Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 477

Ingawa ufunuo wa asilia ulitokea baada ya Petro kuanza kumfuata Yesu, katika asili alikuwa, tangu mwanzo kabisa, mtu ambaye alikuwa tayari kujiwasilisha kwa Roho Mtakatifu na kumtafuta Kristo. Utiifu wake wa Roho Mtakatifu ulikuwa safi: hakutafuta umaarufu na mali, lakini badala yake alikuwa amepewa motisha na utii wa ukweli. Ingawa kuna nyakati tatu ambapo Petro alikana kumjua Kristo, na ingawa alimjaribu Bwana Yesu, udhaifu kidogo kama huu wa kibinadamu haukubeba uhusiano wa asilia yake, na haukuathiri harakati zake za mbeleni, na huwezi kuthibitisha kikamilifu ya kuwa majaribu yake yalikuwa kitendo cha mpinga Kristo. Udhaifu wa kawaida wa kibinadamu ni kitu ambacho kimo kwa watu wote duniani—je, unatarajia Petro kuwa tofauti vyovyote vile? Je, si watu wana mtazamo fulani kuhusu Petro kwa sababu alifanya makosa mengi ya kijinga? Na je, si watu wanampenda Paulo kwa sababu ya kazi yote aliyoifanya, na nyaraka zote alizoandika? Itakuwaje mtu kuwa na uwezo wa kuona kupitia kiini cha mwanadamu? Hakika, je, wale ambao kwa kweli wana hisia wanaweza kuona kitu chenye thamani ndogo kama hiyo? Ingawa miaka mingi ya matukio ya uchungu ya Petro hayajanakiliwa katika Biblia, hii haithibitishi kuwa Petro hakuwa na matukio halisi, au kwamba Petro hakufanywa mkamilifu. Ni jinsi gani kazi ya Mungu inaweza kueleweka na mwanadamu? Kumbukumbu kwenye Biblia hazikuchaguliwa binafsi na Yesu, lakini zilikusanywa na vizazi vya baadaye. Kwa njia hii, si yote ambayo yaliandikwa katika Biblia yalichaguliwa kulingana na mawazo na mwanadamu? Zaidi ya hayo, hatima ya Petro na Paulo hazijaelezwa kwa dhati katika nyaraka, kwa hivyo mwanadamu anawahukumu Petro na Paulo kulingana na mtazamo wake mwenyewe, na kulingana na matakwa yake mwenyewe. Na kwa kuwa Paulo alifanya kazi kubwa sana, kwa sababu “michango” yake ilikuwa mikuu sana, yeye alipata imani ya umma. Je, si mwanadamu anamakinika tu na vitu vya juu juu tu. Inakuwaje mwanadamu kuwa na uwezo wa kuona kupitia kwa kiini cha mwanadamu? Bila kutaja, kwa kuwa Paulo amekuwa mlengwa wa ibada kwa maelfu ya miaka, ni nani ambaye atathubutu kukana kazi yake kwa haraka? Petro alikuwa mvuvi tu, hivyo ni jinsi gani mchango wake ungekuwa mkubwa kama ule wa Paulo? Kwa msingi wa mchango, Paulo angepaswa kuzawadiwa kabla ya Petro, na inapaswa kuwa yeye ndiye angekuwa amehitimu vyema zaidi kupata kibali cha Mungu. Nani angeweza kufikiri kuwa, katika kumtendea Paulo, Mungu alimfanya tu afanye kazi kupitia vipawa vyake, ilhali Mungu alimfanya Petro kuwa mkamilifu. Si kwa njia yoyote kweli ya kwamba Bwana Yesu alikuwa amefanya mpango kwa ajili ya Petro na Paulo tangu mwanzo kabisa: Badala yake, walifanywa wakamilifu au kuwekwa kazini kulingana na tabia zao za kiasili. Na kwa hivyo, kitu ambacho wanadamu wanachoona kama michango ya nje ya mwanadamu tu, ilhali anachoona Mungu ni kiini cha mtu, na vile vile kama njia ambayo mwanadamu hufuatilia tangu mwanzo, na motisha inayosukuma harakati ya mwanadamu. Watu hupima mwanadamu kulingana na dhana zao, na kulingana na mitazamo yao wenyewe, na bado hatima ya mwisho ya mwanadamu haiamuliwi kulingana na mambo ya nje ya mwanadamu. Na kwa hivyo Mimi ninasema kwamba kama njia unayochukua tangu mwanzo ni njia ya mafanikio, na mtazamo wako kuhusu harakati ni sahihi tangu mwanzo, basi wewe ni kama ya Petro; kama njia ambayo unatembea ni njia ya kushindwa, basi gharama yoyote ambayo unalipa, hatima yako itakuwa sawa na ile ya Paulo. Yawayo yoyote, hatima yako, na kama utafaulu ama hautafaulu, yote yanaamuliwa na kama njia unayotafuta ni sahihi ama si sahihi, badala ya kujitolea kwako, au gharama ambayo wewe hulipa. Kiini cha Petro na kiini cha Paulo, na malengo ambayo walifuatilia, yalikuwa tofauti; mwanadamu hana uwezo wa kugundua vitu hivi, na Mungu pekee anaweza kuyajua kwa ujumla wao. Kwa kuwa kitu ambacho Mungu huona ni kiini cha mwanadamu, ilhali mwanadamu hajui chochote kuhusu kiini chake mwenyewe. Mwanadamu hana uwezo wa kukitazama kiini ndani ya mwanadamu ama kimo chake halisi, na hivyo hana uwezo wa kutambua sababu za kutofaulu ama kufaulu kwa Paulo na Petro. Sababu ya wanadamu wengi kumuabudu Paulo na wala si Petro ni kuwa Paulo alitumika katika kazi ya umma, na mwanadamu anaweza kutambua kazi hii, na hivyo watu wanakiri “mafanikio” ya Paulo. Matukio ya Petro, wakati huo huo, hayaonekani na mwanadamu, na kwamba kile alichotafuta hakipatikani na mwanadamu, na hivyo mwanadamu hana moyo wa kutaka kumjua Petro.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp