Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 245

Tabia ya Mungu ni mada ambayo inaonekana kuwa dhahania sana na ambayo haikubaliwi kwa urahisi, kwani tabia Yake ni tofauti na hulka ya binadamu. Mungu, vilevile, anazo hisia za anasa, hasira, huzuni, na furaha, lakini hisia kama hizo zinatofautiana pia na zile za binadamu. Mungu anayo nafsi Yake mwenyewe na kile Anachokimiliki. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukionyesha ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Nafsi Yake, kile Anachomiliki, pamoja na dutu na utambulisho vyote haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, kumtuliza binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa mwanadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini mema, changamfu, au ngumu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa wale walio hai miongoni mwa vitu vyote, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia yake ni ishara ya mamlaka na kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, na kizuri. Aidha, ni ishara ya namna ambavyo Mungu hawezi kukandamizwa au kushambuliwa na giza na kikosi chochote cha adui, pamoja na ishara ya namna ambavyo hawezi kuwa (na kwa kweli haruhusiwi kuwa) kukasirishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanaoweza au wanaweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini hulka ya binadamu si zaidi ya ishara tu ya hali ya kuwa na mamlaka ya juu zaidi kiasi cha binadamu dhidi ya wanyama. Binadamu mwenyewe hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuzidi nafsi, bali ni dutu tu inayotii kwa njia ya woga kutawaliwa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Anasa ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa hali ya kuwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa mwanadamu; furaha Yake ni ile ya hali ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi ya yote, ishara ya msaada. Hasira ya Mungu inatokana na uwepo wa dhuluma na vurugu inayosababisha ambayo inamdhuru mwanadamu Wake; kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na cha kupendeza. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya mwanadamu, ambaye kwake Ana matumaini lakini ambaye ameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya mwanadamu asiye na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule binadamu mzuri lakini mwenye hisia kinzani. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya urembo na wema Wake. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na mwanadamu kupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na furaha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko furaha. Furaha Yake ni ishara ya mwanadamu kuwa huru dhidi ya mateso na kuingia katika ulimwengu wa mwangaza. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote zipo kwa makusudio ya masilahi yake mwenyewe, na wala si za haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, na kidogo kati ya vyote neema ya Mbinguni. Hisia za mwanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo si za mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo binadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa kwa pumzi moja. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na mwenye heshima kila wakati, huku naye binadamu siku zote akiwa chini na kila wakati akikosa thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa mwanadamu; binadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na hufanya kazi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia uwepo wa mwanadamu, ilhali binadamu hachangii kitu katika mwangaza au haki. Hata kama binadamu anashughulika kwa muda, yeye ni mnyonge na hawezi kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake na wala si wengine. Binadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mbinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo na haki, wema, na urembo, huku naye binadamu akiwa mrithi na mwonyeshaji wa vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na urembo, ilhali binadamu anaweza, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa njia ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp