, acha kufanya maovu mengi sana, na usikize madai Yangu katika wasaa wako. Kisha mimi Nitahisi furaha. Kama mngetoa (au kusaidia) kwa ukweli moja kwa elfu ya juhudi mnazoweka katika mwili, basi Nasema hungekuwa na dhambi mara kwa mara na midomo mbovu. Je, hili si dhahiri?

Kadri dhambi zako zilivyo nyingi, ndivyo nafasi zako za kupata hatima iliyo nzuri zilivyo chache. Kinyume chake, kadri dhambi zako zilivyo chache, ndivyo nafasi zako za kusifiwa na Mungu zilivyo nyingi. Kama dhambi zako zitaongezeka hadi kiwango ambapo haiwezekani Mimi kukusamehe, basi utakuwa umepoteza kabisa nafasi yako ya kusamehewa. Hivyo hatima yako haitakuwa juu bali chini. Kama huniamini basi kuwa jasiri na ufanye maovu, na kisha uone kile kitakachokupata. Kama wewe ni mtu mwenye ari anayetenda ukweli basi kwa hakika una fursa ya kusamehewa dhambi zako, na kiwango cha kutotii kwako kitakuwa kidogo zaidi na zaidi. Kama wewe ni mtu asiye radhi kutenda ukweli basi hakika dhambi zako mbele ya Mungu zitaongezeka, kiwango cha kutotii kwako kitakua zaidi na zaidi, mpaka wakati wa mwisho ambapo utakuwa umeangamia kabisa, na huo ndio wakati ambao ndoto yako ya kufurahisha ya kupokea baraka itaharibiwa. Usizichukulie dhambi zako kama makosa ya mtu asiye mkomavu au mpumbavu, usitumie kisingizio kwamba hukutenda ukweli kwa sababu ubora wako wa tabia ulio duni ulifanya isiwezekane kuutenda, na hata zaidi, usizichukulie tu dhambi ulizofanya kama matendo ya mtu ambaye hakujua vizuri zaidi. Kama unajua vizuri kujisamehe na unajua vizuri kujitendea kwa ukarimu, basi Ninasema wewe ni mwoga ambaye kamwe hataupata ukweli, na dhambi zako kamwe hazitakoma kukusumbua, lakini zitakuzuia kuwahi kutosheleza madai ya ukweli na kukufanya milele kuwa mwenzi mwaminifu wa Shetani. Ushauri Wangu kwako bado ni: Usiwe makini sana kwa hatima yako tu na kutotilia maanani dhambi zako zilizofichika; zichukulie dhambi zako kwa makini, na usikose kutilia maanani dhambi zako zote kwa sababu ya kujali kuhusu hatima yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp