Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 205

07/08/2020

Mnafaa kujitolea kila kitu chenu kwa ajili ya kazi Yangu. Mnapaswa kufanya kazi inayonifaidi Mimi. Nataka Niwaambie kuhusu yale yote ambayo hamna ufahamu kamili kuyahusu ili muweze kupata yale yote mnayokosa kutoka Kwangu. Hata ingawa kasoro zenu ni nyingi kiasi kwamba haziwezi kuhesabika, Nina nia ya kuendelea kufanya kazi Ninayopaswa kuwa Nikifanya kwenu, kuwapa huruma Zangu za mwisho ili mpate kufaidika kutoka Kwangu, na mpate utukufu ambao hauko ndani yenu na ambao dunia haijawahi kuuona. Nimefanya kazi kwa miaka mingi sana, ilhali hakuna yeyote miongoni mwa binadamu ambaye amewahi kunijua. Nataka kuwaambia siri ambazo sijawahi kumwambia mtu yeyote yule.

Miongoni mwa binadamu, Nilikuwa roho ambaye hawakuweza kuona, Roho ambayo hawangeweza kuigusa. Kwa sababu ya hatua Zangu tatu za kazi duniani (kuumba ulimwengu, ukombozi, na kuiharibu), Naonekana miongoni mwao katika nyakati tofauti (kamwe sio hadharani) ili kutenda kazi Yangu miongoni mwa binadamu. Mara ya kwanza Nilipokuja miongoni mwa binadamu ilikuwa katika Enzi ya Ukombozi. Bila shaka Nilikuja miongoni mwa jamii ya Wayahudi; kwa hivyo watu wa kwanza kumwona Mungu Akija ulimwenguni walikuwa Wayahudi. Sababu Yangu ya kufanya kazi hii mwenyewe ilikuwa kwa sababu Nilitaka kutumia kupata mwili Kwangu kama sadaka ya dhambi katika kazi Yangu ya ukombozi. Kwa hivyo watu wa kwanza kuniona Mimi walikuwa Wayahudi wa Enzi ya Neema. Huo ndio ulikuwa wakati wa kwanza Mimi kufanya kazi Nikiwa katika mwili. Katika Enzi ya Ufalme, kazi Yangu ni kushinda na kutakasa, kwa hivyo kwa mara nyingine Nafanya kazi ya uchungaji katika mwili. Hii ni mara Yangu ya pili kufanya kazi katika mwili. Katika hatua mbili za mwisho za kazi, wanachokutana nacho watu si tena Roho asiyeonekana, asiyeshikika, bali ni mwanadamu ambaye ni Roho Aliyefanyika mwili. Hivyo kwa macho ya binadamu, Nilikuwa tena mtu asiye na sura wala hisia za Mungu. Zaidi ya hayo, Mungu ambaye watu huona, si wa kiume pekee, bali pia ni wa kike, kitu ambacho ni cha kushtua na kushangaza kwao. Muda baada ya muda, kazi Yangu ya ajabu huziondoa imani za kale ambazo zimekuwa kwa miaka mingi sana. Watu hushangazwa! Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho aliyoongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee, bali pia kike. Wako sawa kwamba wote wanazaliwa kwa binadamu, na tofauti kwamba mmoja anachukuliwa katika mimba na Roho Mtakatifu na mwingine Anazaliwa kwa mwanadamu lakini Anatoka kwa Roho moja kwa moja. Wako sawa kwa namna kwamba wote kupata miili kwa Mungu hutenda kazi ya Baba yao, na kutofautiana kwa namna kwamba mmoja Anafanya kazi ya ukombozi na mwingine anafanya kazi ya ushindi. Wote wanamwakilisha Mungu Baba, lakini mmoja ni Bwana wa Ukombozi aliyejaa upendo, ukarimu na huruma, na yule mwingine ni Mungu wa uhaki Aliyejaa hasira na hukumu. Mmoja ni Jemadari Mkuu Anayeanzisha kazi ya ukombozi na mwingine ni Mungu wa uhaki wa kukamilisha kazi ya kutamalaki. Mmoja ni Mwanzo na mwingine Mwisho. Mmoja ni mwili usio na dhambi na mwingine ni mwili unaokamilisha ukombozi, Anaendelea na kazi hiyo na kamwe hana dhambi hata. Wote ni Roho mmoja lakini wanaishi katika miili tofauti na walizaliwa katika sehemu tofauti. Na wametenganishwa na maelfu kadhaa ya miaka. Ilhali kazi Zao ni kijalizo kwa nyingine, hazina mgongano kamwe na zinaweza kuzungumziwa kwa wakati mmoja. Wote ni watu, lakini mmoja ni mtoto wa kiume na mwingine mtoto mchanga wa kike. Katika hii miaka yote, ambayo watu wamekiona si Roho pekee na mwanamume, bali pia vitu vingi visivyoambatana na fikira za binadamu, na kwa hivyo hawawezi kunielewa kikamilifu kamwe. Wanashinda wakiniamini mara nyingine na mara nyingine wakiwa na shaka Kunihusu, na iwapo Nipo kwa uhakika na ilhali Mimi ni ndoto ya mawazo. Ndio maana mpaka siku ya leo, watu hawatambui Mungu ni nini. Unaweza kweli kunieleza kwa sentensi moja? Unaweza kweli kusema kwa uhakika kwamba “Yesu si mwingine ila ni Mungu, na Mungu si mwingine ila Yesu”? Una ujasiri wa kusema kwamba “Mungu si mwingine bali Roho na Roho si mwingine bali ni Mungu”? Una ujasiri wa kusema kwamba “Mungu ni binadamu tu aliyevalia mwili?” Kwa kwelu una ujasiri wa kusema kuwa “Taswira ya Yesu ni taswira kubwa ya Mungu?” Unaweza kuelezea kwa umakinifu tabia ya Mungu na umbo kwa uwezo wa kipawa chako cha maneno? Unaweza hakika thubutu kusema kuwa Mungu Aliumba kiume pekee, sio kike, kwa mfano Wake mwenyewe? Ukisema hivi, basi kusingekuwepo na mwanamke miongoni mwa wateule Wangu na hata zaidi wanawake wasingekuwa aina miongoni mwa wanadamu. Sasa, unajua hakika Mungu ni nini? Je, Mungu ni binadamu? Je, Mungu ni Roho? Je, Mungu kwa uhakika ni wa kiume? Je, ni Yesu pekee Anayeweza kukamilisha kazi ambayo Ninataka kufanya? Ukichagua moja tu kati ya haya kujumulisha kiini Changu, basi utakuwa muumini mjinga kabisa. Nikifanya kazi kama mwili uliopatikana mara moja tu, je, unaweza kuniwekea mipaka? Je, unaweza hakika kuniangalia mara moja na ukajua yaliyo ndani Yangu? Je, unaweza hakika kunieleza kikamilifu kwa mujibu tu wa yale ambayo umeyafahamu wakati wa maisha yako? Na iwapo katika kuingia Kwangu kwa mwili mara mbili Nafanya kazi inayofanana, utanichukulia vipi? Unaweza kuniacha milele msalabani nikiwa na misumari? Je, Mungu Anaweza kuwa wa kawaida jinsi unavyosema?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp