Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 591

Leo, harakati ya mwanadamu ya kukuwa mshindi na kufanywa mkamilifu ni vitu ambavyo vinafuatwa kabla yeye hajakuwa na maisha ya mtu wa kawaida duniani, na ndiyo malengo ambayo mwanadamu hutafuta kabla ya utumwa wa Shetani. Kwa kiini, harakati ya mwanadamu ya kukuwa mshindi na kufanywa kamili, au kufanywa wa kutumika vilivyo, ni kutoroka kutoka katika ushawishi wa Shetani. Harakati ya mwanadamu ni kuwa mshindi, lakini matokeo ya mwisho yatakuwa ni kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ni kwa kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani tu ndipo mwanadamu ataweza kuishi maisha ya mtu wa kawaida duniani, maisha ya kumwabudu Mungu. Leo, harakati ya mtu ya kukuwa mshindi na kufanywa kamilifu ndiyo mambo ambayo yanafuatwa kabla ya kuwa na maisha ya mtu wa kawaida duniani. Haya yanafuatwa kimsingi kwa ajili ya kutakaswa na kuweka ukweli katika vitendo, na ili kufanikisha ibada ya Muumba. Kama mwanadamu anamiliki maisha ya mtu wa kawaida duniani, maisha ambayo hayana taabu na matatizo, basi mwanadamu hawezi kushiriki katika harakati za kuwa mshindi. “Kuwa mshindi” na “kufanywa kamili” ni malengo ambayo Mungu humpa mwanadamu kufuatilia, na katika ufukuziaji wa malengo haya, Yeye husababisha mwanadamu kuweka ukweli katika vitendo na kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye umuhimu. Lengo ni kumkamilisha mtu na kumpata yeye, na harakati ya kukuwa mshindi na kufanywa kamili ni njia tu. Kama, hapo mbeleni, mwanadamu ataingia kwenye hatima ya ajabu, hakutakuwepo na kurejelea kuwa mshindi na kukamilika, kutakuwepo tu na kila kiumbe kikitekeleza wajibu wake. Leo, mwanadamu anafanywa kufuata mambo haya tu ili kufafanua upeo wa mwanadamu, ili harakati ya mwanadamu ilengwe zaidi na iwe ya utendaji zaidi. Bila hayo, harakati ya mwanadamu ya kuingia katika uzima wa milele ingekuwa sio dhahiri na ya kudhania, na kama ingekuwa hivyo, je, si mwanadamu hata angelikuwa hafifu hata zaidi? Kufuata njia hii, bila malengo au kanuni—je, hii sio kujidanganya? Hatimaye, harakati hii ingekuwa kama kawaida bila mazao; na mwishowe, mwanadamu bado angemilikiwa na Shetani na hangeweza kujinasua mwenyewe kutokana nayo. Mbona ajikabili mwenyewe kwenye harakati kama hii isiyo na sababu? Wakati mwanadamu ataingia kwenye hatima ya milele, mwanadamu atamwabudu Muumba, na kwa sababu mwanadamu amepata wokovu na kuingia ahera, mwanadamu hawezi kimbiza malengo yoyote, wala, zaidi ya hayo, yeye hatakuwa na haja ya kuhangaika kuwa atazingirwa na Shetani. Kwa wakati huu, mwanadamu atajua nafasi yake, na atatekeleza wajibu wake, na hata kama hataadibiwa au kuhukumiwa, kila mtu atatekeleza jukumu lake. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa kiumbe katika sura na hadhi pia. Hakutakuwepo tena na tofauti ya juu na chini; kila mtu atatekeleza tu kazi tofauti. Bado mwanadamu ataishi katika hatima ya wanadamu yenye utaratibu na ifaayo, mwanadamu atatekeleza wajibu wake kwa ajili ya kumwabudu Muumba, na wanadamu kama hawa ni wanadamu wa milele. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa amepata maisha yaliyoangaziwa na Mungu, maisha chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, na maisha pamoja na Mungu. Wanadamu wataishi maisha ya kawaida duniani, na wanadamu wote wataingia katika njia sahihi. Mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 utakuwa umemshinda Shetani kabisa, ambayo ina maana kuwa Mungu atakuwa amerejesha sura ya awali ya mwanadamu kufuatia kuumbwa kwake, na kwa hivyo, nia ya awali ya Mungu itakuwa imetimizwa. Hapo mwanzo, kabla mwanadamu hajapotoshwa na Shetani, mwanadamu aliishi maisha ya kawaida duniani. Baadaye, alipopotoshwa na Shetani, mwanadamu alipoteza maisha haya ya kawaida, na kwa hivyo kazi ya Mungu ya usimamizi ikaanza, na vita dhidi ya Shetani ikaanza ili kurejesha maisha ya kawaida ya mwanadamu. Ni wakati tu ambapo usimamizi wa kazi ya Mungu wa miaka 6,000 utafikia kikomo ndipo maisha ya mwanadamu yatakapoanza rasmi hapa duniani, ni wakati huo tu ndipo mwanadamu atakapokuwa na maisha mazuri, na Mungu atarejesha lengo la kumuumba mwanadamu hapo mwanzoni, na pia kufanana kwake kwa asili na mwanadamu. Na kwa hivyo, punde tu atakuwa na maisha ya kawaida ya mwanadamu duniani, mwanadamu hatafuatilia kuwa mshindi ama kuwa kamili, kwa kuwa mwanadamu atakuwa mtakatifu. Ushindi na ukamilifu uliosemwa na mwanadamu ndiyo malengo yaliyopewa mwanadamu ili kufuata wakati wa vita kati ya Mungu na Shetani, na yapo tu kwa sababu mwanadamu amepotoshwa. Ni kwa kukupa lengo, na kukufanya wewe kufuata lengo hili, ndipo Shetani atashindwa. Kukuambia uwe mshindi au ufanywe kamili ama utumike kunahitaji ya kwamba uwe na ushuhuda ili umwaibishe Shetani. Mwishowe, mwanadamu ataishi maisha ya mwanadamu wa kawaida duniani, na mwanadamu atakuwa mtakatifu, na wakati hii itatendeka, je, watatafuta kuwa washindi? Je, wote si viumbe? Kuwa mshindi na kuwa yule aliyekamilika yote mawili yanaelekezwa kwa Shetani, na uchafu wa mwanadamu. Je, hii “mshindi” si kuhusu ushindi dhidi ya Shetani na majeshi ya uhasama? Unaposema kuwa wewe umefanywa mkamilifu, nini hicho ndani yako ambacho kimekamilishwa? Je, si kuwa umevua mwenyewe tabia potovu ya kishetani, ili uweze kufaulu kupata upendo mkuu wa Mungu? Mambo kama haya yanasemekana kuhusu mambo machafu ndani ya mtu, na kuhusu Shetani; na hayasemwi kuhusu Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp