Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 586

06/08/2020

Huruma Zangu ni kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho la tabia Yangu ya haki na zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka shtaka rasmi lililoandikwa; wao pia, wataishi katika hali ya taharuki na woga kukiwepo na maafa, ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika enzi zote zilizopita. Na wafuasi Wangu wote ambao hawakuwa wakimtii mwingine yeyote yule ila Mimi watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na uridhisho usio na kifani na kuishi kwa raha ambayo sijawahi mpa mwanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia maovu yao. Tangu Nilipoanza kumwongoza mwanadamu, Nimekuwa Nikitamani kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Na sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao waovu na kufurahia hilo. Siku Yangu tayari imefika na siwezi kusubiri zaidi!

Kazi Yangu ya mwisho si kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, kazi Yangu ni kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote niliyofanya ni sahihi na ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, wala nguvu za asili, ambao ulimleta mwanadamu. Kinyume na hili, Mimi Ndiye ambaye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, mwanadamu anaweza tu kuangamia na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna yeyote atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; mwanadamu atakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde lisiloepukika la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa pekee wa mwanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la pekee la mwanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa mwanadamu. Bila Mimi, mwanadamu atasimama kabisa. Bila Mimi, mwanadamu atakumbana na msiba mkuu huku akikanyagwa na mapepo, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila Mimi Nikiwa na matumaini kwamba mwanadamu atanilipa kwa kutenda mema. Ingawa wachache wanaweza kunilipa, bado Nahitimisha safari Yangu duniani na Nianze kazi ambayo itatokea baada ya hapa, kwa sababu safari Yangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali sana kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu. Huu ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa. Maafa haya hutoka Kwangu na ni wazi kwamba Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamtaweza kuonekana kuwa Wema mbele Yangu, hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuwa vinafaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na ulionyesha tu woga au hali yenu ya uthabiti. Kwa mintarafu hii, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya. Shaka Yangu inaendelea kuhusu vitendo na tabia zenu ambazo Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba sitawahurumia wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Nisingependa kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hataweza kupokea huruma Yangu tena, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp