Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 584

23/09/2020

Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele na katika mpango Wangu mpya, kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya ili wale ambao wataniona watajipiga kifuani na kuulilia uwepo Wangu bila kukoma. Kwani Ninaleta mwisho wa mwanadamu duniani, na baada ya hapo, Nitaweka wazi tabia Yangu kwa mwanadamu ili wanijuao na wasionijua watayashibisha macho yao na kuona kwamba kweli, nimekuja kwa wanadamu, duniani mahali ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Nimuumbe mwanadamu. Matilaba yangu ni kuona mnafuatilia kwa moyo wenu wote kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinamkaribia mwanadamu tena, karibu na wale wote wanaonipinga.

Pamoja na mbingu, Ninaanza kazi ambayo ni lazima Niifanye. Kwa hivyo Mimi husafiri kati ya misururu ya watu na kupita kati ya mbingu na ardhi. Hakuna mtu anayetambua mienendo Yangu au kuitambua maneno Yangu. Kwa hivyo, mpango Wangu bado unaendelea kwa urahisi. Ni vile tu hisia zenu zimekuwa ngumu kiasi kwamba hamjui hatua za kazi Yangu hata kidogo. Hata hivyo, siku moja, mtakuja kutambua kusudio Langu. Leo hii, Ninaishi miongoni mwenu na Ninasumbuka pamoja nanyi. Kwa muda mrefu, Nimeelewa mtazamo alio nao mwanadamu juu Yangu. Nisingependa kutangaza wazi, wala kutoa mifano zaidi ya kile kinachoniumiza ili kuwaaibisha. Ombi Langu la pekee ni kwamba myaweke moyoni yale yote mliyoyafanya kwa ajili ya hukumu siku tutakapokutana tena. Nisingependa kumshutumu yeyote miongoni mwenu kwa njia isiyo ya kweli, kwa sababu Nimekuwa Nikifanya mambo kwa njia ya haki, bila upendeleo, na yenye heshima. Bila shaka Ningependa kwamba nyinyi pia ni waadilifu na hamtafanya lolote lililo kinyume na mbingu na ardhi na dhamiri yenu. Haya pekee ndiyo Ninayowauliza. Wengi wanasumbuka na hawana amani kwa sababu wametenda maovu mabaya, na wengi wanaona aibu kwamba hawajawahi tenda lolote zuri. Tena wapo pia wengi ambao hawatahayari kutokana na dhambi zao na badala yake, wanakuwa wabaya zaidi, huku wakizitoa kabisa barakoa inayoficha sura zao mbaya—ambayo ilikuwa bado haijaonyeshwa kikamilifu—ili kujaribu tabia Yangu. Huwa sijali au sitilii maanani matendo ya mtu yeyote mmoja. Badala yake, Mimi hufanya kazi Ninayopaswa kufanya, kujifunza maarifa, kuzunguka katika nchi au kufanya lile ambalo lilanipendeza. Katika wakati muhimu, Mimi hurejelea kazi Yangu miongoni mwa wanadamu kama Nilivyopanga, bila kuchelewa hata kidogo, na hili hufanywa kwa urahisi na kwa makini. Hata hivyo, kuna watu ambao wanawekwa pembeni katika kila hatua ya kazi Yangu, kwa sababu Ninadharau hali yao ya kujipendekeza na hali ya kujifanya wanyenyekevu. Wale wanaonichukia hakika watatelekezwa, iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda. Kwa ufupi, Ninataka wale wote Ninaowadharau kuwa mbali Nami. Ni dhahiri kwamba, sitawahurumia wale waovu ambao wamebaki katika makao Yangu. Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia, sina wasiwasi wa kuzitupa nje zile nyoyo zote zinazostahili dharau, kwa kuwa Nina mpango Wangu Mwenyewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp