Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 126

Kila hatua ya kazi ya Mungu mwenye mwili inawakilisha kazi yake ya enzi yote, na haiwakilishi kipindi fulani kama kazi ya mwanadamu. Na hivyo mwisho wa kazi ya kufanyika Kwake mwili mara ya mwisho haimaanishi kwamba kazi Yake imefikia mwisho kabisa, kwa maana kazi Yake katika mwili inawakilisha enzi yote, na haiwakilishi kipindi tu ambacho Anafanya kazi Yake katika mwili tu. Ni kwamba tu Anakamilisha kazi Yake ya enzi yote wakati ambapo yupo katika mwili, ambayo baadaye inaenea sehemu zote. Baada ya Mungu mwenye mwili kutimiza huduma yake, atawakabidhi wale wote wanaoifuata kazi Yake ya baadaye. Kwa njia hii kazi Yake ya enzi yote itaendelezwa bila kusitishwa. Kazi ya enzi yote ya kufanyika kuwa mwili itachukuliwa tu kuwa imekamilika baada ya kuenea ulimwenguni kote. Kazi ya Mungu mwenye mwili huanzisha enzi mpya, na wale wanaoiendeleza kazi Yake ni watu wanaotumiwa Naye. Kazi inayofanywa na mwanadamu yote ipo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili, na haina uwezo wa kwenda zaidi ya mawanda haya. Ikiwa Mungu mwenye mwili haji kufanya kazi Yake, mwanadamu hana uwezo wa kuhitimisha enzi ya zamani, na hana uwezo wa kuikaribisha enzi mpya. Kazi inayofanywa na mwanadamu ipo tu ndani ya wajibu wake ambao unawezekana kibinadamu, na haiwakilishi kazi ya Mungu. Ni Mungu mwenye mwili pekee ndiye anayeweza kuja na kukamilisha kazi ambayo Anapaswa kuifanya, na mbali na Yeye, hakuna anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Bila shaka, kile Ninachozungumzia ni kuhusiana na kazi ya kufanyika mwili. Huyu Mungu mwenye mwili, kwanza anachukua hatua ya kazi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu, baada ya hapo Anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu. Lengo la kazi hii ni kumshinda mwanadamu. Kwa upande mmoja, Mungu mwenye mwili hapatani na mitazamo ya mwanadamu, aidha, anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu, na kwa hivyo mwanadamu anakuza mawazo zaidi ya kukosoa kuhusu Yeye. Anafanya kazi ya ushindi miongoni mwa wanadamu ambaye ana dhana nyingi sana kumhusu Yeye. Bila kujali jinsi wanavyomchukulia, Atakapokuwa Amekamilisha huduma Yake, wanadamu wote watakuwa ni wenyeji wa utawala wake. Ukweli wa kazi hii hauonekani tu miongoni mwa Wachina, bali wao wanawakilisha namna ambavyo wanadamu wote watakavyoshindwa. Matokeo yanayoonekana kwa watu hawa ni kitangulizi cha matokeo yatakayoonekana kwa wanadamu wote, na matokeo ya kazi Anayofanya wakati ujao yatazidi sana matokeo kwa watu hawa. Kazi ya Mungu mwenye mwili haihusishi mshindo mkubwa wa tarumbeta, wala haijakita katika mafumbo. Ni halisi na ya kweli, na ni kazi ambayo moja kujumlisha na moja ni sawa sawa na mbili. Hajafichwa kwa mtu yeyote, na wala haimdanganyi mtu yeyote. Kile ambacho watu wanaona ni vitu halisi, na kile ambacho mwanadamu anapata ni ukweli halisi na maarifa. Kazi itakapokamilika, mwanadamu atakuwa na maarifa mapya juu Yake, na wale ambao kweli wanamtafuta Mungu hawatakuwa na dhana yoyote juu Yake. Haya sio tu matokeo ya kazi Yake kwa Wachina, lakini pia inawakilisha matokeo ya kazi yake katika kuwashinda wanadamu wote, kwa maana hakuna kitu ambacho ni cha manufaa zaidi katika kazi ya kuwashinda watu kuliko mwili huu, na kazi ya mwili huu, na kila kitu cha mwili huu. Vina manufaa katika kazi Yake leo, na vina manufaa katika kazi Yake hapo baadaye. Mwili huu utawashinda wanadamu wote na utawapata wanadamu wote. Hakuna kazi bora zaidi ambayo kwayo wanadamu wote watamwona Mungu, na kumtii Mungu, na kumfahamu Mungu. Kazi inayofanywa na mwanadamu inawakilisha tu mawanda finyu, na Mungu anapofanya kazi Yake hazungumzi na watu fulani, bali Anazungumza na wanadamu wote, na wale wote wanaoikubali kazi Yake. Mwisho Anaoutangaza ni mwisho wa wanadamu wote, na sio mwisho wa mtu fulani tu. Hamtendei mtu yeyote kwa umahususi, wala hamkandamizi mtu yeyote, na Anafanya kazi kwa ajili ya, na Anazungumza na wanadamu wote. Na kwa hiyo Mungu huyu katika mwili amekwisha waainisha wanadamu wote kulingana na aina yao, tayari amekwisha wauhukumu wanadamu wote, na amwekwishapangilia hatima inayofaa kwa wanadamu wote. Ingawa Mungu anafanya kazi Yake China tu, kwa hakika ameshaamua kazi ya ulimwengu mzima. Hawezi kusubiri hadi kazi Yake itakapoenea miongoni mwa wanadamu wote kabla ya kutoa matamshi Yake na kuweka mipango hatua kwa hatua. Hivyo, sio kwamba utakuwa umechelewa sana? Sasa Anaweza kabisa kukamilisha kazi ya wakati ujao kabla ya wakati huo. Kwa sababu Yule anayefanya kazi ni Mungu mwenye mwili, Anafanya kazi isiyokuwa na mipaka ndani ya mawanda yenye mipaka, na baadaye Atamfanya mwanadamu atekeleze jukumu ambalo mwanadamu anapaswa kulitekeleza; hii ni kanuni ya kazi Yake. Anaweza kuishi tu na mwanadamu kwa muda, na hawezi kushirikiana na mwanadamu hadi kazi ya enzi zote itakapokamilika. Ni kwa sababu Yeye ni Mungu kwamba Yeye hutabiri kazi Yake ya Wakati ujao kabla ya wakati. Baada ya hapo, Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina kwa maneno Yake, na mwanadamu ataingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua kulingana na neno Lake. Hakuna atakayekwepa, na wote wanapaswa kutenda kulingana na hili. Hivyo, katika wakati ujao, enzi itaongozwa na maneno Yake, na sio kuongozwa na Roho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp